Juzuu 19 وقال الذين

Kuanzia Surat Al-Furqan 25:21 hadi Surat An-Naml 27:55

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

Surat Al-Furqan

۞ وَقَالَ ٱلَّذِينَ لَا يَرۡجُونَ لِقَآءَنَا لَوۡلَآ أُنزِلَ عَلَيۡنَا ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ أَوۡ نَرَىٰ رَبَّنَاۗ لَقَدِ ٱسۡتَكۡبَرُواْ فِيٓ أَنفُسِهِمۡ وَعَتَوۡ عُتُوّٗا كَبِيرٗا ٢١

Waqālal-ladhīna lā yarjūna liqā'anā lawlā unzila 'alaynal-malā'ikatu aw narā rabbanā laqadistakbarū fī anfusihim wa'ataw 'utuwwan kabīrā

NA WALISEMA wale wasio taraji kukutana nasi: Mbona sisi hatuteremshiwi Malaika au hatumwoni Mola wetu Mlezi? Kwa yakini hawa wamejiona bora nafsi zao, na wamepanda kichwa vikubwa mno! 21

يَوۡمَ يَرَوۡنَ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ لَا بُشۡرَىٰ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُجۡرِمِينَ وَيَقُولُونَ حِجۡرٗا مَّحۡجُورٗا ٢٢

Yawma yarawnal-malā'ikata lā bushrā yawma'idhil lil-mujrimīna wayaqūlūna hijram mahjūrā

Siku watakayo waona Malaika haitakuwa furaha siku hiyo kwa wakosefu. Na watasema: Mungu apishe mbali! 22

وَقَدِمۡنَآ إِلَىٰ مَا عَمِلُواْ مِنۡ عَمَلٖ فَجَعَلۡنَٰهُ هَبَآءٗ مَّنثُورًا ٢٣

Waqadimnā ilā mā 'amilū min 'amalin faja'alnāhu habā'am manthūrā

Na tutayaendea yale waliyo yatenda katika vitendo vyao, tuvifanye kama mavumbi yaliyo tawanyika. 23

أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَنَّةِ يَوۡمَئِذٍ خَيۡرٞ مُّسۡتَقَرّٗا وَأَحۡسَنُ مَقِيلٗا ٢٤

Ashābul-jannati yawma'idhin khayrum mustaqarran wa ahsanu maqīlā

Watu wa Peponi siku hiyo watakuwa katika makaazi bora na mahali penye starehe nzuri. 24

وَيَوۡمَ تَشَقَّقُ ٱلسَّمَآءُ بِٱلۡغَمَٰمِ وَنُزِّلَ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ تَنزِيلًا ٢٥

Wayawma tashaqqaqus-samā'u bil-ghamāmi wanuzzilal-malā'ikatu tanzīlā

Na siku zitapo funguka mbingu kwa mawingu, na wateremshwe Malaika kwa wingi, 25

ٱلۡمُلۡكُ يَوۡمَئِذٍ ٱلۡحَقُّ لِلرَّحۡمَٰنِۚ وَكَانَ يَوۡمًا عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ عَسِيرٗا ٢٦

Al-mulku yawma'idhinil-haqqu lir-rahmāni wakāna yawman 'alal-kāfirīna 'asīrā

Ufalme wa haki siku hiyo utakuwa wa Arrahman, Mwingi wa Rehema, na itakuwa siku ngumu kwa makafiri. 26

وَيَوۡمَ يَعَضُّ ٱلظَّالِمُ عَلَىٰ يَدَيۡهِ يَقُولُ يَٰلَيۡتَنِي ٱتَّخَذۡتُ مَعَ ٱلرَّسُولِ سَبِيلٗا ٢٧

Wayawma ya'adduz-zālimu 'alā yadayhi yaqūlu yālaytanit-takhadhtu ma'ar-rasūli sabīlā

Na siku ambayo mwenye kudhulumu atajiuma mikono yake, na huku anasema: Laiti ningeli shika njia pamoja na Mtume! 27

يَٰوَيۡلَتَىٰ لَيۡتَنِي لَمۡ أَتَّخِذۡ فُلَانًا خَلِيلٗا ٢٨

Yāwaylatā laytanī lam attakhidh fulānan khalīlā

Ee Ole wangu! Laiti nisingeli mfanya fulani kuwa rafiki! 28

لَّقَدۡ أَضَلَّنِي عَنِ ٱلذِّكۡرِ بَعۡدَ إِذۡ جَآءَنِيۗ وَكَانَ ٱلشَّيۡطَٰنُ لِلۡإِنسَٰنِ خَذُولٗا ٢٩

Llaqad adallanī 'anidh-dhikri ba'da idh jā'anī wakānash-shaytānu lil-insāni khadhūlā

Amenipoteza, nikaacha Ukumbusho, baada ya kwisha nijia, na kweli Shet'ani ni khaini kwa mwanaadamu. 29

وَقَالَ ٱلرَّسُولُ يَٰرَبِّ إِنَّ قَوۡمِي ٱتَّخَذُواْ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانَ مَهۡجُورٗا ٣٠

Waqālar-rasūlu yārabbi inna qawmit-takhadhū hādhal-qur'āna mahjūrā

Na Mtume alikuwa akisema: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wameifanya hii Qur'ani ni kihame. 30

وَكَذَٰلِكَ جَعَلۡنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوّٗا مِّنَ ٱلۡمُجۡرِمِينَۗ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ هَادِيٗا وَنَصِيرٗا ٣١

Wakadhālika ja'alnā likulli nabiyyin 'aduwwam minal-mujrimīna wakafā birabbika hādiyan wanasīrā

Na vivi hivi tumemfanyia kila Nabii adui miongoni mwa wakosefu, na Mola wako Mlezi anatosha kuwa Mwenye kuongoa na Mwenye kunusuru. 31

وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَوۡلَا نُزِّلَ عَلَيۡهِ ٱلۡقُرۡءَانُ جُمۡلَةٗ وَٰحِدَةٗۚ كَذَٰلِكَ لِنُثَبِّتَ بِهِۦ فُؤَادَكَۖ وَرَتَّلۡنَٰهُ تَرۡتِيلٗا ٣٢

Waqālal-ladhīna kafarū lawlā nuzzila 'alayhil-qur'ānu jumlatan wāhidatan kadhālika linuthabbita bihī fu'ādaka warattalnāhu tartīlā

Na wakasema walio kufuru: Kwa nini hakuteremshiwa Qur'ani kwa jumla moja? Hayo ni hivyo ili tuuthibitishe moyo wako, na ndio tumeisoma kwa mafungu. 32

وَلَا يَأۡتُونَكَ بِمَثَلٍ إِلَّا جِئۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ وَأَحۡسَنَ تَفۡسِيرًا ٣٣

Walā ya'tūnaka bimathalin illā ji'nāka bil-haqqi wa ahsana tafsīrā

Wala hawatakuletea mfano wowote, ila na Sisi tutakuletea (jawabu) kwa haki, na tafsiri iliyo bora. 33

ٱلَّذِينَ يُحۡشَرُونَ عَلَىٰ وُجُوهِهِمۡ إِلَىٰ جَهَنَّمَ أُوْلَٰٓئِكَ شَرّٞ مَّكَانٗا وَأَضَلُّ سَبِيلٗا ٣٤

Alladhīna yuhsharūna 'alā wujūhihim ilā jahannama ulā'ika sharrum makānan wa adallu sabīlā

Wale ambao watakao kusanywa na kubururwa kifudifudi mpaka kwenye Jahannamu, hao watakuwa na mahali pabaya, ndio wenye kuipotea sana njia. 34

وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ وَجَعَلۡنَا مَعَهُۥٓ أَخَاهُ هَٰرُونَ وَزِيرٗا ٣٥

Walaqad ātaynā mūsal-kitāba waja'alnā ma'ahū akhāhu hārūna wazīrā

Na hakika tulimpa Musa Kitabu na tukamweka pamoja naye nduguye, Harun, kuwa waziri. 35

فَقُلۡنَا ٱذۡهَبَآ إِلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا فَدَمَّرۡنَٰهُمۡ تَدۡمِيرٗا ٣٦

Faqulnadhhabā ilal-qawmil-ladhīna kaddhabū bi'āyātinā fadammarnāhum tadmīrā

. Tukawaambia: Nendeni kwa watu walio kanusha Ishara zetu. Basi tukawateketeza kabisa. 36

وَقَوۡمَ نُوحٖ لَّمَّا كَذَّبُواْ ٱلرُّسُلَ أَغۡرَقۡنَٰهُمۡ وَجَعَلۡنَٰهُمۡ لِلنَّاسِ ءَايَةٗۖ وَأَعۡتَدۡنَا لِلظَّٰلِمِينَ عَذَابًا أَلِيمٗا ٣٧

Waqawma nūhil lammā kaddhabur-rusula aghraqnāhum waja'alnāhum lin-nāsi āyatan wa a'tadnā liz-zālimīna 'adhāban alīmā

Na watu wa Nuhu, walipo wakanusha Mitume, tuliwazamisha, na tukawafanya ni Ishara kwa watu. Na tumewaandalia wenye kudhulumu adhabu chungu. 37

وَعَادٗا وَثَمُودَاْ وَأَصۡحَٰبَ ٱلرَّسِّ وَقُرُونَۢا بَيۡنَ ذَٰلِكَ كَثِيرٗا ٣٨

Wa'ādan wathamūda wa ashābar-rassi waqurūnā bayna dhālika kathīrā

Na tuliwaangamiza kina A'di na Thamudi na watu wa Rass na vizazi vingi vilivyo kuwa kati yao. 38

وَكُلّٗا ضَرَبۡنَا لَهُ ٱلۡأَمۡثَٰلَۖ وَكُلّٗا تَبَّرۡنَا تَتۡبِيرٗا ٣٩

Wakullan darabnā lahul-amthāla wakullan tabbarnā tatbīrā

Na wote tuliwapigia mifano, na wote tuliwaangamiza kabisa kabisa. 39

وَلَقَدۡ أَتَوۡاْ عَلَى ٱلۡقَرۡيَةِ ٱلَّتِيٓ أُمۡطِرَتۡ مَطَرَ ٱلسَّوۡءِۚ أَفَلَمۡ يَكُونُواْ يَرَوۡنَهَاۚ بَلۡ كَانُواْ لَا يَرۡجُونَ نُشُورٗا ٤٠

Walaqad ataw 'alal-qaryatil-latī umtirat mataras-saw'i afalam yakūnū yarawnahā bal kānū lā yarjūna nushūrā

Na kwa yakini wao wanafika kwenye nchi ilio teremshiwa mvua mbaya. Basi, je, hawakuwa wakiiona? Bali walikuwa hawataraji kufufuliwa. 40

وَإِذَا رَأَوۡكَ إِن يَتَّخِذُونَكَ إِلَّا هُزُوًا أَهَٰذَا ٱلَّذِي بَعَثَ ٱللَّهُ رَسُولًا ٤١

Wa idhā ra'awka in yattakhidhūnaka illā huzuwan ahādhal-ladhī ba'athallāhu rasūlā

Na wanapo kuona hawakuchukulii ila ni mzaha tu, na (wanasema): Ati ndiye huyu Mwenyezi Mungu aliye mtuma kuwa Mtume? 41

إِن كَادَ لَيُضِلُّنَا عَنۡ ءَالِهَتِنَا لَوۡلَآ أَن صَبَرۡنَا عَلَيۡهَاۚ وَسَوۡفَ يَعۡلَمُونَ حِينَ يَرَوۡنَ ٱلۡعَذَابَ مَنۡ أَضَلُّ سَبِيلًا ٤٢

In kāda layudillunā 'an ālihatinā lawlā an sabarnā 'alayhā wasawfa ya'lamūna hīna yarawnal-'adhāba man adallu sabīlā

Kwa hakika alikuwa karibu kutupoteza tuiache miungu yetu, ingeli kuwa hatukushikamana nayo kwa kuvumilia. Bado watakuja jua, watakapo iona adhabu, ni nani aliye potea njia. 42

أَرَءَيۡتَ مَنِ ٱتَّخَذَ إِلَٰهَهُۥ هَوَىٰهُ أَفَأَنتَ تَكُونُ عَلَيۡهِ وَكِيلًا ٤٣

Ara'ayta manit-takhadha ilāhahū hawāhu afa'anta takūnu 'alayhi wakīlā

Je! Umemwona aliye yafanya matamanio yake kuwa ndio mungu wake? Basi je, wewe utakuwa ni wakili wake? 43

أَمۡ تَحۡسَبُ أَنَّ أَكۡثَرَهُمۡ يَسۡمَعُونَ أَوۡ يَعۡقِلُونَۚ إِنۡ هُمۡ إِلَّا كَٱلۡأَنۡعَٰمِ بَلۡ هُمۡ أَضَلُّ سَبِيلًا ٤٤

Am tahsabu anna aktharahum yasma'ūna aw ya'qilūna in hum illā kal-an'āmi bal hum adallu sabīlā

Au wewe unadhani kwamba wengi wao wanasikia au wanaelewa? Hao hawakuwa ila ni kama nyama hoa tu, bali wao wamepotea zaidi njia. 44

أَلَمۡ تَرَ إِلَىٰ رَبِّكَ كَيۡفَ مَدَّ ٱلظِّلَّ وَلَوۡ شَآءَ لَجَعَلَهُۥ سَاكِنٗا ثُمَّ جَعَلۡنَا ٱلشَّمۡسَ عَلَيۡهِ دَلِيلٗا ٤٥

Alam tara ilā rabbika kayfa maddaz-zilla walaw shā'a laja'alahū sākinan thumma ja'alnash-shamsa 'alayhi dalīlā

Je! Huoni jinsi Mola wako Mlezi anavyo kitandaza kivuli. Na angeli taka angeli kifanya kikatulia tu. Kisha tumelifanya jua kuwa ni kiongozi wake. 45

ثُمَّ قَبَضۡنَٰهُ إِلَيۡنَا قَبۡضٗا يَسِيرٗا ٤٦

Thumma qabadnāhu ilaynā qabdan yasīrā

Kisha tunakivutia kwetu kidogo kidogo. 46

وَهُوَ ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلَّيۡلَ لِبَاسٗا وَٱلنَّوۡمَ سُبَاتٗا وَجَعَلَ ٱلنَّهَارَ نُشُورٗا ٤٧

Wahuwal-ladhī ja'ala lakumul-layla libāsan wan-nawma subātan waja'alan-nahāra nushūrā

Naye ndiye aliye kufanyieni usiku kuwa ni vazi, na usingizi kuwa mapumziko, na akakufanyieni mchana ni kufufuka. 47

وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَرۡسَلَ ٱلرِّيَٰحَ بُشۡرَۢا بَيۡنَ يَدَيۡ رَحۡمَتِهِۦۚ وَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ طَهُورٗا ٤٨

Wahuwal-ladhī arsalar-riyāha bushrā bayna yaday rahmatihī wa anzalnā minas-samā'i mā'an tahūrā

Naye ndiye anaye zituma pepo kuwa bishara njema kabla ya rehema yake, na tunayateremsha kutoka mbinguni maji safi. 48

لِّنُحۡـِۧيَ بِهِۦ بَلۡدَةٗ مَّيۡتٗا وَنُسۡقِيَهُۥ مِمَّا خَلَقۡنَآ أَنۡعَٰمٗا وَأَنَاسِيَّ كَثِيرٗا ٤٩

Llinuhya bihī baldatam maytan wanusqiyahū mimmā khalaqnā an'āman wa anāsiyya kathīrā

Ili kwa hayo tuihuishe nchi iliyo kufa, na tuwanyweshe wanyama na watu wengi tulio waumba. 49

وَلَقَدۡ صَرَّفۡنَٰهُ بَيۡنَهُمۡ لِيَذَّكَّرُواْ فَأَبَىٰٓ أَكۡثَرُ ٱلنَّاسِ إِلَّا كُفُورٗا ٥٠

Walaqad sarrafnāhu baynahum liyaddhakkarū fa abā aktharun-nāsi illā kufūrā

Na kwa yakini tumeisarifu kati yao wapate kukumbuka. Lakini watu wengi wanakataa ila kukufuru. 50

وَلَوۡ شِئۡنَا لَبَعَثۡنَا فِي كُلِّ قَرۡيَةٖ نَّذِيرٗا ٥١

Walaw shi'nā laba'athnā fī kulli qaryatin nadhīrā

Na tungeli taka tungeli peleka katika kila mji Mwonyaji. 51

فَلَا تُطِعِ ٱلۡكَٰفِرِينَ وَجَٰهِدۡهُم بِهِۦ جِهَادٗا كَبِيرٗا ٥٢

Falā tuti'il-kāfirīna wajāhidhum bihī jihādan kabīrā

Basi usiwat'ii makafiri. Na pambana nao kwayo kwa Jihadi kubwa. 52

۞ وَهُوَ ٱلَّذِي مَرَجَ ٱلۡبَحۡرَيۡنِ هَٰذَا عَذۡبٞ فُرَاتٞ وَهَٰذَا مِلۡحٌ أُجَاجٞ وَجَعَلَ بَيۡنَهُمَا بَرۡزَخٗا وَحِجۡرٗا مَّحۡجُورٗا ٥٣

Wahuwal-ladhī marajal-bahrayni hādhā 'adhbun furātun wahādhā milhun ujājun waja'ala baynahumā barzakhan wahijram mahjūrā

Naye ndiye aliye zipeleka bahari mbili, hii tamu mno, na hii ya chumvi chungu. Na akaweka baina yao kinga na kizuizi kizuiacho. 53

وَهُوَ ٱلَّذِي خَلَقَ مِنَ ٱلۡمَآءِ بَشَرٗا فَجَعَلَهُۥ نَسَبٗا وَصِهۡرٗاۗ وَكَانَ رَبُّكَ قَدِيرٗا ٥٤

Wahuwal-ladhī khalaqa minal-mā'i basharan faja'alahū nasaban wasihran wakāna rabbuka qadīrā

Naye ndiye aliye muumba mwanaadamu kutokana na maji, akamjaalia kuwa na nasaba na ushemeji. Na Mola wako Mlezi ni Muweza. 54

وَيَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَنفَعُهُمۡ وَلَا يَضُرُّهُمۡۗ وَكَانَ ٱلۡكَافِرُ عَلَىٰ رَبِّهِۦ ظَهِيرٗا ٥٥

Waya'budūna min dūnillāhi mā lā yanfa'uhum walā yadurruhum wakānal-kāfiru 'alā rabbihī zahīrā

Na wanayaabudu badala ya Mwenyezi Mungu yasiyo wafaa wala yasiyo wadhuru. Na kafiri daima ni msaidizi wa kumpinga Mola wake Mlezi. 55

وَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ إِلَّا مُبَشِّرٗا وَنَذِيرٗا ٥٦

Wamā arsalnāka illā mubasshiran wanadhīrā

Nasi hatukukutuma ila kuwa ni Mbashiri na Mwonyaji. 56

قُلۡ مَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍ إِلَّا مَن شَآءَ أَن يَتَّخِذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ سَبِيلٗا ٥٧

Qul mā as'alukum 'alayhi min ajrin illā man shā'a an yattakhidha ilā rabbihī sabīlā

Sema: Sikukuombeni ujira juu yake; ila atakaye na ashike njia iendayo kwa Mola wake Mlezi. 57

وَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱلۡحَيِّ ٱلَّذِي لَا يَمُوتُ وَسَبِّحۡ بِحَمۡدِهِۦۚ وَكَفَىٰ بِهِۦ بِذُنُوبِ عِبَادِهِۦ خَبِيرًا ٥٨

Watawakkal 'alal-hayyil-ladhī lā yamūtu wasabbih bihamdihī wakafā bihī bidhunūbi 'ibādihī khabīrā

Na mtegemee Aliye Hai, ambaye hafi. Na umtukuze kwa sifa zake. Na yatosha kwake kuwa yeye ni Mwenye khabari za dhambi za waja wake. 58

ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِۖ ٱلرَّحۡمَٰنُ فَسۡـَٔلۡ بِهِۦ خَبِيرٗا ٥٩

Alladhī khalaqas-samāwāti wal-arda wamā baynahumā fī sittati ayyāmin thummastawā 'alal-'arshir-rahmānu fas'al bihī khabīrā

. Ambaye ameziumba mbingu na ardhi, na viliomo ndani yake kwa siku sita. Kisha akatawala juu ya A'rshi, Arrahman, Mwingi wa Rehema! Uliza khabari zake kwa wamjuaye. 59

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱسۡجُدُواْۤ لِلرَّحۡمَٰنِ قَالُواْ وَمَا ٱلرَّحۡمَٰنُ أَنَسۡجُدُ لِمَا تَأۡمُرُنَا وَزَادَهُمۡ نُفُورٗا۩ ٦٠

Wa idhā qīla lahumusjudū lir-rahmāni qālū wamar-rahmānu anasjudu limā ta'murunā wazādahum nufūrā

Na wanapo ambiwa: Msujudieni Arrahman! Wao husema: Ni nani Arrahman? Je! Tumsujudie unaye tuamrisha wewe tu? Na huwazidishia chuki. 60

تَبَارَكَ ٱلَّذِي جَعَلَ فِي ٱلسَّمَآءِ بُرُوجٗا وَجَعَلَ فِيهَا سِرَٰجٗا وَقَمَرٗا مُّنِيرٗا ٦١

Tabārakal-ladhī ja'ala fis-samā'i burūjan waja'ala fīhā sirājan waqamaram munīrā

Ametukuka aliye zijaalia nyota mbinguni, na akajaalia humo taa na mwezi unao ng'ara. 61

وَهُوَ ٱلَّذِي جَعَلَ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَ خِلۡفَةٗ لِّمَنۡ أَرَادَ أَن يَذَّكَّرَ أَوۡ أَرَادَ شُكُورٗا ٦٢

Wahuwal-ladhī ja'alal-layla wan-nahāra khilfatal liman arāda an yaddhakkara aw arāda shukūrā

Naye ndiye aliye fanya usiku na mchana kufuatana kwa nafuu ya anaye taka kukumbuka, au anaye taka kushukuru. 62

وَعِبَادُ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلَّذِينَ يَمۡشُونَ عَلَى ٱلۡأَرۡضِ هَوۡنٗا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ ٱلۡجَٰهِلُونَ قَالُواْ سَلَٰمٗا ٦٣

Wa'ibādur-rahmānil-ladhīna yamshūna 'alal-ardi hawnan wa idhā khātabahumul-jāhilūna qālū salāmā

Na waja wa Arrahman Mwingi wa Rehema ni wale wanao tembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemeza hujibu: Salama! 63

وَٱلَّذِينَ يَبِيتُونَ لِرَبِّهِمۡ سُجَّدٗا وَقِيَٰمٗا ٦٤

Walladhīna yabītūna lirabbihim sujjadan waqiyāmā

Na wale wanao kesha kwa ajili ya Mola wao Mlezi kwa kusujudu na kusimama. 64

وَٱلَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا ٱصۡرِفۡ عَنَّا عَذَابَ جَهَنَّمَۖ إِنَّ عَذَابَهَا كَانَ غَرَامًا ٦٥

Walladhīna yaqūlūna rabbanasrif 'annā 'adhāba jahannama inna 'adhābahā kāna gharāmā

Na wale wanao sema: Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu ya Jahannamu. Hakika adhabu yake ikimpata mtu haimwachi. 65

إِنَّهَا سَآءَتۡ مُسۡتَقَرّٗا وَمُقَامٗا ٦٦

Innahā sā'at mustaqarran wamuqāmā

Hakika hiyo ni kituo na makao mabaya. 66

وَٱلَّذِينَ إِذَآ أَنفَقُواْ لَمۡ يُسۡرِفُواْ وَلَمۡ يَقۡتُرُواْ وَكَانَ بَيۡنَ ذَٰلِكَ قَوَامٗا ٦٧

Walladhīna idhā anfaqū lam yusrifū walam yaqturū wakāna bayna dhālika qawāmā

Na wale ambao wanapo tumia hawatumii kwa fujo wala hawafanyi ubakhili, bali wanakuwa katikati baina ya hayo. 67

وَٱلَّذِينَ لَا يَدۡعُونَ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَ وَلَا يَقۡتُلُونَ ٱلنَّفۡسَ ٱلَّتِي حَرَّمَ ٱللَّهُ إِلَّا بِٱلۡحَقِّ وَلَا يَزۡنُونَۚ وَمَن يَفۡعَلۡ ذَٰلِكَ يَلۡقَ أَثَامٗا ٦٨

Walladhīna lā yad'ūna ma'allāhi ilāhan ākhara walā yaqtulūnan-nafsal-latī harramallāhu illā bil-haqqi walā yaznūna waman yaf'al dhālika yalqa athāmā

Na wale wasio mwomba mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaui nafsi aliyo iharimisha Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwa haki, wala hawazini - na atakaye fanya hayo atapata madhara, 68

يُضَٰعَفۡ لَهُ ٱلۡعَذَابُ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وَيَخۡلُدۡ فِيهِۦ مُهَانًا ٦٩

Yudā'af lahul-'adhābu yawmal-qiyāmati wayakhlud fīhī muhānā

Atazidishiwa adhabu Siku ya Kiyama, na atadumu humo kwa kufedheheka. 69

إِلَّا مَن تَابَ وَءَامَنَ وَعَمِلَ عَمَلٗا صَٰلِحٗا فَأُوْلَٰٓئِكَ يُبَدِّلُ ٱللَّهُ سَيِّـَٔاتِهِمۡ حَسَنَٰتٖۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمٗا ٧٠

Illā man tāba wa āmana wa'amila 'amalan sālihan fa ulā'ika yubaddilullāhu sayyi'ātihim hasanātin wakānallāhu ghafūrar rahīmā

Isipo kuwa atakaye tubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. 70

وَمَن تَابَ وَعَمِلَ صَٰلِحٗا فَإِنَّهُۥ يَتُوبُ إِلَى ٱللَّهِ مَتَابٗا ٧١

Waman tāba wa'amila sālihan fa innahū yatūbu ilallāhi matābā

Na aliye tubu na akafanya mema, basi hakika huyo ametubu kweli kweli kwa Mwenyezi Mungu. 71

وَٱلَّذِينَ لَا يَشۡهَدُونَ ٱلزُّورَ وَإِذَا مَرُّواْ بِٱللَّغۡوِ مَرُّواْ كِرَامٗا ٧٢

Walladhīna lā yashhadūnaz-zūra wa idhā marrū bil-laghwi marrū kirāmā

Na wale ambao hawatoi ushahidi wa uwongo, na pindi wapitapo penye upuuzi, hupita kwa hishima yao. 72

وَٱلَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُواْ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِمۡ لَمۡ يَخِرُّواْ عَلَيۡهَا صُمّٗا وَعُمۡيَانٗا ٧٣

Walladhīna idhā dhukkirū bi'āyāti rabbihim lam yakhirrū 'alayhā summan wa'umyānā

Na wale ambao wanapo kumbushwa Ishara za Mola wao Mlezi hawajifanyi viziwi nazo, na vipofu. 73

وَٱلَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا هَبۡ لَنَا مِنۡ أَزۡوَٰجِنَا وَذُرِّيَّٰتِنَا قُرَّةَ أَعۡيُنٖ وَٱجۡعَلۡنَا لِلۡمُتَّقِينَ إِمَامًا ٧٤

Walladhīna yaqūlūna rabbanā hab lanā min azwājinā wadhurriyyātinā qurrata a'yunin waj'alnā lil-muttaqīna imāmā

Na wale wanao sema: Mola wetu Mlezi! Tupe katika wake zetu na wenetu yaburudishayo macho, na utujaalie tuwe waongozi kwa wachamngu. 74

أُوْلَٰٓئِكَ يُجۡزَوۡنَ ٱلۡغُرۡفَةَ بِمَا صَبَرُواْ وَيُلَقَّوۡنَ فِيهَا تَحِيَّةٗ وَسَلَٰمًا ٧٥

Ulā'ika yujzawnal-ghurfata bimā sabarū wayulaqqawna fīhā tahiyyatan wasalāmā

Hao ndio watakao lipwa makao ya juu kwa kuwa walisubiri, na watakuta humo maamkio na salamu. 75

خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ حَسُنَتۡ مُسۡتَقَرّٗا وَمُقَامٗا ٧٦

Khālidīna fīhā hasunat mustaqarran wamuqāmā

Wadumu humo - kituo na makao mazuri kabisa. 76

قُلۡ مَا يَعۡبَؤُاْ بِكُمۡ رَبِّي لَوۡلَا دُعَآؤُكُمۡۖ فَقَدۡ كَذَّبۡتُمۡ فَسَوۡفَ يَكُونُ لِزَامَۢا ٧٧

Qul mā ya'ba'u bikum rabbī lawlā du'ā'ukum faqad kaddhabtum fasawfa yakūnu lizāmā

Sema: Mola wangu Mlezi asinge kujalini lau kuwa si kuomba kwenu. Lakini nyinyi mmemkadhibisha. Basi adhabu lazima iwe. 77

Surat Ash-Shu'ara

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

طسٓمٓ ١

Tā Sīn Mīm

T'aa Siin Miim. (T'.S.M.) . 1

تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡمُبِينِ ٢

Tilka āyātul-kitābil-mubīn

Hizi ni Aya za Kitabu kinacho bainisha. 2

لَعَلَّكَ بَٰخِعٞ نَّفۡسَكَ أَلَّا يَكُونُواْ مُؤۡمِنِينَ ٣

La'allaka bākhi'un nafsaka allā yakūnū mu'minīn

Huenda labda ukajikera nafsi yako kwa kuwa hawawi Waumini. 3

إِن نَّشَأۡ نُنَزِّلۡ عَلَيۡهِم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ ءَايَةٗ فَظَلَّتۡ أَعۡنَٰقُهُمۡ لَهَا خَٰضِعِينَ ٤

In nasha' nunazzil 'alayhim minas-samā'i āyatan fazallat a'nāquhum lahā khādi'īn

Tunge penda tungeli wateremshia kutoka mbinguni Ishara zikanyenyekea shingo zao. 4

وَمَا يَأۡتِيهِم مِّن ذِكۡرٖ مِّنَ ٱلرَّحۡمَٰنِ مُحۡدَثٍ إِلَّا كَانُواْ عَنۡهُ مُعۡرِضِينَ ٥

Wamā ya'tīhim min dhikrim minar-rahmāni muhdathin illā kānū 'anhu mu'ridīn

Wala hauwafikii ukumbusho mpya kutoka kwa Arrahman ila wao hujitenga nao. 5

فَقَدۡ كَذَّبُواْ فَسَيَأۡتِيهِمۡ أَنۢبَٰٓؤُاْ مَا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ ٦

Faqad kaddhabū fasaya'tīhim ambā'u mā kānū bihī yastahzi'ūn

Kwa yakini wamekanusha; kwa hivyo zitakuja wafikia khabari za yale waliyo kuwa wakiyafanyia mzaha. 6

أَوَلَمۡ يَرَوۡاْ إِلَى ٱلۡأَرۡضِ كَمۡ أَنۢبَتۡنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوۡجٖ كَرِيمٍ ٧

Awalam yaraw ilal-ardi kam ambatnā fīhā min kulli zawjin karīm

Je! Hawakuiona ardhi, mimea mingapi tumeiotesha humo, ya kila namna nzuri? 7

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ ٨

Inna fī dhālika la'āyatan wamā kāna aktharuhum mu'minīn

Hakika katika haya zipo Ishara. Lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini. 8

وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ ٩

Wa inna rabbaka lahuwal-'azīzur-rahīm

Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. 9

وَإِذۡ نَادَىٰ رَبُّكَ مُوسَىٰٓ أَنِ ٱئۡتِ ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّٰلِمِينَ ١٠

Wa idh nādā rabbuka mūsā ani'til-qawmaz-zālimīn

Na Mola wako Mlezi, alipo mwita Musa, akamwambia: Fika kwa watu madhaalimu, 10

قَوۡمَ فِرۡعَوۡنَۚ أَلَا يَتَّقُونَ ١١

Qawma fir'awna alā yattaqūn

Watu wa Firauni. Hawaogopi? 11

قَالَ رَبِّ إِنِّيٓ أَخَافُ أَن يُكَذِّبُونِ ١٢

Qāla rabbi innī akhāfu an yukaddhibūn

Akasema: Hakika mimi nachelea wasinikanushe. 12

وَيَضِيقُ صَدۡرِي وَلَا يَنطَلِقُ لِسَانِي فَأَرۡسِلۡ إِلَىٰ هَٰرُونَ ١٣

Wayadīqu sadrī walā yantaliqu lisānī fa arsil ilā hārūn

Na kifua changu kina dhiki, na ulimi wangu haukunjuki vyema. Basi mtumie ujumbe Harun. 13

وَلَهُمۡ عَلَيَّ ذَنۢبٞ فَأَخَافُ أَن يَقۡتُلُونِ ١٤

Walahum 'alayya dhambun fa akhāfu an yaqtulūn

Na wao wana kisasi juu yangu, kwa hivyo naogopa wasije kuniuwa. 14

قَالَ كَلَّاۖ فَٱذۡهَبَا بِـَٔايَٰتِنَآۖ إِنَّا مَعَكُم مُّسۡتَمِعُونَ ١٥

Qāla kallā fadhhabā bi'āyātinā innā ma'akum mustami'ūn

Akasema: Siyo hivyo kabisa! Nendeni na miujiza yetu. Hakika Sisi tu pamoja nanyi, tunasikiliza. 15

فَأۡتِيَا فِرۡعَوۡنَ فَقُولَآ إِنَّا رَسُولُ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ١٦

Fa tiyā fir'awna faqūlā innā rasūlu rabbil-'ālamīn

Basi mfikieni Firauni na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote. 16

أَنۡ أَرۡسِلۡ مَعَنَا بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ١٧

An arsil ma'anā banī isrā'īl

Waachilie Wana wa Israili wende nasi. 17

قَالَ أَلَمۡ نُرَبِّكَ فِينَا وَلِيدٗا وَلَبِثۡتَ فِينَا مِنۡ عُمُرِكَ سِنِينَ ١٨

Qāla alam nurabbika fīnā walīdan walabithta fīnā min 'umurika sinīn

(Firauni) akasema: Sisi hatukukulea wewe utotoni, na ukakaa kwetu katika umri wako miaka mingi? 18

وَفَعَلۡتَ فَعۡلَتَكَ ٱلَّتِي فَعَلۡتَ وَأَنتَ مِنَ ٱلۡكَٰفِرِينَ ١٩

Wafa'alta fa'latakal-latī fa'alta wa anta minal-kāfirīn

Na ukatenda kitendo chako ulicho tenda, nawe ukawa miongoni mwa wasio na shukrani? 19

قَالَ فَعَلۡتُهَآ إِذٗا وَأَنَا۠ مِنَ ٱلضَّآلِّينَ ٢٠

Qāla fa'altuhā idhan wa ana minad-dāllīn

(Musa) akasema: Nilitenda hayo hapo nilipo kuwa miongoni mwa wale walio potea. 20

فَفَرَرۡتُ مِنكُمۡ لَمَّا خِفۡتُكُمۡ فَوَهَبَ لِي رَبِّي حُكۡمٗا وَجَعَلَنِي مِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ ٢١

Fafarartu minkum lammā khiftukum fawahaba lī rabbī hukman waja'alanī minal-mursalīn

Basi nilikukimbieni nilipo kuogopeni, tena Mola wangu Mlezi, akanitunukia hukumu, na akanijaali niwe miongoni mwa Mitume. 21

وَتِلۡكَ نِعۡمَةٞ تَمُنُّهَا عَلَيَّ أَنۡ عَبَّدتَّ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ٢٢

Watilka ni'matun tamunnuhā 'alayya an 'abbatta banī isrā'īl

Na hiyo ndiyo neema ya kunisumbulia, na wewe umewatia utumwani Wana wa Israili? 22

قَالَ فِرۡعَوۡنُ وَمَا رَبُّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ٢٣

Qāla fir'awnu wamā rabbul-'ālamīn

Firauni akasema: Na nani huyo Mola Mlezi wa walimwengu wote? 23

قَالَ رَبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَآۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ ٢٤

Qāla rabbus-samāwāti wal-ardi wamā baynahumā in kuntum mūqinīn

Akasema: Ndiye Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na viliomo baina yao, ikiwa nyinyi ni wenye yakini. 24

قَالَ لِمَنۡ حَوۡلَهُۥٓ أَلَا تَسۡتَمِعُونَ ٢٥

Qāla liman hawlahū alā tastami'ūn

(Firauni) akawaambia walio mzunguka: Hamsikilizi? 25

قَالَ رَبُّكُمۡ وَرَبُّ ءَابَآئِكُمُ ٱلۡأَوَّلِينَ ٢٦

Qāla rabbukum warabbu ābā'ikumul-awwalīn

(Musa) akasema: Ndiye Mola wenu Mlezi, na Mola Mlezi wa baba zenu wa kwanza. 26

قَالَ إِنَّ رَسُولَكُمُ ٱلَّذِيٓ أُرۡسِلَ إِلَيۡكُمۡ لَمَجۡنُونٞ ٢٧

Qāla inna rasūlakumul-ladhī ursila ilaykum lamajnūn

(Firauni) akasema: Hakika huyu Mtume wenu aliye tumwa kwenu ni mwendawazimu. 27

قَالَ رَبُّ ٱلۡمَشۡرِقِ وَٱلۡمَغۡرِبِ وَمَا بَيۡنَهُمَآۖ إِن كُنتُمۡ تَعۡقِلُونَ ٢٨

Qāla rabbul-mashriqi wal-maghribi wamā baynahumā in kuntum ta'qilūn

. (Musa) akasema: Ndiye Mola Mlezi wa Mashariki na Magharibi na viliomo baina yao, ikiwa nyinyi mnatia akilini. 28

قَالَ لَئِنِ ٱتَّخَذۡتَ إِلَٰهًا غَيۡرِي لَأَجۡعَلَنَّكَ مِنَ ٱلۡمَسۡجُونِينَ ٢٩

Qāla la init-takhadhta ilāhan ghayrī la aj'alannaka minal-masjūnīn

(Firauni) akasema: Ukimfuata mungu mwengine asiye kuwa mimi, basi bila ya shaka nitakufunga gerezani. 29

قَالَ أَوَلَوۡ جِئۡتُكَ بِشَيۡءٖ مُّبِينٖ ٣٠

Qāla awalaw ji'tuka bishay'im mubīn

Akasema: Je! Ijapo kuwa nitakuletea kitu cha kubainisha wazi? 30

قَالَ فَأۡتِ بِهِۦٓ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ ٣١

Qāla fa ti bihī in kunta minas-sādiqīn

Akasema: Kilete basi, kama wewe ni katika wasemao kweli. 31

فَأَلۡقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ ثُعۡبَانٞ مُّبِينٞ ٣٢

Fa alqā 'asāhu fa idhā hiya thu'bānum mubīn

Basi akaitupa fimbo yake, mara ikawa nyoka wa kuonekana dhaahiri. 32

وَنَزَعَ يَدَهُۥ فَإِذَا هِيَ بَيۡضَآءُ لِلنَّٰظِرِينَ ٣٣

Wanaza'a yadahū fa idhā hiya baydā'u lin-nāzirīn

Na akautoa mkono wake, na mara ukawa mweupe kwa watazamao. 33

قَالَ لِلۡمَلَإِ حَوۡلَهُۥٓ إِنَّ هَٰذَا لَسَٰحِرٌ عَلِيمٞ ٣٤

Qāla lil-mala'i hawlahū inna hādhā lasāhirun 'alīm

(Firauni) akawaambia waheshimiwa walio mzunguka: Hakika huyu ni mchawi mtaalamu. 34

يُرِيدُ أَن يُخۡرِجَكُم مِّنۡ أَرۡضِكُم بِسِحۡرِهِۦ فَمَاذَا تَأۡمُرُونَ ٣٥

Yurīdu an yukhrijakum min ardikum bisihrihī famādhā ta'murūn

Anataka kukutoeni katika nchi yenu kwa uchawi wake. Basi mna shauri gani? 35

قَالُوٓاْ أَرۡجِهۡ وَأَخَاهُ وَٱبۡعَثۡ فِي ٱلۡمَدَآئِنِ حَٰشِرِينَ ٣٦

Qālū arjih wa akhāhu wab'ath fil-madā'ini hāshirīn

Wakasema: Mpe muda yeye na nduguye na uwatume mijini wapigao mbiu ya mgambo. 36

يَأۡتُوكَ بِكُلِّ سَحَّارٍ عَلِيمٖ ٣٧

Ya'tūka bikulli sahhārin 'alīm

Wakuletee kila mchawi bingwa mtaalamu. 37

فَجُمِعَ ٱلسَّحَرَةُ لِمِيقَٰتِ يَوۡمٖ مَّعۡلُومٖ ٣٨

Fajumi'as-saharatu limīqāti yawmim ma'lūm

Basi wakakusanywa wachawi wakati na siku maalumu. 38

وَقِيلَ لِلنَّاسِ هَلۡ أَنتُم مُّجۡتَمِعُونَ ٣٩

Waqīla lin-nāsi hal antum mujtami'ūn

Na watu wakaambiwa: Je! Mtakusanyika? 39

لَعَلَّنَا نَتَّبِعُ ٱلسَّحَرَةَ إِن كَانُواْ هُمُ ٱلۡغَٰلِبِينَ ٤٠

La'allanā nattabi'us-saharata in kānū humul-ghālibīn

Huenda tutawafuata wachawi wakiwa wao ndio watakao shinda. 40

فَلَمَّا جَآءَ ٱلسَّحَرَةُ قَالُواْ لِفِرۡعَوۡنَ أَئِنَّ لَنَا لَأَجۡرًا إِن كُنَّا نَحۡنُ ٱلۡغَٰلِبِينَ ٤١

Falammā jā'as-saharatu qālū lifir'awna a'inna lanā la ajran in kunnā nahnul-ghālibīn

Basi walipo kuja wachawi wakamwambia Firauni: Je! Tutapata ujira tukiwa sisi ndio tulio shinda? 41

قَالَ نَعَمۡ وَإِنَّكُمۡ إِذٗا لَّمِنَ ٱلۡمُقَرَّبِينَ ٤٢

Qāla na'am wa innakum idhal laminal-muqarrabīn

Naam! Na hakika mtakuwa katika watu wa mbele. 42

قَالَ لَهُم مُّوسَىٰٓ أَلۡقُواْ مَآ أَنتُم مُّلۡقُونَ ٤٣

Qāla lahum mūsā alqū mā antum mulqūn

Musa akwaambia: Tupeni mnavyo taka kutupa. 43

فَأَلۡقَوۡاْ حِبَالَهُمۡ وَعِصِيَّهُمۡ وَقَالُواْ بِعِزَّةِ فِرۡعَوۡنَ إِنَّا لَنَحۡنُ ٱلۡغَٰلِبُونَ ٤٤

Fa alqaw hibālahum wa'isiyyahum waqālū bi'izzati fir'awna innā lanahnul-ghālibūn

Basi wakatupa kamba zao na fimbo zao, na wakasema: Kwa nguvu za Firauni hakika sisi hapana shaka ni wenye kushinda. 44

فَأَلۡقَىٰ مُوسَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ تَلۡقَفُ مَا يَأۡفِكُونَ ٤٥

Fa alqā mūsā 'asāhu fa idhā hiya talqafu mā ya'fikūn

Musa tena akatupa fimbo yake, nayo mara ikavimeza walivyo vizua. 45

فَأُلۡقِيَ ٱلسَّحَرَةُ سَٰجِدِينَ ٤٦

Fa ulqiyas-saharatu sājidīn

Hapo wachawi walipinduka wakasujudu. 46

قَالُوٓاْ ءَامَنَّا بِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ٤٧

Qālū āmannā birabbil-'ālamīn

Wakasema: Tunamuamini Mola Mlezi wa walimwengu wote. 47

رَبِّ مُوسَىٰ وَهَٰرُونَ ٤٨

Rabbi mūsā wahārūn

Mola Mlezi wa Musa na Harun. 48

قَالَ ءَامَنتُمۡ لَهُۥ قَبۡلَ أَنۡ ءَاذَنَ لَكُمۡۖ إِنَّهُۥ لَكَبِيرُكُمُ ٱلَّذِي عَلَّمَكُمُ ٱلسِّحۡرَ فَلَسَوۡفَ تَعۡلَمُونَۚ لَأُقَطِّعَنَّ أَيۡدِيَكُمۡ وَأَرۡجُلَكُم مِّنۡ خِلَٰفٖ وَلَأُصَلِّبَنَّكُمۡ أَجۡمَعِينَ ٤٩

Qāla āmantum lahū qabla an ādhana lakum innahū lakabīrukumul-ladhī 'allamakumus-sihra falasawfa ta'lamūna la uqatti'anna aydiyakum wa arjulakum min khilāfin wala'usallibannakum ajma'īn

(Firauni) akasema: Je! Mmemuamini kabla sijakuruhusuni? Bila ya shaka yeye basi ndiye mkubwa wenu aliye kufunzeni uchawi. Basi mtakuja jua! Nitakata mikono yenu na miguu yenu kwa kutafautisha. Na nitakubandikeni misalabani nyote. 49

قَالُواْ لَا ضَيۡرَۖ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا مُنقَلِبُونَ ٥٠

Qālū lā dayra innā ilā rabbinā munqalibūn

Wakasema: Haidhuru, kwani sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi. 50

إِنَّا نَطۡمَعُ أَن يَغۡفِرَ لَنَا رَبُّنَا خَطَٰيَٰنَآ أَن كُنَّآ أَوَّلَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ٥١

Innā natma'u an yaghfira lanā rabbunā khatāyānā an kunnā awwalal-mu'minīn

Hakika sisi tunatumai Mola wetu Mlezi atatusamehe makosa yetu, kwa kuwa ndio wa kwanza wa kuamini. 51

۞ وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنۡ أَسۡرِ بِعِبَادِيٓ إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ ٥٢

Wa awhaynā ilā mūsā an asri bi'ibādī innakum muttaba'ūn

Na tulimuamrisha Musa kwa wahyi: Nenda na waja wangu wakati wa usiku. Kwa hakika mtafuatwa. 52

فَأَرۡسَلَ فِرۡعَوۡنُ فِي ٱلۡمَدَآئِنِ حَٰشِرِينَ ٥٣

Fa arsala fir'awnu fil-madā'ini hāshirīn

Basi Firauni akawatuma mijini wapiga mbiu za mgambo. 53

إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ لَشِرۡذِمَةٞ قَلِيلُونَ ٥٤

Inna hā'ulā'i lashirdhimatun qalīlūn

(Wakieneza): Hakika hawa ni kikundi kidogo. 54

وَإِنَّهُمۡ لَنَا لَغَآئِظُونَ ٥٥

Wa innahum lanā laghā'izūn

Nao wanatuudhi. 55

وَإِنَّا لَجَمِيعٌ حَٰذِرُونَ ٥٦

Wa innā lajamī'un hādhirūn

Na sisi ni wengi, wenye kuchukua hadhari. 56

فَأَخۡرَجۡنَٰهُم مِّن جَنَّٰتٖ وَعُيُونٖ ٥٧

Fa akhrajnāhum min jannātin wa'uyūn

Basi tukawatoa katika mabustani na chemchem, 57

وَكُنُوزٖ وَمَقَامٖ كَرِيمٖ ٥٨

Wakunūzin wamaqāmin karīm

Na makhazina, na vyeo vya hishima, 58

كَذَٰلِكَۖ وَأَوۡرَثۡنَٰهَا بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ٥٩

Kadhālika wa awrathnāhā banī isrā'īl

Kadhaalika; na tukawarithisha hayo Wana wa Israili. 59

فَأَتۡبَعُوهُم مُّشۡرِقِينَ ٦٠

Fa atba'ūhum mushriqīn

Basi wakawafuata lilipo chomoza jua. 60

فَلَمَّا تَرَٰٓءَا ٱلۡجَمۡعَانِ قَالَ أَصۡحَٰبُ مُوسَىٰٓ إِنَّا لَمُدۡرَكُونَ ٦١

Falammā tarā'al-jam'āni qāla ashābu mūsā innā lamudrakūn

Na yalipo onana majeshi mawili haya, watu wa Musa wakasema: Hakika sisi bila ya shaka tumepatikana! 61

قَالَ كَلَّآۖ إِنَّ مَعِيَ رَبِّي سَيَهۡدِينِ ٦٢

Qāla kallā inna ma'iya rabbī sayahdīn

(Musa) akasema: Hasha! Hakika yu pamoja nami Mola wangu Mlezi. Yeye ataniongoa! 62

فَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنِ ٱضۡرِب بِّعَصَاكَ ٱلۡبَحۡرَۖ فَٱنفَلَقَ فَكَانَ كُلُّ فِرۡقٖ كَٱلطَّوۡدِ ٱلۡعَظِيمِ ٦٣

Fa awhaynā ilā mūsā anidrib bi'asākal-bahra fanfalaqa fakāna kullu firqin kat-tawdil-'azīm

Tulimletea wahyi Musa tukamwambia: Piga bahari kwa fimbo yako. Basi ikatengana, na kila sehemu ikawa kama mlima mkubwa. 63

وَأَزۡلَفۡنَا ثَمَّ ٱلۡأٓخَرِينَ ٦٤

Wa azlafnā thammal-ākharīn

Na tukawajongeza hapo wale wengine. 64

وَأَنجَيۡنَا مُوسَىٰ وَمَن مَّعَهُۥٓ أَجۡمَعِينَ ٦٥

Wa anjaynā mūsā wamam ma'ahū ajma'īn

Tukawaokoa Musa na walio kuwa pamoja naye wote. 65

ثُمَّ أَغۡرَقۡنَا ٱلۡأٓخَرِينَ ٦٦

Thumma aghraqnal-ākharīn

Kisha tukawazamisha hao wengine. 66

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ ٦٧

Inna fī dhālika la'āyatan wamā kāna aktharuhum mu'minīn

Hakika bila ya shaka katika hayo ipo Ishara; lakini wengi wao si katika wenye kuamini. 67

وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ ٦٨

Wa inna rabbaka lahuwal-'azīzur-rahīm

Na kwa hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. 68

وَٱتۡلُ عَلَيۡهِمۡ نَبَأَ إِبۡرَٰهِيمَ ٦٩

Watlu 'alayhim naba'a ibrāhīm

Na wasomee khabari za Ibrahim. 69

إِذۡ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوۡمِهِۦ مَا تَعۡبُدُونَ ٧٠

Idh qāla li abīhi waqawmihī mā ta'budūn

Alipo mwambia baba yake na kaumu yake: Mnaabudu nini? 70

قَالُواْ نَعۡبُدُ أَصۡنَامٗا فَنَظَلُّ لَهَا عَٰكِفِينَ ٧١

Qālū na'budu asnāman fanazallu lahā 'ākifīn

Wakasema: Tunaabudu masanamu, daima tunayanyenyekea. 71

قَالَ هَلۡ يَسۡمَعُونَكُمۡ إِذۡ تَدۡعُونَ ٧٢

Qāla hal yasma'ūnakum idh tad'ūn

Akasema: Je! Yanakusikieni mnapo yaita? 72

أَوۡ يَنفَعُونَكُمۡ أَوۡ يَضُرُّونَ ٧٣

Aw yanfa'ūnakum aw yadurrūn

Au yanakufaeni, au yanakudhuruni? 73

قَالُواْ بَلۡ وَجَدۡنَآ ءَابَآءَنَا كَذَٰلِكَ يَفۡعَلُونَ ٧٤

Qālū bal wajadnā ābā'anā kadhālika yaf'alūn

Wakasema: Bali tumewakuta baba zetu wakifanya hivyo hivyo. 74

قَالَ أَفَرَءَيۡتُم مَّا كُنتُمۡ تَعۡبُدُونَ ٧٥

Qāla afara'aytum mā kuntum ta'budūn

Je! Mmewaona hawa mnao waabudu- 75

أَنتُمۡ وَءَابَآؤُكُمُ ٱلۡأَقۡدَمُونَ ٧٦

Antum wa ābā'ukumul-aqdamūn

Nyinyi na baba zenu wa zamani? 76

فَإِنَّهُمۡ عَدُوّٞ لِّيٓ إِلَّا رَبَّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ٧٧

Fa innahum 'aduwwul lī illā rabbal-'ālamīn

Kwani hakika hao ni adui zangu, isipo kuwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. 77

ٱلَّذِي خَلَقَنِي فَهُوَ يَهۡدِينِ ٧٨

Alladhī khalaqanī fahuwa yahdīn

Ambaye ndiye aliye niumba, na Yeye ndiye ananiongoa, 78

وَٱلَّذِي هُوَ يُطۡعِمُنِي وَيَسۡقِينِ ٧٩

Walladhī huwa yut'imunī wayasqīn

Na ambaye ndiye ananilisha na kuninywesha. 79

وَإِذَا مَرِضۡتُ فَهُوَ يَشۡفِينِ ٨٠

Wa idhā maridtu fahuwa yashfīn

Na ninapo ugua ni Yeye ndiye anaye niponesha. 80

وَٱلَّذِي يُمِيتُنِي ثُمَّ يُحۡيِينِ ٨١

Walladhī yumītunī thumma yuhyīn

Na ambaye atanifisha, na kisha atanihuisha. 81

وَٱلَّذِيٓ أَطۡمَعُ أَن يَغۡفِرَ لِي خَطِيٓـَٔتِي يَوۡمَ ٱلدِّينِ ٨٢

Walladhī atma'u an yaghfira lī khatī'atī yawmad-dīn

Na ambaye ndiye ninaye mtumai kunisamehe makosa yangu Siku ya Malipo. 82

رَبِّ هَبۡ لِي حُكۡمٗا وَأَلۡحِقۡنِي بِٱلصَّٰلِحِينَ ٨٣

Rabbi hab lī hukman wa alhiqnī bis-sālihīn

Mola wangu Mlezi! Nitunukie hukumu na uniunganishe na watendao mema. 83

وَٱجۡعَل لِّي لِسَانَ صِدۡقٖ فِي ٱلۡأٓخِرِينَ ٨٤

Waj'al lī lisāna sidqin fil-ākhirīn

Na unijaalie nitajwe kwa wema na watu watakao kuja baadaye. 84

وَٱجۡعَلۡنِي مِن وَرَثَةِ جَنَّةِ ٱلنَّعِيمِ ٨٥

Waj'alnī min warathati jannatin-na'īm

Na unijaalie katika warithi wa Bustani za neema. 85

وَٱغۡفِرۡ لِأَبِيٓ إِنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلضَّآلِّينَ ٨٦

Waghfir li abī innahū kāna minad-dāllīn

Na umsamehe baba yangu, kwani hakika alikuwa miongoni mwa wapotovu. 86

وَلَا تُخۡزِنِي يَوۡمَ يُبۡعَثُونَ ٨٧

Walā tukhzinī yawma yub'athūn

Wala usinihizi Siku watapo fufuliwa. 87

يَوۡمَ لَا يَنفَعُ مَالٞ وَلَا بَنُونَ ٨٨

Yawma lā yanfa'u mālun walā banūn

Siku ambayo kwamba mali hayato faa kitu wala wana. 88

إِلَّا مَنۡ أَتَى ٱللَّهَ بِقَلۡبٖ سَلِيمٖ ٨٩

Illā man atallāha biqalbin salīm

Isipo kuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi. 89

وَأُزۡلِفَتِ ٱلۡجَنَّةُ لِلۡمُتَّقِينَ ٩٠

Wa uzlifatil-jannatu lil-muttaqīn

Na Pepo itasogezwa kwa wachamngu. 90

وَبُرِّزَتِ ٱلۡجَحِيمُ لِلۡغَاوِينَ ٩١

Waburrizatil-jahīmu lil-ghāwīn

Na Jahannamu itadhihirishwa kwa wapotovu. 91

وَقِيلَ لَهُمۡ أَيۡنَ مَا كُنتُمۡ تَعۡبُدُونَ ٩٢

Waqīla lahum ayna mā kuntum ta'budūn

Na wataambiwa: Wako wapi mlio kuwa mkiwaabudu 92

مِن دُونِ ٱللَّهِ هَلۡ يَنصُرُونَكُمۡ أَوۡ يَنتَصِرُونَ ٩٣

Min dūnillāhi hal yansurūnakum aw yantasirūn

Badala ya Mwenyezi Mungu? Je! Wanakusaidieni, au wanajisaidia wenyewe? 93

فَكُبۡكِبُواْ فِيهَا هُمۡ وَٱلۡغَاوُۥنَ ٩٤

Fakubkibū fīhā hum wal-ghāwūn

Basi watavurumizwa humo wao na hao wakosefu, 94

وَجُنُودُ إِبۡلِيسَ أَجۡمَعُونَ ٩٥

Wajunūdu iblīsa ajma'ūn

Na majeshi ya Ibilisi yote. 95

قَالُواْ وَهُمۡ فِيهَا يَخۡتَصِمُونَ ٩٦

Qālū wahum fīhā yakhtasimūn

Watasema, na hali ya kuwa wanazozana humo: 96

تَٱللَّهِ إِن كُنَّا لَفِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٍ ٩٧

Tallāhi in kunnā lafī dalālim mubīn

Wallahi! Kwa yakini tulikuwa katika upotovu ulio dhaahiri, 97

إِذۡ نُسَوِّيكُم بِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ٩٨

Idh nusawwīkum birabbil-'ālamīn

Tulipo kufanyeni ni sawa na Mola Mlezi wa walimwengu wote. 98

وَمَآ أَضَلَّنَآ إِلَّا ٱلۡمُجۡرِمُونَ ٩٩

Wamā adallanā illal-mujrimūn

Tulipo kufanyeni ni sawa na Mola Mlezi wa walimwengu wote. 99

فَمَا لَنَا مِن شَٰفِعِينَ ١٠٠

Famā lanā min shāfi'īn

Basi hatuna waombezi. 100

وَلَا صَدِيقٍ حَمِيمٖ ١٠١

Walā sadīqin hamīm

Wala rafiki wa dhati. 101

فَلَوۡ أَنَّ لَنَا كَرَّةٗ فَنَكُونَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ١٠٢

Falaw anna lanā karratan fanakūna minal-mu'minīn

Laiti tungeli pata kurejea tena tungeli kuwa katika Waumini. 102

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ ١٠٣

Inna fī dhālika la'āyatan wamā kāna aktharuhum mu'minīn

Hakika katika haya ipo Ishara, lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini. 103

وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ ١٠٤

Wa inna rabbaka lahuwal-'azīzur-rahīm

Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. 104

كَذَّبَتۡ قَوۡمُ نُوحٍ ٱلۡمُرۡسَلِينَ ١٠٥

Kaddhabat qawmu nūhinil-mursalīn

Kaumu ya Nuhu waliwakadhibisha Mitume. 105

إِذۡ قَالَ لَهُمۡ أَخُوهُمۡ نُوحٌ أَلَا تَتَّقُونَ ١٠٦

Idh qāla lahum akhūhum nūhun alā tattaqūn

Alipo waambia ndugu yao, Nuhu: Je! Hamchimngu?. 106

إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٞ ١٠٧

Innī lakum rasūlun amīn

Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu. 107

فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ ١٠٨

Fattaqullāha wa atī'ūn

Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. 108

وَمَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ١٠٩

Wamā as'alukum 'alayhi min ajrin in ajriya illā 'alā rabbil-'ālamīn

Na sikutakini juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. 109

فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ ١١٠

Fattaqullāha wa atī'ūn

Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. 110

۞ قَالُوٓاْ أَنُؤۡمِنُ لَكَ وَٱتَّبَعَكَ ٱلۡأَرۡذَلُونَ ١١١

Qālū anu'minu laka wattaba'akal-ardhalūn

Wakasema: Je! Tukuamini wewe, hali wanao kufuata ni watu wa chini?. 111

قَالَ وَمَا عِلۡمِي بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ ١١٢

Qāla wamā 'ilmī bimā kānū ya'malūn

Akasema: Nayajuaje waliyo kuwa wakiyafanya?. 112

إِنۡ حِسَابُهُمۡ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّيۖ لَوۡ تَشۡعُرُونَ ١١٣

In hisābuhum illā 'alā rabbī law tash'urūn

Hisabu yao haiko ila kwa Mola wao Mlezi, laiti mngeli tambua!. 113

وَمَآ أَنَا۠ بِطَارِدِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ١١٤

Wamā ana bitāridil-mu'minīn

Wala mimi si wa kuwafukuza Waumini. 114

إِنۡ أَنَا۠ إِلَّا نَذِيرٞ مُّبِينٞ ١١٥

In ana illā nadhīrum mubīn

Mimi si cho chote ila ni Mwonyaji wa dhaahiri shaahiri. 115

قَالُواْ لَئِن لَّمۡ تَنتَهِ يَٰنُوحُ لَتَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمَرۡجُومِينَ ١١٦

Qālū la il lam tantahi yānūhu latakūnanna minal-marjūmīn

Wakasema: Ikiwa huachi, ewe Nuhu, bila ya shaka utapigwa mawe. 116

قَالَ رَبِّ إِنَّ قَوۡمِي كَذَّبُونِ ١١٧

Qāla rabbi inna qawmī kaddhabūn

Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikanusha. 117

فَٱفۡتَحۡ بَيۡنِي وَبَيۡنَهُمۡ فَتۡحٗا وَنَجِّنِي وَمَن مَّعِيَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ١١٨

Faftah baynī wabaynahum fathan wanajjinī wamam ma'iya minal-mu'minīn

Basi hukumu baina yangu na wao kwa hukumu yako, na uniokoe mimi na walio pamoja nami, Waumini. 118

فَأَنجَيۡنَٰهُ وَمَن مَّعَهُۥ فِي ٱلۡفُلۡكِ ٱلۡمَشۡحُونِ ١١٩

Fa anjaynāhu wamam ma'ahū fil-fulkil-mashhūn

Kwa hivyo tukamwokoa yeye na walio kuwa pamoja naye katika marikebu iliyo sheheni. 119

ثُمَّ أَغۡرَقۡنَا بَعۡدُ ٱلۡبَاقِينَ ١٢٠

Thumma aghraqnā ba'dul-bāqīn

Kisha tukawazamisha baadaye walio bakia. 120

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ ١٢١

Inna fī dhālika la'āyatan wamā kāna aktharuhum mu'minīn

Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. 121

وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ ١٢٢

Wa inna rabbaka lahuwal-'azīzur-rahīm

Kina A'd waliwakanusha Mitume. 122

كَذَّبَتۡ عَادٌ ٱلۡمُرۡسَلِينَ ١٢٣

Kaddhabat 'ādunil-mursalīn

Kina A'd waliwakanusha Mitume. 123

إِذۡ قَالَ لَهُمۡ أَخُوهُمۡ هُودٌ أَلَا تَتَّقُونَ ١٢٤

Idh qāla lahum akhūhum hūdun alā tattaqūn

Alipo waambia ndugu yao, Hud: Je! Hamchimngu? 124

إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٞ ١٢٥

Innī lakum rasūlun amīn

Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. 125

فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ ١٢٦

Fattaqullāha wa atī'ūn

Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini. 126

وَمَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ١٢٧

Wamā as'alukum 'alayhi min ajrin in ajriya illā 'alā rabbil-'ālamīn

Wala sikutakeni juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. 127

أَتَبۡنُونَ بِكُلِّ رِيعٍ ءَايَةٗ تَعۡبَثُونَ ١٢٨

Atabnūna bikulli rī'in āyatan ta'bathūn

Je! Mnajenga juu ya kila mnyanyuko kumbusho la kufanyia upuuzi? 128

وَتَتَّخِذُونَ مَصَانِعَ لَعَلَّكُمۡ تَخۡلُدُونَ ١٢٩

Watattakhidhūna masāni'a la'allakum takhludūn

Na mnajenga majengo ya fakhari kama kwamba mtaishi milele! 129

وَإِذَا بَطَشۡتُم بَطَشۡتُمۡ جَبَّارِينَ ١٣٠

Wa idhā batashtum batashtum jabbārīn

Na mnapo tumia nguvu mnatumia nguvu kwa ujabari. 130

فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ ١٣١

Fattaqullāha wa atī'ūn

Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini. 131

وَٱتَّقُواْ ٱلَّذِيٓ أَمَدَّكُم بِمَا تَعۡلَمُونَ ١٣٢

Wattaqul-ladhī amaddakum bimā ta'lamūn

Na mcheni aliye kupeni haya mnayo yajua. 132

أَمَدَّكُم بِأَنۡعَٰمٖ وَبَنِينَ ١٣٣

Amaddakum bi an'āmin wabanīn

Amekupeni wanyama wa kufuga na wana. 133

وَجَنَّٰتٖ وَعُيُونٍ ١٣٤

Wajannātin wa'uyūn

Na mabustani na chemchem. 134

إِنِّيٓ أَخَافُ عَلَيۡكُمۡ عَذَابَ يَوۡمٍ عَظِيمٖ ١٣٥

Innī akhāfu 'alaykum 'adhāba yawmin 'azīm

Hakika mimi ninakukhofieni adhabu ya Siku Kubwa. 135

قَالُواْ سَوَآءٌ عَلَيۡنَآ أَوَعَظۡتَ أَمۡ لَمۡ تَكُن مِّنَ ٱلۡوَٰعِظِينَ ١٣٦

Qālū sawā'un 'alaynā awa'azta am lam takum minal-wā'izīn

Wakasema: Ni mamoja kwetu, ukitupa mawaidha au hukuwa miongoni mwa watoao mawaidha. 136

إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا خُلُقُ ٱلۡأَوَّلِينَ ١٣٧

In hādhā illā khuluqul-awwalīn

Haya si chochote ila ni mtindo wa watu wa tokea zamani. 137

وَمَا نَحۡنُ بِمُعَذَّبِينَ ١٣٨

Wamā nahnu bimu'addhabīn

Wala sisi hatutaadhibiwa. 138

فَكَذَّبُوهُ فَأَهۡلَكۡنَٰهُمۡۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ ١٣٩

Fakaddhabūhu fa ahlaknāhum inna fī dhālika la'āyatan wamā kāna aktharuhum mu'minīn

Wakamkanusha; nasi tukawaangamiza. Hakika bila ya shaka katika haya ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini. 139

وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ ١٤٠

Wa inna rabbaka lahuwal-'azīzur-rahīm

Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. 140

كَذَّبَتۡ ثَمُودُ ٱلۡمُرۡسَلِينَ ١٤١

Kaddhabat thamūdul-mursalīn

Kina Thamud waliwakanusha Mitume. 141

إِذۡ قَالَ لَهُمۡ أَخُوهُمۡ صَٰلِحٌ أَلَا تَتَّقُونَ ١٤٢

Idh qāla lahum akhūhum sālihun alā tattaqūn

Alipo waambia ndugu yao Swaleh: Je! Hamumchimngu? 142

إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٞ ١٤٣

Innī lakum rasūlun amīn

Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu. 143

فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ ١٤٤

Fattaqullāha wa atī'ūn

Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini. 144

وَمَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ١٤٥

Wamā as'alukum 'alayhi min ajrin in ajriya illā 'alā rabbil-'ālamīn

Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. 145

أَتُتۡرَكُونَ فِي مَا هَٰهُنَآ ءَامِنِينَ ١٤٦

Atutrakūna fī mā hāhunā āminīn

Je! Mtaachwa salama usalimina katika haya yaliyopo hapa? 146

فِي جَنَّٰتٖ وَعُيُونٖ ١٤٧

Fī jannātin wa'uyūn

Katika mabustani, na chemchem? 147

وَزُرُوعٖ وَنَخۡلٖ طَلۡعُهَا هَضِيمٞ ١٤٨

Wazurū'in wanakhlin tal'uhā hadīm

Na konde na mitende yenye makole yaliyo wiva. 148

وَتَنۡحِتُونَ مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتٗا فَٰرِهِينَ ١٤٩

Watanhitūna minal-jibāli buyūtan fārihīn

Na mnachonga milimani majumba kwa ustadi. 149

فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ ١٥٠

Fattaqullāha wa atī'ūn

Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. 150

وَلَا تُطِيعُوٓاْ أَمۡرَ ٱلۡمُسۡرِفِينَ ١٥١

Walā tutī'ū amral-musrifīn

Wala msit'ii amri za walio pindukia mipaka,. 151

ٱلَّذِينَ يُفۡسِدُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا يُصۡلِحُونَ ١٥٢

Alladhīna yufsidūna fil-ardi walā yuslihūn

Ambao wanafanya ufisadi katika nchi, wala hawatengenezi. 152

قَالُوٓاْ إِنَّمَآ أَنتَ مِنَ ٱلۡمُسَحَّرِينَ ١٥٣

Qālū innamā anta minal-musahharīn

Wakasema: Hakika wewe ni miongoni mwa walio rogwa. 153

مَآ أَنتَ إِلَّا بَشَرٞ مِّثۡلُنَا فَأۡتِ بِـَٔايَةٍ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ ١٥٤

Mā anta illā basharum mithlunā fa ti bi'āyatin in kunta minas-sādiqīn

Wewe si chochote ila ni mtu kama sisi. Basi lete Ishara ukiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli. 154

قَالَ هَٰذِهِۦ نَاقَةٞ لَّهَا شِرۡبٞ وَلَكُمۡ شِرۡبُ يَوۡمٖ مَّعۡلُومٖ ١٥٥

Qāla hādhihī nāqatul lahā shirbun walakum shirbu yawmim ma'lūm

Akasema: Huyu ngamia jike; awe na zamu yake ya kunywa, na nyinyi muwe na zamu yenu ya kunywa katika siku maalumu. 155

وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوٓءٖ فَيَأۡخُذَكُمۡ عَذَابُ يَوۡمٍ عَظِيمٖ ١٥٦

Walā tamassūhā bisū'in faya'khudhakum 'adhābu yawmin 'azīm

Wala ms!imguse kwa uwovu, isije ikakushikeni adhabu ya Siku Kubwa. 156

فَعَقَرُوهَا فَأَصۡبَحُواْ نَٰدِمِينَ ١٥٧

Fa'aqarūhā fa asbahū nādimīn

Lakini wakamuuwa, na wakawa wenye kujuta. 157

فَأَخَذَهُمُ ٱلۡعَذَابُۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ ١٥٨

Fa akhadhahumul-'adhābu inna fī dhālika la'āyatan wamā kāna aktharuhum mu'minīn

Basi ikawapata adhabu. Hakika katika hayo ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini. 158

وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ ١٥٩

Wa inna rabbaka lahuwal-'azīzur-rahīm

Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. 159

كَذَّبَتۡ قَوۡمُ لُوطٍ ٱلۡمُرۡسَلِينَ ١٦٠

Kaddhabat qawmu lūtinil-mursalīn

Watu wa Luut'i waliwakanusha Mitume. 160

إِذۡ قَالَ لَهُمۡ أَخُوهُمۡ لُوطٌ أَلَا تَتَّقُونَ ١٦١

Idh qāla lahum akhūhum lūtun alā tattaqūn

Alipo waambia ndugu yao, Luut'i: Je! Hamumchimngu?. 161

إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٞ ١٦٢

Innī lakum rasūlun amīn

Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu kwenu. 162

فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ ١٦٣

Fattaqullāha wa atī'ūn

Basi mcheni Mwenyezi Mungu na nit'iini mimi. 163

وَمَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ١٦٤

Wamā as'alukum 'alayhi min ajrin in ajriya illā 'alā rabbil-'ālamīn

Wala mimi sikutakini ujira juu yake; ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. 164

أَتَأۡتُونَ ٱلذُّكۡرَانَ مِنَ ٱلۡعَٰلَمِينَ ١٦٥

Ata'tūnadh-dhukrāna minal-'ālamīn

Je! Katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume?. 165

وَتَذَرُونَ مَا خَلَقَ لَكُمۡ رَبُّكُم مِّنۡ أَزۡوَٰجِكُمۚ بَلۡ أَنتُمۡ قَوۡمٌ عَادُونَ ١٦٦

Watadharūna mā khalaqa lakum rabbukum min azwājikum bal antum qawmun 'ādūn

Na mnaacha alicho kuumbieni Mola wenu Mlezi katika wake zenu? Ama kweli nyinyi ni watu mnao ruka mipaka!. 166

قَالُواْ لَئِن لَّمۡ تَنتَهِ يَٰلُوطُ لَتَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُخۡرَجِينَ ١٦٧

Qālū la il lam tantahi yālūtu latakūnanna minal-mukhrajīn

Wakasema: Ewe Luut'i! Usipo acha, hapana shaka utakuwa miongoni mwa wanao tolewa mji!. 167

قَالَ إِنِّي لِعَمَلِكُم مِّنَ ٱلۡقَالِينَ ١٦٨

Qāla innī li'amalikum minal-qālīn

Akasema: Hakika mimi ni katika wanao kichukia hichi kitendo chenu. 168

رَبِّ نَجِّنِي وَأَهۡلِي مِمَّا يَعۡمَلُونَ ١٦٩

Rabbi najjinī wa ahlī mimmā ya'malūn

Mola wangu Mlezi! Niokoe mimi na ahali zangu na haya wayatendayo. 169

فَنَجَّيۡنَٰهُ وَأَهۡلَهُۥٓ أَجۡمَعِينَ ١٧٠

Fanajjaynāhu wa ahlahū ajma'īn

Basi tukamwokoa yeye na ahali zake wote,. 170

إِلَّا عَجُوزٗا فِي ٱلۡغَٰبِرِينَ ١٧١

Illā 'ajūzan fil-ghābirīn

Isipo kuwa kikongwe katika walio kaa nyuma. 171

ثُمَّ دَمَّرۡنَا ٱلۡأٓخَرِينَ ١٧٢

Thumma dammarnal-ākharīn

Kisha tukawaangamiza wale wengine. 172

وَأَمۡطَرۡنَا عَلَيۡهِم مَّطَرٗاۖ فَسَآءَ مَطَرُ ٱلۡمُنذَرِينَ ١٧٣

Wa amtarnā 'alayhim mataran fasā'a matarul-mundharīn

Na tukawanyeshea mvua, basi ni ovu mno mvua ya waliyo onywa. 173

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ ١٧٤

Inna fī dhālika la'āyatan wamā kāna aktharuhum mu'minīn

Hakika katika hayo ipo Ishara. Na hawakuwa wengi wao wenye kuamini. 174

وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ ١٧٥

Wa inna rabbaka lahuwal-'azīzur-rahīm

Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. 175

كَذَّبَ أَصۡحَٰبُ لۡـَٔيۡكَةِ ٱلۡمُرۡسَلِينَ ١٧٦

Kaddhaba ashābu l'aykatil-mursalīn

Watu wa Machakani waliwakanusha Mitume. 176

إِذۡ قَالَ لَهُمۡ شُعَيۡبٌ أَلَا تَتَّقُونَ ١٧٧

Idh qāla lahum shu'aybun alā tattaqūn

Shuaibu alipo waambia: Je! Hamfanyi mkamchamngu?. 177

إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٞ ١٧٨

Innī lakum rasūlun amīn

Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu. 178

فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ ١٧٩

Fattaqullāha wa atī'ūn

Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. 179

وَمَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ١٨٠

Wamā as'alukum 'alayhi min ajrin in ajriya illā 'alā rabbil-'ālamīn

Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. 180

۞ أَوۡفُواْ ٱلۡكَيۡلَ وَلَا تَكُونُواْ مِنَ ٱلۡمُخۡسِرِينَ ١٨١

Awful-kayla walā takūnū minal-mukhsirīn

Timizeni kipimo sawa sawa, wala msiwe katika wanao punja. 181

وَزِنُواْ بِٱلۡقِسۡطَاسِ ٱلۡمُسۡتَقِيمِ ١٨٢

Wazinū bil-qistāsil-mustaqīm

Na pimeni kwa haki iliyo nyooka;. 182

وَلَا تَبۡخَسُواْ ٱلنَّاسَ أَشۡيَآءَهُمۡ وَلَا تَعۡثَوۡاْ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُفۡسِدِينَ ١٨٣

Walā tabkhasun-nāsa ashyā'ahum walā ta'thaw fil-ardi mufsidīn

Wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye jeuri kwa ufisadi. 183

وَٱتَّقُواْ ٱلَّذِي خَلَقَكُمۡ وَٱلۡجِبِلَّةَ ٱلۡأَوَّلِينَ ١٨٤

Wattaqul-ladhī khalaqakum wal-jibillatal-awwalīn

Na mcheni aliye kuumbeni nyinyi na vizazi vilivyo tangulia. 184

قَالُوٓاْ إِنَّمَآ أَنتَ مِنَ ٱلۡمُسَحَّرِينَ ١٨٥

Qālū innamā anta minal-musahharīn

Wakasema: Hakika wewe ni katika walio rogwa. 185

وَمَآ أَنتَ إِلَّا بَشَرٞ مِّثۡلُنَا وَإِن نَّظُنُّكَ لَمِنَ ٱلۡكَٰذِبِينَ ١٨٦

Wamā anta illā basharum mithlunā wa in nazunnuka laminal-kādhibīn

Na wewe si chochote ila ni mtu tu kama sisi, na kwa yakini tunakuona wewe ni katika waongo. 186

فَأَسۡقِطۡ عَلَيۡنَا كِسَفٗا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ ١٨٧

Fa asqit 'alaynā kisafam minas-samā'i in kunta minas-sādiqīn

Hebu tuangushie vipande kutoka mbinguni ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli. 187

قَالَ رَبِّيٓ أَعۡلَمُ بِمَا تَعۡمَلُونَ ١٨٨

Qāla rabbī a'lamu bimā ta'malūn

Akasema: Mola wangu Mlezi anajua zaidi mnayo yatenda. 188

فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَهُمۡ عَذَابُ يَوۡمِ ٱلظُّلَّةِۚ إِنَّهُۥ كَانَ عَذَابَ يَوۡمٍ عَظِيمٍ ١٨٩

Fakaddhabūhu fa akhadhahum 'adhābu yawmiz-zullati innahū kāna 'adhāba yawmin 'azīm

Basi walimkanusha, na ikawashika adhabu ya siku ya kivuli. Hakika hiyo ilikuwa adhabu ya siku kubwa. 189

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ ١٩٠

Inna fī dhālika la'āyatan wamā kāna aktharuhum mu'minīn

Hakika katika hayo ipo Ishara, lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini. 190

وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ ١٩١

Wa inna rabbaka lahuwal-'azīzur-rahīm

Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. 191

وَإِنَّهُۥ لَتَنزِيلُ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ١٩٢

Wa innahū latanzīlu rabbil-'ālamīn

Na bila ya shaka hii ni Uteremsho wa Mola Mlezi wa walimwengu wote. 192

نَزَلَ بِهِ ٱلرُّوحُ ٱلۡأَمِينُ ١٩٣

Nazala bihir-rūhul-amīn

Ameuteremsha Roho muaminifu,. 193

عَلَىٰ قَلۡبِكَ لِتَكُونَ مِنَ ٱلۡمُنذِرِينَ ١٩٤

'Alā qalbika litakūna minal-mundhirīn

Juu ya moyo wako, ili uwe katika Waonyaji,. 194

بِلِسَانٍ عَرَبِيّٖ مُّبِينٖ ١٩٥

Bilisānin 'arabiyyim mubīn

Kwa ulimi wa Kiarabu ulio wazi. 195

وَإِنَّهُۥ لَفِي زُبُرِ ٱلۡأَوَّلِينَ ١٩٦

Wa innahū lafī zuburil-awwalīn

Na hakika bila ya shaka haya yamo katika Vitabu vya kale. 196

أَوَلَمۡ يَكُن لَّهُمۡ ءَايَةً أَن يَعۡلَمَهُۥ عُلَمَٰٓؤُاْ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ١٩٧

Awalam yakul lahum āyatan an ya'lamahū 'ulamā'u banī isrā'īl

Je! Haikuwa kwao ni Ishara kwamba wanayajua haya wanazuoni wa Wana wa Israili?. 197

وَلَوۡ نَزَّلۡنَٰهُ عَلَىٰ بَعۡضِ ٱلۡأَعۡجَمِينَ ١٩٨

Walaw nazzalnāhu 'alā ba'dil-a'jamīn

Na lau kuwa tungeli iteremsha juu ya mmoja wa wasio kuwa Waarabu,. 198

فَقَرَأَهُۥ عَلَيۡهِم مَّا كَانُواْ بِهِۦ مُؤۡمِنِينَ ١٩٩

Faqara'ahū 'alayhim mā kānū bihī mu'minīn

Na akawasomea, wasingeli kuwa wenye kuamini. 199

كَذَٰلِكَ سَلَكۡنَٰهُ فِي قُلُوبِ ٱلۡمُجۡرِمِينَ ٢٠٠

Kadhālika salaknāhu fī qulūbil-mujrimīn

Namna hivi tunaingiza katika nyoyo za wakosefu. 200

لَا يُؤۡمِنُونَ بِهِۦ حَتَّىٰ يَرَوُاْ ٱلۡعَذَابَ ٱلۡأَلِيمَ ٢٠١

Lā yu'minūna bihī hattā yarawul-'adhābal-alīm

Hawataiamini mpaka waione adhabu chungu. 201

فَيَأۡتِيَهُم بَغۡتَةٗ وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ ٢٠٢

Faya'tiyahum baghtatan wahum lā yash'urūn

Basi itawafikia kwa ghafla, na hali hawana khabari. 202

فَيَقُولُواْ هَلۡ نَحۡنُ مُنظَرُونَ ٢٠٣

Fayaqūlū hal nahnu munzarūn

Na watasema: Je, tutapewa muhula?. 203

أَفَبِعَذَابِنَا يَسۡتَعۡجِلُونَ ٢٠٤

Afabi'adhābinā yasta'jilūn

Basi, je, wanaihimiza adhabu yetu?. 204

أَفَرَءَيۡتَ إِن مَّتَّعۡنَٰهُمۡ سِنِينَ ٢٠٥

Afara'ayta im matta'nāhum sinīn

Waonaje kama tukiwastarehesha kwa miaka,. 205

ثُمَّ جَآءَهُم مَّا كَانُواْ يُوعَدُونَ ٢٠٦

Thumma jā'ahum mā kānū yū'adūn

Kisha yakawafikia waliyo kuwa wakiahidiwa,. 206

مَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يُمَتَّعُونَ ٢٠٧

Mā aghnā 'anhum mā kānū yumatta'ūn

Yatawafaa nini yale waliyo stareheshewa?. 207

وَمَآ أَهۡلَكۡنَا مِن قَرۡيَةٍ إِلَّا لَهَا مُنذِرُونَ ٢٠٨

Wamā ahlaknā min qaryatin illā lahā mundhirūn

Wala hatukuangamiza mji wo wote ila ulikuwa na waonyaji. 208

ذِكۡرَىٰ وَمَا كُنَّا ظَٰلِمِينَ ٢٠٩

Dhikrā wamā kunnā zālimīn

Kuwa ni ukumbusho. Wala Sisi hatukuwa wenye kudhulumu. 209

وَمَا تَنَزَّلَتۡ بِهِ ٱلشَّيَٰطِينُ ٢١٠

Wamā tanazzalat bihish-shayātīn

Wala Mashet'ani hawakuteremka nayo, 210

وَمَا يَنۢبَغِي لَهُمۡ وَمَا يَسۡتَطِيعُونَ ٢١١

Wamā yambaghī lahum wamā yastatī'ūn

Wala haitakiwi kwao, na wala hawawezi. 211

إِنَّهُمۡ عَنِ ٱلسَّمۡعِ لَمَعۡزُولُونَ ٢١٢

Innahum 'anis-sam'i lama'zūlūn

Hakika hao wametengwa na kusikia. 212

فَلَا تَدۡعُ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَ فَتَكُونَ مِنَ ٱلۡمُعَذَّبِينَ ٢١٣

Falā tad'u ma'allāhi ilāhan ākhara fatakūna minal-mu'addhabīn

Basi usimwombe mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu ukawa miongoni mwa watakao adhibiwa. 213

وَأَنذِرۡ عَشِيرَتَكَ ٱلۡأَقۡرَبِينَ ٢١٤

Wa andhir 'ashīratakal-aqrabīn

Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe. 214

وَٱخۡفِضۡ جَنَاحَكَ لِمَنِ ٱتَّبَعَكَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ٢١٥

Wakhfid janāhaka limanit-taba'aka minal-mu'minīn

Na watwae kwa upole wanao kufuata miongoni mwa Waumini. 215

فَإِنۡ عَصَوۡكَ فَقُلۡ إِنِّي بَرِيٓءٞ مِّمَّا تَعۡمَلُونَ ٢١٦

Fa in 'asawka faqul innī barī'um mimmā ta'malūn

Na ikiwa watakuasi basi sema: Mimi najitenga mbali na hayo mnayo yatenda. 216

وَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱلۡعَزِيزِ ٱلرَّحِيمِ ٢١٧

Watawakkal 'alal-'azīzir-rahīm

Na umtegemee Mtukufu Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. 217

ٱلَّذِي يَرَىٰكَ حِينَ تَقُومُ ٢١٨

Alladhī yarāka hīna taqūm

Ambaye anakuona unapo simama, 218

وَتَقَلُّبَكَ فِي ٱلسَّٰجِدِينَ ٢١٩

Wataqallubaka fis-sājidīn

Na mageuko yako kati ya wanao sujudu. 219

إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ ٢٢٠

Innahū huwas-samī'ul-'alīm

Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua. 220

هَلۡ أُنَبِّئُكُمۡ عَلَىٰ مَن تَنَزَّلُ ٱلشَّيَٰطِينُ ٢٢١

Hal unabbi'ukum 'alā man tanazzalush-shayātīn

Je! Nikwambieni nani wanawashukia Mashet'ani? 221

تَنَزَّلُ عَلَىٰ كُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٖ ٢٢٢

Tanazzalu 'alā kulli affākin athīm

Wanamshukia kila mzushi mkubwa mwingi wa dhambi. 222

يُلۡقُونَ ٱلسَّمۡعَ وَأَكۡثَرُهُمۡ كَٰذِبُونَ ٢٢٣

Yulqūnas-sam'a wa aktharuhum kādhibūn

Wanawapelekea yale wanayo yasikia; na wengi wao ni waongo. 223

وَٱلشُّعَرَآءُ يَتَّبِعُهُمُ ٱلۡغَاوُۥنَ ٢٢٤

Wash-shu'arā'u yattabi'uhumul-ghāwūn

Na watungaji mashairi ni wapotofu ndio wanawafuata. 224

أَلَمۡ تَرَ أَنَّهُمۡ فِي كُلِّ وَادٖ يَهِيمُونَ ٢٢٥

Alam tara annahum fī kulli wādin yahīmūn

Je! Huwaoni kwamba wao wanatangatanga katika kila bonde? 225

وَأَنَّهُمۡ يَقُولُونَ مَا لَا يَفۡعَلُونَ ٢٢٦

Wa annahum yaqūlūna mā lā yaf'alūn

Na kwamba wao husema wasiyo yatenda? 226

إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ وَذَكَرُواْ ٱللَّهَ كَثِيرٗا وَٱنتَصَرُواْ مِنۢ بَعۡدِ مَا ظُلِمُواْۗ وَسَيَعۡلَمُ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓاْ أَيَّ مُنقَلَبٖ يَنقَلِبُونَ ٢٢٧

Illal-ladhīna āmanū wa'amilus-sālihāti wadhakarullāha kathīran wantasarū mim ba'di mā zulimū wasaya'lamul-ladhīna zalamū ayya munqalabin yanqalibūn

Isipo kuwa wale walio amini, na wakatenda mema, na wakamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi, na wakajitetea wanapo dhulumiwa. Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka. 227

Surat An-Naml

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

طسٓۚ تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱلۡقُرۡءَانِ وَكِتَابٖ مُّبِينٍ ١

Tā Sīn tilka āyātul-qur'āni wakitābim mubīn

T'aa Siin. (T'.S.), Hizi ni Aya za Qur'ani na Kitabu kinacho bainisha; . 1

هُدٗى وَبُشۡرَىٰ لِلۡمُؤۡمِنِينَ ٢

Hudan wabushrā lil-mu'minīn

Uwongofu na bishara kwa Waumini! 2

ٱلَّذِينَ يُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤۡتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَهُم بِٱلۡأٓخِرَةِ هُمۡ يُوقِنُونَ ٣

Alladhīna yuqīmūnas-salawāta wayu'tūnaz-zakawāta wahum bil-ākhirati hum yūqinūn

Ambao wanashika Swala, na wanatoa Zaka, na Akhera wana yakini nayo. 3

إِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ زَيَّنَّا لَهُمۡ أَعۡمَٰلَهُمۡ فَهُمۡ يَعۡمَهُونَ ٤

Innal-ladhīna lā yu'minūna bil-ākhirati zayyannā lahum a'mālahum fahum ya'mahūn

Kwa hakika wale wasio iamini Akhera tumewapambia vitendo vyao, kwa hivyo wanatangatanga ovyo. 4

أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ لَهُمۡ سُوٓءُ ٱلۡعَذَابِ وَهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ هُمُ ٱلۡأَخۡسَرُونَ ٥

Ulā'ikal-ladhīna lahum sū'ul-'adhābi wahum fil-ākhirati humul-akhsarūn

Hao ndio watapata adhabu mbaya kabisa, na hao katika Akhera ndio watapata khasara zaidi. 5

وَإِنَّكَ لَتُلَقَّى ٱلۡقُرۡءَانَ مِن لَّدُنۡ حَكِيمٍ عَلِيمٍ ٦

Wa innaka latulaqqal-qur'āna mil ladun hakīmin 'alīm

Na hakika wewe unafundishwa Qur'ani inayo tokana kwake Mwenye hikima Mwenye kujua. 6

إِذۡ قَالَ مُوسَىٰ لِأَهۡلِهِۦٓ إِنِّيٓ ءَانَسۡتُ نَارٗا سَـَٔاتِيكُم مِّنۡهَا بِخَبَرٍ أَوۡ ءَاتِيكُم بِشِهَابٖ قَبَسٖ لَّعَلَّكُمۡ تَصۡطَلُونَ ٧

Idh qāla mūsā li ahlihī innī ānastu nāran sa'ātīkum minhā bikhabarin aw ātīkum bishihābin qabasil la'allakum tastalūn

(Kumbuka) Musa alipo waambia ahali zake: Hakika nimeona moto, nitakwenda nikuleteeni khabari, au nitakuleteeni kijinga kinacho waka ili mpate kuota moto. 7

فَلَمَّا جَآءَهَا نُودِيَ أَنۢ بُورِكَ مَن فِي ٱلنَّارِ وَمَنۡ حَوۡلَهَا وَسُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ٨

Falammā jā'ahā nūdiya am būrika man fin-nāri waman hawlahā wasubhānallāhi rabbil-'ālamīn

Basi alipo fika ilinadiwa: Amebarikiwa aliomo katika moto huu na walioko pembezoni mwake. Na ametakasika Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote. 8

يَٰمُوسَىٰٓ إِنَّهُۥٓ أَنَا ٱللَّهُ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ ٩

Yāmūsā innahū anallāhul-'azīzul-hakīm

Ewe Musa! Hakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima. 9

وَأَلۡقِ عَصَاكَۚ فَلَمَّا رَءَاهَا تَهۡتَزُّ كَأَنَّهَا جَآنّٞ وَلَّىٰ مُدۡبِرٗا وَلَمۡ يُعَقِّبۡۚ يَٰمُوسَىٰ لَا تَخَفۡ إِنِّي لَا يَخَافُ لَدَيَّ ٱلۡمُرۡسَلُونَ ١٠

Wa alqi 'asāka falammā ra'āhā tahtazzu ka annahā jānnun wallā mudbiran walam yu'aqqib yāmūsā lā takhaf innī lā yakhāfu ladayyal-mursalūn

Na itupe fimbo yako! Alipo iona ikitikisika kama nyoka, aligeuka nyuma wala hakungoja. Ewe Musa! Usikhofu! Hakika hawakhofu mbele yangu Mitume. 10

إِلَّا مَن ظَلَمَ ثُمَّ بَدَّلَ حُسۡنَۢا بَعۡدَ سُوٓءٖ فَإِنِّي غَفُورٞ رَّحِيمٞ ١١

Illā man zalama thumma baddala husnā ba'da sū'in fa innī ghafūrur rahīm

Lakini aliye dhulumu, kisha akabadilisha wema baada ya ubaya, basi Mimi ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. 11

وَأَدۡخِلۡ يَدَكَ فِي جَيۡبِكَ تَخۡرُجۡ بَيۡضَآءَ مِنۡ غَيۡرِ سُوٓءٖۖ فِي تِسۡعِ ءَايَٰتٍ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَقَوۡمِهِۦٓۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَوۡمٗا فَٰسِقِينَ ١٢

Wa adkhil yadaka fī jaybika takhruj baydā'a min ghayri sū'in fī tis'i āyātin ilā fir'awna waqawmihī innahum kānū qawman fāsiqīn

Na ingiza mkono wako katika mfuko wako, utatoka mweupe bila ya maradhi. Ni katika Ishara tisa za kumpelekea Firauni na kaumu yake. Hakika hao walikuwa watu waovu. 12

فَلَمَّا جَآءَتۡهُمۡ ءَايَٰتُنَا مُبۡصِرَةٗ قَالُواْ هَٰذَا سِحۡرٞ مُّبِينٞ ١٣

Falammā jā'athum āyātunā mubsiratan qālū hādhā sihrum mubīn

Basi zilipo wafikia Ishara zetu hizo zenye kuonyesha, wakasema: Huu ni uchawi dhaahiri. 13

وَجَحَدُواْ بِهَا وَٱسۡتَيۡقَنَتۡهَآ أَنفُسُهُمۡ ظُلۡمٗا وَعُلُوّٗاۚ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُفۡسِدِينَ ١٤

Wajahadū bihā wastayqanathā anfusuhum zulman wa'uluwwan fanzur kayfa kāna 'āqibatul-mufsidīn

Na wakazikataa kwa dhulma na kujivuna, na hali ya kuwa nafsi zao zina yakini nazo. Basi angalia ulikuwaje mwisho wa mafisadi! 14

وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا دَاوُۥدَ وَسُلَيۡمَٰنَ عِلۡمٗاۖ وَقَالَا ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ ٱلَّذِي فَضَّلَنَا عَلَىٰ كَثِيرٖ مِّنۡ عِبَادِهِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ١٥

Walaqad ātaynā dāwūda wasulaymāna 'ilman waqālal-hamdu lillāhil-ladhī faddalanā 'alā kathīrim min 'ibādihil-mu'minīn

Na hakika tuliwapa Daudi na Sulaiman ilimu, na wakasema: Alhamdu Lillahi, Kuhimidiwa kote ni kwa Mwenyezi Mungu aliye tufadhilisha kuliko wengi katika waja wake Waumini. 15

وَوَرِثَ سُلَيۡمَٰنُ دَاوُۥدَۖ وَقَالَ يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ عُلِّمۡنَا مَنطِقَ ٱلطَّيۡرِ وَأُوتِينَا مِن كُلِّ شَيۡءٍۖ إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ ٱلۡفَضۡلُ ٱلۡمُبِينُ ١٦

Wawaritha sulaymānu dāwūda waqāla yā'ayyuhan-nāsu 'ullimnā mantiqat-tayri wa ūtīnā min kulli shay'in inna hādhā lahuwal-fadlul-mubīn

Na Sulaiman alimrithi Daudi, na akasema: Enyi watu! Tumefunzwa usemi wa ndege, na tumepewa kila kitu. Hakika hii ni fadhila iliyo dhaahiri. 16

وَحُشِرَ لِسُلَيۡمَٰنَ جُنُودُهُۥ مِنَ ٱلۡجِنِّ وَٱلۡإِنسِ وَٱلطَّيۡرِ فَهُمۡ يُوزَعُونَ ١٧

Wahushira lisulaymāna junūduhū minal-jinni wal-insi wat-tayri fahum yūza'ūn

Na alikusanyiwa Sulaiman majeshi yake ya majini, na watu, na ndege; nayo yakapangwa kwa nidhamu. 17

حَتَّىٰٓ إِذَآ أَتَوۡاْ عَلَىٰ وَادِ ٱلنَّمۡلِ قَالَتۡ نَمۡلَةٞ يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّمۡلُ ٱدۡخُلُواْ مَسَٰكِنَكُمۡ لَا يَحۡطِمَنَّكُمۡ سُلَيۡمَٰنُ وَجُنُودُهُۥ وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ ١٨

Hattā idhā ataw 'alā wādin-namli qālat namlatun yā'ayyuhan-namludkhulū masākinakum lā yahtimannakum sulaymānu wajunūduhū wahum lā yash'urūn

Mpaka walipo fika kwenye bonde la wadudu chungu, alisema mdudu chungu mmoja: Enyi wadudu chungu! Ingieni majumbani mwenu, asikupondeni Sulaiman na majeshi yake bila ya wao kutambua. 18

فَتَبَسَّمَ ضَاحِكٗا مِّن قَوۡلِهَا وَقَالَ رَبِّ أَوۡزِعۡنِيٓ أَنۡ أَشۡكُرَ نِعۡمَتَكَ ٱلَّتِيٓ أَنۡعَمۡتَ عَلَيَّ وَعَلَىٰ وَٰلِدَيَّ وَأَنۡ أَعۡمَلَ صَٰلِحٗا تَرۡضَىٰهُ وَأَدۡخِلۡنِي بِرَحۡمَتِكَ فِي عِبَادِكَ ٱلصَّٰلِحِينَ ١٩

Fatabassama dāhikam min qawlihā waqāla rabbi awzi'nī an ashkura ni'matakal-latī an'amta 'alayya wa'alā wālidayya wa an a'mala sālihan tardāhu wa adkhilnī birahmatika fī 'ibādikas-sālihīn

Basi (Sulaiman) akatabasamu akacheka kwa neno hili, na akasema: Ee Mola wangu Mlezi! Nizindue niishukuru neema yako uliyo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nipate kutenda mema uyapendayo, na uniingize kwa rehema yako katika waja wako wema. 19

وَتَفَقَّدَ ٱلطَّيۡرَ فَقَالَ مَالِيَ لَآ أَرَى ٱلۡهُدۡهُدَ أَمۡ كَانَ مِنَ ٱلۡغَآئِبِينَ ٢٠

Watafaqqadat-tayra faqāla māliya lā aral-hudhuda am kāna minal-ghā'ibīn

Na akawakagua ndege, na akasema: Imekuwaje, mbona simwoni Hud-hud, au amekuwa miongoni mwa walio ghibu? 20

لَأُعَذِّبَنَّهُۥ عَذَابٗا شَدِيدًا أَوۡ لَأَاْذۡبَحَنَّهُۥٓ أَوۡ لَيَأۡتِيَنِّي بِسُلۡطَٰنٖ مُّبِينٖ ٢١

La u'addhibannahū 'adhāban shadīdan aw la adhbahannahū aw laya'tiyannī bisultānim mubīn

Kwa yakini nitamuadhibu kwa adhabu kali, au nitamchinja, au aniletee hoja ya kutosha. 21

فَمَكَثَ غَيۡرَ بَعِيدٖ فَقَالَ أَحَطتُ بِمَا لَمۡ تُحِطۡ بِهِۦ وَجِئۡتُكَ مِن سَبَإِۭ بِنَبَإٖ يَقِينٍ ٢٢

Famakatha ghayra ba'īdin faqāla ahattu bimā lam tuhit bihī waji'tuka min saba'i binaba'in yaqīn

Basi (Hud-hud) akakaa si mbali na akasema: Nimegundua usilo gundua wewe, na ninakujia hivi kutoka nchi ya Sabai, na nakuletea khabari za yakini. 22

إِنِّي وَجَدتُّ ٱمۡرَأَةٗ تَمۡلِكُهُمۡ وَأُوتِيَتۡ مِن كُلِّ شَيۡءٖ وَلَهَا عَرۡشٌ عَظِيمٞ ٢٣

Innī wajattumra'atan tamlikuhum wa ūtiyat min kulli shay'in walahā 'arshun 'azīm

Hakika mimi nimemkuta mwanamke anawatawala, naye amepewa kila kitu, na anacho kiti cha enzi kikubwa. 23

وَجَدتُّهَا وَقَوۡمَهَا يَسۡجُدُونَ لِلشَّمۡسِ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَزَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ أَعۡمَٰلَهُمۡ فَصَدَّهُمۡ عَنِ ٱلسَّبِيلِ فَهُمۡ لَا يَهۡتَدُونَ ٢٤

Wajattuhā waqawmahā yasjudūna lish-shamsi min dūnillāhi wazayyana lahumush-shaytānu a'mālahum fasaddahum 'anis-sabīli fahum lā yahtadūn

Nimemkuta yeye na watu wake wanalisujudia jua badala ya Mwenyezi Mungu; na Shet'ani amewapambia vitendo vyao na akawazuilia Njia. Kwa hivyo hawakuongoka 24

أَلَّاۤ يَسۡجُدُواْۤ لِلَّهِ ٱلَّذِي يُخۡرِجُ ٱلۡخَبۡءَ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَيَعۡلَمُ مَا تُخۡفُونَ وَمَا تُعۡلِنُونَ ٢٥

Allā yasjudū lillāhil-ladhī yukhrijul-khab'a fis-samāwāti wal-ardi waya'lamu mā tukhfūna wamā tu'linūn

Na hawamsujudii Mwenyezi Mungu ambaye huyatoa yaliyo fichikana katika mbingu na ardhi, na anayajua mnayo yaficha na mnayo yatangaza. 25

ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ رَبُّ ٱلۡعَرۡشِ ٱلۡعَظِيمِ۩ ٢٦

Allāhu lā ilāha illā huwa rabbul-'arshil-'azīm

Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye, Mola Mlezi wa A'rshi tukufu 26

۞ قَالَ سَنَنظُرُ أَصَدَقۡتَ أَمۡ كُنتَ مِنَ ٱلۡكَٰذِبِينَ ٢٧

Qāla sananzuru asadaqta am kunta minal-kādhibīn

Akasema (Sulaiman): Tutatazama umesema kweli au wewe ni miongoni mwa waongo. 27

ٱذۡهَب بِّكِتَٰبِي هَٰذَا فَأَلۡقِهۡ إِلَيۡهِمۡ ثُمَّ تَوَلَّ عَنۡهُمۡ فَٱنظُرۡ مَاذَا يَرۡجِعُونَ ٢٨

Idhhab bikitābī hādhā fa alqih ilayhim thumma tawalla 'anhum fanzur mādhā yarji'ūn

Nenda na barua yangu hii na uwafikishie, kisha waache na utazame watarejesha nini. 28

قَالَتۡ يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡمَلَؤُاْ إِنِّيٓ أُلۡقِيَ إِلَيَّ كِتَٰبٞ كَرِيمٌ ٢٩

Qālat yā'ayyuhal-mala'u innī ulqiya ilayya kitābun karīm

(Malkia) akasema: Enyi wahishimiwa! Hakika nimeletewa barua tukufu. 29

إِنَّهُۥ مِن سُلَيۡمَٰنَ وَإِنَّهُۥ بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ ٣٠

Innahū min sulaymāna wa innahū bismillāhir-rahmānir-rahīm

Imetoka kwa Sulaiman nayo ni: Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. 30

أَلَّا تَعۡلُواْ عَلَيَّ وَأۡتُونِي مُسۡلِمِينَ ٣١

Allā ta'lū 'alayya wa tūnī muslimīn

Msinifanyie jeuri, na fikeni kwangu nanyi mmekwisha kuwa wenye kusalimu amri. 31

قَالَتۡ يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡمَلَؤُاْ أَفۡتُونِي فِيٓ أَمۡرِي مَا كُنتُ قَاطِعَةً أَمۡرًا حَتَّىٰ تَشۡهَدُونِ ٣٢

Qālat yā'ayyuhal-mala'u aftūnī fī amrī mā kuntu qāti'atan amran hattā tashhadūn

Akasema: Enyi wahishimiwa! Nipeni shauri katika jambo langu hili, kwani mimi sikati shauri yoyote mpaka mhudhurie. 32

قَالُواْ نَحۡنُ أُوْلُواْ قُوَّةٖ وَأُوْلُواْ بَأۡسٖ شَدِيدٖ وَٱلۡأَمۡرُ إِلَيۡكِ فَٱنظُرِي مَاذَا تَأۡمُرِينَ ٣٣

Qālū nahnu ulū quwwatin wa ulū ba sin shadīdin wal-amru ilayki fanzurī mādhā ta'murīn

Wakasema: Sisi ni wenye nguvu na wakali kwa vita; na amri iko kwako, basi tazama ni nini unaamrisha. 33

قَالَتۡ إِنَّ ٱلۡمُلُوكَ إِذَا دَخَلُواْ قَرۡيَةً أَفۡسَدُوهَا وَجَعَلُوٓاْ أَعِزَّةَ أَهۡلِهَآ أَذِلَّةٗۚ وَكَذَٰلِكَ يَفۡعَلُونَ ٣٤

Qālat innal-mulūka idhā dakhalū qaryatan afsadūhā waja'alū a'izzata ahlihā adhillatan wakadhālika yaf'alūn

Akasema: Hakika wafalme wanapo uingia mji wanauharibu, na wanawafanya wale watukufu wake kuwa wanyonge. Na hivyo ndivyo watendavyo. 34

وَإِنِّي مُرۡسِلَةٌ إِلَيۡهِم بِهَدِيَّةٖ فَنَاظِرَةُۢ بِمَ يَرۡجِعُ ٱلۡمُرۡسَلُونَ ٣٥

Wa innī mursilatun ilayhim bihadiyyatin fanāziratu bima yarji'ul-mursalūn

Lakini mimi nitawapelekea zawadi, nami nitangoja watakayo rudi nayo wajumbe. 35

فَلَمَّا جَآءَ سُلَيۡمَٰنَ قَالَ أَتُمِدُّونَنِ بِمَالٖ فَمَآ ءَاتَىٰنِۦَ ٱللَّهُ خَيۡرٞ مِّمَّآ ءَاتَىٰكُمۚ بَلۡ أَنتُم بِهَدِيَّتِكُمۡ تَفۡرَحُونَ ٣٦

Falammā jā'a sulaymāna qāla atumiddūnani bimālin famā ātānillāhu khayrum mimmā ātākum bal antum bihadiyyatikum tafrahūn

Basi alipo fika (mjumbe) kwa Sulaiman, alisema (Sulaiman): Hivyo ndio nyinyi mnanisaidia kwa mali? Aliyo nipa Mwenyezi Mungu ni bora zaidi kuliko aliyo kupeni nyinyi. Lakini nyinyi mnafurahia hii zawadi yenu. 36

ٱرۡجِعۡ إِلَيۡهِمۡ فَلَنَأۡتِيَنَّهُم بِجُنُودٖ لَّا قِبَلَ لَهُم بِهَا وَلَنُخۡرِجَنَّهُم مِّنۡهَآ أَذِلَّةٗ وَهُمۡ صَٰغِرُونَ ٣٧

Irji' ilayhim falana'tiyannahum bijunūdil lā qibala lahum bihā walanukhrijannahum minhā adhillatan wahum sāghirūn

Rejea kwao! Kwa yakini sisi tutawajia kwa majeshi wasio yaweza kuyakabili. Na hakika tutawatoa humo na hali wao wamekuwa madhalili na wanyonge. 37

قَالَ يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡمَلَؤُاْ أَيُّكُمۡ يَأۡتِينِي بِعَرۡشِهَا قَبۡلَ أَن يَأۡتُونِي مُسۡلِمِينَ ٣٨

Qāla yā'ayyuhal-mala'u ayyukum ya'tīnī bi'arshihā qabla an ya'tūnī muslimīn

Akasema: Enyi wahishimiwa! Ni nani kati yenu atakaye niletea kiti chake cha enzi kabla hawajanijia nao wamekwisha salimu amri. 38

قَالَ عِفۡرِيتٞ مِّنَ ٱلۡجِنِّ أَنَا۠ ءَاتِيكَ بِهِۦ قَبۡلَ أَن تَقُومَ مِن مَّقَامِكَۖ وَإِنِّي عَلَيۡهِ لَقَوِيٌّ أَمِينٞ ٣٩

Qāla 'ifrītum minal-jinni ana ātīka bihī qabla an taqūma mim maqāmika wa innī 'alayhi laqawiyyun amīn

Akasema: Afriti, katika majini: Mimi nitakuletea kabla hujainuka pahala pako hapo. Na mimi kwa hakika nina nguvu na muaminifu. 39

قَالَ ٱلَّذِي عِندَهُۥ عِلۡمٞ مِّنَ ٱلۡكِتَٰبِ أَنَا۠ ءَاتِيكَ بِهِۦ قَبۡلَ أَن يَرۡتَدَّ إِلَيۡكَ طَرۡفُكَۚ فَلَمَّا رَءَاهُ مُسۡتَقِرًّا عِندَهُۥ قَالَ هَٰذَا مِن فَضۡلِ رَبِّي لِيَبۡلُوَنِيٓ ءَأَشۡكُرُ أَمۡ أَكۡفُرُۖ وَمَن شَكَرَ فَإِنَّمَا يَشۡكُرُ لِنَفۡسِهِۦۖ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ رَبِّي غَنِيّٞ كَرِيمٞ ٤٠

Qālal-ladhī 'indahū 'ilmum minal-kitābi ana ātīka bihī qabla an yartadda ilayka tarfuka falammā ra'āhu mustaqirran 'indahū qāla hādhā min fadli rabbī liyabluwanī a'ashkuru am akfuru waman shakara fa innamā yashkuru linafsihī waman kafara fa inna rabbī ghaniyyun karīm

Akasema mwenye ilimu ya Kitabu: Mimi nitakuletea kabla ya kupepesa jicho lako. Basi alipo kiona kimewekwa mbele yake, akasema: Haya ni katika fadhila zake Mola wangu Mlezi, ili anijaribu nitashukuru au nitakufuru. Na mwenye kushukuru, kwa hakika, anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake; na anaye kufuru, kwa hakika Mola wangu Mlezi ni Mkwasi na Karimu. 40

قَالَ نَكِّرُواْ لَهَا عَرۡشَهَا نَنظُرۡ أَتَهۡتَدِيٓ أَمۡ تَكُونُ مِنَ ٱلَّذِينَ لَا يَهۡتَدُونَ ٤١

Qāla nakkirū lahā 'arshahā nanzur atahtadī am takūnu minal-ladhīna lā yahtadūn

Akasema: Mgeuzieni kiti chake cha enzi hiki, tuone ataongoka, au atakuwa miongoni mwa wasio ongoka. 41

فَلَمَّا جَآءَتۡ قِيلَ أَهَٰكَذَا عَرۡشُكِۖ قَالَتۡ كَأَنَّهُۥ هُوَۚ وَأُوتِينَا ٱلۡعِلۡمَ مِن قَبۡلِهَا وَكُنَّا مُسۡلِمِينَ ٤٢

Falammā jā'at qīla ahākadhā 'arshuki qālat ka annahū huwa wa ūtīnal-'ilma min qablihā wakunnā muslimīn

Basi (Malkia) alipo fika akaambiwa: Je! Kiti chako cha enzi ni kama hiki? Akasema: Kama kwamba ndicho hichi. (Sulaiman na watu wake wakasema): Na sisi tumepewa ilimu kabla yake (Malkia), na tukawa Waislamu. 42

وَصَدَّهَا مَا كَانَت تَّعۡبُدُ مِن دُونِ ٱللَّهِۖ إِنَّهَا كَانَتۡ مِن قَوۡمٖ كَٰفِرِينَ ٤٣

Wasaddahā mā kānat ta'budu min dūnillāhi innahā kānat min qawmin kāfirīn

Na yale aliyo kuwa akiyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu yalimzuilia. Hakika yeye (Malkia) alikuwa katika kaumu ya makafiri. 43

قِيلَ لَهَا ٱدۡخُلِي ٱلصَّرۡحَۖ فَلَمَّا رَأَتۡهُ حَسِبَتۡهُ لُجَّةٗ وَكَشَفَتۡ عَن سَاقَيۡهَاۚ قَالَ إِنَّهُۥ صَرۡحٞ مُّمَرَّدٞ مِّن قَوَارِيرَۗ قَالَتۡ رَبِّ إِنِّي ظَلَمۡتُ نَفۡسِي وَأَسۡلَمۡتُ مَعَ سُلَيۡمَٰنَ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ٤٤

Qīla lahadkhulis-sarha falammā ra'athu hasibathu lujjatan wakashafat 'an sāqayhā qāla innahū sarhum mumarradum min qawārīra qālat rabbi innī zalamtu nafsī wa aslamtu ma'a sulaymāna lillāhi rabbil-'ālamīn

Akaambiwa: Liingie behewa la hili jumba. Alipo liona alidhani ni maji, na akapandisha nguo mpaka kwenye miundi yake. (Sulaiman) akasema: Hakika hilo ni behewa lilio sakafiwa kwa viyoo! Akasema (Malkia): Mola wangu Mlezi! Mimi nimejidhulumu nafsi yangu, na sasa nanyenyekea pamoja na Sulaiman kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote. 44

وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَآ إِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمۡ صَٰلِحًا أَنِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ فَإِذَا هُمۡ فَرِيقَانِ يَخۡتَصِمُونَ ٤٥

Walaqad arsalnā ilā thamūda akhāhum sālihan ani'budullāha fa idhā hum farīqāni yakhtasimūn

. Na kwa kina Thamud tulimtuma ndugu yao Swaleh kuwaambia: Muabuduni Mwenyezi Mungu. Basi wakawa makundi mawili yanayo gombana. 45

قَالَ يَٰقَوۡمِ لِمَ تَسۡتَعۡجِلُونَ بِٱلسَّيِّئَةِ قَبۡلَ ٱلۡحَسَنَةِۖ لَوۡلَا تَسۡتَغۡفِرُونَ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ ٤٦

Qāla yāqawmi lima tasta'jilūna bis-sayyi'ati qablal-hasanati lawlā tastaghfirūnallāha la'allakum turhamūn

Akasema: Enyi watu wangu! Kwa nini mnauhimiza uwovu kabla ya wema? Kwa nini hamuombi msamaha kwa Mwenyezi Mungu ili mrehemewe? 46

قَالُواْ ٱطَّيَّرۡنَا بِكَ وَبِمَن مَّعَكَۚ قَالَ طَٰٓئِرُكُمۡ عِندَ ٱللَّهِۖ بَلۡ أَنتُمۡ قَوۡمٞ تُفۡتَنُونَ ٤٧

Qālut-tayyarnā bika wabimam ma'aka qāla tā'irukum 'indallāhi bal antum qawmun tuftanūn

Wakasema: Tuna kisirani nawe na wale walio pamoja nawe. Yeye akasema: Uaguzi wa ukorofi wenu uko kwa Mwenyezi Mungu; lakini nyinyi ni watu mnao jaribiwa. 47

وَكَانَ فِي ٱلۡمَدِينَةِ تِسۡعَةُ رَهۡطٖ يُفۡسِدُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا يُصۡلِحُونَ ٤٨

Wakāna fil-madīnati tis'atu rahtin yufsidūna fil-ardi walā yuslihūn

Na walikuwamo mjini watu tisa wakifanya ufisadi katika nchi wala hawafanyi la maslaha. 48

قَالُواْ تَقَاسَمُواْ بِٱللَّهِ لَنُبَيِّتَنَّهُۥ وَأَهۡلَهُۥ ثُمَّ لَنَقُولَنَّ لِوَلِيِّهِۦ مَا شَهِدۡنَا مَهۡلِكَ أَهۡلِهِۦ وَإِنَّا لَصَٰدِقُونَ ٤٩

Qālū taqāsamū billāhi lanubayyitannahū wa ahlahū thumma lanaqūlanna liwaliyyihī mā shahidnā mahlika ahlihī wa innā lasādiqūn

Wakasema: Apishaneni kwa Mwenyezi Mungu tutamshambulia usiku yeye na ahali zake; kisha tutamwambia mrithi wake: Sisi hatukuona maangamizo ya watu wake, na sisi bila ya shaka tunasema kweli. 49

وَمَكَرُواْ مَكۡرٗا وَمَكَرۡنَا مَكۡرٗا وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ ٥٠

Wamakarū makran wamakarnā makran wahum lā yash'urūn

Basi wakapanga mipango yao, na Sisi tukapanga mipango yetu, na wao hawatambui. 50

فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ مَكۡرِهِمۡ أَنَّا دَمَّرۡنَٰهُمۡ وَقَوۡمَهُمۡ أَجۡمَعِينَ ٥١

Fanzur kayfa kāna 'āqibatu makrihim annā dammarnāhum waqawmahum ajma'īn

Basi angalia ulivyo kuwa mwisho wa mipango yao, ya kwamba tuliwaangamiza wao pamoja na watu wao wote. 51

فَتِلۡكَ بُيُوتُهُمۡ خَاوِيَةَۢ بِمَا ظَلَمُوٓاْۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ ٥٢

Fatilka buyūtuhum khāwiyata bimā zalamū inna fī dhālika la'āyatal liqawmin ya'lamūn

Basi hizo nyumba zao ni tupu kwa sababu ya walivyo dhulumu. Hakika bila ya shaka katika hayo ipo Ishara kwa watu wanao jua. 52

وَأَنجَيۡنَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَكَانُواْ يَتَّقُونَ ٥٣

Wa anjaynal-ladhīna āmanū wakānū yattaqūn

Na tukawaokoa wale walio amini na walio kuwa wanamchamngu. 53

وَلُوطًا إِذۡ قَالَ لِقَوۡمِهِۦٓ أَتَأۡتُونَ ٱلۡفَٰحِشَةَ وَأَنتُمۡ تُبۡصِرُونَ ٥٤

Walūtan idh qāla liqawmihī ata'tūnal-fāhishata wa antum tubsirūn

Na Luut'i alipo waambia watu wake: Je! Mnafanya uchafu nanyi mnaona? 54

أَئِنَّكُمۡ لَتَأۡتُونَ ٱلرِّجَالَ شَهۡوَةٗ مِّن دُونِ ٱلنِّسَآءِۚ بَلۡ أَنتُمۡ قَوۡمٞ تَجۡهَلُونَ ٥٥

A'innakum lata'tūnar-rijāla shahwatam min dūnin-nisā'i bal antum qawmun tajhalūn

Hivyo nyinyi mnawaingilia wanaume kwa matamanio badala ya wanawake? Hakika nyinyi ni watu mnao fanya ujinga kabisa! 55

Maswali

Juzuu 19 inaanzia na kuishia wapi?

Juzuu 19 inaanzia Surat Al-Furqan 25:21 na kuishia Surat An-Naml 27:55.

Ni sura gani zilizo katika Juzuu 19?

Juzuu 19 ina Al-Furqan, Ash-Shu'ara, An-Naml.

Juzuu ni nini?

Juzuu ni moja ya sehemu 30 zenye urefu sawa. Kusoma juzuu moja kila siku kunakamilisha Qur'ani kwa mwezi mmoja.