وَعِبَادُ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلَّذِينَ يَمۡشُونَ عَلَى ٱلۡأَرۡضِ هَوۡنٗا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ ٱلۡجَٰهِلُونَ قَالُواْ سَلَٰمٗا ٦٣
Wa'ibādur-rahmānil-ladhīna yamshūna 'alal-ardi hawnan wa idhā khātabahumul-jāhilūna qālū salāmā
Na waja wa Arrahman Mwingi wa Rehema ni wale wanao tembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemeza hujibu: Salama! 63
Maelezo ya chini
63 Na waja wa Mwenyezi Mungu ni wale wanao nyenyekea duniani. Wakitembea katika ardhi wanatembea kwa utulivu na staha. Hali kadhaalika katika mambo yao yote. Na masafihi katika washirikina wakiwasubu (wakiwatukana) wanawaachilia mbali na shani yao, na wanawaambia: Hatuna shani nanyi. Letu sisi ni Assalamu Alaikum!