وَيَوۡمَ يَعَضُّ ٱلظَّالِمُ عَلَىٰ يَدَيۡهِ يَقُولُ يَٰلَيۡتَنِي ٱتَّخَذۡتُ مَعَ ٱلرَّسُولِ سَبِيلٗا ٢٧
Wayawma ya'adduz-zālimu 'alā yadayhi yaqūlu yālaytanit-takhadhtu ma'ar-rasūli sabīlā
Na siku ambayo mwenye kudhulumu atajiuma mikono yake, na huku anasema: Laiti ningeli shika njia pamoja na Mtume! 27
Maelezo ya chini
27 Siku ya Kiyama mwenye kujidhulumu nafsi yake atajiuma mikono yake kwa hasira na majuto kwa ukafiri wake na kumwendea kinyume Mtume, na kwa kutamani atasema: Laiti lau ningeli mfuata Mtume, nikaifuata njia ya kwendea Peponi, na nikaiepuka njia ya kwendea Motoni!