Surat Ash-Shu'ara, aya 189

26:189

فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَهُمۡ عَذَابُ يَوۡمِ ٱلظُّلَّةِۚ إِنَّهُۥ كَانَ عَذَابَ يَوۡمٍ عَظِيمٍ ١٨٩

Fakaddhabūhu fa akhadhahum 'adhābu yawmiz-zullati innahū kāna 'adhāba yawmin 'azīm

Basi walimkanusha, na ikawashika adhabu ya siku ya kivuli. Hakika hiyo ilikuwa adhabu ya siku kubwa. 189

Maelezo ya chini

189 Lakini wao waliendelea kumkadhibisha. Mwenyezi Mungu akawapatiliza kwa adhabu ya joto kuu mno. Wakawa wanatapa tapa hawana pa kukimbilia. Walipo pata kiwingu cha kuwapa kivuli kukinga mwako wa jua walijikusanya chini yake. Mwenyezi Mungu akawateremshia moto, ukawateketeza wote katika siku ya kitisho kikubwa mno.