Surat Al-Furqan, aya 55

25:55

وَيَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَنفَعُهُمۡ وَلَا يَضُرُّهُمۡۗ وَكَانَ ٱلۡكَافِرُ عَلَىٰ رَبِّهِۦ ظَهِيرٗا ٥٥

Waya'budūna min dūnillāhi mā lā yanfa'uhum walā yadurruhum wakānal-kāfiru 'alā rabbihī zahīrā

Na wanayaabudu badala ya Mwenyezi Mungu yasiyo wafaa wala yasiyo wadhuru. Na kafiri daima ni msaidizi wa kumpinga Mola wake Mlezi. 55

Maelezo ya chini

55 Na baada ya Ishara hizi zenye kuonyesha kuwa Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anaye stahiki kuabudiwa, na kwamba hapana mungu isipo kuwa Yeye, wanatoka kikundi cha watu kuabudu masanamu yasiyo wafaa wala kuwadhuru. Na hawa kwa kujua kwao haya wanamsaidia Shetani, na yeye anawapoteza. Basi hao inakuwa wanasaidiana katika kuipinga Haki ambayo Mwenyezi Mungu anawaitia.