وَكَذَٰلِكَ جَعَلۡنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوّٗا مِّنَ ٱلۡمُجۡرِمِينَۗ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ هَادِيٗا وَنَصِيرٗا ٣١
Wakadhālika ja'alnā likulli nabiyyin 'aduwwam minal-mujrimīna wakafā birabbika hādiyan wanasīrā
Na vivi hivi tumemfanyia kila Nabii adui miongoni mwa wakosefu, na Mola wako Mlezi anatosha kuwa Mwenye kuongoa na Mwenye kunusuru. 31
Maelezo ya chini
31 Kama tulivyo wajaalia watu wako, ewe Muhammad, wanavyo kufanyia uadui na kukukadhibisha, basi kadhaalika tulimjaalia kila Nabii ana maadui miongoni mwa wakosefu, wanao mfanyia uadui na wanaupinga wito wake. Na Mwenyezi Mungu atakunusuru, na atakuongoa mpaka uwashinde. Na Yeye anakutosha kwa uwongofu na kukunusuru.