Surat Al-Furqan, aya 47

25:47

وَهُوَ ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلَّيۡلَ لِبَاسٗا وَٱلنَّوۡمَ سُبَاتٗا وَجَعَلَ ٱلنَّهَارَ نُشُورٗا ٤٧

Wahuwal-ladhī ja'ala lakumul-layla libāsan wan-nawma subātan waja'alan-nahāra nushūrā

Naye ndiye aliye kufanyieni usiku kuwa ni vazi, na usingizi kuwa mapumziko, na akakufanyieni mchana ni kufufuka. 47

Maelezo ya chini

47 Na katika Ishara za Tawhidi ni kuwa tumeufanya usiku ni sitara kwa kiza chake, ndani yake wanaingia viumbe ukawazunguka kama inavyo wazunguka nguo kwa mwenye kuivaa. Na tukawatengenezea malazi, ikawa ni mapumziko kupumzika na machofu, na kwa mwangaza wa jua wanazinduliwa watu watafute maisha yao na riziki zao.