Surat Ash-Shu'ara, aya 27

26:27

قَالَ إِنَّ رَسُولَكُمُ ٱلَّذِيٓ أُرۡسِلَ إِلَيۡكُمۡ لَمَجۡنُونٞ ٢٧

Qāla inna rasūlakumul-ladhī ursila ilaykum lamajnūn

(Firauni) akasema: Hakika huyu Mtume wenu aliye tumwa kwenu ni mwendawazimu. 27

Maelezo ya chini

27 Firauni akwaambia watu wake yale yanayo mtibuwa roho na kumghadhibisha, akautaja Utume wa Musa ni kwao wao, wala si kwake yeye, na akambandikiza wazimu, kwa kuwa ati akiulizwa kitu hujibu kingine, na anamsifu Mola Mlezi kwa sifa za kiajabu ajabu. Na kwa hivyo Firauni anawahimiza wamkadhibishe.