كَذَّبَ أَصۡحَٰبُ لۡـَٔيۡكَةِ ٱلۡمُرۡسَلِينَ ١٧٦
Kaddhaba ashābu l'aykatil-mursalīn
Watu wa Machakani waliwakanusha Mitume. 176
Maelezo ya chini
176 Hichi kisa cha Shuaibu pamoja na Watu wa Al Aykat, Machakani, nao ni msitu wenye miti mizuri, karibu na Madian. Kikundi cha watu waliteremkia hapo na wakakaa. Mwenyezi Mungu akawapelekea Shuaibu kama alivyo wapelekea watu wa Madian. Wakamkadhibisha katika wito wake. Na kwa hivi wakawa wamekanusha risala za Mitume wote.