تَٱللَّهِ إِن كُنَّا لَفِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٍ ٩٧
Tallāhi in kunnā lafī dalālim mubīn
Wallahi! Kwa yakini tulikuwa katika upotovu ulio dhaahiri, 97
Maelezo ya chini
97 Wallahi! Hakika sisi tulikuwa katika dunia yetu tumepotea kweli, na wajinga wa kutupwa, na tumeiacha Haki ambayo haina kificho ndani yake.