إِذَا وَقَعَتِ ٱلۡوَاقِعَةُ ١
Idhā waqa'atil-wāqi'ah
Litakapo tukia hilo Tukio . 1
Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
إِذَا وَقَعَتِ ٱلۡوَاقِعَةُ ١
Idhā waqa'atil-wāqi'ah
Litakapo tukia hilo Tukio . 1
لَيۡسَ لِوَقۡعَتِهَا كَاذِبَةٌ ٢
Laysa liwaq'atihā kādhibah
Hapana cha kukanusha kutukia kwake. 2
خَافِضَةٞ رَّافِعَةٌ ٣
Khāfidatur rāfi'ah
Literemshalo linyanyualo! 3
إِذَا رُجَّتِ ٱلۡأَرۡضُ رَجّٗا ٤
Idhā rujjatil-ardu rajjā
Itakapo tikiswa ardhi kwa mtikiso! 4
وَبُسَّتِ ٱلۡجِبَالُ بَسّٗا ٥
Wabussatil-jibālu bassā
Na milima itapo sagwasagwa! 5
فَكَانَتۡ هَبَآءٗ مُّنۢبَثّٗا ٦
Fakānat habā'am mumbatthā
Iwe mavumbi yanayo peperushwa! 6
وَكُنتُمۡ أَزۡوَٰجٗا ثَلَٰثَةٗ ٧
Wakuntum azwājan thalāthah
Na nyinyi mtakuwa namna tatu: . 7
فَأَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ ٨
Fa ashābul-maymanati mā ashābul-maymanah
Basi watakuwepo wa kuliani; je, ni wepi wa kuliani? 8
وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ ٩
Wa ashābul-mash'amati mā ashābul-mash'amah
Na wa kushotoni; je, ni wepi wa kushotoni? 9
وَٱلسَّٰبِقُونَ ٱلسَّٰبِقُونَ ١٠
Was-sābiqūnas-sābiqūn
Na wa mbele watakuwa mbele. 10
أُوْلَٰٓئِكَ ٱلۡمُقَرَّبُونَ ١١
Ulā'ikal-muqarrabūn
Hao ndio watakao karibishwa 11
فِي جَنَّٰتِ ٱلنَّعِيمِ ١٢
Fī jannātin-na'īm
Katika Bustani zenye neema. 12
ثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ ١٣
Thullatum minal-awwalīn
Fungu kubwa katika wa mwanzo, 13
وَقَلِيلٞ مِّنَ ٱلۡأٓخِرِينَ ١٤
Waqalīlum minal-ākhirīn
Na wachache katika wa mwisho. 14
عَلَىٰ سُرُرٖ مَّوۡضُونَةٖ ١٥
'Alā sururim mawdūnah
Watakuwa juu ya viti vya fakhari vilivyo tonewa. 15
مُّتَّكِـِٔينَ عَلَيۡهَا مُتَقَٰبِلِينَ ١٦
Mmuttaki'īna 'alayhā mutaqābilīn
Wakiviegemea wakielekeana. 16
يَطُوفُ عَلَيۡهِمۡ وِلۡدَٰنٞ مُّخَلَّدُونَ ١٧
Yatūfu 'alayhim wildānum mukhalladūn
Wakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele, 17
بِأَكۡوَابٖ وَأَبَارِيقَ وَكَأۡسٖ مِّن مَّعِينٖ ١٨
Bi akwābin wa abārīqa waka'sim mim ma'īn
Kwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemchem safi. 18
لَّا يُصَدَّعُونَ عَنۡهَا وَلَا يُنزِفُونَ ١٩
Llā yusadda'ūna 'anhā walā yunzifūn
Hawataumwa kichwa kwa vinywaji hivyo wala hawatoleweshwa. 19
وَفَٰكِهَةٖ مِّمَّا يَتَخَيَّرُونَ ٢٠
Wafākihatim mimmā yatakhayyarūn
Na matunda wayapendayo, 20
وَلَحۡمِ طَيۡرٖ مِّمَّا يَشۡتَهُونَ ٢١
Walahmi tayrim mimmā yashtahūn
Na nyama za ndege kama wanavyo tamani. 21
وَحُورٌ عِينٞ ٢٢
Wahūrun 'īn
Na Mahurulaini, 22
كَأَمۡثَٰلِ ٱللُّؤۡلُوِٕ ٱلۡمَكۡنُونِ ٢٣
Ka amthālil-lu'luw'il-maknūn
Walio kama mfano wa lulu zilio hifadhiwa. 23
جَزَآءَۢ بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ ٢٤
Jazā'a bimā kānū ya'malūn
Ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda. 24
لَا يَسۡمَعُونَ فِيهَا لَغۡوٗا وَلَا تَأۡثِيمًا ٢٥
Lā yasma'ūna fīhā laghwan walā ta'thīmā
Humo hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi, 25
إِلَّا قِيلٗا سَلَٰمٗا سَلَٰمٗا ٢٦
Illā qīlan salāman salāmā
Isipo kuwa maneno ya Salama, Salama. 26
وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡيَمِينِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡيَمِينِ ٢٧
Wa ashābul-yamīni mā ashābul-yamīn
Na wale wa mkono wa kulia, ni yepi yatakuwa ya wa kuliani? 27
فِي سِدۡرٖ مَّخۡضُودٖ ٢٨
Fī sidrim makhdūd
Katika mikunazi isiyo na miba, 28
وَطَلۡحٖ مَّنضُودٖ ٢٩
Watalhim mandūd
Na migomba iliyo pangiliwa, 29
وَظِلّٖ مَّمۡدُودٖ ٣٠
Wazillim mamdūd
Na kivuli kilicho tanda, 30
وَمَآءٖ مَّسۡكُوبٖ ٣١
Wamā'im maskūb
Na maji yanayo miminika, 31
وَفَٰكِهَةٖ كَثِيرَةٖ ٣٢
Wafākihatin kathīrah
Na matunda mengi, 32
لَّا مَقۡطُوعَةٖ وَلَا مَمۡنُوعَةٖ ٣٣
Llā maqtū'atin walā mamnū'ah
Hayatindikii wala hayakatazwi, 33
وَفُرُشٖ مَّرۡفُوعَةٍ ٣٤
Wafurushim marfū'ah
Na matandiko yaliyo nyanyuliwa. 34
إِنَّآ أَنشَأۡنَٰهُنَّ إِنشَآءٗ ٣٥
Innā ansha'nāhunna inshā'ā
Hakika Sisi tutawaumba (Mahurulaini) upya, 35
فَجَعَلۡنَٰهُنَّ أَبۡكَارًا ٣٦
Faja'alnāhunna abkārā
Na tutawafanya vijana, 36
عُرُبًا أَتۡرَابٗا ٣٧
'Uruban atrābā
Wanapendana na waume zao, hirimu moja. 37
لِّأَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ ٣٨
Lli ashābil-yamīn
Kwa ajili ya watu wa kuliani. 38
ثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ ٣٩
Thullatum minal-awwalīn
Fungu kubwa katika wa mwanzo, 39
وَثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأٓخِرِينَ ٤٠
Wathullatum minal-ākhirīn
Na fungu kubwa katika wa mwisho. 40
وَأَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ ٤١
Wa ashābush-shimāli mā ashābush-shimāl
Na watu wa kushotoni; je ni yepi ya wa kushotoni? 41
فِي سَمُومٖ وَحَمِيمٖ ٤٢
Fī samūmin wahamīm
Katika upepo wa moto, na maji yanayo chemka, 42
وَظِلّٖ مِّن يَحۡمُومٖ ٤٣
Wazillim min yahmūm
Na kivuli cha moshi mweusi, 43
لَّا بَارِدٖ وَلَا كَرِيمٍ ٤٤
Llā bāridin walā karīm
Si cha kuburudisha wala kustarehesha. 44
إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَبۡلَ ذَٰلِكَ مُتۡرَفِينَ ٤٥
Innahum kānū qabla dhālika mutrafīn
Hakika hao walikuwa kabla ya haya wakiishi maisha ya anasa. 45
وَكَانُواْ يُصِرُّونَ عَلَى ٱلۡحِنثِ ٱلۡعَظِيمِ ٤٦
Wakānū yusirrūna 'alal-hinthil-'azīm
Na walikuwa wakishikilia kufanya madhambi makubwa, 46
وَكَانُواْ يَقُولُونَ أَئِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابٗا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَبۡعُوثُونَ ٤٧
Wakānū yaqūlūna a'idhā mitnā wakunnā turāban wa'izāman a'innā lamab'ūthūn
Na walikuwa wakisema: Tutakapo kufa na tukawa udongo na mafupa, ati ndio tutafufuliwa? 47
أَوَءَابَآؤُنَا ٱلۡأَوَّلُونَ ٤٨
Awa'ābā'unal-awwalūn
Au baba zetu wa zamani? 48
قُلۡ إِنَّ ٱلۡأَوَّلِينَ وَٱلۡأٓخِرِينَ ٤٩
Qul innal-awwalīna wal-ākhirīn
Sema: Hakika wa zamani na wa mwisho 49
لَمَجۡمُوعُونَ إِلَىٰ مِيقَٰتِ يَوۡمٖ مَّعۡلُومٖ ٥٠
Lamajmū'ūna ilā mīqāti yawmim ma'lūm
Bila ya shaka watakusanywa kwa wakati wa siku maalumu. 50
ثُمَّ إِنَّكُمۡ أَيُّهَا ٱلضَّآلُّونَ ٱلۡمُكَذِّبُونَ ٥١
Thumma innakum ayyuhad-dāllūnal-mukaddhibūn
Kisha nyinyi, mlio potea, mnao kanusha, 51
لَأٓكِلُونَ مِن شَجَرٖ مِّن زَقُّومٖ ٥٢
La'ākilūna min shajarim min zaqqūm
Kwa yakini mtakula mti wa Zaqqumu. 52
فَمَالِـُٔونَ مِنۡهَا ٱلۡبُطُونَ ٥٣
Famāli'ūna minhal-butūn
Na kwa mti huo mtajaza matumbo. 53
فَشَٰرِبُونَ عَلَيۡهِ مِنَ ٱلۡحَمِيمِ ٥٤
Fashāribūna 'alayhi minal-hamīm
Na juu yake mtakunywa maji yanayo chemka. 54
فَشَٰرِبُونَ شُرۡبَ ٱلۡهِيمِ ٥٥
Fashāribūna shurbal-hīm
Tena mtakunywa kama wanavyo kunywa ngamia wenye kiu. 55
هَٰذَا نُزُلُهُمۡ يَوۡمَ ٱلدِّينِ ٥٦
Hādhā nuzuluhum yawmad-dīn
Hiyo ndiyo karamu yao Siku ya Malipo. 56
نَحۡنُ خَلَقۡنَٰكُمۡ فَلَوۡلَا تُصَدِّقُونَ ٥٧
Nahnu khalaqnākum falawlā tusaddiqūn
Sisi tumekuumbeni; basi hamsadiki? 57
أَفَرَءَيۡتُم مَّا تُمۡنُونَ ٥٨
Afara'aytum mā tumnūn
Je! Mnaiona mbegu ya uzazi mnayo idondokeza? 58
ءَأَنتُمۡ تَخۡلُقُونَهُۥٓ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡخَٰلِقُونَ ٥٩
A'antum takhluqūnahū am nahnul-khāliqūn
Je! Mnaiumba nyinyi, au ni Sisi ndio Waumbaji? 59
نَحۡنُ قَدَّرۡنَا بَيۡنَكُمُ ٱلۡمَوۡتَ وَمَا نَحۡنُ بِمَسۡبُوقِينَ ٦٠
Nahnu qaddarnā baynakumul-mawta wamā nahnu bimasbūqīn
Sisi tumekuwekeeni mauti; na wala Sisi hatushindwi 60
عَلَىٰٓ أَن نُّبَدِّلَ أَمۡثَٰلَكُمۡ وَنُنشِئَكُمۡ فِي مَا لَا تَعۡلَمُونَ ٦١
'Alā an nubaddila amthālakum wanunshi'akum fī mā lā ta'lamūn
Kuwaleta wengine badala yenu na kukuumbeni nyinyi kwa umbo msilo lijua. 61
وَلَقَدۡ عَلِمۡتُمُ ٱلنَّشۡأَةَ ٱلۡأُولَىٰ فَلَوۡلَا تَذَكَّرُونَ ٦٢
Walaqad 'alimtumun-nash'atal-ūlā falawlā tadhakkarūn
Na bila ya shaka mlikwisha jua umbo la kwanza, basi kwa nini hamkumbuki? 62
أَفَرَءَيۡتُم مَّا تَحۡرُثُونَ ٦٣
Afara'aytum mā tahruthūn
Je! Mnaona makulima mnayo yapanda? 63
ءَأَنتُمۡ تَزۡرَعُونَهُۥٓ أَمۡ نَحۡنُ ٱلزَّٰرِعُونَ ٦٤
A'antum tazra'ūnahū am nahnuz-zāri'ūn
Je! Ni nyinyi mnayo yaotesha au ni Sisi ndio wenye kuotesha? 64
لَوۡ نَشَآءُ لَجَعَلۡنَٰهُ حُطَٰمٗا فَظَلۡتُمۡ تَفَكَّهُونَ ٦٥
Law nashā'u laja'alnāhu hutāman fazaltum tafakkahūn
Tungeli taka tungeli yafanya yakawa mapepe, mkabaki mnastaajabu, 65
إِنَّا لَمُغۡرَمُونَ ٦٦
Innā lamughramūn
Mkisema: Hakika sisi tumegharimika; 66
بَلۡ نَحۡنُ مَحۡرُومُونَ ٦٧
Bal nahnu mahrūmūn
Bali sisi tumenyimwa. 67
أَفَرَءَيۡتُمُ ٱلۡمَآءَ ٱلَّذِي تَشۡرَبُونَ ٦٨
Afara'aytumul-mā'al-ladhī tashrabūn
Je! Mnayaona maji mnayo yanywa? 68
ءَأَنتُمۡ أَنزَلۡتُمُوهُ مِنَ ٱلۡمُزۡنِ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡمُنزِلُونَ ٦٩
A'antum anzaltumūhu minal-muzni am nahnul-munzilūn
Je! Ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni au ni Sisi ndio wenye kuyateremsha? 69
لَوۡ نَشَآءُ جَعَلۡنَٰهُ أُجَاجٗا فَلَوۡلَا تَشۡكُرُونَ ٧٠
Law nashā'u ja'alnāhu ujājan falawlā tashkurūn
Tungeli penda tungeli yafanya ya chumvi. Basi mbona hamshukuru? 70
أَفَرَءَيۡتُمُ ٱلنَّارَ ٱلَّتِي تُورُونَ ٧١
Afara'aytumun-nāral-latī tūrūn
Je! Mnauona moto mnao uwasha? 71
ءَأَنتُمۡ أَنشَأۡتُمۡ شَجَرَتَهَآ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡمُنشِـُٔونَ ٧٢
A'antum ansha'tum shajaratahā am nahnul-munshi'ūn
Ni nyinyi mlio uumba mti wake au Sisi ndio Waumbaji? 72
نَحۡنُ جَعَلۡنَٰهَا تَذۡكِرَةٗ وَمَتَٰعٗا لِّلۡمُقۡوِينَ ٧٣
Nahnu ja'alnāhā tadhkiratan wamatā'al lil-muqwīn
Sisi tumeufanya uwe ni ukumbusho na manufaa kwa walioko nyikani. 73
فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ ٧٤
Fasabbih bismi rabbikal-'azīm
Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu. 74
۞ فَلَآ أُقۡسِمُ بِمَوَٰقِعِ ٱلنُّجُومِ ٧٥
Falā uqsimu bimawāqi'in-nujūm
Basi naapa kwa maanguko ya nyota, 75
وَإِنَّهُۥ لَقَسَمٞ لَّوۡ تَعۡلَمُونَ عَظِيمٌ ٧٦
Wa innahū laqasamul law ta'lamūna 'azīm
Na hakika bila ya shaka hichi ni kiapo kikubwa, laiti mngeli jua! 76
إِنَّهُۥ لَقُرۡءَانٞ كَرِيمٞ ٧٧
Innahū laqur'ānun karīm
Hakika hii bila ya shaka ni Qur'ani Tukufu, 77
فِي كِتَٰبٖ مَّكۡنُونٖ ٧٨
Fī kitābim maknūn
Katika Kitabu kilicho hifadhiwa. 78
لَّا يَمَسُّهُۥٓ إِلَّا ٱلۡمُطَهَّرُونَ ٧٩
Llā yamassuhū illal-mutahharūn
Hapana akigusaye ila walio takaswa. 79
تَنزِيلٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ٨٠
Tanzīlum mir rabbil-'ālamīn
Ni uteremsho unao toka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. 80
أَفَبِهَٰذَا ٱلۡحَدِيثِ أَنتُم مُّدۡهِنُونَ ٨١
Afabihādhal-hadīthi antum mudhinūn
Ni maneno haya ndiyo nyinyi mnayapuuza? 81
وَتَجۡعَلُونَ رِزۡقَكُمۡ أَنَّكُمۡ تُكَذِّبُونَ ٨٢
Wataj'alūna rizqakum annakum tukaddhibūn
Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha? 82
فَلَوۡلَآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلۡحُلۡقُومَ ٨٣
Falawlā idhā balaghatil-hulqūm
Yawaje basi itakapo fika roho kwenye koo, 83
وَأَنتُمۡ حِينَئِذٖ تَنظُرُونَ ٨٤
Wa antum hīna'idhin tanzurūn
Na nyinyi wakati huo mnatazama! 84
وَنَحۡنُ أَقۡرَبُ إِلَيۡهِ مِنكُمۡ وَلَٰكِن لَّا تُبۡصِرُونَ ٨٥
Wanahnu aqrabu ilayhi minkum walākil lā tubsirūn
Na Sisi tuko karibu zaidi naye kuliko nyinyi. 85
فَلَوۡلَآ إِن كُنتُمۡ غَيۡرَ مَدِينِينَ ٨٦
Falawlā in kuntum ghayra madīnīn
Na lau kuwa nyinyi hamumo katika mamlaka yangu, 86
تَرۡجِعُونَهَآ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ ٨٧
Tarji'ūnahā in kuntum sādiqīn
Kwanini hamuirudishi hiyo roho, ikiwa nyinyi mnasema kweli? 87
فَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُقَرَّبِينَ ٨٨
Fa ammā in kāna minal-muqarrabīn
Basi akiwa miongoni mwa walio karibishwa, 88
فَرَوۡحٞ وَرَيۡحَانٞ وَجَنَّتُ نَعِيمٖ ٨٩
Farawhun warayhānun wajannatu na'īm
Basi ni raha, na manukato, na Bustani zenye neema. 89
وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ ٩٠
Wa ammā in kāna min ashābil-yamīn
Na akiwa katika watu wa upande wa kulia, 90
فَسَلَٰمٞ لَّكَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ ٩١
Fasalāmul laka min ashābil-yamīn
Basi ni Salamu kwako uliye miongoni mwa watu wa upande wa kulia. 91
وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُكَذِّبِينَ ٱلضَّآلِّينَ ٩٢
Wa ammā in kāna minal-mukaddhibīnad-dāllīn
Na ama akiwa katika walio kadhibisha wapotovu, 92
فَنُزُلٞ مِّنۡ حَمِيمٖ ٩٣
Fanuzulum min hamīm
Basi karamu yake ni maji yanayo chemka, 93
وَتَصۡلِيَةُ جَحِيمٍ ٩٤
Watasliyatu jahīm
Na kutiwa Motoni. 94
إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ حَقُّ ٱلۡيَقِينِ ٩٥
Inna hādhā lahuwa haqqul-yaqīn
Hakika hii ndiyo haki yenye yakini. 95
فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ ٩٦
Fasabbih bismi rabbikal-'azīm
Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkubwa. 96
Nambari za maelezo ya chini zinaelekeza kwenye ukurasa wa aya, ambapo maelezo ya mfasiri yanaonyeshwa.
Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.
Surat Al-Waqi'ah ina aya 96. Ni sura namba 56 ya Qur'ani.
Surat Al-Waqi'ah ni sura Makkiya.
Surat Al-Waqi'ah iko katika juzuu 27.
Ndiyo. Bonyeza Cheza juu ya ukurasa huu, au anza kutoka aya yoyote. Programu ya Qabas pia inakuwezesha kuipakua ili kuisikiliza bila intaneti.