وَٱلنَّجۡمِ إِذَا هَوَىٰ ١
Wan-najmi idhā hawā
Naapa kwa nyota inapo tua! 1
Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
وَٱلنَّجۡمِ إِذَا هَوَىٰ ١
Wan-najmi idhā hawā
Naapa kwa nyota inapo tua! 1
مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمۡ وَمَا غَوَىٰ ٢
Mā dalla sāhibukum wamā ghawā
Mwenzenu huyu hakupotea, wala hakukosea. 2
وَمَا يَنطِقُ عَنِ ٱلۡهَوَىٰٓ ٣
Wamā yantiqu 'anil-hawā
Wala hatamki kwa matamanio. 3
إِنۡ هُوَ إِلَّا وَحۡيٞ يُوحَىٰ ٤
In huwa illā wahyun yūhā
Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa; . 4
عَلَّمَهُۥ شَدِيدُ ٱلۡقُوَىٰ ٥
'Allamahū shadīdul-quwā
Amemfundisha aliye mwingi wa nguvu! 5
ذُو مِرَّةٖ فَٱسۡتَوَىٰ ٦
Dhū mirratin fastawā
Mwenye kutua, akatulia! 6
وَهُوَ بِٱلۡأُفُقِ ٱلۡأَعۡلَىٰ ٧
Wahuwa bil-ufuqil-a'lā
Naye yuko juu kabisa upeo wa macho. 7
ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّىٰ ٨
Thumma danā fatadallā
Kisha akakaribia na akateremka. 8
فَكَانَ قَابَ قَوۡسَيۡنِ أَوۡ أَدۡنَىٰ ٩
Fakāna qāba qawsayni aw adnā
Akawa ni kama baina ya mipinde miwili, au karibu zaidi. 9
فَأَوۡحَىٰٓ إِلَىٰ عَبۡدِهِۦ مَآ أَوۡحَىٰ ١٠
Fa awhā ilā 'abdihī mā awhā
Akamfunulia mja wake (Mwenyezi Mungu) alicho mfunulia. 10
مَا كَذَبَ ٱلۡفُؤَادُ مَا رَأَىٰٓ ١١
Mā kadhabal-fu'ādu mā ra'ā
Moyo haukusema uwongo uliyo yaona. 11
أَفَتُمَٰرُونَهُۥ عَلَىٰ مَا يَرَىٰ ١٢
Afatumārūnahū 'alā mā yarā
Je! Mnabishana naye kwa aliyo yaona? 12
وَلَقَدۡ رَءَاهُ نَزۡلَةً أُخۡرَىٰ ١٣
Walaqad ra'āhu nazlatan ukhrā
Na akamwona mara nyingine, 13
عِندَ سِدۡرَةِ ٱلۡمُنتَهَىٰ ١٤
'Inda sidratil-muntahā
Penye Mkunazi wa mwisho. 14
عِندَهَا جَنَّةُ ٱلۡمَأۡوَىٰٓ ١٥
'Indahā jannatul-ma'wā
Karibu yake ndiyo ipo Bustani inayo kaliwa. 15
إِذۡ يَغۡشَى ٱلسِّدۡرَةَ مَا يَغۡشَىٰ ١٦
Idh yaghshas-sidrata mā yaghshā
Kilipo ufunika huo Mkunazi hicho kilicho ufunuika. 16
مَا زَاغَ ٱلۡبَصَرُ وَمَا طَغَىٰ ١٧
Mā zāghal-basaru wamā taghā
Jicho halikuhangaika wala halikuruka mpaka. 17
لَقَدۡ رَأَىٰ مِنۡ ءَايَٰتِ رَبِّهِ ٱلۡكُبۡرَىٰٓ ١٨
Laqad ra'ā min āyāti rabbihil-kubrā
Kwa yakini aliona katika Ishara kubwa kabisa za Mola wake Mlezi. 18
أَفَرَءَيۡتُمُ ٱللَّٰتَ وَٱلۡعُزَّىٰ ١٩
Afara'aytumul-lāta wal-'uzzā
Je! Mmemuona Lata na Uzza? 19
وَمَنَوٰةَ ٱلثَّالِثَةَ ٱلۡأُخۡرَىٰٓ ٢٠
Wamanawātath-thālithatal-ukhrā
Na Manaat, mwingine wa tatu? 20
أَلَكُمُ ٱلذَّكَرُ وَلَهُ ٱلۡأُنثَىٰ ٢١
Alakumudh-dhakaru walahul-unthā
Je! Nyinyi mnao wana wanaume na Yeye ndio awe na wanawake? 21
تِلۡكَ إِذٗا قِسۡمَةٞ ضِيزَىٰٓ ٢٢
Tilka idhan qismatun dīzā
Huo ni mgawanyo wa dhulma! 22
إِنۡ هِيَ إِلَّآ أَسۡمَآءٞ سَمَّيۡتُمُوهَآ أَنتُمۡ وَءَابَآؤُكُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلۡطَٰنٍۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَمَا تَهۡوَى ٱلۡأَنفُسُۖ وَلَقَدۡ جَآءَهُم مِّن رَّبِّهِمُ ٱلۡهُدَىٰٓ ٢٣
In hiya illā asmā'un sammaytumūhā antum wa ābā'ukum mā anzalallāhu bihā min sultānin in yattabi'ūna illaz-zanna wamā tahwal-anfusu walaqad jā'ahum mir rabbihimul-hudā
Hayo hayakuwa ila ni majina mliyo wapa nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuleta uthibitisho wowote juu ya hayo. Hawafuati ila dhana tu na kipendacho nafsi. Na kwa yakini uwongofu ulikwisha wafikia kutoka kwa Mola wao Mlezi. 23
أَمۡ لِلۡإِنسَٰنِ مَا تَمَنَّىٰ ٢٤
Am lil-insāni mā tamannā
Ati mtu anakipata kila anacho kitamani? 24
فَلِلَّهِ ٱلۡأٓخِرَةُ وَٱلۡأُولَىٰ ٢٥
Falillāhil-ākhiratu wal-ūlā
Mwenyezi Mungu tu ndiye Mwenye dunia na Akhera. 25
۞ وَكَم مِّن مَّلَكٖ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ لَا تُغۡنِي شَفَٰعَتُهُمۡ شَيۡـًٔا إِلَّا مِنۢ بَعۡدِ أَن يَأۡذَنَ ٱللَّهُ لِمَن يَشَآءُ وَيَرۡضَىٰٓ ٢٦
Wakam mim malakin fis-samāwāti lā tughnī shafā'atuhum shay'an illā mim ba'di an ya'dhanallāhu liman yashā'u wayardā
Na wako Malaika wangapi mbinguni, ambao uombezi wao hautafaa chochote isipo kuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia. 26
إِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ لَيُسَمُّونَ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ تَسۡمِيَةَ ٱلۡأُنثَىٰ ٢٧
Innal-ladhīna lā yu'minūna bil-ākhirati layusammūnal-malā'ikata tasmiyatal-unthā
Hakika wasio amini Akhera bila ya shaka wao ndio wanawaita Malaika kwa majina ya kike. 27
وَمَا لَهُم بِهِۦ مِنۡ عِلۡمٍۖ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّۖ وَإِنَّ ٱلظَّنَّ لَا يُغۡنِي مِنَ ٱلۡحَقِّ شَيۡـٔٗا ٢٨
Wamā lahum bihī min 'ilmin in yattabi'ūna illaz-zanna wa innaz-zanna lā yughnī minal-haqqi shay'ā
Nao hawana ujuzi wowote kwa hayo isipo kuwa wanafuata dhana tu. Na dhana haisaidii chochote mbele ya haki. 28
فَأَعۡرِضۡ عَن مَّن تَوَلَّىٰ عَن ذِكۡرِنَا وَلَمۡ يُرِدۡ إِلَّا ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا ٢٩
Fa a'rid 'am man tawallā 'an dhikrinā walam yurid illal-hayawātad-dunyā
Basi mwachilie mbali anaye upa kisogo ukumbusho wetu, na wala hataki ila maisha ya dunia. 29
ذَٰلِكَ مَبۡلَغُهُم مِّنَ ٱلۡعِلۡمِۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِمَنِ ٱهۡتَدَىٰ ٣٠
Dhālika mablaghuhum minal-'ilmi inna rabbaka huwa a'lamu biman dalla 'an sabīlihī wahuwa a'lamu bimanihtadā
Huo ndio mwisho wao wa ujuzi. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuipotea njia yake, na Yeye ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuongoka. 30
وَلِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ لِيَجۡزِيَ ٱلَّذِينَ أَسَٰٓـُٔواْ بِمَا عَمِلُواْ وَيَجۡزِيَ ٱلَّذِينَ أَحۡسَنُواْ بِٱلۡحُسۡنَى ٣١
Walillāhi mā fis-samāwāti wamā fil-ardi liyajziyal-ladhīna asā'ū bimā 'amilū wayajziyal-ladhīna ahsanū bil-husnā
Ni vya Mwenyezi Mungu vyote viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, ili awalipe walio tenda ubaya kwa waliyo yatenda, na walio tenda mema awalipe mema. 31
ٱلَّذِينَ يَجۡتَنِبُونَ كَبَٰٓئِرَ ٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡفَوَٰحِشَ إِلَّا ٱللَّمَمَۚ إِنَّ رَبَّكَ وَٰسِعُ ٱلۡمَغۡفِرَةِۚ هُوَ أَعۡلَمُ بِكُمۡ إِذۡ أَنشَأَكُم مِّنَ ٱلۡأَرۡضِ وَإِذۡ أَنتُمۡ أَجِنَّةٞ فِي بُطُونِ أُمَّهَٰتِكُمۡۖ فَلَا تُزَكُّوٓاْ أَنفُسَكُمۡۖ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَنِ ٱتَّقَىٰٓ ٣٢
Alladhīna yajtanibūna kabā'iral-ithmi wal-fawāhisha illal-lamama inna rabbaka wāsi'ul-maghfirati huwa a'lamu bikum idh ansha'akum minal-ardi wa idh antum ajinnatun fī butūni ummahātikum falā tuzakkū anfusakum huwa a'lamu bimanit-taqā
Ambao wanajiepusha na madhambi makuu na vitendo vichafu, isipo kuwa makosa khafifu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mkunjufu wa maghfira, naye anakujueni sana tangu alipo kuumbeni kutoka kwenye ardhi, na mlipo kuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msijisifu usafi. Yeye anamjua sana mwenye kujikinga na maovu. 32
أَفَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي تَوَلَّىٰ ٣٣
Afara'aytal-ladhī tawallā
Je! Umemwona yule aliye geuka? 33
وَأَعۡطَىٰ قَلِيلٗا وَأَكۡدَىٰٓ ٣٤
Wa a'tā qalīlan wa akdā
Na akatoa kidogo, kisha akajizuia? 34
أَعِندَهُۥ عِلۡمُ ٱلۡغَيۡبِ فَهُوَ يَرَىٰٓ ٣٥
A'indahū 'ilmul-ghaybi fahuwa yarā
Je! Anayo huyo ilimu ya ghaibu, basi ndio anaona? 35
أَمۡ لَمۡ يُنَبَّأۡ بِمَا فِي صُحُفِ مُوسَىٰ ٣٦
Am lam yunabba' bimā fī suhufi mūsā
Au hakuambiwa yaliyomo katika Vitabu vya Musa? 36
وَإِبۡرَٰهِيمَ ٱلَّذِي وَفَّىٰٓ ٣٧
Wa ibrāhīmal-ladhī waffā
Na vya Ibrahimu aliye timiza ahadi? 37
أَلَّا تَزِرُ وَازِرَةٞ وِزۡرَ أُخۡرَىٰ ٣٨
Allā taziru wāziratun wizra ukhrā
Ya kwamba hakika nafsi iliyo beba madhambi haibebi madhambi ya mwengine? 38
وَأَن لَّيۡسَ لِلۡإِنسَٰنِ إِلَّا مَا سَعَىٰ ٣٩
Wa al laysa lil-insāni illā mā sa'ā
Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyo yafanya mwenyewe? 39
وَأَنَّ سَعۡيَهُۥ سَوۡفَ يُرَىٰ ٤٠
Wa anna sa'yahū sawfa yurā
Na kwamba vitendo vyake vitaonekana? 40
ثُمَّ يُجۡزَىٰهُ ٱلۡجَزَآءَ ٱلۡأَوۡفَىٰ ٤١
Thumma yujzāhul-jazā'al-awfā
Kisha ndio atalipwa malipo yake kwa ukamilifu. 41
وَأَنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلۡمُنتَهَىٰ ٤٢
Wa anna ilā rabbikal-muntahā
Na kwamba kwao Mola wako Mlezi ndio mwisho. 42
وَأَنَّهُۥ هُوَ أَضۡحَكَ وَأَبۡكَىٰ ٤٣
Wa annahū huwa adhaka wa abkā
Na kwamba Yeye ndiye anaye leta kicheko na kilio. 43
وَأَنَّهُۥ هُوَ أَمَاتَ وَأَحۡيَا ٤٤
Wa annahū huwa amāta wa ahyā
Na kwamba Yeye ndiye anaye fisha na kuhuisha. 44
وَأَنَّهُۥ خَلَقَ ٱلزَّوۡجَيۡنِ ٱلذَّكَرَ وَٱلۡأُنثَىٰ ٤٥
Wa annahū khalaqaz-zawjaynidh-dhakara wal-unthā
Na kwamba Yeye ndiye aliye umba jozi, dume na jike 45
مِن نُّطۡفَةٍ إِذَا تُمۡنَىٰ ٤٦
Min nutfatin idhā tumnā
Kutokana na mbegu ya uzazi inapo miminwa. 46
وَأَنَّ عَلَيۡهِ ٱلنَّشۡأَةَ ٱلۡأُخۡرَىٰ ٤٧
Wa anna 'alayhin-nash'atal-ukhrā
Na kwamba ni juu yake ufufuo mwengine. 47
وَأَنَّهُۥ هُوَ أَغۡنَىٰ وَأَقۡنَىٰ ٤٨
Wa annahū huwa aghnā wa aqnā
Na kwamba ni Yeye ndiye anaye tosheleza na kukinaisha. 48
وَأَنَّهُۥ هُوَ رَبُّ ٱلشِّعۡرَىٰ ٤٩
Wa annahū huwa rabbush-shi'rā
Na kwamba hakika Yeye ndiye Mola Mlezi wa nyota ya Shii'ra. 49
وَأَنَّهُۥٓ أَهۡلَكَ عَادًا ٱلۡأُولَىٰ ٥٠
Wa annahū ahlaka 'ādanil-ūlā
Na kwamba Yeye ndiye aliye waangamiza A'di wa kwanza, 50
وَثَمُودَاْ فَمَآ أَبۡقَىٰ ٥١
Wathamūda famā abqā
Na Thamudi hakuwabakisha, 51
وَقَوۡمَ نُوحٖ مِّن قَبۡلُۖ إِنَّهُمۡ كَانُواْ هُمۡ أَظۡلَمَ وَأَطۡغَىٰ ٥٢
Waqawma nūhim min qablu innahum kānū hum azlama wa atghā
Na kabla yao kaumu ya Nuhu. Na hao hakika walikuwa ni madhaalimu zaidi, na waovu zaidi; 52
وَٱلۡمُؤۡتَفِكَةَ أَهۡوَىٰ ٥٣
Wal-mu'tafikata ahwā
Na miji iliyo pinduliwa, ni Yeye aliye ipindua. 53
فَغَشَّىٰهَا مَا غَشَّىٰ ٥٤
Faghasshāhā mā ghasshā
Vikaifunika vilivyo funika. 54
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكَ تَتَمَارَىٰ ٥٥
Fabi'ayyi ālā'i rabbika tatamārā
Basi neema gani ya Mola wako Mlezi unayo ifanyia shaka? 55
هَٰذَا نَذِيرٞ مِّنَ ٱلنُّذُرِ ٱلۡأُولَىٰٓ ٥٦
Hādhā nadhīrum minan-nudhuril-ūlā
Hili ni Onyo katika maonyo yale yale ya zamani. 56
أَزِفَتِ ٱلۡأٓزِفَةُ ٥٧
Azifatil-āzifah
Kiyama kimekaribia! 57
لَيۡسَ لَهَا مِن دُونِ ٱللَّهِ كَاشِفَةٌ ٥٨
Laysa lahā min dūnillāhi kāshifah
Hapana wa kukifichua isipo kuwa Mwenyezi Mungu. 58
أَفَمِنۡ هَٰذَا ٱلۡحَدِيثِ تَعۡجَبُونَ ٥٩
Afamin hādhal-hadīthi ta'jabūn
Je! Mnayastaajabia maneno haya? 59
وَتَضۡحَكُونَ وَلَا تَبۡكُونَ ٦٠
Watadhakūna walā tabkūn
Na mnacheka, wala hamlii? 60
وَأَنتُمۡ سَٰمِدُونَ ٦١
Wa antum sāmidūn
Nanyi mmeghafilika? 61
فَٱسۡجُدُواْۤ لِلَّهِۤ وَٱعۡبُدُواْ۩ ٦٢
Fasjudū lillāhi wa'budū
Basi msujudieni Mwenyezi Mungu, na mumuabudu. 62
Nambari za maelezo ya chini zinaelekeza kwenye ukurasa wa aya, ambapo maelezo ya mfasiri yanaonyeshwa.
Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.
Surat An-Najm ina aya 62. Ni sura namba 53 ya Qur'ani.
Surat An-Najm ni sura Makkiya.
Surat An-Najm iko katika juzuu 27.
Ndiyo. Bonyeza Cheza juu ya ukurasa huu, au anza kutoka aya yoyote. Programu ya Qabas pia inakuwezesha kuipakua ili kuisikiliza bila intaneti.