Surat Al-Qamar القمر

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

ٱقۡتَرَبَتِ ٱلسَّاعَةُ وَٱنشَقَّ ٱلۡقَمَرُ ١

Iqtarabatis-sā'atu wanshaqqal-qamar

Saa imekaribia, na mwezi umepasuka! 1

وَإِن يَرَوۡاْ ءَايَةٗ يُعۡرِضُواْ وَيَقُولُواْ سِحۡرٞ مُّسۡتَمِرّٞ ٢

Wa in yaraw āyatan yu'ridū wayaqūlū sihrum mustamirr

Na wakiona Ishara hugeuka upande na husema: Huu uchawi tu unazidi kuendelea. 2

وَكَذَّبُواْ وَٱتَّبَعُوٓاْ أَهۡوَآءَهُمۡۚ وَكُلُّ أَمۡرٖ مُّسۡتَقِرّٞ ٣

Wakaddhabū wattaba'ū ahwā'ahum wakullu amrim mustaqirr

Na wamekanusha na wamefuata matamanio yao. Na kila jambo ni lenye kuthibiti. 3

وَلَقَدۡ جَآءَهُم مِّنَ ٱلۡأَنۢبَآءِ مَا فِيهِ مُزۡدَجَرٌ ٤

Walaqad jā'ahum minal-ambā'i mā fīhi muzdajar

Na bila ya shaka zimewajia khabari zenye makaripio. 4

حِكۡمَةُۢ بَٰلِغَةٞۖ فَمَا تُغۡنِ ٱلنُّذُرُ ٥

Hikmatu bālighatun famā tughnin-nudhur

Hikima kaamili; lakini maonyo hayafai kitu! 5

فَتَوَلَّ عَنۡهُمۡۘ يَوۡمَ يَدۡعُ ٱلدَّاعِ إِلَىٰ شَيۡءٖ نُّكُرٍ ٦

Fatawalla 'anhum yawma yad'ud-dā'i ilā shay'in nukur

Basi jiepushe nao. Siku atakapo ita mwitaji kuliendea jambo linalo chusha; . 6

خُشَّعًا أَبۡصَٰرُهُمۡ يَخۡرُجُونَ مِنَ ٱلۡأَجۡدَاثِ كَأَنَّهُمۡ جَرَادٞ مُّنتَشِرٞ ٧

Khussha'an absāruhum yakhrujūna minal-ajdāthi ka annahum jarādum muntashir

Macho yao yatainama; watatoka makaburini kama nzige walio tawanyika! 7

مُّهۡطِعِينَ إِلَى ٱلدَّاعِۖ يَقُولُ ٱلۡكَٰفِرُونَ هَٰذَا يَوۡمٌ عَسِرٞ ٨

Mmuhti'īna ilad-dā'i yaqūlul-kāfirūna hādhā yawmun 'asir

Wanamkimbilia mwitaji, na makafiri wanasema: Hii ni siku ngumu. 8

۞ كَذَّبَتۡ قَبۡلَهُمۡ قَوۡمُ نُوحٖ فَكَذَّبُواْ عَبۡدَنَا وَقَالُواْ مَجۡنُونٞ وَٱزۡدُجِرَ ٩

Kaddhabat qablahum qawmu nūhin fakaddhabū 'abdanā waqālū majnūnun wazdujir

Kabla yao kaumu ya Nuhu walikanusha; wakamkanusha mja wetu, na wakasema ni mwendawazimu, na akakaripiwa. 9

فَدَعَا رَبَّهُۥٓ أَنِّي مَغۡلُوبٞ فَٱنتَصِرۡ ١٠

Fada'ā rabbahū annī maghlūbun fantasir

Basi akamwomba Mola wake Mlezi akasema: Kwa hakika mimi nimeshindwa, basi ninusuru! 10

فَفَتَحۡنَآ أَبۡوَٰبَ ٱلسَّمَآءِ بِمَآءٖ مُّنۡهَمِرٖ ١١

Fafatahnā abwābas-samā'i bimā'im munhamir

Basi tukaifungua milango ya mbingu kwa maji yanayo miminika. 11

وَفَجَّرۡنَا ٱلۡأَرۡضَ عُيُونٗا فَٱلۡتَقَى ٱلۡمَآءُ عَلَىٰٓ أَمۡرٖ قَدۡ قُدِرَ ١٢

Wafajjarnal-arda 'uyūnan fal-taqal-mā'u 'alā amrin qad qudir

Na tukazipasua ardhi kwa chemchem, yakakutana maji kwa jambo lilio kadiriwa. 12

وَحَمَلۡنَٰهُ عَلَىٰ ذَاتِ أَلۡوَٰحٖ وَدُسُرٖ ١٣

Wahamalnāhu 'alā dhāti alwāhin wadusur

Na tukamchukua kwenye safina ya mbao na kamba. 13

تَجۡرِي بِأَعۡيُنِنَا جَزَآءٗ لِّمَن كَانَ كُفِرَ ١٤

Tajrī bi a'yuninā jazā'al liman kāna kufir

Ikawa inakwenda kwa nadhari yetu, kuwa ni malipo kwa alivyo kuwa amekanushwa. 14

وَلَقَد تَّرَكۡنَٰهَآ ءَايَةٗ فَهَلۡ مِن مُّدَّكِرٖ ١٥

Walaqat taraknāhā āyatan fahal mim muddakir

Na bila ya shaka tuliiacha iwe ni Ishara. Lakini je, yupo anaye kumbuka? 15

فَكَيۡفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ ١٦

Fakayfa kāna 'adhābī wanudhur

Basi ilikuwaje adhabu yangu, na maonyo yangu. 16

وَلَقَدۡ يَسَّرۡنَا ٱلۡقُرۡءَانَ لِلذِّكۡرِ فَهَلۡ مِن مُّدَّكِرٖ ١٧

Walaqad yassarnal-qur'āna lidh-dhikri fahal mim muddakir

Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo anaye kumbuka? 17

كَذَّبَتۡ عَادٞ فَكَيۡفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ ١٨

Kaddhabat 'ādun fakayfa kāna 'adhābī wanudhur

Kina A'di walikanusha. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu? 18

إِنَّآ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ رِيحٗا صَرۡصَرٗا فِي يَوۡمِ نَحۡسٖ مُّسۡتَمِرّٖ ١٩

Innā arsalnā 'alayhim rīhan sarsaran fī yawmi nahsim mustamirr

Hakika Sisi tuliwapelekea upepo wa kimbunga katika siku korofi mfululizo, 19

تَنزِعُ ٱلنَّاسَ كَأَنَّهُمۡ أَعۡجَازُ نَخۡلٖ مُّنقَعِرٖ ٢٠

Tanzi'un-nāsa ka annahum a'jāzu nakhlim munqa'ir

Ukiwang'oa watu kama vigogo vya mitende vilio ng'olewa. 20

فَكَيۡفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ ٢١

Fakayfa kāna 'adhābī wanudhur

Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu? 21

وَلَقَدۡ يَسَّرۡنَا ٱلۡقُرۡءَانَ لِلذِّكۡرِ فَهَلۡ مِن مُّدَّكِرٖ ٢٢

Walaqad yassarnal-qur'āna lidh-dhikri fahal mim muddakir

Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani nyepesi kufahamika; lakini yupo anaye kumbuka? 22

كَذَّبَتۡ ثَمُودُ بِٱلنُّذُرِ ٢٣

Kaddhabat thamūdu bin-nudhur

Thamudi waliwakanusha Waonyaji. 23

فَقَالُوٓاْ أَبَشَرٗا مِّنَّا وَٰحِدٗا نَّتَّبِعُهُۥٓ إِنَّآ إِذٗا لَّفِي ضَلَٰلٖ وَسُعُرٍ ٢٤

Faqālū abasharam minnā wāhidan nattabi'uhū innā idhal lafī dalālin wasu'ur

Wakasema: Ati tumfuate binaadamu mmoja katika sisi? Basi hivyo sisi tutakuwa katika upotofu na kichaa! 24

أَءُلۡقِيَ ٱلذِّكۡرُ عَلَيۡهِ مِنۢ بَيۡنِنَا بَلۡ هُوَ كَذَّابٌ أَشِرٞ ٢٥

A'ulqiyadh-dhikru 'alayhi mim bayninā bal huwa kaddhābun ashir

Ni yeye tu aliye teremshiwa huo ukumbusho kati yetu sote? Bali huyu ni mwongo mwenye kiburi! 25

سَيَعۡلَمُونَ غَدٗا مَّنِ ٱلۡكَذَّابُ ٱلۡأَشِرُ ٢٦

Saya'lamūna ghadam manil-kaddhābul-ashir

Kesho watajua ni nani huyo mwongo mwenye kiburi. 26

إِنَّا مُرۡسِلُواْ ٱلنَّاقَةِ فِتۡنَةٗ لَّهُمۡ فَٱرۡتَقِبۡهُمۡ وَٱصۡطَبِرۡ ٢٧

Innā mursilun-nāqati fitnatal lahum fartaqibhum wastabir

Hakika Sisi tutawapelekea ngamia jike ili kuwajaribu, basi watazame tu na ustahamili. 27

وَنَبِّئۡهُمۡ أَنَّ ٱلۡمَآءَ قِسۡمَةُۢ بَيۡنَهُمۡۖ كُلُّ شِرۡبٖ مُّحۡتَضَرٞ ٢٨

Wanabbi'hum annal-mā'a qismatu baynahum kullu shirbim muhtadar

Na waambie kwamba maji yatagawanywa baina yao; kila sehemu ya maji itahudhuriwa na aliye khusika. 28

فَنَادَوۡاْ صَاحِبَهُمۡ فَتَعَاطَىٰ فَعَقَرَ ٢٩

Fanādaw sāhibahum fata'ātā fa'aqar

Basi wakamwita mtu wao akaja akamchinja. 29

فَكَيۡفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ ٣٠

Fakayfa kāna 'adhābī wanudhur

Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu! 30

إِنَّآ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ صَيۡحَةٗ وَٰحِدَةٗ فَكَانُواْ كَهَشِيمِ ٱلۡمُحۡتَظِرِ ٣١

Innā arsalnā 'alayhim sayhatan wāhidatan fakānū kahashīmil-muhtazir

Hakika Sisi tuliwapelekea ukelele mmoja tu, wakawa kama mabuwa ya kujengea uwa. 31

وَلَقَدۡ يَسَّرۡنَا ٱلۡقُرۡءَانَ لِلذِّكۡرِ فَهَلۡ مِن مُّدَّكِرٖ ٣٢

Walaqad yassarnal-qur'āna lidh-dhikri fahal mim muddakir

Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kwa kukumbuka, lakini yupo akumbukaye? 32

كَذَّبَتۡ قَوۡمُ لُوطِۭ بِٱلنُّذُرِ ٣٣

Kaddhabat qawmu lūti bin-nudhur

Kaumu Lut'i nao waliwakadhibisha Waonyaji. 33

إِنَّآ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ حَاصِبًا إِلَّآ ءَالَ لُوطٖۖ نَّجَّيۡنَٰهُم بِسَحَرٖ ٣٤

Innā arsalnā 'alayhim hāsiban illā āla lūtin najjaynāhum bisahar

Hakika Sisi tukawapelekea kimbunga cha vijiwe, isipo kuwa wafuasi wa Lut'i. Hao tuliwaokoa karibu na alfajiri. 34

نِّعۡمَةٗ مِّنۡ عِندِنَاۚ كَذَٰلِكَ نَجۡزِي مَن شَكَرَ ٣٥

Nni'matam min 'indinā kadhālika najzī man shakar

Kwa neema inayo toka kwetu. Hivyo ndivyo tumlipavyo anaye shukuru. 35

وَلَقَدۡ أَنذَرَهُم بَطۡشَتَنَا فَتَمَارَوۡاْ بِٱلنُّذُرِ ٣٦

Walaqad andharahum batshatanā fatamāraw bin-nudhur

Na hakika yeye aliwaonya adhabu yetu; lakini wao waliyatilia shaka hayo maonyo. 36

وَلَقَدۡ رَٰوَدُوهُ عَن ضَيۡفِهِۦ فَطَمَسۡنَآ أَعۡيُنَهُمۡ فَذُوقُواْ عَذَابِي وَنُذُرِ ٣٧

Walaqad rāwadūhu 'an dayfihī fatamasnā a'yunahum fadhūqū 'adhābī wanudhur

Na walimtaka awape wageni wake. Tukayapofua macho yao, na tukawaambia: Onjeni basi adhabu na maonyo yangu! 37

وَلَقَدۡ صَبَّحَهُم بُكۡرَةً عَذَابٞ مُّسۡتَقِرّٞ ٣٨

Walaqad sabbahahum bukratan 'adhābum mustaqirr

Na iliwafikia wakati wa asubuhi adhabu yangu ya kuendelea. 38

فَذُوقُواْ عَذَابِي وَنُذُرِ ٣٩

Fadhūqū 'adhābī wanudhur

Basi onjeni adhabu na maonyo yangu!< 39

وَلَقَدۡ يَسَّرۡنَا ٱلۡقُرۡءَانَ لِلذِّكۡرِ فَهَلۡ مِن مُّدَّكِرٖ ٤٠

Walaqad yassarnal-qur'āna lidh-dhikri fahal mim muddakir

Na hakika tumeisahilisha Qur'ani kuikumbuka. Lakini yupo anaye kumbuka? 40

وَلَقَدۡ جَآءَ ءَالَ فِرۡعَوۡنَ ٱلنُّذُرُ ٤١

Walaqad jā'a āla fir'awnan-nudhur

Na Waonyaji waliwafikia watu wa Firauni. 41

كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا كُلِّهَا فَأَخَذۡنَٰهُمۡ أَخۡذَ عَزِيزٖ مُّقۡتَدِرٍ ٤٢

Kaddhabū bi'āyātinā kullihā fa akhadhnāhum akhdha 'azīzim muqtadir

Walizikadhibisha Ishara zetu zote, nasi tukawashika kama anavyo shika Mwenye nguvu Mwenye uweza. 42

أَكُفَّارُكُمۡ خَيۡرٞ مِّنۡ أُوْلَٰٓئِكُمۡ أَمۡ لَكُم بَرَآءَةٞ فِي ٱلزُّبُرِ ٤٣

Akuffārukum khayrum min ulā'ikum am lakum barā'atun fiz-zubur

Je! Makafiri wenu ni bora kuliko hao, au yameandikwa vitabuni kuwa nyinyi hamtiwi makosani? 43

أَمۡ يَقُولُونَ نَحۡنُ جَمِيعٞ مُّنتَصِرٞ ٤٤

Am yaqūlūna nahnu jamī'um muntasir

Au ndio wanasema: Sisi ni wengi tutashinda tu. 44

سَيُهۡزَمُ ٱلۡجَمۡعُ وَيُوَلُّونَ ٱلدُّبُرَ ٤٥

Sayuhzamul-jam'u wayuwallūnad-dubur

Wingi wao huu utashindwa, na wao watasukumwa nyuma. 45

بَلِ ٱلسَّاعَةُ مَوۡعِدُهُمۡ وَٱلسَّاعَةُ أَدۡهَىٰ وَأَمَرُّ ٤٦

Balis-sā'atu maw'iduhum was-sā'atu adhā wa amarr

Bali Saa ya Kiyama ndio miadi yao, na Saa hiyo ni nzito zaidi na chungu zaidi. 46

إِنَّ ٱلۡمُجۡرِمِينَ فِي ضَلَٰلٖ وَسُعُرٖ ٤٧

Innal-mujrimīna fī dalālin wasu'ur

Hakika wakosefu wamo katika upotofu na wazimu. 47

يَوۡمَ يُسۡحَبُونَ فِي ٱلنَّارِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمۡ ذُوقُواْ مَسَّ سَقَرَ ٤٨

Yawma yushabūna fin-nāri 'alā wujūhihim dhūqū massa saqar

Siku watakapo kokotwa Motoni kifudifudi waambiwe: Onjeni mguso wa Jahannamu! 48

إِنَّا كُلَّ شَيۡءٍ خَلَقۡنَٰهُ بِقَدَرٖ ٤٩

Innā kulla shay'in khalaqnāhu biqadar

Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo. 49

وَمَآ أَمۡرُنَآ إِلَّا وَٰحِدَةٞ كَلَمۡحِۭ بِٱلۡبَصَرِ ٥٠

Wamā amrunā illā wāhidatun kalamhi bil-basar

Na amri yetu haikuwa ila ni moja tu, kama kupepesa jicho. 50

وَلَقَدۡ أَهۡلَكۡنَآ أَشۡيَاعَكُمۡ فَهَلۡ مِن مُّدَّكِرٖ ٥١

Walaqad ahlaknā ashyā'akum fahal mim muddakir

Na bila ya shaka tumekwisha waangamiza wenzenu. Lakini yupo anaye kumbuka? 51

وَكُلُّ شَيۡءٖ فَعَلُوهُ فِي ٱلزُّبُرِ ٥٢

Wakullu shay'in fa'alūhu fiz-zubur

Na kila jambo walilo lifanya limo vitabuni. 52

وَكُلُّ صَغِيرٖ وَكَبِيرٖ مُّسۡتَطَرٌ ٥٣

Wakullu saghīrin wakabīrim mustatar

Na kila kidogo na kikubwa kimeandikwa. 53

إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي جَنَّٰتٖ وَنَهَرٖ ٥٤

Innal-muttaqīna fī jannātin wanahar

Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na mito. 54

فِي مَقۡعَدِ صِدۡقٍ عِندَ مَلِيكٖ مُّقۡتَدِرِۭ ٥٥

Fī maq'adi sidqin 'inda malīkim muqtadir

Katika makalio ya haki kwa Mfalme Mwenye uweza. 55

Nambari za maelezo ya chini zinaelekeza kwenye ukurasa wa aya, ambapo maelezo ya mfasiri yanaonyeshwa.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Maswali

Surat Al-Qamar ina aya ngapi?

Surat Al-Qamar ina aya 55. Ni sura namba 54 ya Qur'ani.

Je, Surat Al-Qamar ni Makkiya au Madaniya?

Surat Al-Qamar ni sura Makkiya.

Surat Al-Qamar iko katika juzuu gani?

Surat Al-Qamar iko katika juzuu 27.

Je, naweza kusikiliza Surat Al-Qamar?

Ndiyo. Bonyeza Cheza juu ya ukurasa huu, au anza kutoka aya yoyote. Programu ya Qabas pia inakuwezesha kuipakua ili kuisikiliza bila intaneti.