Surat Adh-Dhariyat الذاريات

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلذَّٰرِيَٰتِ ذَرۡوٗا ١

Wadh-dhāriyāti dharwā

Naapa kwa pepo zinazo tawanya! 1

فَٱلۡحَٰمِلَٰتِ وِقۡرٗا ٢

Fal-hāmilāti wiqrā

Na zinazo beba mizigo! 2

فَٱلۡجَٰرِيَٰتِ يُسۡرٗا ٣

Fal-jāriyāti yusrā

Na zinazo kwenda kwa wepesi. 3

فَٱلۡمُقَسِّمَٰتِ أَمۡرًا ٤

Fal-muqassimāti amrā

Na zinazo gawanya kwa amri! 4

إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَصَادِقٞ ٥

Innamā tū'adūna lasādiq

Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka ni kweli! 5

وَإِنَّ ٱلدِّينَ لَوَٰقِعٞ ٦

Wa innad-dīna lawāqi'

Na kwa hakika malipo bila ya shaka yatatokea. 6

وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلۡحُبُكِ ٧

Was-samā'i dhātil-hubuk

Naapa kwa mbingu zenye njia! 7

إِنَّكُمۡ لَفِي قَوۡلٖ مُّخۡتَلِفٖ ٨

Innakum lafī qawlim mukhtalif

Hakika nyinyi bila ya shaka mmo katika kauli inayo khitalifiana. 8

يُؤۡفَكُ عَنۡهُ مَنۡ أُفِكَ ٩

Yu'faku 'anhu man ufik

Anageuzwa kutokana na haki mwenye kugeuzwa. 9

قُتِلَ ٱلۡخَرَّٰصُونَ ١٠

Qutilal-kharrāsūn

Wazushi wameangamizwa. 10

ٱلَّذِينَ هُمۡ فِي غَمۡرَةٖ سَاهُونَ ١١

Alladhīna hum fī ghamratin sāhūn

Ambao wameghafilika katika ujinga. 11

يَسۡـَٔلُونَ أَيَّانَ يَوۡمُ ٱلدِّينِ ١٢

Yas'alūna ayyāna yawmud-dīn

Wanauliza: Ni lini hiyo siku ya malipo? 12

يَوۡمَ هُمۡ عَلَى ٱلنَّارِ يُفۡتَنُونَ ١٣

Yawma hum 'alan-nāri yuftanūn

Hiyo ni siku watakayo adhibiwa Motoni. 13

ذُوقُواْ فِتۡنَتَكُمۡ هَٰذَا ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تَسۡتَعۡجِلُونَ ١٤

Dhūqū fitnatakum hādhal-ladhī kuntum bihī tasta'jilūn

Onjeni adhabu yenu! Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyahimiza. 14

إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي جَنَّٰتٖ وَعُيُونٍ ١٥

Innal-muttaqīna fī jannātin wa'uyūn

Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem. 15

ءَاخِذِينَ مَآ ءَاتَىٰهُمۡ رَبُّهُمۡۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَبۡلَ ذَٰلِكَ مُحۡسِنِينَ ١٦

Ākhidhīna mā ātāhum rabbuhum innahum kānū qabla dhālika muhsinīn

Wanapokea aliyo wapa Mola wao Mlezi. Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya wakifanya mema. 16

كَانُواْ قَلِيلٗا مِّنَ ٱلَّيۡلِ مَا يَهۡجَعُونَ ١٧

Kānū qalīlam minal-layli mā yahja'ūn

Walikuwa wakilala kidogo tu usiku. 17

وَبِٱلۡأَسۡحَارِ هُمۡ يَسۡتَغۡفِرُونَ ١٨

Wabil-ashāri hum yastaghfirūn

Na kabla ya alfajiri wakiomba maghfira. 18

وَفِيٓ أَمۡوَٰلِهِمۡ حَقّٞ لِّلسَّآئِلِ وَٱلۡمَحۡرُومِ ١٩

Wafī amwālihim haqqul lis-sā'ili wal-mahrūm

Na katika mali yao ipo haki ya mwenye kuomba na asiye omba. 19

وَفِي ٱلۡأَرۡضِ ءَايَٰتٞ لِّلۡمُوقِنِينَ ٢٠

Wafil-ardi āyātul lil-mūqinīn

Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini. 20

وَفِيٓ أَنفُسِكُمۡۚ أَفَلَا تُبۡصِرُونَ ٢١

Wafī anfusikum afalā tubsirūn

Na pia katika nafsi zenu - Je! Hamwoni? 21

وَفِي ٱلسَّمَآءِ رِزۡقُكُمۡ وَمَا تُوعَدُونَ ٢٢

Wafis-samā'i rizqukum wamā tū'adūn

Na katika mbingu ziko riziki zenu na mliyo ahidiwa. 22

فَوَرَبِّ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ إِنَّهُۥ لَحَقّٞ مِّثۡلَ مَآ أَنَّكُمۡ تَنطِقُونَ ٢٣

Fawarabbis-samā'i wal-ardi innahū lahaqqum mithla mā annakum tantiqūn

Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, hakika haya ni kweli kama ilivyo kweli kuwa nyinyi mnasema. 23

هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ضَيۡفِ إِبۡرَٰهِيمَ ٱلۡمُكۡرَمِينَ ٢٤

Hal atāka hadīthu dayfi ibrāhīmal-mukramīn

Je! Imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanao hishimiwa? 24

إِذۡ دَخَلُواْ عَلَيۡهِ فَقَالُواْ سَلَٰمٗاۖ قَالَ سَلَٰمٞ قَوۡمٞ مُّنكَرُونَ ٢٥

Idh dakhalū 'alayhi faqālū salāman qāla salāmun qawmum munkarūn

Walipo ingia kwake wakasema: Salama! Na yeye akasema: Salama! Nyinyi ni watu nisio kujueni. 25

فَرَاغَ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ فَجَآءَ بِعِجۡلٖ سَمِينٖ ٢٦

Farāgha ilā ahlihī fajā'a bi'ijlin samīn

Akenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliye nona. 26

فَقَرَّبَهُۥٓ إِلَيۡهِمۡ قَالَ أَلَا تَأۡكُلُونَ ٢٧

Faqarrabahū ilayhim qāla alā ta'kulūn

Akawakaribisha, akasema: Mbona hamli? 27

فَأَوۡجَسَ مِنۡهُمۡ خِيفَةٗۖ قَالُواْ لَا تَخَفۡۖ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَٰمٍ عَلِيمٖ ٢٨

Fa awjasa minhum khīfatan qālū lā takhaf wabassharūhu bighulāmin 'alīm

Akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: Usiwe na khofu, nao wakambashiria kupata kijana mwenye ilimu. 28

فَأَقۡبَلَتِ ٱمۡرَأَتُهُۥ فِي صَرَّةٖ فَصَكَّتۡ وَجۡهَهَا وَقَالَتۡ عَجُوزٌ عَقِيمٞ ٢٩

Fa aqbalatimra'atuhū fī sarratin fasakkat wajhahā waqālat 'ajūzun 'aqīm

Ndipo mkewe akawaelekea, na huku anasema na akijipiga usoni kwa mastaajabu, na kusema: Mimi ni kikongwe na tasa! 29

قَالُواْ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡحَكِيمُ ٱلۡعَلِيمُ ٣٠

Qālū kadhāliki qāla rabbuki innahū huwal-hakīmul-'alīm

Wakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyo sema Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mwenye kujua. 30

۞ قَالَ فَمَا خَطۡبُكُمۡ أَيُّهَا ٱلۡمُرۡسَلُونَ ٣١

Qāla famā khatbukum ayyuhal-mursalūn

AKASEMA: Basi ujumbe wenu ni nini, enyi mlio tumwa? 31

قَالُوٓاْ إِنَّآ أُرۡسِلۡنَآ إِلَىٰ قَوۡمٖ مُّجۡرِمِينَ ٣٢

Qālū innā ursilnā ilā qawmim mujrimīn

Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa watu wakosefu, 32

لِنُرۡسِلَ عَلَيۡهِمۡ حِجَارَةٗ مِّن طِينٖ ٣٣

Linursila 'alayhim hijāratam min tīn

Tuwatupie mawe ya udongo, 33

مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ لِلۡمُسۡرِفِينَ ٣٤

Mmusawwamatan 'inda rabbika lil-musrifīn

Yaliyo tiwa alama kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa ajili ya wanao pindukia mipaka. 34

فَأَخۡرَجۡنَا مَن كَانَ فِيهَا مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ٣٥

Fa akhrajnā man kāna fīhā minal-mu'minīn

Kwa hivyo tutawatoa katika hao wale walio amini. 35

فَمَا وَجَدۡنَا فِيهَا غَيۡرَ بَيۡتٖ مِّنَ ٱلۡمُسۡلِمِينَ ٣٦

Famā wajadnā fīhā ghayra baytim minal-muslimīn

Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu! 36

وَتَرَكۡنَا فِيهَآ ءَايَةٗ لِّلَّذِينَ يَخَافُونَ ٱلۡعَذَابَ ٱلۡأَلِيمَ ٣٧

Wataraknā fīhā āyatal lilladhīna yakhāfūnal-'adhābal-alīm

Na tukaacha humo Ishara kwa ajili ya wanao iogopa adhabu chungu. 37

وَفِي مُوسَىٰٓ إِذۡ أَرۡسَلۡنَٰهُ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ بِسُلۡطَٰنٖ مُّبِينٖ ٣٨

Wafī mūsā idh arsalnāhu ilā fir'awna bisultānim mubīn

Na katika khabari za Musa, tulipo mtuma kwa Firauni na hoja wazi. 38

فَتَوَلَّىٰ بِرُكۡنِهِۦ وَقَالَ سَٰحِرٌ أَوۡ مَجۡنُونٞ ٣٩

Fatawallā biruknihī waqāla sāhirun aw majnūn

Lakini alipuuza kwa sababu ya nguvu zake na akasema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu! 39

فَأَخَذۡنَٰهُ وَجُنُودَهُۥ فَنَبَذۡنَٰهُمۡ فِي ٱلۡيَمِّ وَهُوَ مُلِيمٞ ٤٠

Fa akhadhnāhu wajunūdahū fanabadhnāhum fil-yammi wahuwa mulīm

Basi tukamkamata yeye na majeshi yake na tukawatupa baharini, na yeye ndiye wa kulaumiwa. 40

وَفِي عَادٍ إِذۡ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمُ ٱلرِّيحَ ٱلۡعَقِيمَ ٤١

Wafī 'ādin idh arsalnā 'alayhimur-rīhal-'aqīm

Na katika khabari za A'di tulipo wapelekea upepo wa kukata uzazi. 41

مَا تَذَرُ مِن شَيۡءٍ أَتَتۡ عَلَيۡهِ إِلَّا جَعَلَتۡهُ كَٱلرَّمِيمِ ٤٢

Mā tadharu min shay'in atat 'alayhi illā ja'alathu kar-ramīm

Haukuacha chochote ulicho kifikia ila ulikifanya kama kilio nyambuka. 42

وَفِي ثَمُودَ إِذۡ قِيلَ لَهُمۡ تَمَتَّعُواْ حَتَّىٰ حِينٖ ٤٣

Wafī thamūda idh qīla lahum tamatta'ū hattā hīn

Na katika khabari za Thamudi walipo ambiwa: Jifurahisheni kwa muda mdogo tu. 43

فَعَتَوۡاْ عَنۡ أَمۡرِ رَبِّهِمۡ فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّٰعِقَةُ وَهُمۡ يَنظُرُونَ ٤٤

Fa'ataw 'an amri rabbihim fa akhadhathumus-sā'iqatu wahum yanzurūn

Wakaasi amri ya Mola wao Mlezi. Basi uliwanyakua moto wa radi nao wanaona. 44

فَمَا ٱسۡتَطَٰعُواْ مِن قِيَامٖ وَمَا كَانُواْ مُنتَصِرِينَ ٤٥

Famastatā'ū min qiyāmin wamā kānū muntasirīn

Basi hawakuweza kusimama wala hawakuwa wenye kujitetea. 45

وَقَوۡمَ نُوحٖ مِّن قَبۡلُۖ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَوۡمٗا فَٰسِقِينَ ٤٦

Waqawma nūhim min qablu innahum kānū qawman fāsiqīn

Na kaumu ya Nuhu hapo mbele. Hakika hao walikuwa watu wapotovu. 46

وَٱلسَّمَآءَ بَنَيۡنَٰهَا بِأَيۡيْدٖ وَإِنَّا لَمُوسِعُونَ ٤٧

Was-samā'a banaynāhā bi aydin wa innā lamūsi'ūn

Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio twenye uwezo wa kuzitanua. 47

وَٱلۡأَرۡضَ فَرَشۡنَٰهَا فَنِعۡمَ ٱلۡمَٰهِدُونَ ٤٨

Wal-arda farashnāhā fani'mal-māhidūn

Na ardhi tumeitandaza; basi watandazaji wazuri namna gani Sisi! 48

وَمِن كُلِّ شَيۡءٍ خَلَقۡنَا زَوۡجَيۡنِ لَعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ ٤٩

Wamin kulli shay'in khalaqnā zawjayni la'allakum tadhakkarūn

Na katika kila kitu tumeumba kwa jozi ili mzingatie. 49

فَفِرُّوٓاْ إِلَى ٱللَّهِۖ إِنِّي لَكُم مِّنۡهُ نَذِيرٞ مُّبِينٞ ٥٠

Fafirrū ilallāhi innī lakum minhu nadhīrum mubīn

Basi kimbilieni kwa Mwenyezi Mungu, hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake. 50

وَلَا تَجۡعَلُواْ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَۖ إِنِّي لَكُم مِّنۡهُ نَذِيرٞ مُّبِينٞ ٥١

Walā taj'alū ma'allāhi ilāhan ākhara innī lakum minhu nadhīrum mubīn

Wala msifanye kuwa kuna mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake. 51

كَذَٰلِكَ مَآ أَتَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا قَالُواْ سَاحِرٌ أَوۡ مَجۡنُونٌ ٥٢

Kadhālika mā atal-ladhīna min qablihim mir rasūlin illā qālū sāhirun aw majnūn

Basi ndio hivyo hivyo, hakuwajia kabla yao Mtume ila walisema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu. 52

أَتَوَاصَوۡاْ بِهِۦۚ بَلۡ هُمۡ قَوۡمٞ طَاغُونَ ٥٣

Atawāsaw bihī bal hum qawmun tāghūn

Je! Wameambizana kwa haya? Bali hawa ni watu waasi. 53

فَتَوَلَّ عَنۡهُمۡ فَمَآ أَنتَ بِمَلُومٖ ٥٤

Fatawalla 'anhum famā anta bimalūm

Basi waachilie mbali, nawe hulaumiwi. 54

وَذَكِّرۡ فَإِنَّ ٱلذِّكۡرَىٰ تَنفَعُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ٥٥

Wadhakkir fa innadh-dhikrā tanfa'ul-mu'minīn

Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini. 55

وَمَا خَلَقۡتُ ٱلۡجِنَّ وَٱلۡإِنسَ إِلَّا لِيَعۡبُدُونِ ٥٦

Wamā khalaqtul-jinna wal-insa illā liya'budūn

Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi. 56

مَآ أُرِيدُ مِنۡهُم مِّن رِّزۡقٖ وَمَآ أُرِيدُ أَن يُطۡعِمُونِ ٥٧

Mā urīdu minhum mir rizqin wamā urīdu an yut'imūn

Na sitaki kwao riziki, wala sitaki wanilishe.Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti. 57

إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلرَّزَّاقُ ذُو ٱلۡقُوَّةِ ٱلۡمَتِينُ ٥٨

Innallāha huwar-razzāqu dhul-quwwatil-matīn

Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti. 58

فَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُواْ ذَنُوبٗا مِّثۡلَ ذَنُوبِ أَصۡحَٰبِهِمۡ فَلَا يَسۡتَعۡجِلُونِ ٥٩

Fa inna lilladhīna zalamū dhanūbam mithla dhanūbi ashābihim falā yasta'jilūn

Hakika walio dhulumu wana fungu lao la adhabu kama fungu la wenzao. Basi wasinihimize. 59

فَوَيۡلٞ لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن يَوۡمِهِمُ ٱلَّذِي يُوعَدُونَ ٦٠

Fawaylul lilladhīna kafarū min yawmihimul-ladhī yū'adūn

Ole wao walio ikanusha siku yao waliyo ahidiwa. 60

Nambari za maelezo ya chini zinaelekeza kwenye ukurasa wa aya, ambapo maelezo ya mfasiri yanaonyeshwa.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Aya maarufu

Maswali

Surat Adh-Dhariyat ina aya ngapi?

Surat Adh-Dhariyat ina aya 60. Ni sura namba 51 ya Qur'ani.

Je, Surat Adh-Dhariyat ni Makkiya au Madaniya?

Surat Adh-Dhariyat ni sura Makkiya.

Surat Adh-Dhariyat iko katika juzuu gani?

Surat Adh-Dhariyat iko katika juzuu 26, 27.

Je, naweza kusikiliza Surat Adh-Dhariyat?

Ndiyo. Bonyeza Cheza juu ya ukurasa huu, au anza kutoka aya yoyote. Programu ya Qabas pia inakuwezesha kuipakua ili kuisikiliza bila intaneti.