قٓۚ وَٱلۡقُرۡءَانِ ٱلۡمَجِيدِ ١
Qāf wal-qur'ānil-majīd
Qaaf. Naapa kwa Qur'ani tukufu! 1
Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
قٓۚ وَٱلۡقُرۡءَانِ ٱلۡمَجِيدِ ١
Qāf wal-qur'ānil-majīd
Qaaf. Naapa kwa Qur'ani tukufu! 1
بَلۡ عَجِبُوٓاْ أَن جَآءَهُم مُّنذِرٞ مِّنۡهُمۡ فَقَالَ ٱلۡكَٰفِرُونَ هَٰذَا شَيۡءٌ عَجِيبٌ ٢
Bal 'ajibū an jā'ahum mundhirum minhum faqālal-kāfirūna hādhā shay'un 'ajīb
Bali wanastaajabu kwamba amewafikia mwonyaji kutoka miongoni mwao, na wakasema makafiri: Hili ni jambo la ajabu! 2
أَءِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابٗاۖ ذَٰلِكَ رَجۡعُۢ بَعِيدٞ ٣
A'idhā mitnā wakunnā turāban dhālika raj'u ba'īd
Ati tukifa na tukawa udongo? Kurejea huko kuko mbali! 3
قَدۡ عَلِمۡنَا مَا تَنقُصُ ٱلۡأَرۡضُ مِنۡهُمۡۖ وَعِندَنَا كِتَٰبٌ حَفِيظُۢ ٤
Qad 'alimnā mā tanqusul-ardu minhum wa'indanā kitābun hafīz
Hakika Sisi tunajua kiasi cha kila kinacho punguzwa na ardhi kutokana nao. Na kwetu kipo Kitabu kinacho hifadhi yote. 4
بَلۡ كَذَّبُواْ بِٱلۡحَقِّ لَمَّا جَآءَهُمۡ فَهُمۡ فِيٓ أَمۡرٖ مَّرِيجٍ ٥
Bal kaddhabū bil-haqqi lammā jā'ahum fahum fī amrim marīj
Lakini waliikanusha Haki ilipo wajia; kwa hivyo wamo katika mambo ya mkorogo. 5
أَفَلَمۡ يَنظُرُوٓاْ إِلَى ٱلسَّمَآءِ فَوۡقَهُمۡ كَيۡفَ بَنَيۡنَٰهَا وَزَيَّنَّٰهَا وَمَا لَهَا مِن فُرُوجٖ ٦
Afalam yanzurū ilas-samā'i fawqahum kayfa banaynāhā wazayyannāhā wamā lahā min furūj
Je! Hawaangalii mbingu zilizo juu yao! Vipi tulivyo zijenga, na tukazipamba. Wala hazina nyufa. 6
وَٱلۡأَرۡضَ مَدَدۡنَٰهَا وَأَلۡقَيۡنَا فِيهَا رَوَٰسِيَ وَأَنۢبَتۡنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوۡجِۭ بَهِيجٖ ٧
Wal-arda madadnāhā wa alqaynā fīhā rawāsiya wa ambatnā fīhā min kulli zawji bahīj
Na ardhi tumeitandaza na tukaiwekea milima, na tukaiotesha mimea mizuri ya kila namna. 7
تَبۡصِرَةٗ وَذِكۡرَىٰ لِكُلِّ عَبۡدٖ مُّنِيبٖ ٨
Tabsiratan wadhikrā likulli 'abdim munīb
Yawe haya ni kifumbua macho na ukumbusho kwa kila mja mwenye kuelekea. 8
وَنَزَّلۡنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ مُّبَٰرَكٗا فَأَنۢبَتۡنَا بِهِۦ جَنَّٰتٖ وَحَبَّ ٱلۡحَصِيدِ ٩
Wanazzalnā minas-samā'i mā'am mubārakan fa ambatnā bihī jannātin wahabbal-hasīd
Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji yaliyo barikiwa, na kwa hayo tukaotesha mabustani na nafaka za kuvunwa. 9
وَٱلنَّخۡلَ بَاسِقَٰتٖ لَّهَا طَلۡعٞ نَّضِيدٞ ١٠
Wan-nakhla bāsiqātil lahā tal'un nadīd
Na mitende mirefu yenye makole yaliyo zaa kwa wingi, 10
رِّزۡقٗا لِّلۡعِبَادِۖ وَأَحۡيَيۡنَا بِهِۦ بَلۡدَةٗ مَّيۡتٗاۚ كَذَٰلِكَ ٱلۡخُرُوجُ ١١
Rrizqal lil-'ibādi wa ahyaynā bihī baldatam maytan kadhālikal-khurūj
Ili iwe ni riziki kwa waja wangu. Na tukaifufua kwa maji nchi iliyo kuwa imekufa. Kama hivyo ndivyo utakavyo kuwa ufufuaji. 11
كَذَّبَتۡ قَبۡلَهُمۡ قَوۡمُ نُوحٖ وَأَصۡحَٰبُ ٱلرَّسِّ وَثَمُودُ ١٢
Kaddhabat qablahum qawmu nūhin wa ashābur-rassi wathamūd
Kabla yao walikadhibisha kaumu ya Nuhu na wakaazi wa Rassi na Thamudi. 12
وَعَادٞ وَفِرۡعَوۡنُ وَإِخۡوَٰنُ لُوطٖ ١٣
Wa'ādun wafir'awnu wa ikhwānu lūt
Na A'di na Firauni na kaumu ya Lut'i. 13
وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡأَيۡكَةِ وَقَوۡمُ تُبَّعٖۚ كُلّٞ كَذَّبَ ٱلرُّسُلَ فَحَقَّ وَعِيدِ ١٤
Wa ashābul-aykati waqawmu tubba'in kullun kaddhabar-rusula fahaqqa wa'īd
Na wakaazi wa Machakani, na watu wa Tubbaa'. Wote hao waliwakanusha Mitume, kwa hivyo onyo likathibitika juu yao. 14
أَفَعَيِينَا بِٱلۡخَلۡقِ ٱلۡأَوَّلِۚ بَلۡ هُمۡ فِي لَبۡسٖ مِّنۡ خَلۡقٖ جَدِيدٖ ١٥
Afa'ayīnā bil-khalqil-awwali bal hum fī labsim min khalqin jadīd
Kwani tulichoka kwa kuumba mara ya kwanza. Bali wao wamo katika shaka tu juu ya umbo jipya. 15
وَلَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ وَنَعۡلَمُ مَا تُوَسۡوِسُ بِهِۦ نَفۡسُهُۥۖ وَنَحۡنُ أَقۡرَبُ إِلَيۡهِ مِنۡ حَبۡلِ ٱلۡوَرِيدِ ١٦
Walaqad khalaqnal-insāna wana'lamu mā tuwaswisu bihī nafsuhū wanahnu aqrabu ilayhi min hablil-warīd
Na hakika tumemuumba mtu, nasi tunayajua yanayo mpitikia katika nafsi yake. Na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake. 16
إِذۡ يَتَلَقَّى ٱلۡمُتَلَقِّيَانِ عَنِ ٱلۡيَمِينِ وَعَنِ ٱلشِّمَالِ قَعِيدٞ ١٧
Idh yatalaqqal-mutalaqqiyāni 'anil-yamīni wa'anish-shimāli qa'īd
Wanapo pokea wapokeaji wawili, wanao kaa kuliani na kushotoni. 17
مَّا يَلۡفِظُ مِن قَوۡلٍ إِلَّا لَدَيۡهِ رَقِيبٌ عَتِيدٞ ١٨
Mmā yalfizu min qawlin illā ladayhi raqībun 'atīd
Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari. 18
وَجَآءَتۡ سَكۡرَةُ ٱلۡمَوۡتِ بِٱلۡحَقِّۖ ذَٰلِكَ مَا كُنتَ مِنۡهُ تَحِيدُ ١٩
Wajā'at sakratul-mawti bil-haqqi dhālika mā kunta minhu tahīd
Na uchungu wa kutoka roho utamjia kwa haki. Hayo ndiyo uliyo kuwa ukiyakimbia. 19
وَنُفِخَ فِي ٱلصُّورِۚ ذَٰلِكَ يَوۡمُ ٱلۡوَعِيدِ ٢٠
Wanufikha fis-sūri dhālika yawmul-wa'īd
Na litapulizwa baragumu. Hiyo ndiyo Siku ya Miadi. 20
وَجَآءَتۡ كُلُّ نَفۡسٖ مَّعَهَا سَآئِقٞ وَشَهِيدٞ ٢١
Wajā'at kullu nafsim ma'ahā sā'iqun washahīd
Na kila nafsi itakuja na pamoja nayo mchungaji na shahidi. 21
لَّقَدۡ كُنتَ فِي غَفۡلَةٖ مِّنۡ هَٰذَا فَكَشَفۡنَا عَنكَ غِطَآءَكَ فَبَصَرُكَ ٱلۡيَوۡمَ حَدِيدٞ ٢٢
Llaqad kunta fī ghaflatim min hādhā fakashafnā 'anka ghitā'aka fabasarukal-yawma hadīd
(Aambiwe): Kwa hakika ulikuwa umeghafilika na haya; basi leo tumekuondolea pazia lako, na kwa hivyo kuona kwako leo ni kukali. 22
وَقَالَ قَرِينُهُۥ هَٰذَا مَا لَدَيَّ عَتِيدٌ ٢٣
Waqāla qarīnuhū hādhā mā ladayya 'atīd
Na mwenzake atasema: Huyu niliye naye mimi kesha tayarishwa. 23
أَلۡقِيَا فِي جَهَنَّمَ كُلَّ كَفَّارٍ عَنِيدٖ ٢٤
Alqiyā fī jahannama kulla kaffārin 'anīd
Mtupeni katika Jahannamu kila kafiri mwenye inda, 24
مَّنَّاعٖ لِّلۡخَيۡرِ مُعۡتَدٖ مُّرِيبٍ ٢٥
Mmannā'il lil-khayri mu'tadim murīb
Akatazaye kheri, arukaye mipaka, mwenye kutia shaka, 25
ٱلَّذِي جَعَلَ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَ فَأَلۡقِيَاهُ فِي ٱلۡعَذَابِ ٱلشَّدِيدِ ٢٦
Alladhī ja'ala ma'allāhi ilāhan ākhara fa alqiyāhu fil-'adhābish-shadīd
Aliye weka mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi mtupeni katika adhabu kali. 26
۞ قَالَ قَرِينُهُۥ رَبَّنَا مَآ أَطۡغَيۡتُهُۥ وَلَٰكِن كَانَ فِي ضَلَٰلِۭ بَعِيدٖ ٢٧
Qāla qarīnuhū rabbanā mā atghaytuhū walākin kāna fī dalāli ba'īd
Mwenzake aseme: Ee Mola wetu Mlezi! Sikumpoteza mimi, bali yeye mwenyewe alikuwa katika upotovu wa mbali. 27
قَالَ لَا تَخۡتَصِمُواْ لَدَيَّ وَقَدۡ قَدَّمۡتُ إِلَيۡكُم بِٱلۡوَعِيدِ ٢٨
Qāla lā takhtasimū ladayya waqad qaddamtu ilaykum bil-wa'īd
(Mwenyezi Mungu) aseme: Msigombane mbele yangu. Nilikuleteeni mbele onyo langu. 28
مَا يُبَدَّلُ ٱلۡقَوۡلُ لَدَيَّ وَمَآ أَنَا۠ بِظَلَّٰمٖ لِّلۡعَبِيدِ ٢٩
Mā yubaddalul-qawlu ladayya wamā ana bizallāmil lil-'abīd
Mbele yangu haibadilishwi kauli, wala Mimi siwadhulumu waja wangu. 29
يَوۡمَ نَقُولُ لِجَهَنَّمَ هَلِ ٱمۡتَلَأۡتِ وَتَقُولُ هَلۡ مِن مَّزِيدٖ ٣٠
Yawma naqūlu lijahannama halimtala'ti wataqūlu hal mim mazīd
Siku tutapo iambia Jahannamu: Je! Umejaa? Nayo itasema: Je! Kuna ziada? 30
وَأُزۡلِفَتِ ٱلۡجَنَّةُ لِلۡمُتَّقِينَ غَيۡرَ بَعِيدٍ ٣١
Wa uzlifatil-jannatu lil-muttaqīna ghayra ba'īd
Na Pepo italetwa karibu kwa ajili ya wachamngu, haitakuwa mbali. 31
هَٰذَا مَا تُوعَدُونَ لِكُلِّ أَوَّابٍ حَفِيظٖ ٣٢
Hādhā mā tū'adūna likulli awwābin hafīz
Haya ndiyo mnayo ahidiwa kwa kila mwenye kurejea kwa Mwenyezi Mungu na akajilinda. 32
مَّنۡ خَشِيَ ٱلرَّحۡمَٰنَ بِٱلۡغَيۡبِ وَجَآءَ بِقَلۡبٖ مُّنِيبٍ ٣٣
Mman khashiyar-rahmāna bil-ghaybi wajā'a biqalbim munīb
Mwenye kumwogopa Mwingi wa Rehema hali kuwa hamwoni, na akaja kwa moyo ulio elekea 33
ٱدۡخُلُوهَا بِسَلَٰمٖۖ ذَٰلِكَ يَوۡمُ ٱلۡخُلُودِ ٣٤
Udkhulūhā bisalāmin dhālika yawmul-khulūd
(Ataambiwa) ingieni kwa salama. Hiyo ndiyo siku ya daima dawamu. 34
لَهُم مَّا يَشَآءُونَ فِيهَا وَلَدَيۡنَا مَزِيدٞ ٣٥
Lahum mā yashā'ūna fīhā waladaynā mazīd
Humo watapata wakitakacho, na kwetu yako ya ziada. 35
وَكَمۡ أَهۡلَكۡنَا قَبۡلَهُم مِّن قَرۡنٍ هُمۡ أَشَدُّ مِنۡهُم بَطۡشٗا فَنَقَّبُواْ فِي ٱلۡبِلَٰدِ هَلۡ مِن مَّحِيصٍ ٣٦
Wakam ahlaknā qablahum min qarnin hum ashaddu minhum batshan fanaqqabū fil-bilādi hal mim mahīs
Na kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao walio kuwa na nguvu zaidi kuliko hawa! Nao walitanga tanga katika nchi nyingi. Je! Walipata pa kukimbilia? 36
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَذِكۡرَىٰ لِمَن كَانَ لَهُۥ قَلۡبٌ أَوۡ أَلۡقَى ٱلسَّمۡعَ وَهُوَ شَهِيدٞ ٣٧
Inna fī dhālika ladhikrā liman kāna lahū qalbun aw alqas-sam'a wahuwa shahīd
Hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia. 37
وَلَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ وَمَا مَسَّنَا مِن لُّغُوبٖ ٣٨
Walaqad khalaqnas-samāwāti wal-arda wamā baynahumā fī sittati ayyāmin wamā massanā mil lughūb
Na bila ya shaka Sisi tumeziumba mbingu na ardhi na vilio baina yao mnamo siku sita; na wala hayakutugusa machofu. 38
فَٱصۡبِرۡ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ قَبۡلَ طُلُوعِ ٱلشَّمۡسِ وَقَبۡلَ ٱلۡغُرُوبِ ٣٩
Fasbir 'alā mā yaqūlūna wasabbih bihamdi rabbika qabla tulū'ish-shamsi waqablal-ghurūb
Basi vumilia kwa hayo wasemayo, na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuchwa. 39
وَمِنَ ٱلَّيۡلِ فَسَبِّحۡهُ وَأَدۡبَٰرَ ٱلسُّجُودِ ٤٠
Waminal-layli fasabbihhu wa adbāras-sujūd
Na katika usiku pia mtakase, na baada ya kusujudu. 40
وَٱسۡتَمِعۡ يَوۡمَ يُنَادِ ٱلۡمُنَادِ مِن مَّكَانٖ قَرِيبٖ ٤١
Wastami' yawma yunādil-munādi mim makānin qarīb
Na sikiliza siku atapo nadi mwenye kunadi kutoka pahala karibu. 41
يَوۡمَ يَسۡمَعُونَ ٱلصَّيۡحَةَ بِٱلۡحَقِّۚ ذَٰلِكَ يَوۡمُ ٱلۡخُرُوجِ ٤٢
Yawma yasma'ūnas-sayhata bil-haqqi dhālika yawmul-khurūj
Siku watakapo sikia ukelele wa haki. Hiyo ndiyo siku ya kufufuka. 42
إِنَّا نَحۡنُ نُحۡيِۦ وَنُمِيتُ وَإِلَيۡنَا ٱلۡمَصِيرُ ٤٣
Innā nahnu nuhyī wanumītu wa ilaynal-masīr
Hakika Sisi tunahuisha na tunafisha, na kwetu Sisi ndio marejeo. 43
يَوۡمَ تَشَقَّقُ ٱلۡأَرۡضُ عَنۡهُمۡ سِرَاعٗاۚ ذَٰلِكَ حَشۡرٌ عَلَيۡنَا يَسِيرٞ ٤٤
Yawma tashaqqaqul-ardu 'anhum sirā'an dhālika hashrun 'alaynā yasīr
Siku itapo wapasukia ardhi mbio mbio! Mkusanyo huo kwetu ni mwepesi. 44
نَّحۡنُ أَعۡلَمُ بِمَا يَقُولُونَۖ وَمَآ أَنتَ عَلَيۡهِم بِجَبَّارٖۖ فَذَكِّرۡ بِٱلۡقُرۡءَانِ مَن يَخَافُ وَعِيدِ ٤٥
Nnahnu a'lamu bimā yaqūlūna wamā anta 'alayhim bijabbārin fadhakkir bil-qur'āni man yakhāfu wa'īd
Sisi tunajua kabisa wayasemayo. Wala wewe si mwenye kuwatawalia kwa ujabari. Basi mkumbushe kwa Qur'ani anaye liogopa onyo. 45
Nambari za maelezo ya chini zinaelekeza kwenye ukurasa wa aya, ambapo maelezo ya mfasiri yanaonyeshwa.
Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.
Surat Qaf ina aya 45. Ni sura namba 50 ya Qur'ani.
Surat Qaf ni sura Makkiya.
Surat Qaf iko katika juzuu 26.
Ndiyo. Bonyeza Cheza juu ya ukurasa huu, au anza kutoka aya yoyote. Programu ya Qabas pia inakuwezesha kuipakua ili kuisikiliza bila intaneti.