فَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُواْ ذَنُوبٗا مِّثۡلَ ذَنُوبِ أَصۡحَٰبِهِمۡ فَلَا يَسۡتَعۡجِلُونِ ٥٩
Fa inna lilladhīna zalamū dhanūbam mithla dhanūbi ashābihim falā yasta'jilūn
Hakika walio dhulumu wana fungu lao la adhabu kama fungu la wenzao. Basi wasinihimize. 59
Maelezo ya chini
59 Hakika hao walio jidhulumu nafsi zao kwa ukafiri na kukanusha wana fungu lao la adhabu mfano wa fungu la wenzao katika kaumu zilizo kwisha pita. Basi wasifanye haraka kuhimiza adhabu ishuke kabla ya wakati wake.