Surat Ad-Dukhan الدخان

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

حمٓ ١

Hā Mīm

H'a Mim . 1

وَٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡمُبِينِ ٢

Wal-kitābil-mubīn

Naapa kwa Kitabu kinacho bainisha! 2

إِنَّآ أَنزَلۡنَٰهُ فِي لَيۡلَةٖ مُّبَٰرَكَةٍۚ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ ٣

Innā anzalnāhu fī laylatim mubārakatin innā kunnā mundhirīn

Hakika tumekiteremsha katika usiku ulio barikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji. 3

فِيهَا يُفۡرَقُ كُلُّ أَمۡرٍ حَكِيمٍ ٤

Fīhā yufraqu kullu amrin hakīm

Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikima! 4

أَمۡرٗا مِّنۡ عِندِنَآۚ إِنَّا كُنَّا مُرۡسِلِينَ ٥

Amram min 'indinā innā kunnā mursilīn

Jambo litokalo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma. 5

رَحۡمَةٗ مِّن رَّبِّكَۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ ٦

Rahmatam mir rabbika innahū huwas-samī'ul-'alīm

Ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kujua. 6

رَبِّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَآۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ ٧

Rabbis-samāwāti wal-ardi wamā baynahumā in kuntum mūqinīn

Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, ikiwa nyinyi mna yakini. 7

لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۖ رَبُّكُمۡ وَرَبُّ ءَابَآئِكُمُ ٱلۡأَوَّلِينَ ٨

Lā ilāha illā huwa yuhyī wayumītu rabbukum warabbu ābā'ikumul-awwalīn

Hakuna mungu ila Yeye; anahuisha na anafisha- Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa mwanzo. 8

بَلۡ هُمۡ فِي شَكّٖ يَلۡعَبُونَ ٩

Bal hum fī shakkin yal'abūn

Lakini wao wanacheza katika shaka. 9

فَٱرۡتَقِبۡ يَوۡمَ تَأۡتِي ٱلسَّمَآءُ بِدُخَانٖ مُّبِينٖ ١٠

Fartaqib yawma ta'tis-samā'u bidukhānim mubīn

Basi ingoje siku ambayo mbingu zitakapo leta moshi ulio dhaahiri, 10

يَغۡشَى ٱلنَّاسَۖ هَٰذَا عَذَابٌ أَلِيمٞ ١١

Yaghshan-nāsa hādhā 'adhābun alīm

Utakao wafunika watu: Hii ni adhabu chungu! 11

رَّبَّنَا ٱكۡشِفۡ عَنَّا ٱلۡعَذَابَ إِنَّا مُؤۡمِنُونَ ١٢

Rrabbanakshif 'annal-'adhāba innā mu'minūn

Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini. 12

أَنَّىٰ لَهُمُ ٱلذِّكۡرَىٰ وَقَدۡ جَآءَهُمۡ رَسُولٞ مُّبِينٞ ١٣

Annā lahumudh-dhikrā waqad jā'ahum rasūlum mubīn

Nini faida ya kukumbuka kwao? Na alikwisha wafikia Mtume mwenye kubainisha. 13

ثُمَّ تَوَلَّوۡاْ عَنۡهُ وَقَالُواْ مُعَلَّمٞ مَّجۡنُونٌ ١٤

Thumma tawallaw 'anhu waqālū mu'allamum majnūn

Na wao wakamgeuzia uso, na wakasema: Huyu amefunzwa, naye ni mwendawazimu. 14

إِنَّا كَاشِفُواْ ٱلۡعَذَابِ قَلِيلًاۚ إِنَّكُمۡ عَآئِدُونَ ١٥

Innā kāshiful-'adhābi qalīlan innakum 'ā'idūn

Hakika sisi tutaiondoa adhabu kidogo, lakini nyinyi kwa yakini mtarejea vile vile! 15

يَوۡمَ نَبۡطِشُ ٱلۡبَطۡشَةَ ٱلۡكُبۡرَىٰٓ إِنَّا مُنتَقِمُونَ ١٦

Yawma nabtishul-batshatal-kubrā innā muntaqimūn

Siku tutayo yashambulia mashambulio makubwa, bila ya shaka Sisi ni wenye kutesa. 16

۞ وَلَقَدۡ فَتَنَّا قَبۡلَهُمۡ قَوۡمَ فِرۡعَوۡنَ وَجَآءَهُمۡ رَسُولٞ كَرِيمٌ ١٧

Walaqad fatannā qablahum qawma fir'awna wajā'ahum rasūlun karīm

Na hakika kabla ya hawa tuliwafanyia mtihani watu wa Firauni, na aliwafikia Mtume Mtukufu. 17

أَنۡ أَدُّوٓاْ إِلَيَّ عِبَادَ ٱللَّهِۖ إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٞ ١٨

An addū ilayya 'ibādallāhi innī lakum rasūlun amīn

Akasema: Nipeni waja wa Mwenyezi Mungu; kwa hakika mimi kwenu ni Mtume Muaminifu. 18

وَأَن لَّا تَعۡلُواْ عَلَى ٱللَّهِۖ إِنِّيٓ ءَاتِيكُم بِسُلۡطَٰنٖ مُّبِينٖ ١٩

Wa al lā ta'lū 'alallāhi innī ātīkum bisultānim mubīn

Na msimfanyie kiburi Mwenyezi Mungu; hakika mimi nitakuleteeni uthibitisho ulio wazi. 19

وَإِنِّي عُذۡتُ بِرَبِّي وَرَبِّكُمۡ أَن تَرۡجُمُونِ ٢٠

Wa innī 'udhtu birabbī warabbikum an tarjumūn

Nami najikinga kwa Mola wangu Mlezi na ndiye Mola wenu Mlezi pia, ili msinipige mawe. 20

وَإِن لَّمۡ تُؤۡمِنُواْ لِي فَٱعۡتَزِلُونِ ٢١

Wa il lam tu'minū lī fa'tazilūn

Na ikiwa hamniamini, basi jitengeni nami. 21

فَدَعَا رَبَّهُۥٓ أَنَّ هَٰٓؤُلَآءِ قَوۡمٞ مُّجۡرِمُونَ ٢٢

Fada'ā rabbahū anna hā'ulā'i qawmum mujrimūn

Ndipo akamwomba Mola wake Mlezi: Hakika watu hawa ni wakosefu. 22

فَأَسۡرِ بِعِبَادِي لَيۡلًا إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ ٢٣

Fa asri bi'ibādī laylan innakum muttaba'ūn

Mwenyezi Mungu akasema: Basi nenda na waja wangu usiku. Kwa yakini mtafuatwa. 23

وَٱتۡرُكِ ٱلۡبَحۡرَ رَهۡوًاۖ إِنَّهُمۡ جُندٞ مُّغۡرَقُونَ ٢٤

Watrukil-bahra rahwan innahum jundum mughraqūn

Na iache bahari vivyo hivyo imeachana, hakika wao hao ni jeshi litakalo zamishwa. 24

كَمۡ تَرَكُواْ مِن جَنَّٰتٖ وَعُيُونٖ ٢٥

Kam tarakū min jannātin wa'uyūn

Mabustani mangapi, na chemchem ngapi waliziacha! 25

وَزُرُوعٖ وَمَقَامٖ كَرِيمٖ ٢٦

Wazurū'in wamaqāmin karīm

Na mimea na vyeo vitukufu! 26

وَنَعۡمَةٖ كَانُواْ فِيهَا فَٰكِهِينَ ٢٧

Wana'matin kānū fīhā fākihīn

Na neema walizo kuwa wakijistareheshea! 27

كَذَٰلِكَۖ وَأَوۡرَثۡنَٰهَا قَوۡمًا ءَاخَرِينَ ٢٨

Kadhālika wa awrathnāhā qawman ākharīn

Ndio hivyo! Na tukawarithisha haya watu wenginewe. 28

فَمَا بَكَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلسَّمَآءُ وَٱلۡأَرۡضُ وَمَا كَانُواْ مُنظَرِينَ ٢٩

Famā bakat 'alayhimus-samā'u wal-ardu wamā kānū munzarīn

La mbingu wala ardhi hazikuwalilia, wala hawakupewa muhula. 29

وَلَقَدۡ نَجَّيۡنَا بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ مِنَ ٱلۡعَذَابِ ٱلۡمُهِينِ ٣٠

Walaqad najjaynā banī isrā'īla minal-'adhābil-muhīn

Na bila ya shaka tuliwaokoa Wana wa Israili katika adhabu ya kuwadhalilisha, 30

مِن فِرۡعَوۡنَۚ إِنَّهُۥ كَانَ عَالِيٗا مِّنَ ٱلۡمُسۡرِفِينَ ٣١

Min fir'awna innahū kāna 'āliyam minal-musrifīn

Ya Firauni. Hakika yeye alikuwa jeuri katika wenye kupindukia mipaka. 31

وَلَقَدِ ٱخۡتَرۡنَٰهُمۡ عَلَىٰ عِلۡمٍ عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ ٣٢

Walaqadikhtarnāhum 'alā 'ilmin 'alal-'ālamīn

Na tuliwakhiari kwa ujuzi wetu kuliko walimwengu wenginewe. 32

وَءَاتَيۡنَٰهُم مِّنَ ٱلۡأٓيَٰتِ مَا فِيهِ بَلَٰٓؤٞاْ مُّبِينٌ ٣٣

Wa ātaynāhum minal-āyāti mā fīhi balā'um mubīn

Na tukawapa katika ishara zenye majaribio yaliyo wazi. 33

إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ لَيَقُولُونَ ٣٤

Inna hā'ulā'i layaqūlūn

Hakika hawa wanasema: 34

إِنۡ هِيَ إِلَّا مَوۡتَتُنَا ٱلۡأُولَىٰ وَمَا نَحۡنُ بِمُنشَرِينَ ٣٥

In hiya illā mawtatunal-ūlā wamā nahnu bimunsharīn

Hapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatufufuliwi. 35

فَأۡتُواْ بِـَٔابَآئِنَآ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ ٣٦

Fa tū bi'ābā'inā in kuntum sādiqīn

Basi warudisheni baba zetu, ikiwa nyinyi mnasema kweli. 36

أَهُمۡ خَيۡرٌ أَمۡ قَوۡمُ تُبَّعٖ وَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ أَهۡلَكۡنَٰهُمۡۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ مُجۡرِمِينَ ٣٧

Ahum khayrun am qawmu tubba'in walladhīna min qablihim ahlaknāhum innahum kānū mujrimīn

Je! Ni wao bora au watu wa Tubbaa' na walio kuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wakosefu. 37

وَمَا خَلَقۡنَا ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَا لَٰعِبِينَ ٣٨

Wamā khalaqnas-samāwāti wal-arda wamā baynahumā lā'ibīn

Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo baina yake kwa mchezo. 38

مَا خَلَقۡنَٰهُمَآ إِلَّا بِٱلۡحَقِّ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ ٣٩

Mā khalaqnāhumā illā bil-haqqi walākinna aktharahum lā ya'lamūn

Hatukuviumba hivyo ila kwa Haki, lakini wengi wao hawajui. 39

إِنَّ يَوۡمَ ٱلۡفَصۡلِ مِيقَٰتُهُمۡ أَجۡمَعِينَ ٤٠

Inna yawmal-fasli mīqātuhum ajma'īn

Hakika siku ya Uamuzi ni wakati ulio wekwa kwa wao wote. 40

يَوۡمَ لَا يُغۡنِي مَوۡلًى عَن مَّوۡلٗى شَيۡـٔٗا وَلَا هُمۡ يُنصَرُونَ ٤١

Yawma lā yughnī mawlan 'am mawlan shay'an walā hum yunsarūn

Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote, wala hawatanusuriwa. 41

إِلَّا مَن رَّحِمَ ٱللَّهُۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ ٤٢

Illā mar rahimallāhu innahū huwal-'azīzur-rahīm

Isipo kuwa atakaye mrehemu Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. 42

إِنَّ شَجَرَتَ ٱلزَّقُّومِ ٤٣

Inna shajarataz-zaqqūm

Hakika Mti wa Zaqqum, 43

طَعَامُ ٱلۡأَثِيمِ ٤٤

Ta'āmul-athīm

Ni chakula cha mwenye dhambi. 44

كَٱلۡمُهۡلِ يَغۡلِي فِي ٱلۡبُطُونِ ٤٥

Kal-muhli yaghlī fil-butūn

Kama shaba iliyo yayushwa, hutokota matumboni 45

كَغَلۡيِ ٱلۡحَمِيمِ ٤٦

Kaghalyil-hamīm

Kama kutokota kwa maji ya moto. 46

خُذُوهُ فَٱعۡتِلُوهُ إِلَىٰ سَوَآءِ ٱلۡجَحِيمِ ٤٧

Khudhūhu fa'tilūhu ilā sawā'il-jahīm

(Itasemwa:) Mkamateni na mtupeni katikati ya Jahannamu! 47

ثُمَّ صُبُّواْ فَوۡقَ رَأۡسِهِۦ مِنۡ عَذَابِ ٱلۡحَمِيمِ ٤٨

Thumma subbū fawqa ra'sihī min 'adhābil-hamīm

Kisha mmwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji yanayo chemka. 48

ذُقۡ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡكَرِيمُ ٤٩

Dhuq innaka antal-'azīzul-karīm

Onja! Ati wewe ndiye mwenye nguvu, mtukufu! 49

إِنَّ هَٰذَا مَا كُنتُم بِهِۦ تَمۡتَرُونَ ٥٠

Inna hādhā mā kuntum bihī tamtarūn

Hakika haya ndiyo mliyo kuwa mkiyatilia shaka. 50

إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي مَقَامٍ أَمِينٖ ٥١

Innal-muttaqīna fī maqāmin amīn

Hakika wachamngu watakuwa katika mahali pa amani, 51

فِي جَنَّٰتٖ وَعُيُونٖ ٥٢

Fī jannātin wa'uyūn

Katika mabustani na chemchem, 52

يَلۡبَسُونَ مِن سُندُسٖ وَإِسۡتَبۡرَقٖ مُّتَقَٰبِلِينَ ٥٣

Yalbasūna min sundusin wa istabraqim mutaqābilīn

Watavaa hariri nyepesi na hariri nzito wakikabiliana, 53

كَذَٰلِكَ وَزَوَّجۡنَٰهُم بِحُورٍ عِينٖ ٥٤

Kadhālika wazawwajnāhum bihūrin 'īn

Hivi ndivyo itakavyo kuwa, na tutawaoza mahurilaini. 54

يَدۡعُونَ فِيهَا بِكُلِّ فَٰكِهَةٍ ءَامِنِينَ ٥٥

Yad'ūna fīhā bikulli fākihatin āminīn

Humo watataka kila aina ya matunda, na wakae kwa amani. 55

لَا يَذُوقُونَ فِيهَا ٱلۡمَوۡتَ إِلَّا ٱلۡمَوۡتَةَ ٱلۡأُولَىٰۖ وَوَقَىٰهُمۡ عَذَابَ ٱلۡجَحِيمِ ٥٦

Lā yadhūqūna fīhal-mawta illal-mawtatal-ūlā wawaqāhum 'adhābal-jahīm

Humo hawataonja mauti ila mauti yale ya kwanza, na (Mwenyezi Mungu) atawalinda na adhabu ya Jahannamu, 56

فَضۡلٗا مِّن رَّبِّكَۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ ٥٧

Fadlam mir rabbika dhālika huwal-fawzul-'azīm

Kuwa ni fadhila zitokazo kwa Mola wako Mlezi. Huko ndiko kufuzu kukubwa. 57

فَإِنَّمَا يَسَّرۡنَٰهُ بِلِسَانِكَ لَعَلَّهُمۡ يَتَذَكَّرُونَ ٥٨

Fa innamā yassarnāhu bilisānika la'allahum yatadhakkarūn

Basi tumeifanya nyepesi hii Qur'ani kwa ulimi wako, ili wapate kukumbuka. 58

فَٱرۡتَقِبۡ إِنَّهُم مُّرۡتَقِبُونَ ٥٩

Fartaqib innahum murtaqibūn

Ngoja tu, na wao wangoje pia. 59

Nambari za maelezo ya chini zinaelekeza kwenye ukurasa wa aya, ambapo maelezo ya mfasiri yanaonyeshwa.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Maswali

Surat Ad-Dukhan ina aya ngapi?

Surat Ad-Dukhan ina aya 59. Ni sura namba 44 ya Qur'ani.

Je, Surat Ad-Dukhan ni Makkiya au Madaniya?

Surat Ad-Dukhan ni sura Makkiya.

Surat Ad-Dukhan iko katika juzuu gani?

Surat Ad-Dukhan iko katika juzuu 25.

Je, naweza kusikiliza Surat Ad-Dukhan?

Ndiyo. Bonyeza Cheza juu ya ukurasa huu, au anza kutoka aya yoyote. Programu ya Qabas pia inakuwezesha kuipakua ili kuisikiliza bila intaneti.