إِنۡ هِيَ إِلَّا مَوۡتَتُنَا ٱلۡأُولَىٰ وَمَا نَحۡنُ بِمُنشَرِينَ ٣٥
In hiya illā mawtatunal-ūlā wamā nahnu bimunsharīn
Hapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatufufuliwi. 35
Maelezo ya chini
35 Hakika hawa wanao kadhibisha kufufuliwa bila ya shaka wanasema: Hapana kufa ila kwa haya haya mauti yetu ya kwanza ya duniani, wala sisi hatutafufuliwa tena.