إِنَّآ أَنزَلۡنَٰهُ فِي لَيۡلَةٖ مُّبَٰرَكَةٍۚ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ ٣
Innā anzalnāhu fī laylatim mubārakatin innā kunnā mundhirīn
Hakika tumekiteremsha katika usiku ulio barikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji. 3
Maelezo ya chini
3 Hakika Sisi tumeanza kuiteremsha Qur'ani katika usiku ulio jaa kheri, wenye baraka nyingi, kwani ni mwendo wetu kuonya kwa kuwatuma Mitume na kuteremsha Vitabu.