۞ وَلَقَدۡ فَتَنَّا قَبۡلَهُمۡ قَوۡمَ فِرۡعَوۡنَ وَجَآءَهُمۡ رَسُولٞ كَرِيمٌ ١٧
Walaqad fatannā qablahum qawma fir'awna wajā'ahum rasūlun karīm
Na hakika kabla ya hawa tuliwafanyia mtihani watu wa Firauni, na aliwafikia Mtume Mtukufu. 17
Maelezo ya chini
17 Na bila ya shaka tulikwisha wafanyia mtihani, kabla ya makafiri wa Makka, kaumu ya Firauni kwa kuwaitia kwenye Imani, na akawajia Musa, Mtume Mtukufu kwa Mwenyezi Mungu. Wakamkataa kwa inda tu. Na huo ndio mtindo wa hawa washirikina.