إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي مَقَامٍ أَمِينٖ ٥١
Innal-muttaqīna fī maqāmin amīn
Hakika wachamngu watakuwa katika mahali pa amani, 51
Maelezo ya chini
51 Hakika hao ambao wamejikinga nafsi zao na maasi kwa kufuata ut'iifu wa Mwenyezi Mungu wapo pahala patukufu ambapo ndani yake wao wanajipatia amani kwa nafsi zao.