Surat Al-Qiyamah القيامة

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

لَآ أُقۡسِمُ بِيَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ ١

Lā uqsimu biyawmil-qiyāmah

Ninaapa kwa Siku ya Kiyama! 1

وَلَآ أُقۡسِمُ بِٱلنَّفۡسِ ٱللَّوَّامَةِ ٢

Walā uqsimu bin-nafsil-lawwāmah

Na ninaapa kwa nafsi inayo jilaumu! 2

أَيَحۡسَبُ ٱلۡإِنسَٰنُ أَلَّن نَّجۡمَعَ عِظَامَهُۥ ٣

Ayahsabul-insānu allan najma'a 'izāmah

Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake? 3

بَلَىٰ قَٰدِرِينَ عَلَىٰٓ أَن نُّسَوِّيَ بَنَانَهُۥ ٤

Balā qādirīna 'alā an nusawwiya banānah

Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake! 4

بَلۡ يُرِيدُ ٱلۡإِنسَٰنُ لِيَفۡجُرَ أَمَامَهُۥ ٥

Bal yurīdul-insānu liyafjura amāmah

Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilioko mbele yake. 5

يَسۡـَٔلُ أَيَّانَ يَوۡمُ ٱلۡقِيَٰمَةِ ٦

Yas'alu ayyāna yawmul-qiyāmah

Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama? 6

فَإِذَا بَرِقَ ٱلۡبَصَرُ ٧

Fa idhā bariqal-basar

Basi jicho litapo dawaa! 7

وَخَسَفَ ٱلۡقَمَرُ ٨

Wakhasafal-qamar

Na mwezi utapo patwa! 8

وَجُمِعَ ٱلشَّمۡسُ وَٱلۡقَمَرُ ٩

Wajumi'ash-shamsu wal-qamar

Na likakusanywa jua na mwezi! 9

يَقُولُ ٱلۡإِنسَٰنُ يَوۡمَئِذٍ أَيۡنَ ٱلۡمَفَرُّ ١٠

Yaqūlul-insānu yawma'idhin aynal-mafarr

Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio? 10

كَلَّا لَا وَزَرَ ١١

Kallā lā wazar

La! Hapana pa kukimbilia! 11

إِلَىٰ رَبِّكَ يَوۡمَئِذٍ ٱلۡمُسۡتَقَرُّ ١٢

Ilā rabbika yawma'idhinil-mustaqarr

Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu. 12

يُنَبَّؤُاْ ٱلۡإِنسَٰنُ يَوۡمَئِذِۭ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ ١٣

Yunabba'ul-insānu yawma'idhi bimā qaddama wa akkhar

Siku hiyo ataambiwa aliyo yatanguliza na aliyo yaakhirisha. 13

بَلِ ٱلۡإِنسَٰنُ عَلَىٰ نَفۡسِهِۦ بَصِيرَةٞ ١٤

Balil-insānu 'alā nafsihī basīrah

Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake. 14

وَلَوۡ أَلۡقَىٰ مَعَاذِيرَهُۥ ١٥

Walaw alqā ma'ādhīrah

Na ingawa atatoa chungu ya udhuru. 15

لَا تُحَرِّكۡ بِهِۦ لِسَانَكَ لِتَعۡجَلَ بِهِۦٓ ١٦

Lā tuharrik bihī lisānaka lita'jala bih

Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka. 16

إِنَّ عَلَيۡنَا جَمۡعَهُۥ وَقُرۡءَانَهُۥ ١٧

Inna 'alaynā jam'ahū waqur'ānah

Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha. 17

فَإِذَا قَرَأۡنَٰهُ فَٱتَّبِعۡ قُرۡءَانَهُۥ ١٨

Fa idhā qara'nāhu fattabi' qur'ānah

Tunapo usoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake. 18

ثُمَّ إِنَّ عَلَيۡنَا بَيَانَهُۥ ١٩

Thumma inna 'alaynā bayānah

Kisha ni juu yetu kuubainisha. 19

كَلَّا بَلۡ تُحِبُّونَ ٱلۡعَاجِلَةَ ٢٠

Kallā bal tuhibbūnal-'ājilah

Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani, 20

وَتَذَرُونَ ٱلۡأٓخِرَةَ ٢١

Watadharūnal-ākhirah

Na mnaacha maisha ya Akhera. 21

وُجُوهٞ يَوۡمَئِذٖ نَّاضِرَةٌ ٢٢

Wujūhun yawma'idhin nādirah

Zipo nyuso siku hiyo zitao ng'ara, 22

إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٞ ٢٣

Ilā rabbihā nāzirah

Zinamwangallia Mola wao Mlezi. 23

وَوُجُوهٞ يَوۡمَئِذِۭ بَاسِرَةٞ ٢٤

Wawujūhun yawma'idhi bāsirah

Na zipo nyuso siku hiyo zitakao kunjana. 24

تَظُنُّ أَن يُفۡعَلَ بِهَا فَاقِرَةٞ ٢٥

Tazunnu an yuf'ala bihā fāqirah

Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo. 25

كَلَّآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلتَّرَاقِيَ ٢٦

Kallā idhā balaghatit-tarāqiy

La, hasha! (Roho) itakapo fikia kwenye mafupa ya koo, 26

وَقِيلَ مَنۡۜ رَاقٖ ٢٧

Waqīla man rāq

Na pakasemwa: Nani wa kumganga? 27

وَظَنَّ أَنَّهُ ٱلۡفِرَاقُ ٢٨

Wazanna annahul-firāq

Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki; 28

وَٱلۡتَفَّتِ ٱلسَّاقُ بِٱلسَّاقِ ٢٩

Wal-taffatis-sāqu bis-sāq

Na utapo ambatishwa muundi kwa muundi, 29

إِلَىٰ رَبِّكَ يَوۡمَئِذٍ ٱلۡمَسَاقُ ٣٠

Ilā rabbika yawma'idhinil-masāq

Siku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako Mlezi! 30

فَلَا صَدَّقَ وَلَا صَلَّىٰ ٣١

Falā saddaqa walā sallā

Kwa sababu hakusadiki, wala hakuswali. 31

وَلَٰكِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ٣٢

Walākin kaddhaba watawallā

Bali alikanusha, na akageuka. 32

ثُمَّ ذَهَبَ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ يَتَمَطَّىٰٓ ٣٣

Thumma dhahaba ilā ahlihī yatamattā

Kisha akenda kwa ahali zake kwa matao. 33

أَوۡلَىٰ لَكَ فَأَوۡلَىٰ ٣٤

Awlā laka fa awlā

Ole wako, ole wako! 34

ثُمَّ أَوۡلَىٰ لَكَ فَأَوۡلَىٰٓ ٣٥

Thumma awlā laka fa awlā

Kisha Ole wako, ole wako! 35

أَيَحۡسَبُ ٱلۡإِنسَٰنُ أَن يُتۡرَكَ سُدًى ٣٦

Ayahsabul-insānu an yutraka sudā

Ati anadhani binaadamu kuwa ataachwa bure? 36

أَلَمۡ يَكُ نُطۡفَةٗ مِّن مَّنِيّٖ يُمۡنَىٰ ٣٧

Alam yaku nutfatam mim maniyyin yumnā

Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa? 37

ثُمَّ كَانَ عَلَقَةٗ فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ ٣٨

Thumma kāna 'alaqatan fakhalaqa fasawwā

Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo. 38

فَجَعَلَ مِنۡهُ ٱلزَّوۡجَيۡنِ ٱلذَّكَرَ وَٱلۡأُنثَىٰٓ ٣٩

Faja'ala minhuz-zawjaynidh-dhakara wal-unthā

Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke. 39

أَلَيۡسَ ذَٰلِكَ بِقَٰدِرٍ عَلَىٰٓ أَن يُحۡـِۧيَ ٱلۡمَوۡتَىٰ ٤٠

Alaysa dhālika biqādirin 'alā an yuhyal-mawtā

Je! Huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu? 40

Nambari za maelezo ya chini zinaelekeza kwenye ukurasa wa aya, ambapo maelezo ya mfasiri yanaonyeshwa.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Maswali

Surat Al-Qiyamah ina aya ngapi?

Surat Al-Qiyamah ina aya 40. Ni sura namba 75 ya Qur'ani.

Je, Surat Al-Qiyamah ni Makkiya au Madaniya?

Surat Al-Qiyamah ni sura Makkiya.

Surat Al-Qiyamah iko katika juzuu gani?

Surat Al-Qiyamah iko katika juzuu 29.

Je, naweza kusikiliza Surat Al-Qiyamah?

Ndiyo. Bonyeza Cheza juu ya ukurasa huu, au anza kutoka aya yoyote. Programu ya Qabas pia inakuwezesha kuipakua ili kuisikiliza bila intaneti.