Surat Al-Insan الانسان

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

هَلۡ أَتَىٰ عَلَى ٱلۡإِنسَٰنِ حِينٞ مِّنَ ٱلدَّهۡرِ لَمۡ يَكُن شَيۡـٔٗا مَّذۡكُورًا ١

Hal atā 'alal-insāni hīnum minad-dahri lam yakun shay'an mmadhkūrā

Hakika kilimpitia binaadamu kipindi katika zama ambacho kwamba hakuwa kitu kinacho tajwa. 1

إِنَّا خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ مِن نُّطۡفَةٍ أَمۡشَاجٖ نَّبۡتَلِيهِ فَجَعَلۡنَٰهُ سَمِيعَۢا بَصِيرًا ٢

Innā khalaqnal-insāna min nutfatin amshājin nabtalīhi faja'alnāhu samī'ā basīrā

Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyo changanyika, tumfanyie mtihani. Kwa hivyo tukamfanya mwenye kusikia, mwenye kuona. 2

إِنَّا هَدَيۡنَٰهُ ٱلسَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرٗا وَإِمَّا كَفُورًا ٣

Innā hadaynāhus-sabīla immā shākiran wa immā kafūrā

Hakika Sisi tumembainishia Njia. Ama ni mwenye kushukuru, au mwenye kukufuru. 3

إِنَّآ أَعۡتَدۡنَا لِلۡكَٰفِرِينَ سَلَٰسِلَاْ وَأَغۡلَٰلٗا وَسَعِيرًا ٤

Innā a'tadnā lil-kāfirīna salāsila wa aghlālan wasa'īrā

Hakika HaSisi tumewaandalia makafiri minyororo na pingu na Moto mkali. 4

إِنَّ ٱلۡأَبۡرَارَ يَشۡرَبُونَ مِن كَأۡسٖ كَانَ مِزَاجُهَا كَافُورًا ٥

Innal-abrāra yashrabūna min ka sin kāna mizājuhā kāfūrā

Hakika watu wema watakunywa katika vinywaji vilivyo changanyika na kafuri! 5

عَيۡنٗا يَشۡرَبُ بِهَا عِبَادُ ٱللَّهِ يُفَجِّرُونَهَا تَفۡجِيرٗا ٦

'Aynan yashrabu bihā 'ibādullāhi yufajjirūnahā tafjīrā

Ni chemchem watakao inywa waja wa Mwenyezi Mungu, wakiifanya imiminike kwa wingi. 6

يُوفُونَ بِٱلنَّذۡرِ وَيَخَافُونَ يَوۡمٗا كَانَ شَرُّهُۥ مُسۡتَطِيرٗا ٧

Yūfūna bin-nadhri wayakhāfūna yawman kāna sharruhū mustatīrā

Wanatimiza ahadi,na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana, 7

وَيُطۡعِمُونَ ٱلطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِۦ مِسۡكِينٗا وَيَتِيمٗا وَأَسِيرًا ٨

Wayut'imūnat-ta'āma 'alā hubbihī miskīnan wayatīman wa asīrā

Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa. 8

إِنَّمَا نُطۡعِمُكُمۡ لِوَجۡهِ ٱللَّهِ لَا نُرِيدُ مِنكُمۡ جَزَآءٗ وَلَا شُكُورًا ٩

Innamā nut'imukum liwajhillāhi lā nurīdu minkum jazā'an walā shukūrā

Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani. 9

إِنَّا نَخَافُ مِن رَّبِّنَا يَوۡمًا عَبُوسٗا قَمۡطَرِيرٗا ١٠

Innā nakhāfu mir rabbinā yawman 'abūsan qamtarīrā

Hakika sisi tunaiogopa kwa Mola wetu Mlezi hiyo siku yenye shida na taabu. 10

فَوَقَىٰهُمُ ٱللَّهُ شَرَّ ذَٰلِكَ ٱلۡيَوۡمِ وَلَقَّىٰهُمۡ نَضۡرَةٗ وَسُرُورٗا ١١

Fawaqāhumullāhu sharra dhālikal-yawmi walaqqāhum nadratan wasurūrā

Basi Mwenyezi Mungu atwalinda na shari ya siku hiyo, na atawakutanisha na raha na furaha. 11

وَجَزَىٰهُم بِمَا صَبَرُواْ جَنَّةٗ وَحَرِيرٗا ١٢

Wajazāhum bimā sabarū jannatan waharīrā

Na atawajazi Bustani za Peponi na maguo ya hariri kwa vile walivyo subiri. 12

مُّتَّكِـِٔينَ فِيهَا عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِۖ لَا يَرَوۡنَ فِيهَا شَمۡسٗا وَلَا زَمۡهَرِيرٗا ١٣

Mmuttaki'īna fīhā 'alal-arā'iki lā yarawna fīhā shamsan walā zamharīrā

Humo wataegemea juu ya viti vya enzi, hawataona humo jua kali wala baridi kali. 13

وَدَانِيَةً عَلَيۡهِمۡ ظِلَٰلُهَا وَذُلِّلَتۡ قُطُوفُهَا تَذۡلِيلٗا ١٤

Wadāniyatan 'alayhim zilāluhā wadhullilat qutūfuhā tadhlīlā

Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada ya matunda yataning'inia mpaka chini. 14

وَيُطَافُ عَلَيۡهِم بِـَٔانِيَةٖ مِّن فِضَّةٖ وَأَكۡوَابٖ كَانَتۡ قَوَارِيرَا۠ ١٥

Wayutāfu 'alayhim bi'āniyatim min fiddatin wa akwābin kānat qawārīraā

Na watapitishiwa vyombo vya fedha na vikombe vya vigae, 15

قَوَارِيرَاْ مِن فِضَّةٖ قَدَّرُوهَا تَقۡدِيرٗا ١٦

Qawārīra min fiddatin qaddarūhā taqdīrā

Vya fedha safi kama kiyoo, wamevipima kwa vipimo. 16

وَيُسۡقَوۡنَ فِيهَا كَأۡسٗا كَانَ مِزَاجُهَا زَنجَبِيلًا ١٧

Wayusqawna fīhā ka san kāna mizājuhā zanjabīlā

Na humo watanyweshwa kinywaji kilicho changanyika na tangawizi. 17

عَيۡنٗا فِيهَا تُسَمَّىٰ سَلۡسَبِيلٗا ١٨

'Aynan fīhā tusammā salsabīlā

Hiyo ni chemchem iliyo humo inaitwa Salsabil. 18

۞ وَيَطُوفُ عَلَيۡهِمۡ وِلۡدَٰنٞ مُّخَلَّدُونَ إِذَا رَأَيۡتَهُمۡ حَسِبۡتَهُمۡ لُؤۡلُؤٗا مَّنثُورٗا ١٩

Wayatūfu 'alayhim wildānum mukhalladūna idhā ra'aytahum hasibtahum lu'lu'am manthūrā

Na watawazungukia kuwatumikia wavulana wasio pevuka, ukiwaona utawafikiri ni lulu zilizo tawanywa. 19

وَإِذَا رَأَيۡتَ ثَمَّ رَأَيۡتَ نَعِيمٗا وَمُلۡكٗا كَبِيرًا ٢٠

Wa idhā ra'ayta thamma ra'ayta na'īman wamulkan kabīrā

Na utakapo yaona, utakuwa umeona neema na ufalme mkubwa. 20

عَٰلِيَهُمۡ ثِيَابُ سُندُسٍ خُضۡرٞ وَإِسۡتَبۡرَقٞۖ وَحُلُّوٓاْ أَسَاوِرَ مِن فِضَّةٖ وَسَقَىٰهُمۡ رَبُّهُمۡ شَرَابٗا طَهُورًا ٢١

'Āliyahum thiyābu sundusin khudrun wa istabraqun wahullū asāwira min fiddatin wasaqāhum rabbuhum sharāban tahūrā

Juu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi, na hariri nzito ya at'ilasi. Na watavikwa vikuku vya fedha, na Mola wao Mlezi atawanywesha kinywaji safi kabisa. 21

إِنَّ هَٰذَا كَانَ لَكُمۡ جَزَآءٗ وَكَانَ سَعۡيُكُم مَّشۡكُورًا ٢٢

Inna hādhā kāna lakum jazā'an wakāna sa'yukum mashkūrā

Hakika haya ni malipo yenu; na juhudi zenu zimekubaliwa. 22

إِنَّا نَحۡنُ نَزَّلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡقُرۡءَانَ تَنزِيلٗا ٢٣

Innā nahnu nazzalnā 'alaykal-qur'āna tanzīlā

Hakika Sisi tumekuteremshia Qur'ani kidogo kidogo. 23

فَٱصۡبِرۡ لِحُكۡمِ رَبِّكَ وَلَا تُطِعۡ مِنۡهُمۡ ءَاثِمًا أَوۡ كَفُورٗا ٢٤

Fasbir lihukmi rabbika walā tuti' minhum āthiman aw kafūrā

Basi ngojea hukumu ya Mola wako Mlezi wala usimt'ii miongoni mwao mwenye dhambi au mwenye kufuru. 24

وَٱذۡكُرِ ٱسۡمَ رَبِّكَ بُكۡرَةٗ وَأَصِيلٗا ٢٥

Wadhkurisma rabbika bukratan wa asīlā

Na likumbuke jina la Mola wako Mlezi asubuhi na jioni; 25

وَمِنَ ٱلَّيۡلِ فَٱسۡجُدۡ لَهُۥ وَسَبِّحۡهُ لَيۡلٗا طَوِيلًا ٢٦

Waminal-layli fasjud lahū wasabbihhu laylan tawīlā

Na usiku msujudie Yeye, na umtakase usiku, wakati mrefu. 26

إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ يُحِبُّونَ ٱلۡعَاجِلَةَ وَيَذَرُونَ وَرَآءَهُمۡ يَوۡمٗا ثَقِيلٗا ٢٧

Inna hā'ulā'i yuhibbūnal-'ājilata wayadharūna warā'ahum yawman thaqīlā

Kwa hakika watu hawa wanapenda maisha ya kidunia, na wanaiacha nyuma yao siku nzito. 27

نَّحۡنُ خَلَقۡنَٰهُمۡ وَشَدَدۡنَآ أَسۡرَهُمۡۖ وَإِذَا شِئۡنَا بَدَّلۡنَآ أَمۡثَٰلَهُمۡ تَبۡدِيلًا ٢٨

Nnahnu khalaqnāhum washadadnā asrahum wa idhā shi'nā baddalnā amthālahum tabdīlā

Sisi tumewaumba, na tukavitia nguvu viungo vyao. Na tukitaka tutawabadilisha mfano wao wawe badala yao. 28

إِنَّ هَٰذِهِۦ تَذۡكِرَةٞۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ سَبِيلٗا ٢٩

Inna hādhihī tadhkiratun faman shā'at-takhadha ilā rabbihī sabīlā

Hakika haya ni mawaidha; basi anaye taka atashika Njia ya kwenda kwa Mola wake Mlezi. 29

وَمَا تَشَآءُونَ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمٗا ٣٠

Wamā tashā'ūna illā an yashā'allāhu innallāha kāna 'alīman hakīmā

Wala hamwezi kutaka ila atakapo Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye ilimu, Mwenye hikima. 30

يُدۡخِلُ مَن يَشَآءُ فِي رَحۡمَتِهِۦۚ وَٱلظَّٰلِمِينَ أَعَدَّ لَهُمۡ عَذَابًا أَلِيمَۢا ٣١

Yudkhilu man yashā'u fī rahmatihī waz-zālimīna a'adda lahum 'adhāban alīmā

Humuingiza amtakaye katika rehema yake. Na wenye kudhulumu amewawekea adhabu iliyo chungu. 31

Nambari za maelezo ya chini zinaelekeza kwenye ukurasa wa aya, ambapo maelezo ya mfasiri yanaonyeshwa.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Maswali

Surat Al-Insan ina aya ngapi?

Surat Al-Insan ina aya 31. Ni sura namba 76 ya Qur'ani.

Je, Surat Al-Insan ni Makkiya au Madaniya?

Surat Al-Insan ni sura Madaniya.

Surat Al-Insan iko katika juzuu gani?

Surat Al-Insan iko katika juzuu 29.

Je, naweza kusikiliza Surat Al-Insan?

Ndiyo. Bonyeza Cheza juu ya ukurasa huu, au anza kutoka aya yoyote. Programu ya Qabas pia inakuwezesha kuipakua ili kuisikiliza bila intaneti.