إِنَّآ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ حَاصِبًا إِلَّآ ءَالَ لُوطٖۖ نَّجَّيۡنَٰهُم بِسَحَرٖ ٣٤
Innā arsalnā 'alayhim hāsiban illā āla lūtin najjaynāhum bisahar
Hakika Sisi tukawapelekea kimbunga cha vijiwe, isipo kuwa wafuasi wa Lut'i. Hao tuliwaokoa karibu na alfajiri. 34
Maelezo ya chini
34 Hakika Sisi tuliwapelekea upepo mkali wa kuwatupia changarawe. Isipo kuwa watu wa Lut'i walio amini. Hao tuliwaokoa na adhabu hii mwisho wa usiku.