Surat Al-Qalam القلم

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

نٓۚ وَٱلۡقَلَمِ وَمَا يَسۡطُرُونَ ١

Nūn wal-qalami wamā yasturūn

Nuun. Naapa kwa kalamu na yale wayaandikayo! 1

مَآ أَنتَ بِنِعۡمَةِ رَبِّكَ بِمَجۡنُونٖ ٢

Mā anta bini'mati rabbika bimajnūn

Kwa neema ya Mola wako Mlezi wewe si mwendawazimu. 2

وَإِنَّ لَكَ لَأَجۡرًا غَيۡرَ مَمۡنُونٖ ٣

Wa inna laka la ajran ghayra mamnūn

Na kwa hakika wewe una malipo yasiyo katika. 3

وَإِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٖ ٤

Wa innaka la'alā khuluqin 'azīm

Na hakika wewe una tabia tukufu. 4

فَسَتُبۡصِرُ وَيُبۡصِرُونَ ٥

Fasatubsiru wayubsirūn

Karibu utaona, na wao wataona! 5

بِأَييِّكُمُ ٱلۡمَفۡتُونُ ٦

Bi ayyikumul-maftūn

Ni nani kati yenu aliye pandwa na wazimu. 6

إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُهۡتَدِينَ ٧

Inna rabbaka huwa a'lamu biman dalla 'an sabīlihī wahuwa a'lamu bil-muhtadīn

Hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye ajuaye zaidi nani aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anaye wajua zaidi walio ongoka. 7

فَلَا تُطِعِ ٱلۡمُكَذِّبِينَ ٨

Falā tuti'il-mukaddhibīn

Basi usiwat'ii wanao kadhibisha. 8

وَدُّواْ لَوۡ تُدۡهِنُ فَيُدۡهِنُونَ ٩

Waddū law tudhinu fayudhinūn

Wanatamani lau unge lainisha ili nao wakulainishie. 9

وَلَا تُطِعۡ كُلَّ حَلَّافٖ مَّهِينٍ ١٠

Walā tuti' kulla hallāfim mahīn

Wala usimt'ii kila mwingi wa kuapa wa kudharauliwa, 10

هَمَّازٖ مَّشَّآءِۭ بِنَمِيمٖ ١١

Hammāzim masshā'i binamīm

Mtapitapi apitae akifitini. 11

مَّنَّاعٖ لِّلۡخَيۡرِ مُعۡتَدٍ أَثِيمٍ ١٢

Mmannā'il lil-khayri mu'tadin athīm

Mwenye kuzuia kheri, dhaalimu, mwingi wa madhambi, 12

عُتُلِّۭ بَعۡدَ ذَٰلِكَ زَنِيمٍ ١٣

'Utulli ba'da dhālika zanīm

Mkavu, na juu ya hayo, mshari, amejipachika tu. 13

أَن كَانَ ذَا مَالٖ وَبَنِينَ ١٤

An kāna dhā mālin wabanīn

Ati kwa kuwa ana mali na watoto! 14

إِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِ ءَايَٰتُنَا قَالَ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ ١٥

Idhā tutlā 'alayhi āyātunā qāla asātīrul-awwalīn

Anapo somewa Aya zetu, husema: Hizi ni simulizi za uwongo za watu wa zamani! 15

سَنَسِمُهُۥ عَلَى ٱلۡخُرۡطُومِ ١٦

Sanasimuhū 'alal-khurtūm

Tutamtia kovu juu ya pua yake. 16

إِنَّا بَلَوۡنَٰهُمۡ كَمَا بَلَوۡنَآ أَصۡحَٰبَ ٱلۡجَنَّةِ إِذۡ أَقۡسَمُواْ لَيَصۡرِمُنَّهَا مُصۡبِحِينَ ١٧

Innā balawnāhum kamā balawnā ashābal-jannati idh aqsamū layasrimunnahā musbihīn

Hakika tumewajaribu hawa kama tulivyo wajaribu wale wenye shamba, walipo apa kwamba watayavuna mazao yake itakapo kuwa asubuhi. 17

وَلَا يَسۡتَثۡنُونَ ١٨

Walā yastathnūn

Wala hawakusema: Mungu akipenda! 18

فَطَافَ عَلَيۡهَا طَآئِفٞ مِّن رَّبِّكَ وَهُمۡ نَآئِمُونَ ١٩

Fatāfa 'alayhā tā'ifum mir rabbika wahum nā'imūn

Basi lilitokea tukio juu yake kutoka kwa Mola wako Mlezi, nao wamelala! 19

فَأَصۡبَحَتۡ كَٱلصَّرِيمِ ٢٠

Fa asbahat kas-sarīm

Likawa kama usiku wa giza. 20

فَتَنَادَوۡاْ مُصۡبِحِينَ ٢١

Fatanādaw musbihīn

Asubuhi wakaitana. 21

أَنِ ٱغۡدُواْ عَلَىٰ حَرۡثِكُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰرِمِينَ ٢٢

Anighdū 'alā harthikum in kuntum sārimīn

Ya kwamba nendeni kondeni mwenu ikiwa mnataka kuvuna. 22

فَٱنطَلَقُواْ وَهُمۡ يَتَخَٰفَتُونَ ٢٣

Fantalaqū wahum yatakhāfatūn

Basi walikwenda na huku wakinong'onezana, 23

أَن لَّا يَدۡخُلَنَّهَا ٱلۡيَوۡمَ عَلَيۡكُم مِّسۡكِينٞ ٢٤

Al lā yadkhulannahal-yawma 'alaykum miskīn

Ya kuwa leo hata masikini mmoja asikuingilieni. 24

وَغَدَوۡاْ عَلَىٰ حَرۡدٖ قَٰدِرِينَ ٢٥

Waghadaw 'alā hardin qādirīn

Na walikwenda asubuhi, nao wameshikilia azimio hilo. 25

فَلَمَّا رَأَوۡهَا قَالُوٓاْ إِنَّا لَضَآلُّونَ ٢٦

Falammā ra'awhā qālū innā ladāllūn

Basi walipo liona, wakasema: Hakika tumepotea! 26

بَلۡ نَحۡنُ مَحۡرُومُونَ ٢٧

Bal nahnu mahrūmūn

Bali tumenyimwa! 27

قَالَ أَوۡسَطُهُمۡ أَلَمۡ أَقُل لَّكُمۡ لَوۡلَا تُسَبِّحُونَ ٢٨

Qāla awsatuhum alam aqul lakum lawlā tusabbihūn

Mbora wao akasema: Sikukwambieni, kwa nini hamumtakasi Mwenyezi Mungu? 28

قَالُواْ سُبۡحَٰنَ رَبِّنَآ إِنَّا كُنَّا ظَٰلِمِينَ ٢٩

Qālū subhāna rabbinā innā kunnā zālimīn

Wakasema: Ametakasika Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tulikuwa wenye kudhulumu. 29

فَأَقۡبَلَ بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖ يَتَلَٰوَمُونَ ٣٠

Fa aqbala ba'duhum 'alā ba'din yatalāwamūn

Basi wakakabiliana kulaumiana wao kwa wao. 30

قَالُواْ يَٰوَيۡلَنَآ إِنَّا كُنَّا طَٰغِينَ ٣١

Qālū yāwaylanā innā kunnā tāghīn

Wakasema: Ole wetu! Tulikuwa tumeikiuka mipaka! 31

عَسَىٰ رَبُّنَآ أَن يُبۡدِلَنَا خَيۡرٗا مِّنۡهَآ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا رَٰغِبُونَ ٣٢

'Asā rabbunā an yubdilanā khayram minhā innā ilā rabbinā rāghibūn

Asaa Mola wetu Mlezi akatubadilishia lilio bora kuliko hili. Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi. 32

كَذَٰلِكَ ٱلۡعَذَابُۖ وَلَعَذَابُ ٱلۡأٓخِرَةِ أَكۡبَرُۚ لَوۡ كَانُواْ يَعۡلَمُونَ ٣٣

Kadhālikal-'adhābu wala'adhābul-ākhirati akbaru law kānū ya'lamūn

Namna hivi yanakuwa mateso, na bila ya shaka mateso ya Akhera ni makubwa zaidi, laiti wangeli jua! 33

إِنَّ لِلۡمُتَّقِينَ عِندَ رَبِّهِمۡ جَنَّٰتِ ٱلنَّعِيمِ ٣٤

Inna lil-muttaqīna 'inda rabbihim jannātin-na'īm

Hakika wachamngu watakuwa na Bustani za neema kwa Mola wao Mlezi. 34

أَفَنَجۡعَلُ ٱلۡمُسۡلِمِينَ كَٱلۡمُجۡرِمِينَ ٣٥

Afanaj'alul-muslimīna kal-mujrimīn

Kwani tutawafanya Waislamu kama wakosefu? 35

مَا لَكُمۡ كَيۡفَ تَحۡكُمُونَ ٣٦

Mā lakum kayfa tahkumūn

Mna nini? Mnahukumu vipi? 36

أَمۡ لَكُمۡ كِتَٰبٞ فِيهِ تَدۡرُسُونَ ٣٧

Am lakum kitābun fīhi tadrusūn

Au mnacho kitabu ambacho ndani yake mnasoma? 37

إِنَّ لَكُمۡ فِيهِ لَمَا تَخَيَّرُونَ ٣٨

Inna lakum fīhi lamā takhayyarūn

Kuwa mtapata humo mnayo yapenda? 38

أَمۡ لَكُمۡ أَيۡمَٰنٌ عَلَيۡنَا بَٰلِغَةٌ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ إِنَّ لَكُمۡ لَمَا تَحۡكُمُونَ ٣٩

Am lakum aymānun 'alaynā bālighatun ilā yawmil-qiyāmati inna lakum lamā tahkumūn

Au mnazo ahadi za viapo juu yetu za kufika Siku ya Kiyama ya kuwa hakika mtapata kila mnayo jihukumia? 39

سَلۡهُمۡ أَيُّهُم بِذَٰلِكَ زَعِيمٌ ٤٠

Salhum ayyuhum bidhālika za'īm

Waulize: Ni nani miongoni mwao dhamini wa haya? 40

أَمۡ لَهُمۡ شُرَكَآءُ فَلۡيَأۡتُواْ بِشُرَكَآئِهِمۡ إِن كَانُواْ صَٰدِقِينَ ٤١

Am lahum shurakā'u falya'tū bishurakā'ihim in kānū sādiqīn

Au wanao washirika? Basi wawalete washirika wao wakiwa wanasema kweli. 41

يَوۡمَ يُكۡشَفُ عَن سَاقٖ وَيُدۡعَوۡنَ إِلَى ٱلسُّجُودِ فَلَا يَسۡتَطِيعُونَ ٤٢

Yawma yukshafu 'an sāqin wayud'awna ilas-sujūdi falā yastatī'ūn

Siku utakapo wekwa wazi mundi, na wataitwa kusujudu, lakini hawataweza, 42

خَٰشِعَةً أَبۡصَٰرُهُمۡ تَرۡهَقُهُمۡ ذِلَّةٞۖ وَقَدۡ كَانُواْ يُدۡعَوۡنَ إِلَى ٱلسُّجُودِ وَهُمۡ سَٰلِمُونَ ٤٣

Khāshi'atan absāruhum tarhaquhum dhillatun waqad kānū yud'awna ilas-sujūdi wahum sālimūn

Macho yao yatainama chini, fedheha itawafunika. Na hakika walikuwa wakiitwa wasujudu walipo kuwa wazima 43

فَذَرۡنِي وَمَن يُكَذِّبُ بِهَٰذَا ٱلۡحَدِيثِۖ سَنَسۡتَدۡرِجُهُم مِّنۡ حَيۡثُ لَا يَعۡلَمُونَ ٤٤

Fadharnī waman yukaddhibu bihādhal-hadīthi sanastadrijuhum min haythu lā ya'lamūn

Basi niache na wanao kadhibisha maneno haya! Tutawavutia kidogo kidogo kwa mahali wasipo pajua. 44

وَأُمۡلِي لَهُمۡۚ إِنَّ كَيۡدِي مَتِينٌ ٤٥

Wa umlī lahum inna kaydī matīn

Na ninawapururia muhula; hakika hila zangu ni imara. 45

أَمۡ تَسۡـَٔلُهُمۡ أَجۡرٗا فَهُم مِّن مَّغۡرَمٖ مُّثۡقَلُونَ ٤٦

Am tas'aluhum ajran fahum mim maghramim muthqalūn

Au unawaomba ujira, na wao wanaemewa na gharama hiyo? 46

أَمۡ عِندَهُمُ ٱلۡغَيۡبُ فَهُمۡ يَكۡتُبُونَ ٤٧

Am 'indahumul-ghaybu fahum yaktubūn

Au iko kwao siri, basi wao wanaiandika? 47

فَٱصۡبِرۡ لِحُكۡمِ رَبِّكَ وَلَا تَكُن كَصَاحِبِ ٱلۡحُوتِ إِذۡ نَادَىٰ وَهُوَ مَكۡظُومٞ ٤٨

Fasbir lihukmi rabbika walā takun kasāhibil-hūti idh nādā wahuwa makzūm

Basi ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi, wala usiwe kama mmezwa na samaki, alipo nadi naye kazongwa. 48

لَّوۡلَآ أَن تَدَٰرَكَهُۥ نِعۡمَةٞ مِّن رَّبِّهِۦ لَنُبِذَ بِٱلۡعَرَآءِ وَهُوَ مَذۡمُومٞ ٤٩

Llawlā an tadārakahū ni'matum mir rabbihī lanubidha bil-'arā'i wahuwa madhmūm

Kama isingeli mfikia neema kutoka kwa Mola wake Mlezi, bila ya shaka angeli tupwa ufukweni naye ni mwenye kulaumiwa. 49

فَٱجۡتَبَٰهُ رَبُّهُۥ فَجَعَلَهُۥ مِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ ٥٠

Fajtabāhu rabbuhū faja'alahū minas-sālihīn

Lakini Mola wake Mlezi alimteua na akamfanya miongoni mwa watu wema. 50

وَإِن يَكَادُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَيُزۡلِقُونَكَ بِأَبۡصَٰرِهِمۡ لَمَّا سَمِعُواْ ٱلذِّكۡرَ وَيَقُولُونَ إِنَّهُۥ لَمَجۡنُونٞ ٥١

Wa in yakādul-ladhīna kafarū layuzliqūnaka bi absārihim lammā sami'udh-dhikra wayaqūlūna innahū lamajnūn

Na walio kufuru hukaribia kukutelezesha kwa macho yao, wanapo sikia mawaidha, na wanasema: Hakika yeye ni mwendawazimu. 51

وَمَا هُوَ إِلَّا ذِكۡرٞ لِّلۡعَٰلَمِينَ ٥٢

Wamā huwa illā dhikrul lil-'ālamīn

Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote. 52

Nambari za maelezo ya chini zinaelekeza kwenye ukurasa wa aya, ambapo maelezo ya mfasiri yanaonyeshwa.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Aya maarufu

Maswali

Surat Al-Qalam ina aya ngapi?

Surat Al-Qalam ina aya 52. Ni sura namba 68 ya Qur'ani.

Je, Surat Al-Qalam ni Makkiya au Madaniya?

Surat Al-Qalam ni sura Makkiya.

Surat Al-Qalam iko katika juzuu gani?

Surat Al-Qalam iko katika juzuu 29.

Je, naweza kusikiliza Surat Al-Qalam?

Ndiyo. Bonyeza Cheza juu ya ukurasa huu, au anza kutoka aya yoyote. Programu ya Qabas pia inakuwezesha kuipakua ili kuisikiliza bila intaneti.