ٱلۡحَآقَّةُ ١
Al-hāqqah
Tukio la haki. 1
Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
ٱلۡحَآقَّةُ ١
Al-hāqqah
Tukio la haki. 1
مَا ٱلۡحَآقَّةُ ٢
Mal-hāqqah
Nini hilo Tukio la haki? 2
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡحَآقَّةُ ٣
Wamā adrāka mal-hāqqah
Na nini kitakujuulisha nini hilo Tukio la haki? 3
كَذَّبَتۡ ثَمُودُ وَعَادُۢ بِٱلۡقَارِعَةِ ٤
Kaddhabat thamūdu wa'ādu bil-qāri'ah
Thamudi na A'di waliukadhibisha Msiba unao situsha. 4
فَأَمَّا ثَمُودُ فَأُهۡلِكُواْ بِٱلطَّاغِيَةِ ٥
Fa ammā thamūdu fa uhlikū bit-tāghiyah
Basi Thamudi waliangamizwa kwa balaa kubwa mno. 5
وَأَمَّا عَادٞ فَأُهۡلِكُواْ بِرِيحٖ صَرۡصَرٍ عَاتِيَةٖ ٦
Wa ammā 'ādun fa uhlikū birīhin sarsarin 'ātiyah
Na ama A'di waliangamizwa kwa upepo mkali usio zuilika. 6
سَخَّرَهَا عَلَيۡهِمۡ سَبۡعَ لَيَالٖ وَثَمَٰنِيَةَ أَيَّامٍ حُسُومٗاۖ فَتَرَى ٱلۡقَوۡمَ فِيهَا صَرۡعَىٰ كَأَنَّهُمۡ أَعۡجَازُ نَخۡلٍ خَاوِيَةٖ ٧
Sakkharahā 'alayhim sab'a layālin wathamāniyata ayyāmin husūman fataral-qawma fīhā sar'ā ka annahum a'jāzu nakhlin khāwiyah
Alio wapelekea masiku saba, na siku nane, mfululizo bila ya kusita. Utaona watu wamepinduka kama kwamba ni magongo ya mitende yalio wazi ndani. 7
فَهَلۡ تَرَىٰ لَهُم مِّنۢ بَاقِيَةٖ ٨
Fahal tarā lahum mim bāqiyah
Basi je! Unamwona mmoja wao aliye baki? 8
وَجَآءَ فِرۡعَوۡنُ وَمَن قَبۡلَهُۥ وَٱلۡمُؤۡتَفِكَٰتُ بِٱلۡخَاطِئَةِ ٩
Wajā'a fir'awnu waman qablahū wal-mu'tafikātu bil-khāti'ah
Na Firauni na walio mtangulia, na miji iliyo pinduliwa chini juu, walileta khatia. 9
فَعَصَوۡاْ رَسُولَ رَبِّهِمۡ فَأَخَذَهُمۡ أَخۡذَةٗ رَّابِيَةً ١٠
Fa'asaw rasūla rabbihim fa akhadhahum akhdhatar rābiyah
Wakamuasi Mtume wa Mola wao Mlezi, ndipo Yeye Mola akawakamata kwa mkamato ulio zidi nguvu. 10
إِنَّا لَمَّا طَغَا ٱلۡمَآءُ حَمَلۡنَٰكُمۡ فِي ٱلۡجَارِيَةِ ١١
Innā lammā taghal-mā'u hamalnākum fil-jāriyah
Maji yalipo furika Sisi tulikupandisheni katika safina, 11
لِنَجۡعَلَهَا لَكُمۡ تَذۡكِرَةٗ وَتَعِيَهَآ أُذُنٞ وَٰعِيَةٞ ١٢
Linaj'alahā lakum tadhkiratan wata'iyahā udhunun wā'iyah
Ili tuyafanye hayo kuwa ni waadhi kwenu na kila sikio linalo sikia liyahifadhi. 12
فَإِذَا نُفِخَ فِي ٱلصُّورِ نَفۡخَةٞ وَٰحِدَةٞ ١٣
Fa idhā nufikha fis-sūri nafkhatun wāhidah
. Na litapo pulizwa barugumu mpulizo mmoja tu, 13
وَحُمِلَتِ ٱلۡأَرۡضُ وَٱلۡجِبَالُ فَدُكَّتَا دَكَّةٗ وَٰحِدَةٗ ١٤
Wahumilatil-ardu wal-jibālu fadukkatā dakkatan wāhidah
Na ardhi na milima ikaondolewa, na ikavunjwa kwa mvunjo mmoja, 14
فَيَوۡمَئِذٖ وَقَعَتِ ٱلۡوَاقِعَةُ ١٥
Fayawma'idhin waqa'atil-wāqi'ah
Siku hiyo ndio Tukio litatukia. 15
وَٱنشَقَّتِ ٱلسَّمَآءُ فَهِيَ يَوۡمَئِذٖ وَاهِيَةٞ ١٦
Wanshaqqatis-samā'u fahiya yawma'idhin wāhiyah
Na mbingu zitapasuka, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu kabisa. 16
وَٱلۡمَلَكُ عَلَىٰٓ أَرۡجَآئِهَاۚ وَيَحۡمِلُ عَرۡشَ رَبِّكَ فَوۡقَهُمۡ يَوۡمَئِذٖ ثَمَٰنِيَةٞ ١٧
Wal-malaku 'alā arjā'ihā wayahmilu 'arsha rabbika fawqahum yawma'idhin thamāniyah
Na Malaika watakuwa pembezoni mwa mbingu; na wanane juu ya hawa watakuwa wamebeba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi. 17
يَوۡمَئِذٖ تُعۡرَضُونَ لَا تَخۡفَىٰ مِنكُمۡ خَافِيَةٞ ١٨
Yawma'idhin tu'radūna lā takhfā minkum khāfiyah
Siku hiyo mtahudhurishwa - haitafichika siri yoyote yenu. 18
فَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ فَيَقُولُ هَآؤُمُ ٱقۡرَءُواْ كِتَٰبِيَهۡ ١٩
Fa ammā man ūtiya kitābahū biyamīnihī fayaqūlu hā'umuqra'ū kitābiyah
Basi ama atakaye pewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema: Haya someni kitabu changu! 19
إِنِّي ظَنَنتُ أَنِّي مُلَٰقٍ حِسَابِيَهۡ ٢٠
Innī zanantu annī mulāqin hisābiyah
Hakika nalijua ya kuwa nitapokea hisabu yangu. 20
فَهُوَ فِي عِيشَةٖ رَّاضِيَةٖ ٢١
Fahuwa fī 'īshatir rādiyah
Basi yeye atakuwa katika maisha ya kupendeza, 21
فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٖ ٢٢
Fī jannatin 'āliyah
Katika Bustani ya juu, 22
قُطُوفُهَا دَانِيَةٞ ٢٣
Qutūfuhā dāniyah
Matunda yake yakaribu. 23
كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ هَنِيٓـَٔۢا بِمَآ أَسۡلَفۡتُمۡ فِي ٱلۡأَيَّامِ ٱلۡخَالِيَةِ ٢٤
Kulū washrabū hanī'ā bimā aslaftum fil-ayyāmil-khāliyah
Waambiwe: Kuleni na mnywe kwa furaha kwa sababu ya mlivyo tanguliza katika siku zilizo pita. 24
وَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِشِمَالِهِۦ فَيَقُولُ يَٰلَيۡتَنِي لَمۡ أُوتَ كِتَٰبِيَهۡ ٢٥
Wa ammā man ūtiya kitābahū bishimālihī fayaqūlu yālaytanī lam ūta kitābiyah
Na ama atakaye pewa kitabu chake katika mkono wake wa kushoto, basi yeye atasema: Laiti nisingeli pewa kitabu changu! 25
وَلَمۡ أَدۡرِ مَا حِسَابِيَهۡ ٢٦
Walam adri mā hisābiyah
Wala nisingeli jua nini hisabu yangu. 26
يَٰلَيۡتَهَا كَانَتِ ٱلۡقَاضِيَةَ ٢٧
Yālaytahā kānatil-qādiyah
Laiti mauti ndiyo yangeli kuwa ya kunimaliza kabisa. 27
مَآ أَغۡنَىٰ عَنِّي مَالِيَهۡۜ ٢٨
Mā aghnā 'annī māliyah
Mali yangu hayakunifaa kitu. 28
هَلَكَ عَنِّي سُلۡطَٰنِيَهۡ ٢٩
Halaka 'annī sultāniyah
Madaraka yangu yamenipotea. 29
خُذُوهُ فَغُلُّوهُ ٣٠
Khudhūhu faghullūh
(Pasemwe): Mshikeni! Mtieni pingu! 30
ثُمَّ ٱلۡجَحِيمَ صَلُّوهُ ٣١
Thummal-jahīma sallūh
Kisha mtupeni Motoni! 31
ثُمَّ فِي سِلۡسِلَةٖ ذَرۡعُهَا سَبۡعُونَ ذِرَاعٗا فَٱسۡلُكُوهُ ٣٢
Thumma fī silsilatin dhar'uhā sab'ūna dhirā'an faslukūh
Tena mtatizeni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabiini! 32
إِنَّهُۥ كَانَ لَا يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ ٱلۡعَظِيمِ ٣٣
Innahū kāna lā yu'minu billāhil-'azīm
Kwani huyo hakika alikuwa hamuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, 33
وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ ٣٤
Walā yahuddu 'alā ta'āmil-miskīn
Wala hahimizi kulisha masikini. 34
فَلَيۡسَ لَهُ ٱلۡيَوۡمَ هَٰهُنَا حَمِيمٞ ٣٥
Falaysa lahul-yawma hāhunā hamīm
Basi leo hapa hana jamaa wa kumwonea uchungu, 35
وَلَا طَعَامٌ إِلَّا مِنۡ غِسۡلِينٖ ٣٦
Walā ta'āmun illā min ghislīn
Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni. 36
لَّا يَأۡكُلُهُۥٓ إِلَّا ٱلۡخَٰطِـُٔونَ ٣٧
Llā ya'kuluhū illal-khāti'ūn
Chakula hicho hawakili ila wakosefu. 37
فَلَآ أُقۡسِمُ بِمَا تُبۡصِرُونَ ٣٨
Falā uqsimu bimā tubsirūn
Basi naapa kwa mnavyo viona, 38
وَمَا لَا تُبۡصِرُونَ ٣٩
Wamā lā tubsirūn
Na msivyo viona, 39
إِنَّهُۥ لَقَوۡلُ رَسُولٖ كَرِيمٖ ٤٠
Innahū laqawlu rasūlin karīm
Kwa hakika hii ni kauli iliyo letwa na Mjumbe mwenye hishima. 40
وَمَا هُوَ بِقَوۡلِ شَاعِرٖۚ قَلِيلٗا مَّا تُؤۡمِنُونَ ٤١
Wamā huwa biqawli shā'irin qalīlam mā tu'minūn
Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana mnayo yaamini. 41
وَلَا بِقَوۡلِ كَاهِنٖۚ قَلِيلٗا مَّا تَذَكَّرُونَ ٤٢
Walā biqawli kāhinin qalīlam mā tadhakkarūn
Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayo yakumbuka. 42
تَنزِيلٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ٤٣
Tanzīlum mir rabbil-'ālamīn
Ni uteremsho utokao kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. 43
وَلَوۡ تَقَوَّلَ عَلَيۡنَا بَعۡضَ ٱلۡأَقَاوِيلِ ٤٤
Walaw taqawwala 'alaynā ba'dal-aqāwīl
Na lau kama angeli tuzulia baadhi ya maneno tu, 44
لَأَخَذۡنَا مِنۡهُ بِٱلۡيَمِينِ ٤٥
La akhadhnā minhu bil-yamīn
Bila ya shaka tungeli mshika kwa mkono wa kulia, 45
ثُمَّ لَقَطَعۡنَا مِنۡهُ ٱلۡوَتِينَ ٤٦
Thumma laqata'nā minhul-watīn
Kisha kwa hakika tungeli mkata mshipa mkubwa wa moyo! 46
فَمَا مِنكُم مِّنۡ أَحَدٍ عَنۡهُ حَٰجِزِينَ ٤٧
Famā minkum min ahadin 'anhu hājizīn
Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeli weza kutuzuia. 47
وَإِنَّهُۥ لَتَذۡكِرَةٞ لِّلۡمُتَّقِينَ ٤٨
Wa innahū latadhkiratul lil-muttaqīn
Kwa hakika hii ni mawaidha kwa wachamngu. 48
وَإِنَّا لَنَعۡلَمُ أَنَّ مِنكُم مُّكَذِّبِينَ ٤٩
Wa innā lana'lamu anna minkum mukaddhibīn
Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba miongoni mwenu wapo wanao kadhibisha. 49
وَإِنَّهُۥ لَحَسۡرَةٌ عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ ٥٠
Wa innahū lahasratun 'alal-kāfirīn
Na hakika bila ya shaka itakuwa ni majuto kwa wanao kataa. 50
وَإِنَّهُۥ لَحَقُّ ٱلۡيَقِينِ ٥١
Wa innahū lahaqqul-yaqīn
Na hakika hii bila ya shaka ni haki ya yakini. 51
فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ ٥٢
Fasabbih bismi rabbikal-'azīm
Basi litakase jina la Mola wako Mlezi Mtukufu. 52
Nambari za maelezo ya chini zinaelekeza kwenye ukurasa wa aya, ambapo maelezo ya mfasiri yanaonyeshwa.
Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.
Surat Al-Haqqah ina aya 52. Ni sura namba 69 ya Qur'ani.
Surat Al-Haqqah ni sura Makkiya.
Surat Al-Haqqah iko katika juzuu 29.
Ndiyo. Bonyeza Cheza juu ya ukurasa huu, au anza kutoka aya yoyote. Programu ya Qabas pia inakuwezesha kuipakua ili kuisikiliza bila intaneti.