Surat Al-Mursalat المرسلات

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلۡمُرۡسَلَٰتِ عُرۡفٗا ١

Wal-mursalāti 'urfā

Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole! 1

فَٱلۡعَٰصِفَٰتِ عَصۡفٗا ٢

Fal-'āsifāti 'asfā

Na zinazo vuma kwa kasi! 2

وَٱلنَّٰشِرَٰتِ نَشۡرٗا ٣

Wan-nāshirāti nashrā

Na zikaeneza maeneo yote! 3

فَٱلۡفَٰرِقَٰتِ فَرۡقٗا ٤

Fal-fāriqāti farqā

Na zinazo farikisha zikatawanya! 4

فَٱلۡمُلۡقِيَٰتِ ذِكۡرًا ٥

Fal-mulqiyāti dhikrā

Na zinazo peleka mawaidha! 5

عُذۡرًا أَوۡ نُذۡرًا ٦

'Udhran aw nudhrā

Kwa kuudhuru au kuonya, 6

إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَوَٰقِعٞ ٧

Innamā tū'adūna lawāqi'

Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatakuwa! 7

فَإِذَا ٱلنُّجُومُ طُمِسَتۡ ٨

Fa idhan-nujūmu tumisat

Wakati nyota zitakapo futwa, 8

وَإِذَا ٱلسَّمَآءُ فُرِجَتۡ ٩

Wa idhas-samā'u furijat

Na mbingu zitakapo pasuliwa, 9

وَإِذَا ٱلۡجِبَالُ نُسِفَتۡ ١٠

Wa idhal-jibālu nusifat

Na milima itakapo peperushwa, 10

وَإِذَا ٱلرُّسُلُ أُقِّتَتۡ ١١

Wa idhar-rusulu uqqitat

Na Mitume watakapo wekewa wakati wao, 11

لِأَيِّ يَوۡمٍ أُجِّلَتۡ ١٢

Li ayyi yawmin ujjilat

Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo? 12

لِيَوۡمِ ٱلۡفَصۡلِ ١٣

Liyawmil-fasl

Kwa siku ya kupambanua! 13

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِ ١٤

Wamā adrāka mā yawmul-fasl

Na nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ni nini? 14

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ ١٥

Waylun yawma'idhil lil-mukaddhibīn

Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha! 15

أَلَمۡ نُهۡلِكِ ٱلۡأَوَّلِينَ ١٦

Alam nuhlikil-awwalīn

Kwani hatukuwaangamiza walio tangulia? 16

ثُمَّ نُتۡبِعُهُمُ ٱلۡأٓخِرِينَ ١٧

Thumma nutbi'uhumul-ākhirīn

Kisha tukawafuatilizia walio fuatia? 17

كَذَٰلِكَ نَفۡعَلُ بِٱلۡمُجۡرِمِينَ ١٨

Kadhālika naf'alu bil-mujrimīn

Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu! 18

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ ١٩

Waylun yawma'idhil lil-mukaddhibīn

Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! 19

أَلَمۡ نَخۡلُقكُّم مِّن مَّآءٖ مَّهِينٖ ٢٠

Alam nakhlukkum mim mā'im mahīn

Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa? 20

فَجَعَلۡنَٰهُ فِي قَرَارٖ مَّكِينٍ ٢١

Faja'alnāhu fī qarārim makīn

Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti? 21

إِلَىٰ قَدَرٖ مَّعۡلُومٖ ٢٢

Ilā qadarim ma'lūm

Mpaka muda maalumu? 22

فَقَدَرۡنَا فَنِعۡمَ ٱلۡقَٰدِرُونَ ٢٣

Faqadarnā fani'mal-qādirūn

Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria. 23

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ ٢٤

Waylun yawma'idhil lil-mukaddhibīn

Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! 24

أَلَمۡ نَجۡعَلِ ٱلۡأَرۡضَ كِفَاتًا ٢٥

Alam naj'alil-arda kifātā

Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya 25

أَحۡيَآءٗ وَأَمۡوَٰتٗا ٢٦

Ahyā'an wa amwātā

Walio hai na maiti? 26

وَجَعَلۡنَا فِيهَا رَوَٰسِيَ شَٰمِخَٰتٖ وَأَسۡقَيۡنَٰكُم مَّآءٗ فُرَاتٗا ٢٧

Waja'alnā fīhā rawāsiya shāmikhātin wa asqaynākum mā'an furātā

Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu? 27

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ ٢٨

Waylun yawma'idhil lil-mukaddhibīn

Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! 28

ٱنطَلِقُوٓاْ إِلَىٰ مَا كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ ٢٩

Intaliqū ilā mā kuntum bihī tukaddhibūn

Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha! 29

ٱنطَلِقُوٓاْ إِلَىٰ ظِلّٖ ذِي ثَلَٰثِ شُعَبٖ ٣٠

Intaliqū ilā zillin dhī thalāthi shu'ab

Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu! 30

لَّا ظَلِيلٖ وَلَا يُغۡنِي مِنَ ٱللَّهَبِ ٣١

Llā zalīlin walā yughnī minal-lahab

Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako. 31

إِنَّهَا تَرۡمِي بِشَرَرٖ كَٱلۡقَصۡرِ ٣٢

Innahā tarmī bishararin kal-qasr

Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba! 32

كَأَنَّهُۥ جِمَٰلَتٞ صُفۡرٞ ٣٣

Ka annahū jimālatun sufr

Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano! 33

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ ٣٤

Waylun yawma'idhil lil-mukaddhibīn

Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! 34

هَٰذَا يَوۡمُ لَا يَنطِقُونَ ٣٥

Hādhā yawmu lā yantiqūn

Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu, 35

وَلَا يُؤۡذَنُ لَهُمۡ فَيَعۡتَذِرُونَ ٣٦

Walā yu'dhanu lahum faya'tadhirūn

Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru. 36

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ ٣٧

Waylun yawma'idhil lil-mukaddhibīn

Ole wao siku hiyo hao walio kanusha! 37

هَٰذَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِۖ جَمَعۡنَٰكُمۡ وَٱلۡأَوَّلِينَ ٣٨

Hādhā yawmul-fasli jama'nākum wal-awwalīn

Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia. 38

فَإِن كَانَ لَكُمۡ كَيۡدٞ فَكِيدُونِ ٣٩

Fa in kāna lakum kaydun fakīdūn

kiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi! 39

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ ٤٠

Waylun yawma'idhil lil-mukaddhibīn

Ole wao siku hiyo hao walio kanusha! 40

إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي ظِلَٰلٖ وَعُيُونٖ ٤١

Innal-muttaqīna fī zilālin wa'uyūn

Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem, 41

وَفَوَٰكِهَ مِمَّا يَشۡتَهُونَ ٤٢

Wafawākiha mimmā yashtahūn

Na matunda wanayo yapenda, 42

كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ هَنِيٓـَٔۢا بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ ٤٣

Kulū washrabū hanī'ā bimā kuntum ta'malūn

Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda. 43

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ ٤٤

Innā kadhālika najzil-muhsinīn

Hakika ndio kama hivyo tunavyo walipa watendao mema. 44

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ ٤٥

Waylun yawma'idhil lil-mukaddhibīn

Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! 45

كُلُواْ وَتَمَتَّعُواْ قَلِيلًا إِنَّكُم مُّجۡرِمُونَ ٤٦

Kulū watamatta'ū qalīlan innakum mujrimūn

Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu! 46

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ ٤٧

Waylun yawma'idhil lil-mukaddhibīn

Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! 47

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱرۡكَعُواْ لَا يَرۡكَعُونَ ٤٨

Wa idhā qīla lahumurka'ū lā yarka'ūn

Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami. 48

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ ٤٩

Waylun yawma'idhil lil-mukaddhibīn

Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! 49

فَبِأَيِّ حَدِيثِۭ بَعۡدَهُۥ يُؤۡمِنُونَ ٥٠

Fabi'ayyi hadīthi ba'dahū yu'minūn

Basi maneno gani baada ya haya watayaamini? 50

Nambari za maelezo ya chini zinaelekeza kwenye ukurasa wa aya, ambapo maelezo ya mfasiri yanaonyeshwa.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Maswali

Surat Al-Mursalat ina aya ngapi?

Surat Al-Mursalat ina aya 50. Ni sura namba 77 ya Qur'ani.

Je, Surat Al-Mursalat ni Makkiya au Madaniya?

Surat Al-Mursalat ni sura Makkiya.

Surat Al-Mursalat iko katika juzuu gani?

Surat Al-Mursalat iko katika juzuu 29.

Je, naweza kusikiliza Surat Al-Mursalat?

Ndiyo. Bonyeza Cheza juu ya ukurasa huu, au anza kutoka aya yoyote. Programu ya Qabas pia inakuwezesha kuipakua ili kuisikiliza bila intaneti.