Surat An-Naba النبإ

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

عَمَّ يَتَسَآءَلُونَ ١

'Amma yatasā'alūn

WANAULIZANA nini? 1

عَنِ ٱلنَّبَإِ ٱلۡعَظِيمِ ٢

'Anin-naba'il-'azīm

Ile khabari kuu! 2

ٱلَّذِي هُمۡ فِيهِ مُخۡتَلِفُونَ ٣

Alladhī hum fīhi mukhtalifūn

Ambayo kwayo wanakhitalifiana. 3

كَلَّا سَيَعۡلَمُونَ ٤

Kallā saya'lamūn

La! Karibu watakuja jua. 4

ثُمَّ كَلَّا سَيَعۡلَمُونَ ٥

Thumma kallā saya'lamūn

Tena la! Karibu watakuja jua. 5

أَلَمۡ نَجۡعَلِ ٱلۡأَرۡضَ مِهَٰدٗا ٦

Alam naj'alil-arda mihādā

kaKwani hatukuifanya ardhi ma tandiko? 6

وَٱلۡجِبَالَ أَوۡتَادٗا ٧

Wal-jibāla awtādā

kama Na milima vigingi? 7

وَخَلَقۡنَٰكُمۡ أَزۡوَٰجٗا ٨

Wakhalaqnākum azwājā

Na tukakuumbeni kwa jozi? 8

وَجَعَلۡنَا نَوۡمَكُمۡ سُبَاتٗا ٩

Waja'alnā nawmakum subātā

Na tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko? 9

وَجَعَلۡنَا ٱلَّيۡلَ لِبَاسٗا ١٠

Waja'alnal-layla libāsā

Na tukaufanya usiku ni nguo? 10

وَجَعَلۡنَا ٱلنَّهَارَ مَعَاشٗا ١١

Waja'alnan-nahāra ma'āshā

Na tukaufanya mchana ni wa kuchumia maisha? 11

وَبَنَيۡنَا فَوۡقَكُمۡ سَبۡعٗا شِدَادٗا ١٢

Wabanaynā fawqakum sab'an shidādā

Na tukajenga juu yenu saba zenye nguvu? 12

وَجَعَلۡنَا سِرَاجٗا وَهَّاجٗا ١٣

Waja'alnā sirājan wahhājā

Na tukaifanya taa yenye mwanga na joto; 13

وَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلۡمُعۡصِرَٰتِ مَآءٗ ثَجَّاجٗا ١٤

Wa anzalnā minal-mu'sirāti mā'an thajjājā

Na tukateremsha maji yanayo anguka kwa kasi kutoka mawinguni, 14

لِّنُخۡرِجَ بِهِۦ حَبّٗا وَنَبَاتٗا ١٥

Llinukhrija bihī habban wanabātā

Ili tutoe kwayo nafaka na mimea. 15

وَجَنَّٰتٍ أَلۡفَافًا ١٦

Wajannātin alfāfā

Na mabustani yenye miti iliyo kamatana. 16

إِنَّ يَوۡمَ ٱلۡفَصۡلِ كَانَ مِيقَٰتٗا ١٧

Inna yawmal-fasli kāna mīqātā

Hakika siku ya uamuzi imewekewa wakati wake, 17

يَوۡمَ يُنفَخُ فِي ٱلصُّورِ فَتَأۡتُونَ أَفۡوَاجٗا ١٨

Yawma yunfakhu fis-sūri fata'tūna afwājā

Siku litapo pulizwa barugumu, nanyi mtakuja kwa makundi, 18

وَفُتِحَتِ ٱلسَّمَآءُ فَكَانَتۡ أَبۡوَٰبٗا ١٩

Wafutihatis-samā'u fakānat abwābā

Na mbingu zitafunguliwa, ziwe milango. 19

وَسُيِّرَتِ ٱلۡجِبَالُ فَكَانَتۡ سَرَابًا ٢٠

Wasuyyiratil-jibālu fakānat sarābā

Na milima itaondolewa na itakuwa kama sarabi. 20

إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتۡ مِرۡصَادٗا ٢١

Inna jahannama kānat mirsādā

Hakika Jahannamu inangojea! 21

لِّلطَّٰغِينَ مَـَٔابٗا ٢٢

Llit-tāghīna ma'ābā

Kwa walio asi ndio makaazi yao, 22

لَّٰبِثِينَ فِيهَآ أَحۡقَابٗا ٢٣

Llābithīna fīhā ahqābā

Wakae humo karne baada ya karne, 23

لَّا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرۡدٗا وَلَا شَرَابًا ٢٤

Llā yadhūqūna fīhā bardan walā sharābā

Hawataonja humo chochote kibaridi wala kinywaji, 24

إِلَّا حَمِيمٗا وَغَسَّاقٗا ٢٥

Illā hamīman waghassāqā

Ila maji yamoto sana na usaha, 25

جَزَآءٗ وِفَاقًا ٢٦

Jazā'an wifāqā

Ndio jaza muwafaka. 26

إِنَّهُمۡ كَانُواْ لَا يَرۡجُونَ حِسَابٗا ٢٧

Innahum kānū lā yarjūna hisābā

Hakika hao hawakuwa wakitaraji kuwa kuna hisabu. 27

وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا كِذَّابٗا ٢٨

Wakaddhabū bi'āyātinā kiddhābā

Na wakikanusha Aya zetu kwa nguvu. 28

وَكُلَّ شَيۡءٍ أَحۡصَيۡنَٰهُ كِتَٰبٗا ٢٩

Wakulla shay'in ahsaynāhu kitābā

Na kila kitu Sisi tumekidhibiti kwa kukiandika. 29

فَذُوقُواْ فَلَن نَّزِيدَكُمۡ إِلَّا عَذَابًا ٣٠

Fadhūqū falan nazīdakum illā 'adhābā

Basi onjeni! Nasi hatutakuzidishieni ila adhabu! 30

إِنَّ لِلۡمُتَّقِينَ مَفَازًا ٣١

Inna lil-muttaqīna mafāzā

Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu, 31

حَدَآئِقَ وَأَعۡنَٰبٗا ٣٢

Hadā'iqa wa a'nābā

Mabustani na mizabibu, 32

وَكَوَاعِبَ أَتۡرَابٗا ٣٣

Wakawā'iba atrābā

Na wake walio lingana nao, 33

وَكَأۡسٗا دِهَاقٗا ٣٤

Waka'san dihāqā

Na bilauri zilizo jaa, 34

لَّا يَسۡمَعُونَ فِيهَا لَغۡوٗا وَلَا كِذَّٰبٗا ٣٥

Llā yasma'ūna fīhā laghwan walā kiddhābā

Hawatasikia humo upuuzi wala uwongo, 35

جَزَآءٗ مِّن رَّبِّكَ عَطَآءً حِسَابٗا ٣٦

Jazā'am mir rabbika 'atā'an hisābā

Malipo kutoka kwa Mola wako Mlezi, kipawa cha kutosha. 36

رَّبِّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا ٱلرَّحۡمَٰنِۖ لَا يَمۡلِكُونَ مِنۡهُ خِطَابٗا ٣٧

Rrabbis-samāwāti wal-ardi wamā baynahumar-rahmāni lā yamlikūna minhu khitābā

Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, Arrahman, Mwingi wa rehema; hawamiliki usemi mbele yake! 37

يَوۡمَ يَقُومُ ٱلرُّوحُ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ صَفّٗاۖ لَّا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنۡ أَذِنَ لَهُ ٱلرَّحۡمَٰنُ وَقَالَ صَوَابٗا ٣٨

Yawma yaqūmur-rūhu wal-malā'ikatu saffal lā yatakallamūna illā man adhina lahur-rahmānu waqāla sawābā

Siku atakapo simama Roho na Malaika kwa safu. Hawatasema ila Mwingi wa rehema aliye mruhusu, na atasema yaliyo sawa tu. 38

ذَٰلِكَ ٱلۡيَوۡمُ ٱلۡحَقُّۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ مَـَٔابًا ٣٩

Dhālikal-yawmul-haqqu faman shā'at-takhadha ilā rabbihī ma'ābā

Hiyo ndiyo Siku ya haki. Basi anaye taka na ashike njia arejee kwa Mola wake Mlezi 39

إِنَّآ أَنذَرۡنَٰكُمۡ عَذَابٗا قَرِيبٗا يَوۡمَ يَنظُرُ ٱلۡمَرۡءُ مَا قَدَّمَتۡ يَدَاهُ وَيَقُولُ ٱلۡكَافِرُ يَٰلَيۡتَنِي كُنتُ تُرَٰبَۢا ٤٠

Innā andharnākum 'adhāban qarīban yawma yanzurul-mar'u mā qaddamat yadāhu wayaqūlul-kāfiru yālaytanī kuntu turābā

Hakika tumekuhadharisheni adhabu iliyo karibu kufika; Siku ambayo mtu atakapo ona yaliyo tangulizwa na mikono yake; na kafiri atasema: Laiti ningeli kuwa udongo! 40

Nambari za maelezo ya chini zinaelekeza kwenye ukurasa wa aya, ambapo maelezo ya mfasiri yanaonyeshwa.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Maswali

Surat An-Naba ina aya ngapi?

Surat An-Naba ina aya 40. Ni sura namba 78 ya Qur'ani.

Je, Surat An-Naba ni Makkiya au Madaniya?

Surat An-Naba ni sura Makkiya.

Surat An-Naba iko katika juzuu gani?

Surat An-Naba iko katika juzuu 30.

Je, naweza kusikiliza Surat An-Naba?

Ndiyo. Bonyeza Cheza juu ya ukurasa huu, au anza kutoka aya yoyote. Programu ya Qabas pia inakuwezesha kuipakua ili kuisikiliza bila intaneti.