Surat Al-Mutaffifin المطففين

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَيۡلٞ لِّلۡمُطَفِّفِينَ ١

Waylul lil-mutaffifīn

Ole wao hao wapunjao! 1

ٱلَّذِينَ إِذَا ٱكۡتَالُواْ عَلَى ٱلنَّاسِ يَسۡتَوۡفُونَ ٢

Alladhīna idhaktālū 'alan-nāsi yastawfūn

Ambao wanapo jipimia kwa watu hudai watimiziwe. 2

وَإِذَا كَالُوهُمۡ أَو وَّزَنُوهُمۡ يُخۡسِرُونَ ٣

Wa idhā kālūhum aw wazanūhum yukhsirūn

Na wao wanapo wapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza. 3

أَلَا يَظُنُّ أُوْلَٰٓئِكَ أَنَّهُم مَّبۡعُوثُونَ ٤

Alā yazunnu ulā'ika annahum mab'ūthūn

Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa . 4

لِيَوۡمٍ عَظِيمٖ ٥

Liyawmin 'azīm

Katika Siku iliyo kuu! 5

يَوۡمَ يَقُومُ ٱلنَّاسُ لِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ٦

Yawma yaqūmun-nāsu lirabbil-'ālamīn

Siku watapo msimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote? 6

كَلَّآ إِنَّ كِتَٰبَ ٱلۡفُجَّارِ لَفِي سِجِّينٖ ٧

Kallā inna kitābal-fujjāri lafī sijjīn

Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin. 7

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا سِجِّينٞ ٨

Wamā adrāka mā sijjīn

Unajua nini Sijjin? 8

كِتَٰبٞ مَّرۡقُومٞ ٩

Kitābum marqūm

Kitabu kilicho andikwa. 9

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ ١٠

Waylun yawma'idhil lil-mukaddhibīn

Ole wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha! 10

ٱلَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوۡمِ ٱلدِّينِ ١١

Alladhīna yukaddhibūna biyawmid-dīn

Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo. 11

وَمَا يُكَذِّبُ بِهِۦٓ إِلَّا كُلُّ مُعۡتَدٍ أَثِيمٍ ١٢

Wamā yukaddhibu bihī illā kullu mu'tadin athīm

Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi. 12

إِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِ ءَايَٰتُنَا قَالَ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ ١٣

Idhā tutlā 'alayhi āyātunā qāla asātīrul-awwalīn

Anapo somewa Aya zetu husema: Ni visa vya watu wa kale! 13

كَلَّاۖ بَلۡۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ ١٤

Kallā bal rāna 'alā qulūbihim mā kānū yaksibūn

Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao walio kuwa wakiyachuma. 14

كَلَّآ إِنَّهُمۡ عَن رَّبِّهِمۡ يَوۡمَئِذٖ لَّمَحۡجُوبُونَ ١٥

Kallā innahum 'ar rabbihim yawma'idhil lamahjūbūn

Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa na neema za Mola wao Mlezi. 15

ثُمَّ إِنَّهُمۡ لَصَالُواْ ٱلۡجَحِيمِ ١٦

Thumma innahum lasālul-jahīm

Kisha wataingia Motoni! 16

ثُمَّ يُقَالُ هَٰذَا ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ ١٧

Thumma yuqālu hādhal-ladhī kuntum bihī tukaddhibūn

Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyakadhabisha. 17

كَلَّآ إِنَّ كِتَٰبَ ٱلۡأَبۡرَارِ لَفِي عِلِّيِّينَ ١٨

Kallā inna kitābal-abrāri lafī 'illiyyīn

Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika I'liyyin. 18

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا عِلِّيُّونَ ١٩

Wamā adrāka mā 'illiyyūn

Na nini kitakacho kujuvya nini I'liyyin? 19

كِتَٰبٞ مَّرۡقُومٞ ٢٠

Kitābum marqūm

Kitabu kilicho andikwa. 20

يَشۡهَدُهُ ٱلۡمُقَرَّبُونَ ٢١

Yashhaduhul-muqarrabūn

Wanakishuhudia walio karibishwa. 21

إِنَّ ٱلۡأَبۡرَارَ لَفِي نَعِيمٍ ٢٢

Innal-abrāra lafī na'īm

Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema. 22

عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِ يَنظُرُونَ ٢٣

'Alal-arā'iki yanzurūn

Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia. 23

تَعۡرِفُ فِي وُجُوهِهِمۡ نَضۡرَةَ ٱلنَّعِيمِ ٢٤

Ta'rifu fī wujūhihim nadratan-na'īm

Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema, 24

يُسۡقَوۡنَ مِن رَّحِيقٖ مَّخۡتُومٍ ٢٥

Yusqawna mir rahīqim makhtūm

Watanyweshwa kinywaji safi kiliyo tiwa muhuri, 25

خِتَٰمُهُۥ مِسۡكٞۚ وَفِي ذَٰلِكَ فَلۡيَتَنَافَسِ ٱلۡمُتَنَٰفِسُونَ ٢٦

Khitāmuhū miskun wafī dhālika falyatanāfasil-mutanāfisūn

Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindanie wenye kushindana. 26

وَمِزَاجُهُۥ مِن تَسۡنِيمٍ ٢٧

Wamizājuhū min tasnīm

Na mchanganyiko wake ni Tasniim, 27

عَيۡنٗا يَشۡرَبُ بِهَا ٱلۡمُقَرَّبُونَ ٢٨

'Aynan yashrabu bihal-muqarrabūn

Chemchem watakayo inywa walio kurubishwa. 28

إِنَّ ٱلَّذِينَ أَجۡرَمُواْ كَانُواْ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ يَضۡحَكُونَ ٢٩

Innal-ladhīna ajramū kānū minal-ladhīna āmanū yadhakūn

Kwa hakika wale walio kuwa wakosefu walikuwa wakiwacheka walio amini. 29

وَإِذَا مَرُّواْ بِهِمۡ يَتَغَامَزُونَ ٣٠

Wa idhā marrū bihim yataghāmazūn

Na wanapo pita karibu yao wakikonyezana. 30

وَإِذَا ٱنقَلَبُوٓاْ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِمُ ٱنقَلَبُواْ فَكِهِينَ ٣١

Wa idhanqalabū ilā ahlihimunqalabū fakihīn

Na wanapo rudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi. 31

وَإِذَا رَأَوۡهُمۡ قَالُوٓاْ إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ لَضَآلُّونَ ٣٢

Wa idhā ra'awhum qālū inna hā'ulā'i ladāllūn

Na wanapo waona husema: Hakika hawa ndio khasa walio potea. 32

وَمَآ أُرۡسِلُواْ عَلَيۡهِمۡ حَٰفِظِينَ ٣٣

Wamā ursilū 'alayhim hāfizīn

Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao. 33

فَٱلۡيَوۡمَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنَ ٱلۡكُفَّارِ يَضۡحَكُونَ ٣٤

Fal-yawmal-ladhīna āmanū minal-kuffāri yadhakūn

Basi leo walio amini ndio watawacheka makafiri, 34

عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِ يَنظُرُونَ ٣٥

'Alal-arā'iki yanzurūn

Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia. 35

هَلۡ ثُوِّبَ ٱلۡكُفَّارُ مَا كَانُواْ يَفۡعَلُونَ ٣٦

Hal thuwwibal-kuffāru mā kānū yaf'alūn

Je! makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda? 36

Nambari za maelezo ya chini zinaelekeza kwenye ukurasa wa aya, ambapo maelezo ya mfasiri yanaonyeshwa.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Maswali

Surat Al-Mutaffifin ina aya ngapi?

Surat Al-Mutaffifin ina aya 36. Ni sura namba 83 ya Qur'ani.

Je, Surat Al-Mutaffifin ni Makkiya au Madaniya?

Surat Al-Mutaffifin ni sura Makkiya.

Surat Al-Mutaffifin iko katika juzuu gani?

Surat Al-Mutaffifin iko katika juzuu 30.

Je, naweza kusikiliza Surat Al-Mutaffifin?

Ndiyo. Bonyeza Cheza juu ya ukurasa huu, au anza kutoka aya yoyote. Programu ya Qabas pia inakuwezesha kuipakua ili kuisikiliza bila intaneti.