إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنشَقَّتۡ ١
Idhas-samā'unshaqqat
Itapo chanika mbingu! 1
Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنشَقَّتۡ ١
Idhas-samā'unshaqqat
Itapo chanika mbingu! 1
وَأَذِنَتۡ لِرَبِّهَا وَحُقَّتۡ ٢
Wa adhinat lirabbihā wahuqqat
Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza! 2
وَإِذَا ٱلۡأَرۡضُ مُدَّتۡ ٣
Wa idhal-ardu muddat
Na ardhi itakapo tanuliwa! 3
وَأَلۡقَتۡ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتۡ ٤
Wa alqat mā fīhā watakhallat
Na kuvitoa vilivyo kuwa ndani yake, ikawa tupu! 4
وَأَذِنَتۡ لِرَبِّهَا وَحُقَّتۡ ٥
Wa adhinat lirabbihā wahuqqat
Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza! 5
يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡإِنسَٰنُ إِنَّكَ كَادِحٌ إِلَىٰ رَبِّكَ كَدۡحٗا فَمُلَٰقِيهِ ٦
Yā'ayyuhal-insānu innaka kādihun ilā rabbika kadhan famulāqīh
Ewe mtu! Hakika wewe unajikusuru kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta. 6
فَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ ٧
Fa ammā man ūtiya kitābahū biyamīnih
Ama atakaye pewa daftari lake kwa mkono wa kulia! 7
فَسَوۡفَ يُحَاسَبُ حِسَابٗا يَسِيرٗا ٨
Fasawfa yuhāsabu hisāban yasīrā
Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi! 8
وَيَنقَلِبُ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ مَسۡرُورٗا ٩
Wayanqalibu ilā ahlihī masrūrā
Na arudi kwa ahali zake na furaha. 9
وَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ وَرَآءَ ظَهۡرِهِۦ ١٠
Wa ammā man ūtiya kitābahū warā'a zahrih
Na ama atakaye pewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake, 10
فَسَوۡفَ يَدۡعُواْ ثُبُورٗا ١١
Fasawfa yad'ū thubūrā
Basi huyo ataomba kuteketea. 11
وَيَصۡلَىٰ سَعِيرًا ١٢
Wayaslā sa'īrā
Na ataingia Motoni. 12
إِنَّهُۥ كَانَ فِيٓ أَهۡلِهِۦ مَسۡرُورًا ١٣
Innahū kāna fī ahlihī masrūrā
Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake. 13
إِنَّهُۥ ظَنَّ أَن لَّن يَحُورَ ١٤
Innahū zanna al lan yahūr
Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena. 14
بَلَىٰٓۚ إِنَّ رَبَّهُۥ كَانَ بِهِۦ بَصِيرٗا ١٥
Balā inna rabbahū kāna bihī basīrā
Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona! 15
فَلَآ أُقۡسِمُ بِٱلشَّفَقِ ١٦
Falā uqsimu bish-shafaq
Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapo kuchwa, 16
وَٱلَّيۡلِ وَمَا وَسَقَ ١٧
Wallayli wamā wasaq
Na kwa usiku na unavyo vikusanya, 17
وَٱلۡقَمَرِ إِذَا ٱتَّسَقَ ١٨
Wal-qamari idhat-tasaq
Na kwa mwezi unapo pevuka, 18
لَتَرۡكَبُنَّ طَبَقًا عَن طَبَقٖ ١٩
Latarkabunna tabaqan 'an tabaq
Lazima mtapanda t'abaka kwa t'abaka! 19
فَمَا لَهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ ٢٠
Famā lahum lā yu'minūn
Basi wana nini hawaamini? 20
وَإِذَا قُرِئَ عَلَيۡهِمُ ٱلۡقُرۡءَانُ لَا يَسۡجُدُونَۤ۩ ٢١
Wa idhā quri'a 'alayhimul-qur'ānu lā yasjudūn
Na wanapo somewa Qur'ani hawasujudu? 21
بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يُكَذِّبُونَ ٢٢
Balil-ladhīna kafarū yukaddhibūn
Bali walio kufuru wanakanusha tu. 22
وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا يُوعُونَ ٢٣
Wallāhu a'lamu bimā yū'ūn
Na Mwenyezi Mungu anajua wanayo yadhamiria. 23
فَبَشِّرۡهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ٢٤
Fabasshirhum bi'adhābin alīm
Basi wabashirie adhabu chungu! 24
إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَهُمۡ أَجۡرٌ غَيۡرُ مَمۡنُونِۭ ٢٥
Illal-ladhīna āmanū wa'amilus-sālihāti lahum ajrun ghayru mamnūn
Isipo kuwa wale walio amini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usio malizika. 25
Nambari za maelezo ya chini zinaelekeza kwenye ukurasa wa aya, ambapo maelezo ya mfasiri yanaonyeshwa.
Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.
Surat Al-Inshiqaq ina aya 25. Ni sura namba 84 ya Qur'ani.
Surat Al-Inshiqaq ni sura Makkiya.
Surat Al-Inshiqaq iko katika juzuu 30.
Ndiyo. Bonyeza Cheza juu ya ukurasa huu, au anza kutoka aya yoyote. Programu ya Qabas pia inakuwezesha kuipakua ili kuisikiliza bila intaneti.