إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنفَطَرَتۡ ١
Idhas-samā'unfatarat
Mbingu itapo chanika! 1
Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنفَطَرَتۡ ١
Idhas-samā'unfatarat
Mbingu itapo chanika! 1
وَإِذَا ٱلۡكَوَاكِبُ ٱنتَثَرَتۡ ٢
Wa idhal-kawākibuntatharat
Na nyota zitapo tawanyika! 2
وَإِذَا ٱلۡبِحَارُ فُجِّرَتۡ ٣
Wa idhal-bihāru fujjirat
Na bahari zitakapo pasuliwa! 3
وَإِذَا ٱلۡقُبُورُ بُعۡثِرَتۡ ٤
Wa idhal-qubūru bu'thirat
Na makaburi yatapo fukuliwa! 4
عَلِمَتۡ نَفۡسٞ مَّا قَدَّمَتۡ وَأَخَّرَتۡ ٥
'Alimat nafsum mā qaddamat wa akkharat
Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilicho bakisha nyuma. 5
يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡإِنسَٰنُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ ٱلۡكَرِيمِ ٦
Yā'ayyuhal-insānu mā gharraka birabbikal-karīm
Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu? 6
ٱلَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّىٰكَ فَعَدَلَكَ ٧
Alladhī khalaqaka fasawwāka fa'adalak
Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha! 7
فِيٓ أَيِّ صُورَةٖ مَّا شَآءَ رَكَّبَكَ ٨
Fī ayyi sūratim mā shā'a rakkabak
Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga. 8
كَلَّا بَلۡ تُكَذِّبُونَ بِٱلدِّينِ ٩
Kallā bal tukaddhibūna bid-dīn
Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo. 9
وَإِنَّ عَلَيۡكُمۡ لَحَٰفِظِينَ ١٠
Wa inna 'alaykum lahāfizīn
Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu, 10
كِرَامٗا كَٰتِبِينَ ١١
Kirāman kātibīn
Waandishi wenye hishima, 11
يَعۡلَمُونَ مَا تَفۡعَلُونَ ١٢
Ya'lamūna mā taf'alūn
Wanayajua mnayo yatenda. 12
إِنَّ ٱلۡأَبۡرَارَ لَفِي نَعِيمٖ ١٣
Innal-abrāra lafī na'īm
Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema, 13
وَإِنَّ ٱلۡفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٖ ١٤
Wa innal-fujjāra lafī jahīm
Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni; 14
يَصۡلَوۡنَهَا يَوۡمَ ٱلدِّينِ ١٥
Yaslawnahā yawmad-dīn
Wataingia humo Siku ya Malipo. 15
وَمَا هُمۡ عَنۡهَا بِغَآئِبِينَ ١٦
Wamā hum 'anhā bighā'ibīn
Na hawatoacha kuwamo humo. 16
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ ١٧
Wamā adrāka mā yawmud-dīn
Na nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani? 17
ثُمَّ مَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ ١٨
Thumma mā adrāka mā yawmud-dīn
Tena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani? 18
يَوۡمَ لَا تَمۡلِكُ نَفۡسٞ لِّنَفۡسٖ شَيۡـٔٗاۖ وَٱلۡأَمۡرُ يَوۡمَئِذٖ لِّلَّهِ ١٩
Yawma lā tamliku nafsul linafsin shay'an wal-amru yawma'idhi lillāh
Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu. 19
Nambari za maelezo ya chini zinaelekeza kwenye ukurasa wa aya, ambapo maelezo ya mfasiri yanaonyeshwa.
Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.
Surat Al-Infitar ina aya 19. Ni sura namba 82 ya Qur'ani.
Surat Al-Infitar ni sura Makkiya.
Surat Al-Infitar iko katika juzuu 30.
Ndiyo. Bonyeza Cheza juu ya ukurasa huu, au anza kutoka aya yoyote. Programu ya Qabas pia inakuwezesha kuipakua ili kuisikiliza bila intaneti.