Surat At-Takwir التكوير

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

إِذَا ٱلشَّمۡسُ كُوِّرَتۡ ١

Idhash-shamsu kuwwirat

Jua litakapo kunjwa! 1

وَإِذَا ٱلنُّجُومُ ٱنكَدَرَتۡ ٢

Wa idhan-nujūmunkadarat

Na nyota zikazimwa! 2

وَإِذَا ٱلۡجِبَالُ سُيِّرَتۡ ٣

Wa idhal-jibālu suyyirat

Na milima ikaondolewa! 3

وَإِذَا ٱلۡعِشَارُ عُطِّلَتۡ ٤

Wa idhal-'ishāru 'uttilat

Na ngamia wenye mimba pevu watakapo achwa wasishughulikiwe, 4

وَإِذَا ٱلۡوُحُوشُ حُشِرَتۡ ٥

Wa idhal-wuhūshu hushirat

Na wanyama wa mwituni wakakusanywa! 5

وَإِذَا ٱلۡبِحَارُ سُجِّرَتۡ ٦

Wa idhal-bihāru sujjirat

Na bahari zikawaka moto! 6

وَإِذَا ٱلنُّفُوسُ زُوِّجَتۡ ٧

Wa idhan-nufūsu zuwwijat

Na nafsi zikaunganishwa! 7

وَإِذَا ٱلۡمَوۡءُۥدَةُ سُئِلَتۡ ٨

Wa idhal-maw'ūdatu su'ilat

Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa! 8

بِأَيِّ ذَنۢبٖ قُتِلَتۡ ٩

Bi ayyi dhambin qutilat

Kwa kosa gani aliuliwa? 9

وَإِذَا ٱلصُّحُفُ نُشِرَتۡ ١٠

Wa idhas-suhufu nushirat

Na madaftari yatakapo enezwa, 10

وَإِذَا ٱلسَّمَآءُ كُشِطَتۡ ١١

Wa idhas-samā'u kushitat

Na mbingu itapo tanduliwa, 11

وَإِذَا ٱلۡجَحِيمُ سُعِّرَتۡ ١٢

Wa idhal-jahīmu su''irat

Na Jahannamu itapo chochewa, 12

وَإِذَا ٱلۡجَنَّةُ أُزۡلِفَتۡ ١٣

Wa idhal-jannatu uzlifat

Na Pepo ikasogezwa, 13

عَلِمَتۡ نَفۡسٞ مَّآ أَحۡضَرَتۡ ١٤

'Alimat nafsum mā ahdarat

Kila nafsi itajua ilicho kihudhurisha. 14

فَلَآ أُقۡسِمُ بِٱلۡخُنَّسِ ١٥

Falā uqsimu bil-khunnas

Naapa kwa nyota zinapo rejea nyuma, 15

ٱلۡجَوَارِ ٱلۡكُنَّسِ ١٦

Al-jawāril-kunnas

Zinazo kwenda, kisha zikajificha, 16

وَٱلَّيۡلِ إِذَا عَسۡعَسَ ١٧

Wallayli idhā 'as'as

Na kwa usiku unapo pungua, 17

وَٱلصُّبۡحِ إِذَا تَنَفَّسَ ١٨

Was-subhi idhā tanaffas

Na kwa asubuhi inapo pambazuka, 18

إِنَّهُۥ لَقَوۡلُ رَسُولٖ كَرِيمٖ ١٩

Innahū laqawlu rasūlin karīm

Kwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu, 19

ذِي قُوَّةٍ عِندَ ذِي ٱلۡعَرۡشِ مَكِينٖ ٢٠

Dhī quwwatin 'inda dhil-'arshi makīn

Mwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye Kiti cha Enzi, 20

مُّطَاعٖ ثَمَّ أَمِينٖ ٢١

Mmutā'in thamma amīn

Anaye t'iiwa, tena muaminifu. 21

وَمَا صَاحِبُكُم بِمَجۡنُونٖ ٢٢

Wamā sāhibukum bimajnūn

Na wala huyu mwenzenu hana wazimu. 22

وَلَقَدۡ رَءَاهُ بِٱلۡأُفُقِ ٱلۡمُبِينِ ٢٣

Walaqad ra'āhu bil-ufuqil-mubīn

Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi. 23

وَمَا هُوَ عَلَى ٱلۡغَيۡبِ بِضَنِينٖ ٢٤

Wamā huwa 'alal-ghaybi bidanīn

Wala yeye si bakhili kwa mambo ya ghaibu. 24

وَمَا هُوَ بِقَوۡلِ شَيۡطَٰنٖ رَّجِيمٖ ٢٥

Wamā huwa biqawli shaytānir rajīm

Wala hii si kauli ya Shetani maluuni. 25

فَأَيۡنَ تَذۡهَبُونَ ٢٦

Fa ayna tadhhabūn

Basi mnakwenda wapi? 26

إِنۡ هُوَ إِلَّا ذِكۡرٞ لِّلۡعَٰلَمِينَ ٢٧

In huwa illā dhikrul lil-'ālamīn

Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote. 27

لِمَن شَآءَ مِنكُمۡ أَن يَسۡتَقِيمَ ٢٨

Liman shā'a minkum an yastaqīm

Kwa yule miongoni mwenu anaye taka kwenda sawa. 28

وَمَا تَشَآءُونَ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ رَبُّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ٢٩

Wamā tashā'ūna illā an yashā'allāhu rabbul-'ālamīn

Wala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote. 29

Nambari za maelezo ya chini zinaelekeza kwenye ukurasa wa aya, ambapo maelezo ya mfasiri yanaonyeshwa.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Maswali

Surat At-Takwir ina aya ngapi?

Surat At-Takwir ina aya 29. Ni sura namba 81 ya Qur'ani.

Je, Surat At-Takwir ni Makkiya au Madaniya?

Surat At-Takwir ni sura Makkiya.

Surat At-Takwir iko katika juzuu gani?

Surat At-Takwir iko katika juzuu 30.

Je, naweza kusikiliza Surat At-Takwir?

Ndiyo. Bonyeza Cheza juu ya ukurasa huu, au anza kutoka aya yoyote. Programu ya Qabas pia inakuwezesha kuipakua ili kuisikiliza bila intaneti.