Surat 'Abasa عبس

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

عَبَسَ وَتَوَلَّىٰٓ ١

'Abasa watawallā

Alikunja kipaji na akageuka! 1

أَن جَآءَهُ ٱلۡأَعۡمَىٰ ٢

An jā'ahul-a'mā

Kwa sababu alimjia kipofu! 2

وَمَا يُدۡرِيكَ لَعَلَّهُۥ يَزَّكَّىٰٓ ٣

Wamā yudrīka la'allahū yazzakkā

Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika? 3

أَوۡ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ ٱلذِّكۡرَىٰٓ ٤

Aw yaddhakkaru fatanfa'ahudh-dhikrā

Au atawaidhika, na mawaidha yamfae? 4

أَمَّا مَنِ ٱسۡتَغۡنَىٰ ٥

Ammā manistaghnā

Ama ajionaye hana haja! 5

فَأَنتَ لَهُۥ تَصَدَّىٰ ٦

Fa anta lahū tasaddā

Wewe ndio unamshughulikia? 6

وَمَا عَلَيۡكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ ٧

Wamā 'alayka allā yazzakkā

Na si juu yako kama hakutakasika. 7

وَأَمَّا مَن جَآءَكَ يَسۡعَىٰ ٨

Wa ammā man jā'aka yas'ā

Ama anaye kujia kwa juhudi . 8

وَهُوَ يَخۡشَىٰ ٩

Wahuwa yakhshā

Naye anaogopa! 9

فَأَنتَ عَنۡهُ تَلَهَّىٰ ١٠

Fa anta 'anhu talahhā

Ndio wewe unampuuza? 10

كَلَّآ إِنَّهَا تَذۡكِرَةٞ ١١

Kallā innahā tadhkirah

Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana. 11

فَمَن شَآءَ ذَكَرَهُۥ ١٢

Faman shā'a dhakarah

Basi anaye penda akumbuke. 12

فِي صُحُفٖ مُّكَرَّمَةٖ ١٣

Fī suhufim mukarramah

Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa, 13

مَّرۡفُوعَةٖ مُّطَهَّرَةِۭ ١٤

Mmarfū'atim mutahharah

Zilizo inuliwa, zilizo takaswa. 14

بِأَيۡدِي سَفَرَةٖ ١٥

Bi aydī safarah

Zimo mikononi mwa Malaika waandishi, 15

كِرَامِۭ بَرَرَةٖ ١٦

Kirāmi bararah

Watukufu, wema. 16

قُتِلَ ٱلۡإِنسَٰنُ مَآ أَكۡفَرَهُۥ ١٧

Qutilal-insānu mā akfarah

Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha? 17

مِنۡ أَيِّ شَيۡءٍ خَلَقَهُۥ ١٨

Min ayyi shay'in khalaqah

Kwa kitu gani amemuumba? 18

مِن نُّطۡفَةٍ خَلَقَهُۥ فَقَدَّرَهُۥ ١٩

Min nutfatin khalaqahū faqaddarah

Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria. 19

ثُمَّ ٱلسَّبِيلَ يَسَّرَهُۥ ٢٠

Thummas-sabīla yassarah

Kisha akamsahilishia njia. 20

ثُمَّ أَمَاتَهُۥ فَأَقۡبَرَهُۥ ٢١

Thumma amātahū fa aqbarah

Kisha akamfisha, akamtia kaburini. 21

ثُمَّ إِذَا شَآءَ أَنشَرَهُۥ ٢٢

Thumma idhā shā'a ansharah

Kisha apendapo atamfufua. 22

كَلَّا لَمَّا يَقۡضِ مَآ أَمَرَهُۥ ٢٣

Kallā lammā yaqdi mā amarah

La! Hajamaliza aliyo muamuru. 23

فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَٰنُ إِلَىٰ طَعَامِهِۦٓ ٢٤

Falyanzuril-insānu ilā ta'āmih

Hebu mtu na atazame chakula chake. 24

أَنَّا صَبَبۡنَا ٱلۡمَآءَ صَبّٗا ٢٥

Annā sababnal-mā'a sabbā

Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu, 25

ثُمَّ شَقَقۡنَا ٱلۡأَرۡضَ شَقّٗا ٢٦

Thumma shaqaqnal-arda shaqqā

Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu, 26

فَأَنۢبَتۡنَا فِيهَا حَبّٗا ٢٧

Fa ambatnā fīhā habbā

Kisha tukaotesha humo nafaka, 27

وَعِنَبٗا وَقَضۡبٗا ٢٨

Wa'inaban waqadbā

Na zabibu, na mimea ya majani, 28

وَزَيۡتُونٗا وَنَخۡلٗا ٢٩

Wazaytūnan wanakhlā

Na mizaituni, na mitende, 29

وَحَدَآئِقَ غُلۡبٗا ٣٠

Wahadā'iqa ghulbā

Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara, 30

وَفَٰكِهَةٗ وَأَبّٗا ٣١

Wafākihatan wa abbā

Na matunda, na malisho ya wanyama; 31

مَّتَٰعٗا لَّكُمۡ وَلِأَنۡعَٰمِكُمۡ ٣٢

Mmatā'al lakum wali'an'āmikum

Kwa manufaa yenu na mifugo yenu. 32

فَإِذَا جَآءَتِ ٱلصَّآخَّةُ ٣٣

Fa idhā jā'atis-sākkhah

Basi utakapo kuja ukelele, 33

يَوۡمَ يَفِرُّ ٱلۡمَرۡءُ مِنۡ أَخِيهِ ٣٤

Yawma yafirrul-mar'u min akhīh

Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye, 34

وَأُمِّهِۦ وَأَبِيهِ ٣٥

Wa ummihī wa abīh

Na mamaye na babaye, 35

وَصَٰحِبَتِهِۦ وَبَنِيهِ ٣٦

Wasāhibatihī wabanīh

Na mkewe na wanawe. 36

لِكُلِّ ٱمۡرِيٕٖ مِّنۡهُمۡ يَوۡمَئِذٖ شَأۡنٞ يُغۡنِيهِ ٣٧

Likullimriy'im minhum yawma'idhin sha'nun yughnīh

Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha 37

وُجُوهٞ يَوۡمَئِذٖ مُّسۡفِرَةٞ ٣٨

Wujūhun yawma'idhim musfirah

Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri, 38

ضَاحِكَةٞ مُّسۡتَبۡشِرَةٞ ٣٩

Dāhikatum mustabshirah

Zitacheka, zitachangamka; 39

وَوُجُوهٞ يَوۡمَئِذٍ عَلَيۡهَا غَبَرَةٞ ٤٠

Wawujūhun yawma'idhin 'alayhā ghabarah

Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi, 40

تَرۡهَقُهَا قَتَرَةٌ ٤١

Tarhaquhā qatarah

Giza totoro litazifunika, 41

أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡكَفَرَةُ ٱلۡفَجَرَةُ ٤٢

Ulā'ika humul-kafaratul-fajarah

Hao ndio makafiri watenda maovu 42

Nambari za maelezo ya chini zinaelekeza kwenye ukurasa wa aya, ambapo maelezo ya mfasiri yanaonyeshwa.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Maswali

Surat 'Abasa ina aya ngapi?

Surat 'Abasa ina aya 42. Ni sura namba 80 ya Qur'ani.

Je, Surat 'Abasa ni Makkiya au Madaniya?

Surat 'Abasa ni sura Makkiya.

Surat 'Abasa iko katika juzuu gani?

Surat 'Abasa iko katika juzuu 30.

Je, naweza kusikiliza Surat 'Abasa?

Ndiyo. Bonyeza Cheza juu ya ukurasa huu, au anza kutoka aya yoyote. Programu ya Qabas pia inakuwezesha kuipakua ili kuisikiliza bila intaneti.