Surat An-Nazi'at النازعات

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلنَّٰزِعَٰتِ غَرۡقٗا ١

Wan-nāzi'āti gharqā

Naapa kwa wanao komoa kwa nguvu! 1

وَٱلنَّٰشِطَٰتِ نَشۡطٗا ٢

Wan-nāshitāti nashtā

Na kwa wanao toa kwa upole! 2

وَٱلسَّٰبِحَٰتِ سَبۡحٗا ٣

Was-sābihāti sabhā

Na wanao ogelea! 3

فَٱلسَّٰبِقَٰتِ سَبۡقٗا ٤

Fas-sābiqāti sabqā

Wakishindana mbio! 4

فَٱلۡمُدَبِّرَٰتِ أَمۡرٗا ٥

Fal-mudabbirāti amrā

Wakidabiri mambo. 5

يَوۡمَ تَرۡجُفُ ٱلرَّاجِفَةُ ٦

Yawma tarjufur-rājifah

Siku kitapo tetemeka cha kutetemeka! 6

تَتۡبَعُهَا ٱلرَّادِفَةُ ٧

Tatba'uhar-rādifah

Kifuate cha kufuatia. 7

قُلُوبٞ يَوۡمَئِذٖ وَاجِفَةٌ ٨

Qulūbun yawma'idhin wājifah

Siku hiyo nyoyo zitapiga piga! 8

أَبۡصَٰرُهَا خَٰشِعَةٞ ٩

Absāruhā khāshi'ah

Macho yatainama chini! 9

يَقُولُونَ أَءِنَّا لَمَرۡدُودُونَ فِي ٱلۡحَافِرَةِ ١٠

Yaqūlūna a'innā lamardūdūna fil-hāfirah

Sasa wanasema: Ati kweli tutarudishwa kwenye hali ya kwanza? 10

أَءِذَا كُنَّا عِظَٰمٗا نَّخِرَةٗ ١١

A'idhā kunnā 'izāman nakhirah

Hata tukiwa mifupa iliyo bunguliwa? 11

قَالُواْ تِلۡكَ إِذٗا كَرَّةٌ خَاسِرَةٞ ١٢

Qālū tilka idhan karratun khāsirah

Wanasema: Basi marejeo hayo ni yenye khasara! 12

فَإِنَّمَا هِيَ زَجۡرَةٞ وَٰحِدَةٞ ١٣

Fa innamā hiya zajratun wāhidah

Kwa hakika hayo ni ukelele mmoja tu, 13

فَإِذَا هُم بِٱلسَّاهِرَةِ ١٤

Fa idhā hum bis-sāhirah

Mara watakuwa kwenye uwanda wa mkutano! 14

هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ مُوسَىٰٓ ١٥

Hal atāka hadīthu mūsā

Je! Imekufikia hadithi ya Musa? 15

إِذۡ نَادَىٰهُ رَبُّهُۥ بِٱلۡوَادِ ٱلۡمُقَدَّسِ طُوًى ١٦

Idh nādāhu rabbuhū bil-wādil-muqaddasi tuwā

Mola wake Mlezi alipo mwita katika bonde takatifu la T'uwaa, akamwambia: 16

ٱذۡهَبۡ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ ١٧

Idhhab ilā fir'awna innahū taghā

Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri 17

فَقُلۡ هَل لَّكَ إِلَىٰٓ أَن تَزَكَّىٰ ١٨

Faqul hal laka ilā an tazakkā

Umwambie: Je! Unapenda kujitakasa? 18

وَأَهۡدِيَكَ إِلَىٰ رَبِّكَ فَتَخۡشَىٰ ١٩

Wa ahdiyaka ilā rabbika fatakhshā

Nami nitakuongoa ufike kwa Mola wako Mlezi, upate kumcha. 19

فَأَرَىٰهُ ٱلۡأٓيَةَ ٱلۡكُبۡرَىٰ ٢٠

Fa arāhul-āyatal-kubrā

Basi alimwonyesha Ishara kubwa. 20

فَكَذَّبَ وَعَصَىٰ ٢١

Fakaddhaba wa'asā

Lakini aliikadhibisha na akaasi. 21

ثُمَّ أَدۡبَرَ يَسۡعَىٰ ٢٢

Thumma adbara yas'ā

Kisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi. 22

فَحَشَرَ فَنَادَىٰ ٢٣

Fahashara fanādā

Akakusanya watu akanadi. 23

فَقَالَ أَنَا۠ رَبُّكُمُ ٱلۡأَعۡلَىٰ ٢٤

Faqāla ana rabbukumul-a'lā

Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa. 24

فَأَخَذَهُ ٱللَّهُ نَكَالَ ٱلۡأٓخِرَةِ وَٱلۡأُولَىٰٓ ٢٥

Fa akhadhahullāhu nakālal-ākhirati wal-ūlā

Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo. 25

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبۡرَةٗ لِّمَن يَخۡشَىٰٓ ٢٦

Inna fī dhālika la'ibratal liman yakhshā

Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanao ogopa. 26

ءَأَنتُمۡ أَشَدُّ خَلۡقًا أَمِ ٱلسَّمَآءُۚ بَنَىٰهَا ٢٧

A'antum ashaddu khalqan amis-samā'u banāhā

Je! Ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliye ijenga! 27

رَفَعَ سَمۡكَهَا فَسَوَّىٰهَا ٢٨

Rafa'a samkahā fasawwāhā

Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri. 28

وَأَغۡطَشَ لَيۡلَهَا وَأَخۡرَجَ ضُحَىٰهَا ٢٩

Wa aghtasha laylahā wa akhraja duhāhā

Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake 29

وَٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ ذَٰلِكَ دَحَىٰهَآ ٣٠

Wal-arda ba'da dhālika dahāhā

Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi. 30

أَخۡرَجَ مِنۡهَا مَآءَهَا وَمَرۡعَىٰهَا ٣١

Akhraja minhā mā'ahā wamar'āhā

Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake, 31

وَٱلۡجِبَالَ أَرۡسَىٰهَا ٣٢

Wal-jibāla arsāhā

Na milima akaisimamisha, 32

مَتَٰعٗا لَّكُمۡ وَلِأَنۡعَٰمِكُمۡ ٣٣

Matā'al lakum wali'an'āmikum

Kwa nafuu yenu na mifugo yenu. 33

فَإِذَا جَآءَتِ ٱلطَّآمَّةُ ٱلۡكُبۡرَىٰ ٣٤

Fa idhā jā'atit-tāmmatul-kubrā

Basi itakapo fika hiyo balaa kubwa, 34

يَوۡمَ يَتَذَكَّرُ ٱلۡإِنسَٰنُ مَا سَعَىٰ ٣٥

Yawma yatadhakkarul-insānu mā sa'ā

Siku ambayo mtu atakumbuka aliyo yafanya, 35

وَبُرِّزَتِ ٱلۡجَحِيمُ لِمَن يَرَىٰ ٣٦

Waburrizatil-jahīmu liman yarā

Na Jahannamu itadhihirishwa kwa mwenye kuona, 36

فَأَمَّا مَن طَغَىٰ ٣٧

Fa ammā man taghā

Basi ama yule aliye zidi ujeuri, 37

وَءَاثَرَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا ٣٨

Wa ātharal-hayawātad-dunyā

Na akakhiari maisha ya dunia, 38

فَإِنَّ ٱلۡجَحِيمَ هِيَ ٱلۡمَأۡوَىٰ ٣٩

Fa innal-jahīma hiyal-ma'wā

Kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake! 39

وَأَمَّا مَنۡ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِۦ وَنَهَى ٱلنَّفۡسَ عَنِ ٱلۡهَوَىٰ ٤٠

Wa ammā man khāfa maqāma rabbihī wanahan-nafsa 'anil-hawā

Na ama yule anaye ogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio, 40

فَإِنَّ ٱلۡجَنَّةَ هِيَ ٱلۡمَأۡوَىٰ ٤١

Fa innal-jannata hiyal-ma'wā

Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake! 41

يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلسَّاعَةِ أَيَّانَ مُرۡسَىٰهَا ٤٢

Yas'alūnaka 'anis-sā'ati ayyāna mursāhā

Wanakuuliza Saa (ya Kiyama) itakuwa lini? 42

فِيمَ أَنتَ مِن ذِكۡرَىٰهَآ ٤٣

Fīma anta min dhikrāhā

Una nini wewe hata uitaje? 43

إِلَىٰ رَبِّكَ مُنتَهَىٰهَآ ٤٤

Ilā rabbika muntahāhā

Kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho wake. 44

إِنَّمَآ أَنتَ مُنذِرُ مَن يَخۡشَىٰهَا ٤٥

Innamā anta mundhiru man yakhshāhā

Kwa hakika wewe ni mwonyaji tu kwa mwenye kuikhofu. 45

كَأَنَّهُمۡ يَوۡمَ يَرَوۡنَهَا لَمۡ يَلۡبَثُوٓاْ إِلَّا عَشِيَّةً أَوۡ ضُحَىٰهَا ٤٦

Ka annahum yawma yarawnahā lam yalbathū illā 'ashiyyatan aw duhāhā

Ni kama kwamba wao siku watapo iona (hiyo Saa) hawakukaa ila jioni moja tu, au mchana wake. 46

Nambari za maelezo ya chini zinaelekeza kwenye ukurasa wa aya, ambapo maelezo ya mfasiri yanaonyeshwa.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Maswali

Surat An-Nazi'at ina aya ngapi?

Surat An-Nazi'at ina aya 46. Ni sura namba 79 ya Qur'ani.

Je, Surat An-Nazi'at ni Makkiya au Madaniya?

Surat An-Nazi'at ni sura Makkiya.

Surat An-Nazi'at iko katika juzuu gani?

Surat An-Nazi'at iko katika juzuu 30.

Je, naweza kusikiliza Surat An-Nazi'at?

Ndiyo. Bonyeza Cheza juu ya ukurasa huu, au anza kutoka aya yoyote. Programu ya Qabas pia inakuwezesha kuipakua ili kuisikiliza bila intaneti.