Surat Al-Balad البلد

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

لَآ أُقۡسِمُ بِهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ ١

Lā uqsimu bihādhal-balad

Naapa kwa Mji huu! 1

وَأَنتَ حِلُّۢ بِهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ ٢

Wa anta hillu bihādhal-balad

Nawe unaukaa Mji huu. 2

وَوَالِدٖ وَمَا وَلَدَ ٣

Wawālidin wamā walad

Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa. 3

لَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ فِي كَبَدٍ ٤

Laqad khalaqnal-insāna fī kabad

Hakika tumemuumba mtu katika taabu. 4

أَيَحۡسَبُ أَن لَّن يَقۡدِرَ عَلَيۡهِ أَحَدٞ ٥

Ayahsabu al lan yaqdira 'alayhi ahad

Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza? 5

يَقُولُ أَهۡلَكۡتُ مَالٗا لُّبَدًا ٦

Yaqūlu ahlaktu mālal lubadā

Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali. 6

أَيَحۡسَبُ أَن لَّمۡ يَرَهُۥٓ أَحَدٌ ٧

Ayahsabu al lam yarahū ahad

Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona? 7

أَلَمۡ نَجۡعَل لَّهُۥ عَيۡنَيۡنِ ٨

Alam naj'al lahū 'aynayn

Kwani hatukumpa macho mawili? 8

وَلِسَانٗا وَشَفَتَيۡنِ ٩

Walisānan washafatayn

Na ulimi, na midomo miwili? 9

وَهَدَيۡنَٰهُ ٱلنَّجۡدَيۡنِ ١٠

Wahadaynāhun-najdayn

Na tukambainishia zote njia mbili? 10

فَلَا ٱقۡتَحَمَ ٱلۡعَقَبَةَ ١١

Falaqtahamal-'aqabah

Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani. 11

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡعَقَبَةُ ١٢

Wamā adrāka mal-'aqabah

Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani? 12

فَكُّ رَقَبَةٍ ١٣

Fakku raqabah

Kumkomboa mtumwa; 13

أَوۡ إِطۡعَٰمٞ فِي يَوۡمٖ ذِي مَسۡغَبَةٖ ١٤

Aw it'āmun fī yawmin dhī masghabah

Au kumlisha siku ya njaa 14

يَتِيمٗا ذَا مَقۡرَبَةٍ ١٥

Yatīman dhā maqrabah

Yatima aliye jamaa, 15

أَوۡ مِسۡكِينٗا ذَا مَتۡرَبَةٖ ١٦

Aw miskīnan dhā matrabah

Au masikini aliye vumbini. 16

ثُمَّ كَانَ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلصَّبۡرِ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلۡمَرۡحَمَةِ ١٧

Thumma kāna minal-ladhīna āmanū watawāsaw bis-sabri watawāsaw bil-marhamah

Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana. 17

أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ ١٨

Ulā'ika ashābul-maymanah

Hao ndio watu wa kheri wa kuliani. 18

وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِنَا هُمۡ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ ١٩

Walladhīna kafarū bi'āyātinā hum ashābul-mash'amah

Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni. 19

عَلَيۡهِمۡ نَارٞ مُّؤۡصَدَةُۢ ٢٠

'Alayhim nārum mu'sadah

Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande. 20

Nambari za maelezo ya chini zinaelekeza kwenye ukurasa wa aya, ambapo maelezo ya mfasiri yanaonyeshwa.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Maswali

Surat Al-Balad ina aya ngapi?

Surat Al-Balad ina aya 20. Ni sura namba 90 ya Qur'ani.

Je, Surat Al-Balad ni Makkiya au Madaniya?

Surat Al-Balad ni sura Makkiya.

Surat Al-Balad iko katika juzuu gani?

Surat Al-Balad iko katika juzuu 30.

Je, naweza kusikiliza Surat Al-Balad?

Ndiyo. Bonyeza Cheza juu ya ukurasa huu, au anza kutoka aya yoyote. Programu ya Qabas pia inakuwezesha kuipakua ili kuisikiliza bila intaneti.