Surat Ash-Shams الشمس

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلشَّمۡسِ وَضُحَىٰهَا ١

Wash-shamsi waduhāhā

Naapa kwa jua na mwangaza wake! 1

وَٱلۡقَمَرِ إِذَا تَلَىٰهَا ٢

Wal-qamari idhā talāhā

Na kwa mwezi unapo lifuatia! 2

وَٱلنَّهَارِ إِذَا جَلَّىٰهَا ٣

Wan-nahāri idhā jallāhā

Na kwa mchana unapo lidhihirisha! 3

وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَغۡشَىٰهَا ٤

Wallayli idhā yaghshāhā

Na kwa usiku unapo lifunika! 4

وَٱلسَّمَآءِ وَمَا بَنَىٰهَا ٥

Was-samā'i wamā banāhā

Na kwa mbingu na kwa aliye ijenga! 5

وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا طَحَىٰهَا ٦

Wal-ardi wamā tahāhā

Na kwa ardhi na kwa aliye itandaza! 6

وَنَفۡسٖ وَمَا سَوَّىٰهَا ٧

Wanafsin wamā sawwāhā

Na kwa nafsi na kwa aliye itengeneza! 7

فَأَلۡهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقۡوَىٰهَا ٨

Fa alhamahā fujūrahā wataqwāhā

Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake! 8

قَدۡ أَفۡلَحَ مَن زَكَّىٰهَا ٩

Qad aflaha man zakkāhā

Hakika amefanikiwa aliye itakasa! 9

وَقَدۡ خَابَ مَن دَسَّىٰهَا ١٠

Waqad khāba man dassāhā

Na hakika amekhasiri aliye iviza. 10

كَذَّبَتۡ ثَمُودُ بِطَغۡوَىٰهَآ ١١

Kaddhabat thamūdu bitaghwāhā

Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao, 11

إِذِ ٱنۢبَعَثَ أَشۡقَىٰهَا ١٢

Idhimba'atha ashqāhā

Alipo simama mwovu wao mkubwa, 12

فَقَالَ لَهُمۡ رَسُولُ ٱللَّهِ نَاقَةَ ٱللَّهِ وَسُقۡيَٰهَا ١٣

Faqāla lahum rasūlullāhi nāqatallāhi wasuqyāhā

Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake. 13

فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمۡدَمَ عَلَيۡهِمۡ رَبُّهُم بِذَنۢبِهِمۡ فَسَوَّىٰهَا ١٤

Fakaddhabūhu fa'aqarūhā fadamdama 'alayhim rabbuhum bidhambihim fasawwāhā

Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa. 14

وَلَا يَخَافُ عُقۡبَٰهَا ١٥

Walā yakhāfu 'uqbāhā

Wala Yeye haogopi matokeo yake. 15

Nambari za maelezo ya chini zinaelekeza kwenye ukurasa wa aya, ambapo maelezo ya mfasiri yanaonyeshwa.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Maswali

Surat Ash-Shams ina aya ngapi?

Surat Ash-Shams ina aya 15. Ni sura namba 91 ya Qur'ani.

Je, Surat Ash-Shams ni Makkiya au Madaniya?

Surat Ash-Shams ni sura Makkiya.

Surat Ash-Shams iko katika juzuu gani?

Surat Ash-Shams iko katika juzuu 30.

Je, naweza kusikiliza Surat Ash-Shams?

Ndiyo. Bonyeza Cheza juu ya ukurasa huu, au anza kutoka aya yoyote. Programu ya Qabas pia inakuwezesha kuipakua ili kuisikiliza bila intaneti.