Dua hujibiwa lini? Nyakati na sababu

Nyakati na hali ambazo dua inatarajiwa zaidi kujibiwa.

1 Mara moja

Maana na chanzo

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Palipo karibu zaidi kwa mja na Mola wake ni pale anapokuwa kasujudu,Basi zidisheni dua".

Imepokelewa Imamu Muslim Daraja: Sahihi

Maelezo

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa mahala palipo karibu zaidi kwa mja na Mola wake ni pale anapokuwa kasujudu; Na hii ni kwa sababu mwenye kusali huweka kiungo bora na kitukufu kuliko vyote katika mwili wake juu ya Ardhi kwa kujinyenyekeza na kujidhalilisha na kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- anapokuwa kasujudu.

Na ameamrisha -Rehema na amani ziwe juu yake- kukithirisha dua katika sijida, yanakusanyika mambo mawili katika hilo, kujidhalilisha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa kauli na vitendo.

Faida

  • Utiifu humzidishia mja ukaribu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Ni Sunna kukithirisha dua katika sijida; kwani ni katika maeneo ya kujibiwa.

Soma kwenye HadeethEnc.com

2 Mara moja

Maana na chanzo

Kutoka kwa Abuu Umama amesema: Alinisimulia Amru bin Abasa radhi za Allah ziwe juu yake kuwa, alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Mahala pa karibu zaidi anapokuwa Mola Mlezi na mja ni katikati ya usiku wa mwisho, ikiwa utaweza kuwa miongoni mwa wanaomtaja Mwenyezi Mungu katika wakati huo basi fanya".

Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na Nasaai Daraja: Sahihi

Maelezo

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mola Mtukufu yu karibu zaidi na mja katika theluthi ya mwisho ya usiku, ikiwa utawezeshwa na ukaweza - Ewe Muumini - kuwa miongoni mwa wanaoabudu, na kuswali, na kumtaja Mwenyezi Mungu na kutubia wakati huu, basi ni jambo ambalo unapaswa kulishika na kujitahidi.

Faida

  • Muislamu anahimizwa kumtaja Mwenyezi Mungu mwisho wa usiku.
  • Nyakati zinazidiana ubora kwa ajili ya kumtaja Mwenyezi Mungu na kuomba dua na kuswali.
  • Amesema Muraik: Katika tofauti baina ya kusema kwake: “Mahala pa karibu zaidi anapokuwa Mola Mlezi na mja,” na kusema kwake: “Mahala pa karibu zaidi anapokuwa mja na Mola wake Mlezi ni pale anapokuwa kasujudu”: Kinachokusudiwa hapa ni kuashiria wakati ambapo Mola anakuwa karibu zaidi na mja, yaani katikati ya usiku, na kinachokusudiwa hapo ni kueleza hali ya ukaribu wa mja na Mola ni pale anapokuwa katika hali ya kusujudu.

Soma kwenye HadeethEnc.com

3 Mara moja

Maana na chanzo

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maliki -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Dua hairejeshwi (inayoombwa) baina ya adhana na kukimiwa swala".

Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na Nasaai Daraja: Sahihi

Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake fadhila za dua baina ya adhana na ikama, nakuwa dua hiyo hairejeshwi na inanafasi kubwa ya kujibiwa, basi muombeni Mwenyezi Mungu ndani ya wakati huu.

Faida

  • Fadhila za wakati huu kwa ajili kuomba dua.
  • Atakapojipamba muombaji kwa adabu za kuomba dua, na akatafuta mahala pake na nyakati zake bora, na akajiepusha na kumuasi Mwenyezi Mungu, na akachukua tahahadhari ya kutotumbukia katika mambo yasiyofaa na yenye kutatiza, na akamdhania vizuri Mwenyezi Mungu: Basi ni rahisi sana kujibiwa, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
  • Amesema Al-Munawi kuhusu kujibiwa dua: Yaani: Baada ya kukusanya sharti za dua na nguzo zake na adabu zake, ikiwa kitapelea kitu chochote basi asilaumu ila nafsi yake.
  • Ni sunna kuomba dua: Ima zijibiwe haraka dua zake, au aepushiwe katika shari mfano wake, au atunziwe Akhera; na hii ni kulingana na hekima ya Mwenyezi Mungu na huruma yake.

Soma kwenye HadeethEnc.com

4 Mara moja

Maana na chanzo

Kutoka kwa Ummu Dardaai na Abuu Dardaai radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akisema: "Dua ya mtu muislamu kwa ndugu yake, anapokuwa hayupo, hujibiwa, kichwani kwake huwa kuna Malaika aliyepewa kazi, kila anapomuombea ndugu yake kwa heri, Malaika aliyepewa kazi hiyo husema: Ewe Mwenyezi Mungu pokea dua, na kwako pia upate mfano wake".

Imepokelewa Imamu Muslim Daraja: Sahihi

Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa dua ya muislamu kwa ndugu yake muislamu, anapokuwa hayupo anayeombewa dua, hujibiwa; kwa sababu huwa na kiwango kikubwa cha utakasifu (Ikhlaswi) na kwamba kichwani kwa muombaji huwa kuna Malaika aliwakilishwa, kila anapomuombea ndugu yake kwa heri, basi anasema Malaika alipewa kazi hiyo: Mwenyezi Mungu apokee dua, na upate pia mfano wa hayo uliyoomba.

Faida

  • Himizo kwa waumini la kutendeana wema wao kwa wao walau hata kwa dua.
  • Dua ya siri inaonyesha dalili wazi juu ya imani ya kweli na udugu.
  • Kufungamanishwa dua na siri; ni kwa sababu hilo huwa katika kiwango kikubwa cha utakasifu, na kuhudhuria moyo.
  • Miongoni mwa sababu za kujibiwa dua ni mtu kumuombea ndugu yake kwa siri.
  • Amesema Nawawi: Fadhila ya dua kwa ndugu yake muislamu kwa siri, na hata akiwaombea watu wengi katika waislamu pia atapata fadhili hii, na hata akiwaombea waislamu wote kwa ujumla, pia inavyoonekana atapata fadhila hizi, na walikuwa baadhi ya wema waliotangulia anapotaka kujiombea mwenyewe basi anamuombea ndugu yake muislamu dua hiyo; kwa sababu inajibiwa, na yeye anapata mfano wake.
  • Hapa kumebainishwa baadhi ya kazi za Malaika, na kwamba wako miongoni mwao aliowapa Mwenyezi Mungu kazi hii.

Soma kwenye HadeethEnc.com

5 Mara moja

Maana na chanzo

Imepokewa Kutoka kwa Nuuman bin Bashiri -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Dua ndio ibada", Kisha akasoma: "Na amesema Mola wenu Mlezi niombeni mimi nitakujibuni, hakika wale wanaofanya kiburi katika ibada yangu wataingia Jahannam wakiwa madhalili" [Ghafir: 60].

Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad Daraja: Sahihi

Maelezo

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa dua ndio ibada, la msingi nikuwa yote iwe safi kwa ajili ya Allah, sawa sawa iwe ni kuomba jambo au kutaka jambo, kwa kumuuomba Allah Mtukufu ampe yenye manufaa kwake, na amkinge na yenye kumdhuru duniani na akhera, au dua ikiwa ni ibada, nayo ni kila anayoyapenda Mwenyezi Mungu na kuyaridhia katika kauli na matendo ya wazi na ya siri, ibada za moyo au za mwili au za mali.

Kisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akatoa ushahidi juu ya hilo pale aliposema: Amesema Allah Mtukufu: "..Niombeni mimi nitakujibuni, hakika wale wanaofanya kiburi katika ibada yangu wataingia Jahannam wakiwa madhalili"

Faida

  • Dua ndio asili ya ibada na wala haifai kuilekeza kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu.
  • Dua inaambatana na uhalisia wa kuabudu na kukiri utajiri wa Mola Mlezi na uwezo wake Yeye Mtukufu, na uhitaji wa mja kwake.
  • Kemeo kali likiwa ni malipo ya kiburi cha kutomuabudu Mwenyezi Mungu na kuacha kumuomba, nakwamba wale wanaofanya jeuri kumuomba Allah wataingia katika Jahannam wakiwa wanyonge madhalili.

Soma kwenye HadeethEnc.com

6 Mara moja

Maana na chanzo

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakuna kitu kinachotukuzwa zaidi kwa Allah Mtukufu kuliko dua".

Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad Daraja: Ni nzuri (Hasan)

Maelezo

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hakuna chochote katika ibada kilicho bora zaidi mbele ya Allah Mtukufu kuliko dua; kwa sababu ndani yake kuna kukiri utajiri wa Allah Mtukufu, na kukiri kushindwa kwa mja na kuhitajia kwake kutoka kwake.

Faida

  • Ubora wa dua nakuwa mwenye kumuomba Allah basi huwa kamtukuza, na amekiri kuwa Yeye ni mkwasi -Aliyetakasika- kwani Masikini haombwi, nakuwa Yeye ni Msikivu, kwani kiziwi haombwi, nakuwa Yeye ni mkarimu, kwani bahili haombwi, nakuwa yeye anahuruma, kwani mkorofi haombwi, nakuwa Yeye anaweza, kwani asiyejiweza haombwi, nakuwa Yeye yuko karibu, kwani aliyembali hasikii, na zinginezo katika sifa za utukufu na za uzuri wa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na Kutukuka-.

Soma kwenye HadeethEnc.com

7 Mara moja

Maana na chanzo

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri hakubali ila vizuri, na hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini kwa yale aliyowaamrisha kwayo Manabii, akasema Allah Mtukufu: "Enyi Mitume! Kuleni katika vile vilivyo vizuri na mtende mema, hakika mimi kwa yale mnayoyafanya ni Mjuzi" [Al-Muuminuun: 51] Na akasema Allah Mtukufu: "Enyi mlioamini! Kuleni katika vizuri miongoni mwa vile tulivyokuruzukuni, na mumshukuru Mwenyezi Mungu ikiwa kweli nyinyi mnamuabudu yeye peke yake" [Al-baqara: 172] akasema: Kisha akataja tukio la mtu mmoja mwenye safari ndefu, nywele zake zimetimka, kajaa vumbi, ananyanyua mikono yake kuelekea mbinguni (anasema) Mola wangu Mola wangu! (wakati huo) chakula chake ni cha haramu, na mavazi yake ni ya haramu, na kinywaji chake ni cha haramu, na lishe yake yote ni ya haramu, itawezekana vipi kujibiwa kwa mtu kama huyo?!".

Imepokelewa Imamu Muslim Daraja: Sahihi

Maelezo

Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu ni mzuri na ni mtakasifu ametakasika na kila mapungufu na aibu na amesifika kwa yote yaliyokamilika, na wala hakubali katika matendo kauli na itikadi isipokuwa ile itakayokuwa nzuri, nayo ni ile iliyotakaswa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, yenye kwenda sambamba na muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na haitakiwi mtu ajikurubishe kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa hayo, na katika mambo yanayosababisha amali kuwa nzuri kwa muumini ni chakula chake kuwa kizuri, na kiwe kimetokana na halali, kwa hilo amali zake zinakuwa njema, na ndio maana Mwenyezi Mungu aliwaamrisha waumini kwa lile alilowaamrisha Mitume, ikiwemo kula halali na kutenda mema, akasema: "Enyi Mitume! Kuleni katika vilivyo vizuri na mtende mema, hakika mimi kwa yale mnayoyafanya ni Mjuzi" Na akasema: "Enyi mlioamini kuleni katika vizuri katika vile tulivyokuruzukuni".

Kisha akatahadharisha rehema na amani ziwe juu yake kula haramu,ambako kunaharibu matendo na kunazuia kukubalika kwake kwa sababu yoyote ile inayoonekana; ikiwemo:

Ya kwanza: Kuwa na safari ndefu iliyo katika misingi ya kumtii Mwenyezi Mungu kama Hija na Jihadi na kuunga udugu na mengineyo.

Ya pili: Nywele kukaa hovyo kwa kutotanwa, na kubadilika rangi ya ngozi na rangi ya nguo kwa sababu ya udongo, basi mtu huyu anakuwa kadharurika.

Ya tatu: Ananyanyua mikono yake juu mbinguni kwa dua.

Ya nne: Anamuomba Mwenyezi Mungu kupitia majina yake na anang'ang'ania katika hilo: Ewe Mola wangu Ewe Mola wangu!

Na pamoja na sababu hizi za kujibiwa dua hakusikilizwa; na hii ni kwa sababu chakula chake na kinywaji chake na mavazi yake ni vya haramu, na afya yake imetokana na haramu, ni mbali sana kwa mtu mwenye sifa kama hizi kujibiwa, na atajibiwa vipi?!

Faida

  • Ukamilifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika dhati yake, na sifa zake, na vitendo vyake, na hukumu zake.
  • Amri ya kutakasa matendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa kumfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  • Kutumia maneno yenye kuhamasisha kufanya matendo, kiasi kwamba alisema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini kwa yale aliyowaamrisha Mitume", anapojua muumini kuwa hili ni katika yale waliyoamrishwa Mitume basi anapata nguvu na anahamasika kulitekeleza.
  • Katika vizuizi vya kujibiwa dua ni kula vya haramu.
  • Katika sababu za kujibiwa dua ni mambo matano: La kwanza: Kuwa na safari ndefu, kwakuwa ndani yake kuna kudhoofika, ambayo ni miongoni mwa sababu kubwa za kujibiwa. La pili: Wakati wa kudharurika. La tatu: kunyoosha mikono kuelekea mbinguni. La nne: Kung'ang'ania kwa Mwenyezi Mungu kwa kurudiarudia kusema ewe Mola Mlezi, na ni katika maneno makubwa ambayo hutumika kwa lengo la kutaka kujibiwa. La tano: Kula chakula kizuri na vinywaji vizuri.
  • Kula halali nzuri ni katika sababu zinazosaidia kutenda amali njema.
  • Amesema Kadhi: Kizuri ni kinyume cha kibaya, akisifiwa Mwenyezi Mungu Mtukufu basi hukusudiwa kuwa ametakasika na mapungufu, na ametukuka hana maafa, na akisifiwa mja moja kwa moja basi hukusudiwa kuwa hana tabia chafu na matendo mabaya, na anajipamba na kinyume cha hayo, na ikisifiwa mali basi hukusudiwa inapokuwa ya halali katika mali bora.

Soma kwenye HadeethEnc.com

Maswali

Kuna nini kwenye ukurasa huu?

Dua hujibiwa lini: kila moja kwa Kiarabu, pamoja na maana yake, hadithi inakotoka, daraja yake na maelezo.

Tafsiri zinatoka wapi?

Kutoka HadeethEnc.com, Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa. Kila hadithi inaonyeshwa kama walivyoichapisha, pamoja na chanzo na daraja yake, na viungo vya asili.

Naweza kupata kikumbusho cha kila siku?

Ndiyo. Programu ya bure ya Qabas kwa Android inakukumbusha adhkar za asubuhi na jioni kila siku na ina kihesabu hicho hicho.