Dua jumuishi za dunia na akhera

Dua fupi zinazoomba kila jema, duniani na akhera.

1 Mara moja

اللَّهُمَّ رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً، وَفِي الآخِرَةِ حَسَنَةً، وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ

Maana na chanzo

Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Ilikuwa Dua aiombayo zaidi Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-:ni "Ewe Mola wetu Mlezi, tupe duniani mazuri, na Akhera mazuri, na utukinge na adhabu ya moto".

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Daraja: Sahihi

Maelezo

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akikithirisha dua kwa dua fupi zenye kukusanya mambo mengi, na miongoni mwake: "Ewe Mwenyezi Mungu! Tupe hapa katika Dunia (mambo) mazuri, na Akhera utupe mazuri na utukinge na adhabu ya moto", Dua hii inakusanya mazuri yote ya Dunia; ikiwemo riziki ya raha na pana na ya halali, na mke mwema, na mtoto kitulizo cha jicho, na starehe, na elimu yenye manufaa, na mfano wa hayo miongoni mwa maombi yanayopendeka na ya halali, na mazuri ya Akhera ni kusalimika na adhabu za kaburi, na kisimamo cha Kiyama na moto, na kupata radhi za Mwenyezi Mungu, na kufaulu kwa kupata neema za kudumu, na kuwekwa karibu na Mola Mlezi Mwingi wa huruma.

Faida

  • Sunna ya kuomba dua kupitia dua zinazokusanya maana pana, kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  • Kwa ukamilifu zaidi ni mtu akusanye katika maombi yake baina ya kheri za Dunia na Akhera.

Soma kwenye HadeethEnc.com

2 Mara moja

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ الْخَيْرِ كُلِّهِ، عَاجِلِهِ وَآجِلِهِ، مَا عَلِمْتُ مِنْهُ وَمَا لَمْ أَعْلَمْ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ الشَّرِّ كُلِّهِ، عَاجِلِهِ وَآجِلِهِ، مَا عَلِمْتُ مِنْهُ وَمَا لَمْ أَعْلَمْ، اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ خَيْرِ مَا سَأَلَكَ عَبْدُكَ وَنَبِيُّكَ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا عَاذَ بِهِ عَبْدُكَ وَنَبِيُّكَ، اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْجَنَّةَ، وَمَا قَرَّبَ إِلَيْهَا مِنْ قَوْلٍ أَوْ عَمَلٍ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ النَّارِ، وَمَا قَرَّبَ إِلَيْهَا مِنْ قَوْلٍ أَوْ عَمَلٍ، وَأَسْأَلُكَ أَنْ تَجْعَلَ كُلَّ قَضَاءٍ قَضَيْتَهُ لِي خَيْرًا

Maana na chanzo

Kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimfundisha dua hii: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba (unipe) kutoka katika heri zote: zile za haraka na za kuchelewa, kwa ninayo yajua na nisiyo yajua, na ninajikinga kwako kutokana na shari zote zinazokuja haraka na zinazochelewa, kwa ninayo yajua na nisiyo yajua. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba (unipe) miongoni mwa heri alizo kuomba mja wako na nabii wako, na ninajikinga kwako (uniepushe) na shari alizo jikinga kwako mja wako na nabii wako. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba pepo, na yaliyo karibu yake miongoni mwa kauli au matendo, na ninajikinga kwako kutokana na moto na yaliyo karibu na moto miongoni mwa kauli au matendo, na ninakuomba ujaalie kila hukumu utakayo hukumu kwangu iwe ni heri"

Imepokelewa na Ibn Majah na Ahmad Daraja: Sahihi

Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimfundisha Aisha radhi za Allah ziwe juu yake dua inayokusanya mambo mengi nayo ni maombi manne:

La kwanza: Dua inayokusanya kila aina ya kheri: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba unipe kutoka katika kheri zote" kwa ujumla wake, "Za haraka" zilizo karibu kwa wakati wake, na "za baadaye" za mbali, "Nilizozijua" katika zile ulizonifundisha, "na zile nisizozijua" katika zile zinazokuwa katika elimu yako ewe Mtukufu, Na hapa kuna kuyakabidhi mambo yote kwa Mwenyezi Mungu Mjuzi Mwenye habari na Mpole; basi Mwenyezi Mungu humchagulia muislamu kilicho bora kati ya hayo na kizuri, "Na ninajilinda" ninashikamana na ninaomba ulinzi "kwako wewe dhidi ya shari zote, zinazokuja haraka na zinazochelewa, ninazozijua na nisizozijua".

Dua ya pili: Nayo ni kinga kwa muislamu ili asichupe mipaka katika dua "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba" na ninakutaka unipe "Katika kheri alizokuomba mja wako na Nabii wako" rehema na amani ziwe juu yake, "na ninajilinda kwako" na ninajiegemeza na kushikamana "kwako kutokana na shari alizojikinga nazo mja wako na Nabii wako" rehema na amani ziwe juu yake, na hii ni dua na ni ombi kutoka kwa Mwenyezi Mungu ampe muombaji yale aliyomuomba na akayataka Nabii Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake kwa ajili ya nafsi yake, pasina kusema aina ya yale aliyoyaomba rehema na amani ziwe juu yake.

Dua ya tatu: Kuomba kuingia peponi na kujiweka mbali na moto, nalo ni ombi la kila muislamu na ndio lengo kuu la matendo yake: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba pepo" na kufauli kuipata "Na yale yanayotuweka karibu nayo miongoni mwa kauli na matendo" mema yenye kukuridhisha, "na ninajilinda kwako kutokana na moto" kiasi kwamba hakuna kukingwa na matendo machafu ila kwa upole wako, "na yale yenye kutuweka karibu nao miongoni mwa kauli na matendo" katika maasi yanayokukasirisha.

Dua ya nne: Kuomba kuridhika na kadari za Mwenyezi Mungu "na ninakuomba uyafanya maamuzi yako uliyoyapitisha yawe ni kheri" na kila jambo alilolihukumu Mwenyezi Mungu kwangu alifanye kuwa ni kheri kwangu, na ni katika dua za kuomba kuridhia hukumu ya Mwenyezi Mungu.

Faida

  • Mtu anatakiwa kuifundisha familia yake yale yenye kuwanufaisha katika mambo ya dini na dunia, kama Mtume rehema na amani ziwe juu yake alivyomfundisha Aisha.
  • Kilicho bora kwa muislamu ni kuhifadhi dua zilizopokelewa kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake; kwa sababu ni katika dua zilizokusanya kheri zote.
  • Wanachuoni wanasema kuhusu hadithi hii: Ni hadithi iliyokusanya kila kitu katika kuomba kheri na kuomba kinga dhidi ya shari, hii ni katika maneno mafupi yenye maana pana aliyopewa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  • Miongoni mwa sababu za kuingia peponi baada ya rehema ya Mwenyezi Mungu: Ni matendo na kauli njema.

Soma kwenye HadeethEnc.com

3 Mara moja

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْعَافِيَةَ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ، اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْعَفْوَ وَالْعَافِيَةَ فِي دِينِي وَدُنْيَايَ وَأَهْلِي وَمَالِي، اللَّهُمَّ اسْتُرْ عَوْرَتِي -أَو: عَوْرَاتِي- وَآمِنْ رَوْعَاتِي، اللَّهُمَّ احْفَظْنِي مِنْ بَيْنِ يَدَيَّ، وَمِنْ خَلْفِي، وَعَنْ يَمِينِي، وَعَنْ شِمَالِي، وَمِنْ فَوْقِي، وَأَعُوذُ بِعَظَمَتِكَ أَنْ أُغْتَالَ مِنْ تَحْتِي

Maana na chanzo

Imepokelewa kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema: Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiacha dua hizi, kila anaposhinda jioni na kila anapoamka: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba unipe afya katika Dunia na Akhera, Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba msamaha na afya katika dini yangu na dunia yangu na familia yangu na mali yangu, ewe Mwenyezi Mungu sitiri uchi wangu -Au aibu zangu- na utie amani yote ninayoyahofia, ewe Mwenyezi Mungu nihifadhi toka mbele yangu, na nyuma yangu, na kuliani kwangu, na kushotoni kwangu, na juu yangu, na ninajilinda kwa utukufu wako nisijekuvamiwa tokea chini yangu".

Imepokelewa na Abu Daud, Nasai, Ibn Majah na Ahmad Daraja: Sahihi

Maelezo

Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiacha maombi haya pindi anaposhinda jioni na pindi anapoamka.

"Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba afya" na kusalimika na magonjwa na mabalaa na shida za dunia, na matamanio na fitina za kidunia "Katika dunia na Akhera" kwa au kwa baadae

"Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba msamaha" na kusalimika na aibu, "Katika dini yangu" kutokana na ushirikina na uzushi na maasi, "na dunia yangu" katika majanga na kero na shari, "na familia yangu" mke wangu na wanangu na ndugu zangu, "na mali yangu" na mali zangu na matendo yangu.

"Ewe Mwenyezi Mungu sitiri uchi wangu" Yaani: Na yale yaliyokwangu katika aibu na dosari na mapungufu na ufute dhambi zangu, "na utie amani hofu yangu" Mfadhaiko wangu na hofu yangu.

"Ewe Mwenyezi Mungu nihifadhi" Na uzuie kwangu balaa miongoni mwa yale yenye kuudhi na mabalaa, "mbele yangu na nyuma yangu, na kuliani kwangu, na kushotoni kwangu, na juu yangu" Kiasi kwamba aliomuomba Mwenyezi Mungu amuhifadhi kutoka pande zote; kwa sababu mabalaa na maafa humfika mtu na kumuelekea kutoka moja kati ya pande hizi.

"Na ninajilinda kwa utukufu wako nisijekuvamiwa" na nisichukuliwe hatua toka chini yangu ghafla, nikaangamia ghafla "kutoka chini yangu" nikaangamia kwa kudidimizwa.

Faida

  • Kudumu na maneno haya kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  • Mwanadam kama alivyo anaamrishwa kumuomba Mwenyezi Mungu afya katika dini, vile vile kaamrishwa kumuomba katika dunia.
  • Amesema Attwayibi: Imekusanya pande zote sita; kwa sababu maafa mengi hutokea katika pande hizo, na akatia mkazo katika upande wa chini kwa sababu maafa ya kutoka chini huwa mabaya zaidi.
  • Kilicho bora wakati wa kusoma Adhkari, wakati wa asubuhi: Ni kuanzia kuchomoza kwa Alfajiri mpaka kuchomoza Jua mwanzo wa mchana, na kuanzia baada ya Lasiri mpaka kabla ya Maghribi, ikiwa atasema baada ya wakati huo, yaani: Akazisoma asubuhi baada ya Jua kunyanyuka itafaa pia, na hata akisema baaada ya Adhudhuri itamfaa pia, na ikiwa atazazisema baada ya Maghrib itamtosheleza pia, huo ndio wakati wa kufanya dhikri.
  • Dalili ikionyesha kuwa dhikri inamuda maalum wakati wa usiku kama kusoma aya mbili za mwisho katika suratul baqara basi hii inakuwa ni baada ya kuzama kwa Jua.

Soma kwenye HadeethEnc.com

4 Mara moja

Maana na chanzo

Kutoka kwa Al-Abbasi bin Abdil Muttwalib radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nifundishe kitu nitakachomuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu. Akasema: "Muombe Allah afya", nikakaa siku kadhaa kisha nikarudi, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nifundishe kitu ambacho nitamuomba Mwenyezi Mungu. Akasema kuniambia: "Ewe Abbasi, ewe ami yake na Mjume wa Mwenyezi Mungu, muombe Mwenyezi Mungu afya katika Dunia na Akhera".

Imepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad Daraja: Ni sahihi kwa sababu ya hadithi nyinginezo

Maelezo

Ami yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake Al-Abbas bin Abdul Muttalib Allah amuwie radhi alimuomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amfundishe dua ya kumuomba Mwenyezi Mungu, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamfundisha amuombe Mwenyezi Mungu afya njema na salama kutokana na balaa na kasoro za Dini, Dunia na Akhera, akasema: Baada ya siku chache nikarejea kwake rehema na amani ziwe juu yake kwa mara nyingine tena nikimuomba anifundishe dua nimuombe Mwenyezi Mungu, akasema rehema na amani ziwe juu yake akimwambia kwa mapenzi na upole: Ewe Abbas, ewe ami wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, muombe Mwenyezi Mungu afya aondoe madhara yote na alete kheri na manufaa katika Dunia na Akhera.

Faida

  • Kurudiarudia kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake jibu hilo hilo kwa Abbasi alipomuuliza kwa mara ya pili kunaonyesha afya ndio jambo la heri zaidi mja analomuomba Mola wake Mlezi.
  • Kumebainishwa fadhila za afya nakuwa imekusanya heri zote katika Dunia na Akhera.
  • Pupa ya Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao ya kutaka kuongeza elimu na heri.

Soma kwenye HadeethEnc.com

Maswali

Kuna nini kwenye ukurasa huu?

Dua jumuishi: kila moja kwa Kiarabu, pamoja na maana yake, hadithi inakotoka, daraja yake na maelezo.

Tafsiri zinatoka wapi?

Kutoka HadeethEnc.com, Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa. Kila hadithi inaonyeshwa kama walivyoichapisha, pamoja na chanzo na daraja yake, na viungo vya asili.

Naweza kupata kikumbusho cha kila siku?

Ndiyo. Programu ya bure ya Qabas kwa Android inakukumbusha adhkar za asubuhi na jioni kila siku na ina kihesabu hicho hicho.