لَّقَدۡ كُنتَ فِي غَفۡلَةٖ مِّنۡ هَٰذَا فَكَشَفۡنَا عَنكَ غِطَآءَكَ فَبَصَرُكَ ٱلۡيَوۡمَ حَدِيدٞ ٢٢
Llaqad kunta fī ghaflatim min hādhā fakashafnā 'anka ghitā'aka fabasarukal-yawma hadīd
(Aambiwe): Kwa hakika ulikuwa umeghafilika na haya; basi leo tumekuondolea pazia lako, na kwa hivyo kuona kwako leo ni kukali. 22
Maelezo ya chini
22 Wataambiwa, kumtisha huyo mwenye kukadhibisha: Hakika wewe huko duniani ulikuwa umeghafilika kabisa na haya unayo sononeka nayo hivi sasa. Basi Sisi tumekuondolea pazia lilio kuwa likikuzuia usiyaone mambo ya Akhera. Basi jicho lako hii leo linaona kwa nguvu.