Surat Qaf, aya 12

50:12

كَذَّبَتۡ قَبۡلَهُمۡ قَوۡمُ نُوحٖ وَأَصۡحَٰبُ ٱلرَّسِّ وَثَمُودُ ١٢

Kaddhabat qablahum qawmu nūhin wa ashābur-rassi wathamūd

Kabla yao walikadhibisha kaumu ya Nuhu na wakaazi wa Rassi na Thamudi. 12

Maelezo ya chini

12 Kabla ya hawa, kaumu nyingi ziliwakadhibisha Mitume- kaumu ya Nuhu, na kaumu nyengine iliyo kuwa ikiitwa "Watu wa Rassi", na wa Thamudi, na wa A'di, na wa Firauni, na kaumu Lut'i, na kaumu iliyo kuwa maarufu kwa jina la "Watu wa Machakani", na kaumu ya Tubbaa' - wote hao waliwakadhibisha Mitume wao. Kwa hivyo wakastahiki maangamizo niliyo waahidi.