Surat Al-Buruj البروج

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلۡبُرُوجِ ١

Was-samā'i dhātil-burūj

Naapa kwa mbingu yenye Buruji! 1

وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡمَوۡعُودِ ٢

Wal-yawmil-maw'ūd

Na kwa siku iliyo ahidiwa! 2

وَشَاهِدٖ وَمَشۡهُودٖ ٣

Washāhidin wamashhūd

Na kwa shahidi na kinacho shuhudiwa! 3

قُتِلَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡأُخۡدُودِ ٤

Qutila ashābul-ukhdūd

Wameangamizwa watu wa makhandaki. 4

ٱلنَّارِ ذَاتِ ٱلۡوَقُودِ ٥

An-nāri dhātil-waqūd

Yenye moto wenye kuni nyingi! 5

إِذۡ هُمۡ عَلَيۡهَا قُعُودٞ ٦

Idh hum 'alayhā qu'ūd

Walipo kuwa wamekaa hapo! 6

وَهُمۡ عَلَىٰ مَا يَفۡعَلُونَ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ شُهُودٞ ٧

Wahum 'alā mā yaf'alūna bil-mu'minīna shuhūd

Na wao ni mashahidi wa yale waliyo kuwa wakiwafanyia Waumini. 7

وَمَا نَقَمُواْ مِنۡهُمۡ إِلَّآ أَن يُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَمِيدِ ٨

Wamā naqamū minhum illā an yu'minū billāhil-'azīzil-hamīd

Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa! 8

ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدٌ ٩

Alladhī lahū mulkus-samāwāti wal-ardi wallāhu 'alā kulli shay'in shahīd

Ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni shaahidi wa kila kitu. 9

إِنَّ ٱلَّذِينَ فَتَنُواْ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ ثُمَّ لَمۡ يَتُوبُواْ فَلَهُمۡ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمۡ عَذَابُ ٱلۡحَرِيقِ ١٠

Innal-ladhīna fatanul-mu'minīna wal-mu'mināti thumma lam yatūbū falahum 'adhābu jahannama walahum 'adhābul-harīq

Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua. 10

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَهُمۡ جَنَّٰتٞ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡكَبِيرُ ١١

Innal-ladhīna āmanū wa'amilus-sālihāti lahum jannātun tajrī min tahtihal-anhāru dhālikal-fawzul-kabīr

Hakika walio amini na wakatenda mema watapata Bustani zenye mito ipitayo kati yake. Huko ndiko kufuzu kukubwa. 11

إِنَّ بَطۡشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ ١٢

Inna batsha rabbika lashadīd

Hakika kutesa kwa Mola wako Mlezi ni kukali. 12

إِنَّهُۥ هُوَ يُبۡدِئُ وَيُعِيدُ ١٣

Innahū huwa yubdi'u wayu'īd

Yeye ndiye anaye anzisha na ndiye anaye rejeza tena, 13

وَهُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلۡوَدُودُ ١٤

Wahuwal-ghafūrul-wadūd

Naye ni Mwenye kusamehe, Mwenye mapenzi, 14

ذُو ٱلۡعَرۡشِ ٱلۡمَجِيدُ ١٥

Dhul-'arshil-majīd

Mwenye Kiti cha Enzi, Mtukufu, 15

فَعَّالٞ لِّمَا يُرِيدُ ١٦

Fa''ālul limā yurīd

Atendaye ayatakayo. 16

هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلۡجُنُودِ ١٧

Hal atāka hadīthul-junūd

Je! Zimekuwasilia khabari za majeshi? 17

فِرۡعَوۡنَ وَثَمُودَ ١٨

Fir'awna wathamūd

Ya Firauni na Thamudi? 18

بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فِي تَكۡذِيبٖ ١٩

Balil-ladhīna kafarū fī takdhīb

Lakini walio kufuru wamo katika kukadhibisha. 19

وَٱللَّهُ مِن وَرَآئِهِم مُّحِيطُۢ ٢٠

Wallāhu min warā'ihim muhīt

Na Mwenyezi Mungu nyuma yao amewazunguka. 20

بَلۡ هُوَ قُرۡءَانٞ مَّجِيدٞ ٢١

Bal huwa qur'ānum majīd

Bali hii ni Qur'ani tukufu 21

فِي لَوۡحٖ مَّحۡفُوظِۭ ٢٢

Fī lawhim mahfūz

Katika Ubao Ulio Hifadhiwa. 22

Nambari za maelezo ya chini zinaelekeza kwenye ukurasa wa aya, ambapo maelezo ya mfasiri yanaonyeshwa.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Maswali

Surat Al-Buruj ina aya ngapi?

Surat Al-Buruj ina aya 22. Ni sura namba 85 ya Qur'ani.

Je, Surat Al-Buruj ni Makkiya au Madaniya?

Surat Al-Buruj ni sura Makkiya.

Surat Al-Buruj iko katika juzuu gani?

Surat Al-Buruj iko katika juzuu 30.

Je, naweza kusikiliza Surat Al-Buruj?

Ndiyo. Bonyeza Cheza juu ya ukurasa huu, au anza kutoka aya yoyote. Programu ya Qabas pia inakuwezesha kuipakua ili kuisikiliza bila intaneti.