Surat Al-A'la الأعلى

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

سَبِّحِ ٱسۡمَ رَبِّكَ ٱلۡأَعۡلَى ١

Sabbihisma rabbikal-a'lā

Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa! 1

ٱلَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ ٢

Alladhī khalaqa fasawwā

Aliye umba, na akaweka sawa! 2

وَٱلَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ ٣

Walladhī qaddara fahadā

Na ambaye amekadiria na akaongoa,. 3

وَٱلَّذِيٓ أَخۡرَجَ ٱلۡمَرۡعَىٰ ٤

Walladhī akhrajal-mar'ā

Na aliye otesha malisho! 4

فَجَعَلَهُۥ غُثَآءً أَحۡوَىٰ ٥

Faja'alahū ghuthā'an ahwā

Kisha akayafanya makavu, meusi. 5

سَنُقۡرِئُكَ فَلَا تَنسَىٰٓ ٦

Sanuqri'uka falā tansā

Tutakusomesha wala hutasahau! 6

إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُۚ إِنَّهُۥ يَعۡلَمُ ٱلۡجَهۡرَ وَمَا يَخۡفَىٰ ٧

Illā mā shā'allāhu innahū ya'lamul-jahra wamā yakhfā

Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana. 7

وَنُيَسِّرُكَ لِلۡيُسۡرَىٰ ٨

Wanuyassiruka lil-yusrā

Na tutakusahilishia yawe mepesi. 8

فَذَكِّرۡ إِن نَّفَعَتِ ٱلذِّكۡرَىٰ ٩

Fadhakkir in nafa'atidh-dhikrā

Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa. 9

سَيَذَّكَّرُ مَن يَخۡشَىٰ ١٠

Sayaddhakkaru man yakhshā

Atakumbuka mwenye kuogopa. 10

وَيَتَجَنَّبُهَا ٱلۡأَشۡقَى ١١

Wayatajannabuhal-ashqā

Na atajitenga mbali nayo mpotovu, 11

ٱلَّذِي يَصۡلَى ٱلنَّارَ ٱلۡكُبۡرَىٰ ١٢

Alladhī yaslan-nāral-kubrā

Ambaye atauingia Moto mkubwa. 12

ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحۡيَىٰ ١٣

Thumma lā yamūtu fīhā walā yahyā

Tena humo hatakufa wala hawi hai. 13

قَدۡ أَفۡلَحَ مَن تَزَكَّىٰ ١٤

Qad aflaha man tazakkā

Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa. 14

وَذَكَرَ ٱسۡمَ رَبِّهِۦ فَصَلَّىٰ ١٥

Wadhakarasma rabbihī fasallā

Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akaswali. 15

بَلۡ تُؤۡثِرُونَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا ١٦

Bal tu'thirūnal-hayawātad-dunyā

Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia! 16

وَٱلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ وَأَبۡقَىٰٓ ١٧

Wal-ākhiratu khayrun wa abqā

Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi. 17

إِنَّ هَٰذَا لَفِي ٱلصُّحُفِ ٱلۡأُولَىٰ ١٨

Inna hādhā lafis-suhufil-ūlā

Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo, 18

صُحُفِ إِبۡرَٰهِيمَ وَمُوسَىٰ ١٩

Suhufi ibrāhīma wamūsā

Vitabu vya Ibrahimu na Musa. 19

Nambari za maelezo ya chini zinaelekeza kwenye ukurasa wa aya, ambapo maelezo ya mfasiri yanaonyeshwa.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Maswali

Surat Al-A'la ina aya ngapi?

Surat Al-A'la ina aya 19. Ni sura namba 87 ya Qur'ani.

Je, Surat Al-A'la ni Makkiya au Madaniya?

Surat Al-A'la ni sura Makkiya.

Surat Al-A'la iko katika juzuu gani?

Surat Al-A'la iko katika juzuu 30.

Je, naweza kusikiliza Surat Al-A'la?

Ndiyo. Bonyeza Cheza juu ya ukurasa huu, au anza kutoka aya yoyote. Programu ya Qabas pia inakuwezesha kuipakua ili kuisikiliza bila intaneti.