Dua baada ya adhana

Unachosema adhana inapoadhiniwa na dua baada ya kumalizika.

1 Mara moja

Maana na chanzo

Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudry -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mtakaposikia wito (Adhana), basi semeni mfano wa yale ayasemayo muadhini".

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Daraja: Sahihi

Maelezo

Anahimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kumjibu muadhini wakati wa kumsikia, na hii ni kwa sisi kusema mfano wa ayasemayo, sentensi kwa sentensi, Anaposema Allaahu Akbaru nasi tunasema Allaahu Akbaru, na anapotamka shahada mbili, nasi tunazitamka baada yake, Linaondolewa tamko la: (Hayya a'las swalaa, Hayya a'lal falaah) hapo tutasema baada yake: Laa haulaa walaa quwwata illaa billaah.

Faida

  • Atamfuatisha muadhini wa kwanza baada ya kumaliza wa kwanza, hata kama waadhini watakuwa wengi; kwa sababu ya ujumla wa hadithi hii.
  • Atamjibu muadhini katika hali zake zote, ikiwa atakuwa hayuko chooni au akikidhi haja.

Soma kwenye HadeethEnc.com

2 Mara moja

Maana na chanzo

Imepokewa kutoka kwa Omar Bin Khattwab- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Atakapo sema Muadhini: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kisha akasema mmoja wenu: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kisha akasema: Ash-hadu An laa ilaha ila llahu, akasema: Ash-hadu An laa ilaha ila llahu. kisha akasema: Ash-hadu Anna Muhammadan Rasuulullahi, Akasema: Ash-hadu Anna Muhammadan Rasuulullahi, kisha akasema: Hayya ala Swalaah, akasema: Laa Haula wala Quwwata ila Billahi, kisha akasema: Hayya ala lfalaah, akasema: Laa Haula walaa Quwwata ila Billahi, kisha akasema: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, akasema: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kisha akasema: Laa ilaha ila llahu, akasema: Laa ilaha ila llahu, kutoka ndani ya moyo wake, basi ataingia peponi".

Imepokelewa Imamu Muslim Daraja: Sahihi

Maelezo

Adhana ni kuwatangazia watu kuwa muda wa swala umeingia, na maneno ya adhana ni maneno yaliyokusanya itikadi ya imani.

Na katika hadithi hii anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kinachotakiwa kisheria wakati wa kusikia adhana, nako msikiaji asema kama anavyosema muadhini, muadhini akisema: "Allahu Akbaru" Mwenye kusikia naye anasema: "Allahu Akbaru" ataendelea hivyo, isipokuwa katika kauli ya muadhini "Hayya alas swalaa", "Hayya alal falaah, atasema mwenye kusikia: "Laa haulaa wala quwwata illaa billaah".

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakaye rudia rudia nyuma ya muadhini kwa utakasifu kutoka moyoni mwake ataingia peponi.

Na maana ya maneno ya adhana ni: "Allahu Akbaru": Yaani: Yeye mtakasifu ni mtakasifu na ni mtukufu na ni mkubwa kuliko kila kitu.

"Ash-hadu an laa ilaaha illa llaah": Yaani: Hapana muabudiwa wa haki zaidi ya Allah.

"Ash-hadu anna Muhammadan Rasuulu llaah" Yaani: Nina kiri na nina shuhudia kwa ulimi wangu na moyo wangu, yakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alimtuma Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ni wajibu kumtii.

"Hayya alas swalaa", Yaani: Njooni katika swala, na kauli ya mwenye kusikia: "Laa haulaa walaa quwwata illa billaah", Yaani hakuna ujanja wa kuvimaliza vikwazo vya ibada, wala nguvu ya kuzifanya na wala uwezo wa chochote ila ni kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

"Hayya alal falaah", Njooni katika sababu ya kufanikiwa, nako ni kufuzu kwa Pepo na kusalimika na moto.

Faida

  • Fadhila za kumjibu muadhini kwa mfano wa yale anayosema, isipokuwa katika hayyalaa mbili, atasema: "Laa haulaa walaa quwwata illa billaah".

Soma kwenye HadeethEnc.com

3 Mara moja

أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، رَضِيتُ بِاللهِ رَبًّا وَبِمُحَمَّدٍ رَسُولًا، وَبِالْإِسْلَامِ دِينًا

Maana na chanzo

Kutoka kwa Sa'd Bin Abi Waqaas Allah amridhie kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakayesema wakati anamsikia muadhini: Ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika nakuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake, nimeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ni Mola wangu na Muhammadi kuwa ni Mtume na Uislamu kuwa ni dini, atasamehewa dhambi zake".

Imepokelewa Imamu Muslim Daraja: Sahihi

Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema wakati akimsikia muadhini "Ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika wake", Yaani: Nina kiri na kukubali na ninatoa habari kuwa hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kila mwenye kuabudiwa kinyume na yeye ni batili, "Na kuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake" Yaani: Yeye ni mja wala haabudiwi, na ni Mjumbe wake haongopi, "Nimeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi" Yaani: Kwa ulezi wake na uungu wake na majina yake na sifa zake, "Na Muhammadi kuwa ni Mtume" Yaani: Kwa yote aliyotumwa kwayo, na akatufikishia, "Na Uislamu" Yaani: Kwa hukumu zote za Uislamu ikiwemo maamrisho na makatazo, "Dini" Yaani: Kwa itikadi na kutii, "Atasamehewa dhambi zake" Yaani: Katika dhambi ndogo.

Faida

  • Kuirudia rudia dua hii wakati wa kusikia adhana ni miongoni mwa mambo yanayofuta madhambi.

Soma kwenye HadeethEnc.com

4 Mara moja

اللَّهُمَّ رَبَّ هَذِهِ الدَّعْوَةِ التَّامَّةِ، وَالصَّلاَةِ القَائِمَةِ، آتِ مُحَمَّدًا الوَسِيلَةَ وَالفَضِيلَةَ، وَابْعَثْهُ مَقَامًا مَحْمُودًا الَّذِي وَعَدْتَهُ

Maana na chanzo

Na kutoka kwa Jaabir bin Abdillah -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayesema wakati anasikia adhana: Allaahumma rabba haadhihid da'watit taamma, was swalaatul qaaima, aati Muhammadanil wasiilata wal fadhwiila, wab'ath-huu maqaaman mahmuudanil ladhii wa a'ttah, (Ewe Mwenyezi Mungu, Mola wa wito huu uliotimia, na swala iliyosimama, mpe Muhammad utetezi na fadhila, na umfufue mahali pakusifiwa ulipomuahidi) basi utakuwa halali kwake utetezi wangu siku ya Kiyama".

Imepokelewa na Al-Bukhaariy Daraja: Sahihi

Maelezo

Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema wakati amemsikia muadhini baada ya kumaliza adhana:

"Ewe Mwenyezi Mungu Mola wa wito huu" nayo ni matamshi ambayo hutumika kuita katika ibada ya Mwenyezi Mungu na swala, "Uliotimia" uliokamilika, wito wa tauhidi na ujumbe, "na swala iliyosimama" yenye kudumu ambayo itasimamishwa hivi punde, "mpe" mgawie, "Muhammadi utetezi" na cheo cha juu peponi ambacho hakimstahiki mwingine ila yeye rehema na amani ziwe juu yake, "na fadhila" cheo cha juu zaidi ya vyeo vya viumbe, "na umfufue" na umpe "nafasi yenye kusifiwa" anayosifiwa mwenye kuwanayo; nao ni utetezi mkuu wa siku ya Kiyama, "uliyomuahidi" kwa kauli yako "Huenda akakufufua Mola wako katika nafasi yenye kusifiwa" ili iwe yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Atakayeomba dua hii atastahiki kuupata utetezi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku ya Kiyama.

Faida

  • Sheria ya kuomba dua hii baada ya kumaliza kurudia nyuma ya muadhini, na ambaye hatosikia adhana; basi hatakiwi kuisema.
  • Ubora wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kiasi kwamba amepewa uwakala na fadhila na nafasi na utetezi mkuu wa kutetea kuhukumiwa baina ya viumbe.
  • Kuthibitisha utetezi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake; kwa kauli yake: "Ataupata utetezi wangu siku ya Kiyama".
  • Utetezi wake rehema na amani ziwe juu yake utakuwa kwa wale waliotenda madhambi makubwa katika umma wake ili wasiingie motoni, au aliyeingia atoke, au katika kuingia peponi pasina hesabu, au kunyanyuliwa daraja aliyeingia.
  • Amesema Attwayyibi: kuanzia mwanzo wa "Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu" huu ndio wito uliotimia, na maneno "Hayya a'la" (njooni katika) ndio swala iliyosimama katika kauli yake wanasimamisha swala, na inawezekana kuwa makusudio ya swala hapa ni dua, na kwa mujibu wa hili kauli yake "na swala iliyosimama" ni kubainishwa wito uliyotimia, na inawezekana kuwa makusudio yake ni swala iliyozoeleka wanayoitwa kwayo kwa wakati huo, na ndilo lililokaribu na maana halisi.
  • Amesema Al-Mulhab: Katika hadithi hii kuna himizo la kuomba dua katika nyakati za swala; kwa sababu ni hali zinazotarajiwa zaidi kujibiwa dua.

Soma kwenye HadeethEnc.com

5 Mara moja

Maana na chanzo

kutoka kwa Abdillah bin Amri bin Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yao- Yakwamba amemsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake anasema: "Mtakapo msikia muadhini basi semeni mfano wa yale anayo yasema, kisha mnitakie rehema, ni kwamba yule atakaye nitakia rehema mara moja Allah atamtakia rehema mara kumi, kisha niombeeni kwa Allah ukaribu, hakika ukaribu huo ni daraja ndani ya Pepo, halipati daraja hilo isipokuwa mja miongoni mwa waja wa Allah, na ninatarajia niwe mimi ndiye huyo mja huyo, na atakayeniombea mimi ukaribu ataupata uombezi".

Imepokelewa Imamu Muslim Daraja: Sahihi

Maelezo

Ameelekeza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mwenye kumsikia muadhini kwa ajili ya swala basi naye amfuatilize nyuma yake, aseme mfano wa kauli zake, isipokuwa haiala mbili (Hayya alas-swalaa, na hayya alal falaah), atasema baada yake: Laa haulaa walaa quwwata illa billaah, kisha atamtakia rehema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baada ya kumalizika kwa adhana, kwani atakayemtakiwa rehema mara moja, basi Mwenyezi Mungu atamtakia rehema kumi kwa sababu ya dua hiyo moja, na maana ya Mwenyezi Mungu kumtakia rehema mja wake: Ni kumsifu mja wake mbele ya Malaika.

Kisha akaamrisha kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ukaribu -Rehema na amani ziwe juu yake-, nayo ni nafasi iliyoko peponi, na ni daraja ya juu zaidi kuliko zote, haimstahiki na wala haiwezekani nafasi hiyo ila kwa mja mmoja katika waja wote wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ninataraji mimi kuwa ndiye mja huyo, na alisema hivyo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa sababu ya kujinyenyekeza; kwa sababu nafasi hiyo ikiwa haistahiki ila kwa mtu mmoja, hawezi kuwa mmoja huyo zaidi ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-; kwa sababu yeye ndiye mbora wa viume wote.

Kisha akabainsha -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayemuombea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nafasi ya ukaribu basi ataupata utetezi wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.

Faida

  • Himizo la kumjibu muadhini.
  • Fadhila za kumtakia rehema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baada ya kumjibu muadhini.
  • Himizo la kumuombea ukaribu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baada ya kumtakia rehema.
  • Kumebainishwa maana ya ukaribu, na ukubwa wa nafasi yake, kiasi kwamba haumstahiki ila mja mmoja pekee.
  • Kumebainishwa ubora wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kiasi ambacho kapendelewa nafasi hiyo ya juu.
  • Atakayemuomba Mwenyezi Mungu ukaribu kwa ajili ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- basi atastahiki kupata uombezi.
  • Kumebainishwa unyenyekevu wake -Rehema na amani ziwe juu yake- kiasi kwamba ameuomba umma wake umuombee dua ili apate nafasi hiyo, pamoja nakuwa nafasi hiyo itakuwa yake.
  • Upana wa fadhila za Mwenyezi Mungu na rehema yake, jema moja linalipwa kwa mema kumi mfano wake.

Soma kwenye HadeethEnc.com

6 Mara moja

Maana na chanzo

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maliki -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Dua hairejeshwi (inayoombwa) baina ya adhana na kukimiwa swala".

Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na Nasaai Daraja: Sahihi

Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake fadhila za dua baina ya adhana na ikama, nakuwa dua hiyo hairejeshwi na inanafasi kubwa ya kujibiwa, basi muombeni Mwenyezi Mungu ndani ya wakati huu.

Faida

  • Fadhila za wakati huu kwa ajili kuomba dua.
  • Atakapojipamba muombaji kwa adabu za kuomba dua, na akatafuta mahala pake na nyakati zake bora, na akajiepusha na kumuasi Mwenyezi Mungu, na akachukua tahahadhari ya kutotumbukia katika mambo yasiyofaa na yenye kutatiza, na akamdhania vizuri Mwenyezi Mungu: Basi ni rahisi sana kujibiwa, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
  • Amesema Al-Munawi kuhusu kujibiwa dua: Yaani: Baada ya kukusanya sharti za dua na nguzo zake na adabu zake, ikiwa kitapelea kitu chochote basi asilaumu ila nafsi yake.
  • Ni sunna kuomba dua: Ima zijibiwe haraka dua zake, au aepushiwe katika shari mfano wake, au atunziwe Akhera; na hii ni kulingana na hekima ya Mwenyezi Mungu na huruma yake.

Soma kwenye HadeethEnc.com

Maswali

Kuna nini kwenye ukurasa huu?

Dua baada ya adhana: kila moja kwa Kiarabu, pamoja na maana yake, hadithi inakotoka, daraja yake na maelezo.

Tafsiri zinatoka wapi?

Kutoka HadeethEnc.com, Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa. Kila hadithi inaonyeshwa kama walivyoichapisha, pamoja na chanzo na daraja yake, na viungo vya asili.

Naweza kupata kikumbusho cha kila siku?

Ndiyo. Programu ya bure ya Qabas kwa Android inakukumbusha adhkar za asubuhi na jioni kila siku na ina kihesabu hicho hicho.