Dua ya kuingia na kutoka msikitini

Maneno yanayosemwa mlangoni mwa msikiti, unapoingia na unapotoka.

1 Mara moja

أعوذ بالله العظيم، وبوجهه الكريم، وسلطانه القديم، من الشيطان الرَّجِيم

Maana na chanzo

Kutoka kwa Abdallahi bin Amru bin A'swi -radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake: Kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, yakwamba yeye alikuwa anapoingia msikitini anasema: "Najilinda kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa uso wake mkarimu, na kwa mamlaka yake ya tangu, kutokana na shetani aliyelaaniwa" Akasema: Hivyo tu? Nikasema ndiyo. Akasema: Mtu anaposema hivyo shetani husema: Huyu kalindwa nami siku yake nzima.

Imepokelewa na Abu Daud Daraja: Ni nzuri (Hasan)

Maelezo

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoingia msikitini anasema: "Najilinda kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu" Yaani: Ninashikamana na kuegemea kwa Mwenyezi Mungu na sifa zake. "Na kwa uso wake Mkarimu" Yaani: Mkarim mtoaji, "Na kwa mamlaka yake) Yaani: Ushindi wake na uweza wake kwa amtakaye katika viumbe wake "Wa tangu" Yaani: Wa zamani na wa milele. "Kutokana na Shetani aliyelaaniwa" Yaani: Aliyetengwa na kufukuzwa kutoka katika rehema ya Mwenyezi Mungu, yaani: Ewe Mwenyezi Mungu nihifadhi kutokana na wasi wasi wake na upotoshaji wake na hatua zake na hatari zake, na udanganyifu wake na upotoshaji wake, kwani yeye ndiye sababu ya upotofu, na ndio mchochezi wa upotofu na ujinga, akaulizwa Abdillah bin Amri "Hivyo tu" Yaani: Je, alivyosema Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni hivyo tu? Akasema: Ndio.

Atakaposema dua hii mwenye kuingia msikitini; Shetani husema: Muingiaji kaihifadhi nafsi yake dhidi yangu wakati wake wote, mchana wake na usiku wake.

Faida

  • Fadhila za kuomba kwa dua hii wakati wa kuingia msikitini, nakuwa dua hii humkinga msemaji wake kutokana na Shetani siku nzima.
  • Tahadhari kutokana na Shetani, nakuwa humuwinda Muislamu; kwa ajili ya kumpoteza na kumshawishi.
  • Mtu atalindwa kutokana na upotofu na udanganyifu wa Shetani kwa kiwango ambacho moyo wake unamwamini Mwenyezi Mungu na kuihudhurisha dua hii, na kuamini kwake ahadi za Mwenyezi Mungu zinazotokana nayo.

Soma kwenye HadeethEnc.com

2 Mara moja

اللَّهُمَّ افْتَحْ لِي أَبْوَابَ رَحْمَتِكَ
اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ فَضْلِكَ

Maana na chanzo

Kutoka kwa Abuu Humaidi au kutoka kwa Abuu Usaidi Amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakapoingia mmoja wenu msikitini basi aseme: Allaahummaf-tah lii abwaaba rahmatika (Ewe Mola wangu, nifungulie milango ya rehema zako), na akitoka aseme: Allaahumma innii as-aluka min fadhlika (Ewe Mola wangu ninakuomba unipe katika fadhila zako)".

Imepokelewa Imamu Muslim Daraja: Sahihi

Maelezo

Ameuelekeza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- umma wake katika dua ambayo husemwa wakati wa kuingia msikitini: "Allaahummaf-tah lii abwaaba rahmatika (Ewe Mola wangu, nifungulie milango ya rehema zako), amuombe Mwenyezi Mungu Mtukufu amuandalie sababu za kupata rehema zake, na akitaka kutoka aseme: Allaahumma innii as-aluka min fadhlika (Ewe Mola wangu ninakuomba unipe katika fadhila zako), amuombe Mwenyezi Mungu Mtukufu ampe katika fadhila zake na ziada ya hisani zake miongoni mwa riziki ya halali.

Faida

  • Sunna ya dua hii wakati wa kuingia msikitini na wakati wa kutoka.
  • Zimetengwa rehema wakati wa kuingia, na fadhila wakati wa kutoka: Kwani mwenye kuingia hushughulika na yale yanayomkurubisha kwa Allah na katika Pepo yake ikawa ni bora ataje rehema, na anapotoka hutembea katika Ardhi kwa ajili ya kutafuta fadhila za Allah miongoni mwa riziki, ikawa ni bora kwake kutaja fadhila.
  • Dua hizi husomwa wakati wa kutaka kuingia msikitini, na wakati wa kutaka kutoka.

Soma kwenye HadeethEnc.com

Maswali

Kuna nini kwenye ukurasa huu?

Dua ya msikiti: kila moja kwa Kiarabu, pamoja na maana yake, hadithi inakotoka, daraja yake na maelezo.

Tafsiri zinatoka wapi?

Kutoka HadeethEnc.com, Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa. Kila hadithi inaonyeshwa kama walivyoichapisha, pamoja na chanzo na daraja yake, na viungo vya asili.

Naweza kupata kikumbusho cha kila siku?

Ndiyo. Programu ya bure ya Qabas kwa Android inakukumbusha adhkar za asubuhi na jioni kila siku na ina kihesabu hicho hicho.