Dua ndani ya swala: kufungua, rukuu, sijda na tashahhud

Dua alizokuwa akisoma Mtume ﷺ ndani ya swala, kuanzia takbira ya kufungua hadi salamu.

1 Mara moja

اللهُمَّ بَاعِدْ بَيْنِي وَبَيْنَ خَطَايَايَ كَمَا بَاعَدْتَ بَيْنَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ، اللهُمَّ نَقِّنِي مِنْ خَطَايَايَ كَمَا يُنَقَّى الثَّوْبُ الْأَبْيَضُ مِنَ الدَّنَسِ، اللهُمَّ اغْسِلْنِي مِنْ خَطَايَايَ بِالثَّلْجِ وَالْمَاءِ وَالْبَرَدِ

Maana na chanzo

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapotoa takbira katika swala ananyamaza kidogo kabla hajaanza kusoma, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nimuweka fidia baba yangu na mama yangu, hebu nieleze kunyamaza kwako kati ya takbira na kisomo: Ni nini unasema: Akasema: Ninasema: Allaahumma baaid bainiy -Ewe Mwenyezi Mungu weka mbali baina yangu- wa baina khatwaayaaya -na baina ya makosa yangu- kamaa baa a'tta bainal mashriqi wal maghribi -kama ulivyoweka mbali baina ya mashariki na magharibi. Allaahumma naqqiniy- Ewe Mwenyezi Mungu nitakase mimi- min khatwaayaaya -kutokana na makosa yangu- kamaa yunaqqath-thaubul abyadhwa -kama inavyotakaswa nguo nyeupe- minad danasi -kutokana na uchafu. Allaahumma ghsilniy -Ewe Mwenyezi Mungu nioshe mimi- min khatwaayaaya -kutokana na makosa yangu- bil maai wath thalji wal baradi -kwa maji na barafu na baridi".

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Daraja: Sahihi

Maelezo

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anaposema “Allahu Akbar” kwa ajili ya swala, alikuwa akitulia kidogo kabla ya kusoma Al-Fatiha, ambamo alikuwa akiianza Swala yake kwa baadhi ya dua, miongoni mwa dua hizo zilizoripotiwa ni kauli yake: "Allaahumma baaid bainii wa baina khatwaa yaaya, kamaa baa'atta bainal mashriqi wal maghribi, Allaahu naqinii min khatwaayaaya, kamaa yunaqqah-thaubal abyadhwa minad-danasi, Allaahuma gh-silnii bil maai wath-thalji wal baradai", Hivyo anamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amtenge mbali na madhambi ili asije akaangukia ndani yake, hata kusiwe na kukutana nayo, kama vile hakuna kukutana baina ya Mashariki na Magharibi, na ikitokea katumbukia ndani yake, basi amtakase kutokana na madhambi hayo kama uchafu unavyotolewa kwenye nguo nyeupe, na amuoshe dhambi zake na kuupoza miale na joto lake, kwa vitakatishi hivi baridi; Maji, theluji na baridi.

Faida

  • Kuificha dua ya ufunguzi wa swala, hata kama swala itakuwa ni ya kusoma kwa sauti.
  • Pupa ya Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao katika kutaka kujua hali za Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika harakati zake na kutulia kwake.
  • Zimekuja namna nyingine za dua ya ufunguzi, na kilicho bora kwa mtu afuatilie dua zilizokuja na kuthibiti kutoka kwake rehema na amani ziwe juu yake, ili asome hii wakati mwingine, na hii wakati mwingine.

Soma kwenye HadeethEnc.com

2 Mara moja

سَمِعَ اللهُ لِمَنْ حَمِدَهُ، اللَّهُمَّ رَبَّنَا لَكَ الْحَمْدُ، مِلْءَ السَّمَاوَاتِ وَمِلْءَ الْأَرْضِ وَمِلْءَ مَا شِئْتَ مِنْ شَيْءٍ بَعْدُ

Maana na chanzo

Imepokewa kutoka kwa Abuu Aufaa -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anaponyanyua mgongo wake kutoka katika rukuu anasema: "Sami'allaahu liman hamidah, Allaahumma Rabbanaa lakal hamdu, mil as samaawaati wamil al Ardhwi wamil amaashi ita min shai in ba'ad".

Imepokelewa Imamu Muslim Daraja: Sahihi

Maelezo

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anaponyanyua mgongo wake kutoka katika rukuuu ndani ya swala, anasema: " Sami'allaahu liman hamidah", Yaani: Atakayemhimidi Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atamjibu, na atakubali himidi zake na atamlipa, kisha atamhimidi kwa kusema: Allaahumma Rabbanaa lakal hamdu, mil as samaawaati, wamil al Adhwi wamil amaa shi ita min shai in baad", himdi zenye kujaza mbingu na ardhi na vilivyo kati yake, na zinajaza ayatakayo Mwenyezi Mungu.

Faida

  • Kumebainishwa anayotakiwa kusema mwenye kusali anaponyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu.
  • Sheria ya kulingana sawa na utulivu baada ya kuinuka kutoka katika rukuu; kwa sababu haiwezekani aseme dhikiri hii ila baada ya kusimama wima na kutulia.
  • Dhikiri hii ni sheria katika swala zote, sawa sawa ziwe za faradhi au za sunna.

Soma kwenye HadeethEnc.com

3 Mara moja

اللَّهمَّ اغْفِرْ لي، وارْحَمْنِي، وعافِني، واهْدِني، وارزقْنِي

Maana na chanzo

Imepokewa Kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema kati ya sijida mbili: "Allaahumma ghfir lii, warhamnii, wa aafiniii, wahdinii, warzuqniii".

Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad Daraja: Ni Nzuri kwa Ushahidi wake mbalimbali

Maelezo

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiomba kati ya sijida mbili katika sala yake kwa dua hizi tano ambazo muislamu anazihitajia kwa uhitaji mkubwa, na zimekusanya heri za dunia na akhera, ikiwemo kuomba msamaha na stara ya madhambi na kufutwa kwake, na kumiminiwa rehema, na kusalimishwa na mambo yenye utata na matamanio na maradhi na magonjwa, na kumuomba Allah uongofu katika haki na kudumu katika hilo, na kupewa imani na elimu na matendo mema, na mali nzuri ya halali.

Faida

  • Sheria ya kuomba dua hii katika kikao kati ya sijida mbili.
  • Ubora wa dua hizi kwa kukusanya heri za dunia na akhera.

Soma kwenye HadeethEnc.com

4 Mara moja

اللهُمَّ اغْفِرْ لِي ذَنْبِي كُلَّهُ دِقَّهُ، وَجِلَّهُ، وَأَوَّلَهُ وَآخِرَهُ وَعَلَانِيَتَهُ وَسِرَّهُ

Maana na chanzo

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akisema katika sijida yake: "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe mimi dhambi zangu ndogo zake na kubwa zake za mwanzo wake na mwisho wake, za wazi zake na za siri zake".

Imepokelewa Imamu Muslim Daraja: Sahihi

Maelezo

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiomba katika sijida yake akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe madhambi yangu" Kwa kuyasitiri, na unikinge na madhara yake; uyasamehe na usiyatazame na uyafute, "yote", nakusudia: "Za ndani" ndogo zake, na chache zake, "pana zake" kubwa zake na nyingi zake, "za mwanzo wake" dhambi ya kwanza, "na za mwisho zake", na zilizo kati yake, "za wazi zake na siri zake" miongoni mwa zile asizozijua yeyote ila wewe Uliyetakasika.

Faida

  • Amesema bin Qayyim: Na kuomba kusamehewa madhambi madogo na makubwa, ya ndani na ya juu, ya mwanzo na ya mwisho, ya siri na ya wazi, kukusanya huku na kueneza huku kwa sababu anataka ikija toba ije kwa yote anayoyajua mja miongoni mwa madhambi, na yale asiyoyajua.
  • Imesemekana kuwa: Alitanguliza "Ya ndani" kabla ya " juu"; kwa sababu muombaji huanza na cha chini kisha anakwenda anapanda, yaani anapanda juu, kwa sababu madhambi makubwa mara nyingi hutokea kwa sababu ya kuendelea na madhambi madogo na kutojali, ni kana kwamba ni njia ya kuyaendea madhambi makubwa, na kinachokuwa ni sababu kina haki ya kutangulizwa kwa ajili ya kuthibitisha na kupandia kwenda juu.
  • Kujinyenyekeza kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kumuomba msamaha kutokana na madhambi yote, madogo na makubwa.
  • Amesema Nawawi: Hapa kuna msisitizo wa dua na kukithirisha matamshi yake hata kama baadhi yake yatatosheleza mengine.

Soma kwenye HadeethEnc.com

5 Mara moja

اللهُمَّ أَعُوذُ بِرِضَاكَ مِنْ سَخَطِكَ، وَبِمُعَافَاتِكَ مِنْ عُقُوبَتِكَ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْكَ لَا أُحْصِي ثَنَاءً عَلَيْكَ أَنْتَ كَمَا أَثْنَيْتَ عَلَى نَفْسِكَ

Maana na chanzo

Kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Siku moja nyakati za usiku nilimkosa kitandani Mtume rehema na amani ziwe juu yake nikaanza kumtafuta ukaangukia mkono wangu ndani ya nyayo zake zikiwa zimesimamishwa akiwa ndani ya msikiti, huku akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu ninajilinda kwa radhi zako kutokana na hasira zako, na salama yako dhidi ya adhabu zako, na ninajilinda kwako kutokana nawe, siwezi kuzidhibiti sifa zako kwa idadi maalum kama ambavyo wewe ulivyoisifu nafsi yako"

Imepokelewa Imamu Muslim Daraja: Sahihi

Maelezo

Anasema Aisha radhi za Allah ziwe juu yake: Nilikuwa nimelala pembezoni mwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, nikamkosa wakati wa usiku, nikagusa kwa mkono wangu sehemu aliyokuwa akiswalia ndani ya chumba; ghafla nikamuona amesujudu na miguu yake ikiwa imesimamishwa, mara nikamsikia akisema:

"Ninajilinda" Na ninapitia "Katika radhi zako dhidi ya hasira zako" juu yangu au juu ya umma wangu, "na" ninaomba kinga "kwa salama yako" na msamaha wako mwingi "kutokana na adhabu zako", "na ninajilinda kwako kutokana nawe" na kwa sifa za uzuri wako kutokana na sifa za utukufu wako, kiasi kwamba hakuna awezaye kukinga dhidi yako ila wewe, hakuna pa kusalimika wala pa kujilinda kutokana na Mwenyezi Mungu ila kwake, "Siwezi kuzihesabu sifa zako" Sina uwezo wala siwezi kufikia kuzidhibiti na kuzihesabu kwa idadi kwa kushindwa kwangu kuzidhibiti kwa wingi neema zako na ihisani yako kama unavyostahiki, hata kama nikijitahidi katika hilo, "Wewe kama ulivyoisifia nafsi yako" wewe ndiye uliyeisifu dhati yako sifa zinazokustahiki, ni nani awezaye kutimiza haki ya sifa zako?!

Faida

  • Sunna ya kuomba dua hii katika sijida.
  • Amesema Miriki: Na katika moja kati ya riwaya za Nasaai: Alikuwa akisema dua hii anapomaliza swala yake na akaelekea kitandani kwake.
  • Sunna ya kumsifia Mwenyezi Mungu kwa sifa zake na kumuomba kwa majina yake yaliyothibiti katika Qur'ani na Sunna.
  • Hapa kuna kumtukuza muumba wakati wa kurukuu na kusujudu.
  • Inafaa kuomba ulinzi kupitia sifa za Mwenyezi Mungu, kama ambavyo inafaa kuomba ulinza kupitia dhati yake Yeye Aliyetakasika na kutukuka.
  • Amesema Al-Khattwabi: Katika maneno haya kuna maana ya ndani sana, nayo: Nikuwa aliomba kinga kwa Mwenyezi Mungu amkinge kupitia radhi zake kutokana na hasira zake, na kwa salama yake dhidi ya adhabu zake, na ridhaa na hasira ni maneno mawili tofauti yanayokwenda sambamba, vile vile kusalimika na kuadhibiwa pia, alipofikia kumtaja ambaye hana kinyume chake ambaye ni Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka alitaka kinga kutokana na Yeye kwake mwenyewe na si kwa mwingine, na maana yake: Ni kuomba msamaha dhidi ya mapungufu ya kutofikia wajibu wa haki stahiki katika kumuabudu, na kumtukuza. Na kauli yake: Sizidhibiti sifa juu yako: Yaani sina uwezo wala siwezi kuzifikia.

Soma kwenye HadeethEnc.com

6 Mara moja

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَعَلَى آلِ مُحَمَّدٍ، كَمَا صَلَّيْتَ عَلَى آلِ إِبْرَاهِيمَ، إِنَّكَ حَمِيدٌ مَجِيدٌ، اللَّهُمَّ بَارِكْ عَلَى مُحَمَّدٍ وَعَلَى آلِ مُحَمَّدٍ، كَمَا بَارَكْتَ عَلَى آلِ إِبْرَاهِيمَ، إِنَّكَ حَمِيدٌ مَجِيدٌ

Maana na chanzo

Kutoka kwa Abdul Rahman Bin Abii Laila amesema: Alikutana nami Ka'bu bin Ujza, akasema: Hivi wataka nikupe zaidi? Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alitoka kwetu sisi, tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumekwishafahamu ni vipi tutakusalimu, sasa ni vipi tutakutakia Rehema? Akasema: "Basi semeni: Ewe Mwenyezi Mungu mpe rehema Muhammadi na juu ya watu wa Muhammadi, kama ulivyompa rehema Ibrahim na juu ya watu wa Ibrahim, hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa, ewe Mwenyezi Mungu shusha baraka juu ya Muhammad na juu ya watu wa Muhammad, kama ulivyoteremsha baraka kwa watu wa Ibrahim, hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa".

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Daraja: Sahihi

Maelezo

Masahaba walimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu namna ya kumtakia rehema? baada ya kujua kwao namna kumuombea amani (salam) katika kikao cha tahiyatu ndani ya swala: "Amani iwe juu yako ewe Nabii na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake...?" Mtume Rehema na amani ziwe juu yake akawaeleza namna ya kumtakia rehema, na maana yake: "Ewe Mwenyezi Mungu mpe rehema Muhammad na juu ya watu wa Muhammad" Yaani: Mtaje kwa sifa nzuri kwa Malaika walioko juu mbinguni, na juu ya wafuasi wake katika dini yake, na waumini katika ndugu zake wa karibu. "Kama ulivyoteremsha rehema juu ya watu wa Ibrahim" Kama ulivyotoa takrima juu ya watu wa Ibrahim amani iwe juu yake, nao ni Ibrahim na Ismail na Is'haka na kizazi chake na wafuasi wao miongoni mwa waumini, basi zipeleke fadhila zako kwa Muhammad rehema na amani ziwe juu yake. "Hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa". Yaani: Mwenye kuhimidiwa katika dhati yako na sifa zako na vitendo vyako, mpana katika utukufu wako na ugawaji riziki wako. "Ewe Mwenyezi Mungu teremsha baraka kwa Muhammad na juu ya watu wa Muhammad kama ulivyoteremsha baraka juu ya watu wa Ibrahim" Yaani: Mpe katika kheri na karama zile zilizo kubwa zaidi na uzizidishe na umdumishie kheri hizo.

Faida

  • Wema waliotangulia walikuwa wakizawadiana kuhusu mambo ya elimu.
  • Uwajibu wa kumtakia rehema Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika tashahudi ya mwisho katika swala.
  • Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliwafundisha Masahaba wake kumtakia amani na rehema juu yake.
  • Namna hii ya kuomba ndio namna sahihi zaidi katika kumtakia rehema Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Soma kwenye HadeethEnc.com

7 Mara moja

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ القَبْرِ، وَمِنْ عَذَابِ النَّارِ، وَمِنْ فِتْنَةِ المَحْيَا وَالمَمَاتِ، وَمِنْ فِتْنَةِ المَسِيحِ الدَّجَّالِ

Maana na chanzo

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake akiomba akisema: "Allaahumma inniy a'udhubika min adhaabil Qabri, wa min adhaabin naari, wamin fitnatil mahyaa wal mamaati, wamin sharri fitnatil masiihiddajjaali" Ewe Mola wangu hakika mimi ninajilinda kwako kutokana na adhabu ya kaburi, na kutokana na adhabu ya moto, na fitina za uhai na za kifo, na kutokana na fitina za masihi dajali".

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Daraja: Sahihi

Maelezo

Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake akiomba kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na mambo manne, baada ya tashahudi ya mwisho na kabla ya swala, na akatuamrisha tuombe kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na mambo hayo,

Jambo la kwanza: Kuomba kinga kutokana na adhabu za kaburi.

Jambo la pili: Kuomba kinga ya kuepukana na adhabu ya moto siku ya Kiyama.

La tatu: Kuomba kinga itokanayo na fitina za uhai ikiwemo matamanio ya dunia yaliyoharamishwa na ikiwemo pia shub-ha (utata) wenye kupoteza, na kutokana na fitina za mauti, yaani muda wa kukata roho, tusije kupinda tukatoka katika Uislamu au Sunna, au fitina za kaburini kama maswali ya Malaika wawili.

Jambo la nne:Kuomba kinga zitokanazo na fitina za Masihi Dajali atakeyetokea zama za mwisho, Mwenyezi Mungu atawapa mtihani waja wake kupitia yeye; na Mtume kamtaja kwa jina kutokana na ukubwa wa fitina zake.

Faida

  • Ombi hili la kinga ni miongoni mwa dua muhimu na ni dua inayokusanya mambo mengi, kwakuwa imekusanya kuomba kinga dhidi ya shari za Duani na Akhera.
  • Kuthibiti uwepo wa adhabu za kaburi nakuwa adhabu hizo ni kweli.
  • Uhatari wa fitina na umuhimu wa kuomba kinga kwa Mwenyezi Mungu na kuomba dua ya kusalimika nazo.
  • Kuthibitika kutokea kwa Dajali na ukubwa wa fitina zake.
  • Sunna ya kusoma dua hii baada ya tashahudi ya mwisho.
  • Sunna ya kuomba dua baada ya matendo mema.

Soma kwenye HadeethEnc.com

8 Mara moja

Maana na chanzo

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Palipo karibu zaidi kwa mja na Mola wake ni pale anapokuwa kasujudu,Basi zidisheni dua".

Imepokelewa Imamu Muslim Daraja: Sahihi

Maelezo

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa mahala palipo karibu zaidi kwa mja na Mola wake ni pale anapokuwa kasujudu; Na hii ni kwa sababu mwenye kusali huweka kiungo bora na kitukufu kuliko vyote katika mwili wake juu ya Ardhi kwa kujinyenyekeza na kujidhalilisha na kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- anapokuwa kasujudu.

Na ameamrisha -Rehema na amani ziwe juu yake- kukithirisha dua katika sijida, yanakusanyika mambo mawili katika hilo, kujidhalilisha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa kauli na vitendo.

Faida

  • Utiifu humzidishia mja ukaribu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Ni Sunna kukithirisha dua katika sijida; kwani ni katika maeneo ya kujibiwa.

Soma kwenye HadeethEnc.com

Maswali

Kuna nini kwenye ukurasa huu?

Dua ndani ya swala: kila moja kwa Kiarabu, pamoja na maana yake, hadithi inakotoka, daraja yake na maelezo.

Tafsiri zinatoka wapi?

Kutoka HadeethEnc.com, Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa. Kila hadithi inaonyeshwa kama walivyoichapisha, pamoja na chanzo na daraja yake, na viungo vya asili.

Naweza kupata kikumbusho cha kila siku?

Ndiyo. Programu ya bure ya Qabas kwa Android inakukumbusha adhkar za asubuhi na jioni kila siku na ina kihesabu hicho hicho.