Dua ya kuomba msamaha (istighfar)

Sayyid al-Istighfar na maneno mengine ya kuomba msamaha kutoka Sunna.

1 Mara moja

اللَّهُمَّ أَنْتَ رَبِّي لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ خَلَقْتَنِي وَأَنَا عَبْدُكَ وَأَنَا عَلَى عَهْدِكَ وَوَعْدِكَ مَا اسْتَطَعْتُ أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا صَنَعْتُ أَبُوءُ لَكَ بِنِعْمَتِكَ عَلَيَّ وَأَبُوءُ لَكَ بِذَنْبِي فَاغْفِرْ لِي فَإِنَّهُ لَا يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا أَنْتَ

Maana na chanzo

Kutoka kwa Shadaad Bin Ausi Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na Amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Bwana wa Istighfari (Dua ya kuomba msamaha) Ni kusema: Allaahumma anta Rabbi Laa ilaaha illaa anta, khalaqtani wa anaa abduka wa ana a'laa a'hdika, wawa'dika mastatwa'tu, auudhubika min Sharri maa swana'tu, abuu ulaka bini'matika alaiyya, wa abuu ulaka bidhambi faghfirlii, fa innahuu laa yaghfirudh-dhunuuba illaa anta" Akasema: "Na atakayeisema dua hii mchana akiwa na yakini nayo, akafa katika mchana wake huo kabla hajafika jioni, basi atakuwa miongoni mwa watu wa peponi, na atakayeisema wakati wa usiku akiwa na yakini nayo, akafariki kabla hajafika asubuhi, basi huyo atakuwa miongoni mwa watu peponi".

Imepokelewa na Al-Bukhaariy Daraja: Sahihi

Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake anaeleza kuwa Istighfari (Kuomba msamaha) kuna matamshi mengi, nakuwa matamshi bora na makubwa zaidi ni mja kusema: "Ewe Mwenyezi Mungu wewe ndiye Mola Mlezi hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa wewe, umeniumba na mimi ni mja wako na mimi nipo juu ya ahadi yako na maonyo yako kwa kiasi niwezavyo, ninataka hifadhi kwako kutokana na shari niliyo ifanya, ninakiri kwa neema zako zilizo juu yangu, na ninakiri kwa madhambi yangu, basi nisamehe mimi, kwani hakuna afutae madhambi isipokuwa wewe. Hivyo basi mja anaanza kukiri upweke wa Mwenyezi Mungu, nakuwa Mwenyezi Mungu ndiye muumba wake na muabudiwa wake hana mshirika wake, na kuwa yeye yuko katika ahadi aliyomuahidi Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, miongoni mwa imani na utiifu kwake, kwa kadiri ya uwezo wake; kwa sababu mja kwa namna yoyote atakavyotekeleza ibada hawezi kutekeleza yote aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu, na wala hawezi kutimiza haki stahiki katika kushukuru neema, nakuwa yeye anajilinda kwa Mwenyezi Mungu, na anajikinga kwake, kwani yeye ndiye mwenye kutakwa ulinzi kutokana na shari zote alizozitengeneza mja, Nakuwa yeye anakiri na kukubali kwa hiari yake neema zake juu yake, na anairudia nafsi yake kwa kukiri na kukubali madhambi yake na maasi yake, Na baada ya kupitia kwa Mwenyezi Mungu, atamuomba Mola wake asitiri makosa yake na amkinge na dhambi zake kwa msamaha wake na fadhila zake na rehema zake, kwani hakuna awezaye kusamehe madhambi ila yeye Mtukufu. Kisha akaeleza rehema na amani ziwe juu yake kuwa dua hii ni katika dhikiri na dua za asubuhi na jioni, nakuwa atakayeisema kwa yakini na kwa kuhudhurisha moyo wake na kwa kuiamini, mwanzo wa siku yake, kwanzia kuchomoza kwa Jua mpaka kupinduka kwake, nao ni wakati wa mchana, akafa, ataingia peponi, Na atakayeisema usiku, nao ni kuanzia kuzama kwa jua mpaka kuchomoza kwa Alfajiri, akafariki kabla hajafika asubuhi, ataingia peponi.

Faida

  • Namna za kuomba msamaha zinatofautiana na baadhi yake ni bora kuliko zingine.
  • Nakuwa ni wajibu kwa mja apupie kumuomba Mwenyezi Mungu kwa dua hii; kwani ndio bwana wa dua zote za kuomba msamaha.

Soma kwenye HadeethEnc.com

2 Mara moja

رَبِّ اغْفِرْ لِي خَطِيئَتِي وَجَهْلِي، وَإِسْرَافِي فِي أَمْرِي كُلِّهِ، وَمَا أَنْتَ أَعْلَمُ بِهِ مِنِّي، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي خَطَايَايَ، وَعَمْدِي وَجَهْلِي وَهَزْلِي، وَكُلُّ ذَلِكَ عِنْدِي، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي مَا قَدَّمْتُ وَمَا أَخَّرْتُ، وَمَا أَسْرَرْتُ وَمَا أَعْلَنْتُ، أَنْتَ المُقَدِّمُ وَأَنْتَ المُؤَخِّرُ، وَأَنْتَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

Maana na chanzo

Kutoka kwa Abuu Mussa radhi za Allah ziwe juu yake, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakwamba yeye alikuwa akiomba kwa dua hii: "Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe mimi makosa yangu, na ujinga wangu, na ubadhirifu wangu katika jambo langu lote, na yale unayoyajua kutoka kwangu, ewe Mola wangu nisamehe makosa yangu, na yale ya makusudi na ujinga wangu na mzaha wangu, na hayo yote yaliyo kwangu, ewe Mola wangu nisamehe niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, na niliyoyaficha na niliyoyatangaza, wewe ndiye muwahishaji na wewe ndiye mcheleweshaji, na wewe juu ya kila kitu ni muweza".

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Daraja: Sahihi

Maelezo

Ilikuwa katika dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake zilizokusanya mambo mengi ni kauli yake:

"Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe makosa yangu" "na dhambi zangu", na yale yaliyotokea kwangu pasina kujua.

"Na ubadhirifu wangu katika jambo langu lote" na uzembe wangu na kuvuka kwangu mipaka.

"Na yale uyajuayo kutoka kwangu" Uliyoyajua ewe Mwenyezi Mungu lakini mimi nimeyasahau.

"Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe makosa yangu na makusudi yangu" Na yale yaliyotokea kwa makusudi na kwa kujua kwangu kuwa ni dhambi.

"Na niliyodhamiria na yale ya mzaha" Na yale yaliyotekea kwa mzaha, na yale yaliyotokea katika hali zote mbili.

"Na hayo yote toka kwangu" Kiasi kwamba yote yaliyotajwa yamekusanya madhambi na aibu zote.

"Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe niliyoyatanguliza" Katika yale yaliyopita, "Na yale niliyoyachelewesha" Katika yale yatakayokuja.

"Na yale niliyoyafanya kwa siri" niliyoyaficha "Na niliyoyatangaza" Na kuyaonyesha wazi.

"Wewe ndiye muwahishaji na wewe ndiye mcheleweshaji" Unamtanguliza umtakaye katika viumbe wako katika rehema zako kwa kumpa taufiki katika yale unayoyaridhia, na wewe ndiye unayemchelewesha umtakaye katika hilo, kwa kumnyima uwezo, hakuna wa kuyapeleka mbele uliyoyachelewesha, na wala hakuna kuyachelewesha mambo uliyoyawahisha.

"Na wewe juu ya kila kitu ni muweza" Yaani: Unauwezo uliokamilika na maamuzi timamu, mfanyaji pasina kizuizi cha yote uyatakayo.

Faida

  • Fadhila za dua hii, na kuipupia kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  • Katazo la kufanya ubadhirifu nakuwa mbadhirifu amejiingiza katika adhabu.
  • Mwenyezi Mungu Mtukufu anamjua mwanadam vizuri zaidi kuliko anavyojijua, hivyo anatakiwa akabidhi mambo yake kwa Mwenyezi Mungu; kwani yeye anaweza kukosea pasina kujua.
  • Mwanadam anaweza kuchukuliwa hatua kwa sababu ya mzaha wake kama anavyochukuliwa katika kukusudia kwake, hivyo ni wajibu kwa mwanadam achukue tahadhari katika mzaha wake.
  • Amesema bin Hajari Al-Asqalaani: Sijaona chochote katika njia za mapokezi ya hadithi hii kuwa dua hii inasomwa mahala fulani, na riwaya zimekuja nyingi zikionyesha mwisho wake... kama kusema ndani ya swala za usiku, na riwaya za mapokezi zimetofautiana, je alikuwa akiisoma kabla ya salaam au baada yake? Na zote mbili zimeelezwa.
  • Je, Mtume rehema na amani ziwe juu yake anakosea na kuomba msamaha? Imesemekana kuwa alisema hivyo kwa unyenyekevu na kwa kuitenza nguvu nafsi yake, na akachukulia kuwa kupitwa na ukamilifu na kuacha kilicho bora ni dhambi, au alikusudia yale yanayotokea kwa kusahau, au yale yaliyotokea kabla ya utume, na imesemwa kuwa: Kutaka msamaha ni ibada hivyo ni lazima kuileta, si kwa sababu ya kutaka kusamehewa pekee, bali ni kwa kumuabu Mwenyezi Mungu, na imesemwa kuwa: Hili ni angalizo na ni funzo kwa umma wake; ili wasijiaminishe na wakaacha kuomba msamaha.

Soma kwenye HadeethEnc.com

3 Mara moja

Maana na chanzo

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, katika yale anayoyasimulia kutoka kwa Mola wake Mtukufu, amesema: "Mja alifanya dhambi akasema: Ee Mola wangu nisamehe dhambi yangu, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mja wangu katenda dhambi, akajua kuwa ana Mola Mlezi mwenye kusamehe dhambi, na humsitiri kwa ndambi hiyo au humuadhibu kwa kutenda dhambi, kisha akarudi tena akatenda dhambi, akasema: Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe dhambi yangu, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Mja wangu katenda dhambi, akajua kuwa ana Mola Mlezi mwenye kusamehe dhambi, na ana adhibu kwa kutenda dhambi, fanya utakavyo nimekusamehe".

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Daraja: Sahihi

Maelezo

Anasimulia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutoka kwa Mola wake Mlezi ya kwamba mja anapofanya dhambi kisha akasema: Ewe Mola wangu nisamehe dhambi yangu, Mwenyezi Mungu husema: Mja wangu katenda dhambi, akajua kuwa ana Mola Mlezi mwenye kusamehe dhambi, akamsitiri na akamsamehe, au akamuadhibu, basi hakika nimemsamehe. Kisha mja akarudi akafanya dhambi, akasema: Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe dhambi yangu, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: Mja wangu katenda dhambi, akajua kuwa ana Mola Mlezi mwenye kusamehe dhambi, akamsitiri na akamsamehe, au akamuadhibu, basi kwa hilo nimemsamehe mja wangu. Kisha mja akarudi akafanya dhambi, akasema: Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe dhambi langu, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: Mja wangu katenda dhambi, akajua kuwa ana Mola Mlezi mwenye kusamehe dhambi, akamsitiri na akamsamehe, au akamuadhibu, basi kwa hilo nimemsamehe mja wangu, afanye atakavyo madamu kila anapofanya dhambi analiacha na anajuta na anaazimia kutolirudia dhambi hilo mara nyingine, madamu ataendelea kufanya hivi, anatenda dhambi na anatubia nitaendelea kumsamehe, kwani toba hubomoa yaliyo kabla yake.

Faida

  • Upana wa huruma ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake na kuwa mwanadamu vyovyote vile atakavyotenda dhambi, vyovyote vile atakavyofanya, atakapotubia kwake na akarejea basi Mwenyezi Mungu humsamehe.
  • Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu hutumai kupata msamaha wa Mola wake Mlezi, na huogopa adhabu yake, hivyo huenda mbio kutubia na wala haendelei kubaki katika maasi.
  • Sharti za toba sahihi: Ni kujiondoa katika dhambi, na kulijutia, na kutia nia ya kutolirudia dhambi, na toba ikiwa ni katika mali za watu au heshima zao au nafsi, hapo huongezeka sharti la nne, nalo: Ni kujivua kutoka kwa mwenye haki yake, au kumpa haki yake.
  • Umuhimu wa elimu ya kumjuwa Mwenyezi Mungu elimu ambayo humfanya mja kujua mambo ya dini yake, akatubia kila anapokosea, hakati tamaa wala hafanyi jeuri kwa kuendelea kubaki katika dhambi.

Soma kwenye HadeethEnc.com

4 Mara moja

Maana na chanzo

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: “Amesema Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka: “Ewe mwanadam, maadamu unaniomba na kunitumainia, nitakusamehe uliyo nayo wala sitojali Ewe mwanadam lau madhambi yako yangefika mawinguni kisha ukaniomba msamaha ningekusamehe wala sijali Ewe mwanadam, lau ungenijia na thamani ya dhambi za dunia, kisha ukakutana nami bila kunishirikisha na chochote, ningekuletea msamaha ujazo sawa na ardhi".

Imepokelewa Imamu Tirmidhiy Daraja: Ni nzuri (Hasan)

Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Hadithil Qudsi (tukufu): Ewe mwanadam, madam unaniomba na kutaraji rehema yangu, wala hujakata tamaa; Nitayasitiri madhambi yako na kuyafuta, bila kujali, hata kama madhambi na maasi haya ni katika madhambi makubwa. Ewe mwanadam! Lau madhambi yako yangekuwa mengi sana kiasi cha kuijaza nafasi ya baina ya mbingu na ardhi mpaka kiasi cha kufikia upenyo wake na kufunika pembe zake, kisha ukaniomba msamaha, basi ningekufutia na kukusamehe madhambi yote, bila kujali wingi wake.

Ewe mwanadam: Lau ungenijia mimi baada ya kufa ukiwa na madhambi na maasi ujazo wa ardhi, na ukafa haliyakuwa unanipwekesha hukunishirikisha na chochote; Ningekutana na madhambi na maasi haya nikiijaza ardhi kwa msamaha; kwa sababu mimi ni mwingi wa msamaha, na ninasamehe madhambi yote isipokuwa shirki.

Faida

  • Upana wa huruma ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na msamaha wake na fadhila zake.
  • Ubora wa tauhidi, nakuwa Mwenyezi Mungu anawasamehe madhambi pamoja na maasi wenye kumpwekesha.
  • Hatari ya ushirikina nakuwa Mwenyezi Mungu hawasamehe washirikina.
  • Amesema bin Rajab: Hadithi hii inakusanya sababu tatu za kusamehewa dhambi: Ya kwanza: Kuomba dua pamoja na matumaini, ya pili: Kutaka msamaha na kuomba toba, ya tatu: Kufa katika tauhidi.
  • Hadithi hii ni katika yale anayoyasimulia Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Mola wake Mlezi, na inaitwa Hadithil Qudsi (tukufu) Hadithi ya kiuungu, na maneno yake na maana yake ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu ila hayana sifa za Qur'ani ambazo inasifika nazo kuliko kitu kingine chochote, kama vile kumuabudu Mwenyezi Mungu kupitia kisomo chake, na kuwa na twahara kwa ajili yake, na kutoa changamoto na miujiza na kadhalika.
  • Dhambi zina aina tatu: Ya kwanza: Kumshirikisha Mwenyezi Mungu; Na dhambi hili haisamehe Mwenyezi Mungu Mtukufu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu amemharamishia Pepo". Ya pili: Ni mja kujidhulumu mwenyewe katika yale yaliyo kati yake na Mola wake Mlezi, kama madhambi na maasi; Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu huyasamehe hayo, na kuyaachilia mbali akitaka. Ya tatu: Ni madhambi ambayo Mwenyezi Mungu haachi chochote katika hayo, nayo ni dhulma ya waja wao kwa wao, hivyo ni lazima kulipiza kisasi.

Soma kwenye HadeethEnc.com

Maswali

Kuna nini kwenye ukurasa huu?

Dua ya kuomba msamaha: kila moja kwa Kiarabu, pamoja na maana yake, hadithi inakotoka, daraja yake na maelezo.

Tafsiri zinatoka wapi?

Kutoka HadeethEnc.com, Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa. Kila hadithi inaonyeshwa kama walivyoichapisha, pamoja na chanzo na daraja yake, na viungo vya asili.

Naweza kupata kikumbusho cha kila siku?

Ndiyo. Programu ya bure ya Qabas kwa Android inakukumbusha adhkar za asubuhi na jioni kila siku na ina kihesabu hicho hicho.