Dua za kujikinga kwa Allah

Mambo ambayo Mtume ﷺ alijikinga kwa Allah kutokana nayo.

1 Mara moja

اللهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ زَوَالِ نِعْمَتِكَ، وَتَحَوُّلِ عَافِيَتِكَ، وَفُجَاءَةِ نِقْمَتِكَ، وَجَمِيعِ سَخَطِكَ

Maana na chanzo

kutoka kwa Abdullahi bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Ilikuwa miongoni mwa dua za Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- ni kusema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kutokana na kuondokewa neema zako, na kubadilika kwa afya yako, na kufikiwa ghafla na adhabu zako, na kila aina ya hasira zako"

Imepokelewa Imamu Muslim Daraja: Sahihi

Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliomba kinga ya mambo manne:

La kwanza: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajilinda kwako kutokana na kuondokewa na neema zako" za dini na dunia, na nibakie madhubuti ndani ya Uislamu, na najiweka mbali kutoangukia katika maasi yanayoondosha neema.

La pili: "Na kubadilika ghafla neema zako" Kubadilika kwake na kuwa balaa; ninakuomba afya isiyo na kikomo, na kusalimika dhidi ya mabalaa na magonjwa.

La tatu: "Na kufikwa ghafla na adhabu zako" kama vile balaa au maasi, gharika na adhabu vinapokuja ghafla, huwa hakuna muda wa kutubia na kurekebisha mabaya, na hapa hufikwa na adhabu kali na kubwa mno.

La nne: "na hasira zako zote" na sababu zenye kupelekea kupata hasira zako; kwani yeyote utakayemchukia basi atakuwa kapata hasara.

Na alileta Mtume rehema na amani ziwe juu yake tamko la wingi; ili likusanye mpaka sababu za hasira zake Aliyetakasika na kutukuka miongoni mwa kauli na matendo na itikadi.

Faida

  • Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhitaji kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Kuomba kinga huku kumeambatana na: Taufiki ya kushukuru neema, na hifadhi ya kutotumbukia ndani ya maasi; kwa sababu huondoa neema.
  • Pupa ya kujiweka mbali na maeneo ya hasira za Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Aliomba kinga Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutokana na kufikwa ghafla na hasira za Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwa sababu akiamua kumlipiza mja kwa mabaya anayoyafanya basi yatamfika mabalaa asiyoweza kuyazuia, na hayazuiliwi na viumbe wengine, hata wakikusanyika wote.
  • Alijikinga Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutokana na kutoweka kwa afya yake Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwa sababu endapo Mungu atampendelea kwa kumpa afya yake, basi atakuwa kapata bahati ya kupata kheri zote za dunia na Akhera, ikimuondokea basi atakuwa kapatwa na shari ya dunia na Akhera, kwani afya ndio sababu ya kutengemaa dini na dunia.

Soma kwenye HadeethEnc.com

2 Mara moja

اللهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْعَجْزِ وَالْكَسَلِ وَالْجُبْنِ وَالْبُخْلِ وَالْهَرَمِ وَعَذَابِ الْقَبْرِ، اللهُمَّ آتِ نَفْسِي تَقْوَاهَا، وَزَكِّهَا أَنْتَ خَيْرُ مَنْ زَكَّاهَا، أَنْتَ وَلِيُّهَا وَمَوْلَاهَا، اللهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ عِلْمٍ لَا يَنْفَعُ، وَمِنْ قَلْبٍ لَا يَخْشَعُ، وَمِنْ نَفْسٍ لَا تَشْبَعُ، وَمِنْ دَعْوَةٍ لَا يُسْتَجَابُ لَهَا

Maana na chanzo

Kutoka kwa Zaidi bin Arqam radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Sikwambieni isipokuwa kama alivyokuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: Alikuwa akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kutokana na kushindwa, na uvivu, na uoga, na ubahili, na ukongwe, na adhabu ya kaburi, Ewe Mwenyezi Mungu ipe nafsi yangu uchamungu wake, na uitakase kwani wewe ndiye mbora wa kuitakasa, wewe ndiye msimamizi wa nafsi na mtawala wake. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na elimu isiyo na manufaa, na moyo usiyo nyenyekea, na nafsi isiyo tosheka, na maombi yasiyo jibiwa".

Imepokelewa Imamu Muslim Daraja: Sahihi

Maelezo

Ilikuwa katika dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako" na ninajiegemeza kwako, "Kutokana na kushindwa" kwa kukosa uwezo wa unjanja wenye manufaa, "na uvivu" kwa kushindwa kuendesha mambo, aliyeshindwa hana ujanja, na mvivu hana haja nao, "na uoga" kwa kujizuia kuyaendea yanayopasa kufanywa, "na ubahili" kwa kuzuia yanayopaswa kuyatoa, "na ukongwe" na ukubwa wa umri unaopelekea udhaifu wa mwili, "na adhabu za kaburi" na sababu zinazopelekea katika hayo. "Ewe Mwenyezi Mungu ipe nafsi yangu" na uipe na uiwezeshe katika "uchamungu wake" kwa kufanya uchamungu na kuacha maasi, "na uitakase" na uisafishe kutokana na uchafu na tabia mbaya, "wewe ndiye mbora wa kuitakasa" na wala hakuna wa kuitakasa yeyote zaidi yako, "Wewe ndiye msimamizi wake" na mtetezi wake na msimamizi wake, "na Mola wake" Msimamizi wa mambo yake, na Mola wake Mlezi na mwenye kuineemesha. "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na elimu isiyokuwa na manufaa", kama elimu ya nyota na ukuhani na uchawi, au isiyo na manufaa Akhera, au elimu isiyofanyiwa kazi, "na moyo usionyenyekea" kwako, na wala haujishushi, na wala hautulii, wala hautulizani kwa kukutaja, "na nafsi isiyoshiba" wala isiyokinai kwa yale iliyopewa na Mwenyezi Mungu na akairuzuku miongoni mwa halali nzuri, "na kutokana na maombi" yenye kurudishwa "yasiyopokelewa".

Faida

  • Ni sunna kuomba kinga dhidi ya mambo haya yaliyotajwa katika hadithi.
  • Himizo juu ya uchamungu na kusambaza elimu na kuifanyia kazi.
  • Elimu yenye manufaa inayoitakasa nafsi na kuizalishia hofu ya Mola Mlezi Aliyetakasika na kutukuka, na kutiririka katika viungo vingine vilivyobakia.
  • Moyo wenye unyenyekevu ni ule unaoogopa na kutaharuki wakati wa kutajwa Mwenyezi Mungu kisha ukalainika na kutulia.
  • Chukizo la kuipupia dunia na kutoshiba kutokana na matamanio yake na ladha zake, na ndio maana nafsi inayotokota yenye pupa na starehe za dunia ndio adui mkubwa wa mtu, na ndio maana alijikinga dhidi yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  • Inampasa mja ajitenge mbali na sababu za kukataliwa dua na kutojibiwa kwake.
  • Amesema Nawawi: Hadithi hii na nyinginezo ni miongoni mwa dua zenye vina, ni ushahidi waliousema wanachuoni; kuwa vina visivyotakiwa katika dua ni vile vya kujikalifisha, kwani huondoa utulivu na unyenyekevu na utakasifu, na hupumbaza na kuacha kujinyenyekeza na moyo kuwa mtupu, ama inayofanyika bila kujikalifisha wala kushughulisha akili kwa sababu ya ukamilifu wa ufasaha na mfano wake, au ikawa mtu kaihifadhi, hii haina ubaya, bali ndio nzuri.

Soma kwenye HadeethEnc.com

3 Mara moja

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ مُنْكَرَاتِ الأَخْلاَقِ وَالأَعْمَالِ وَالأَهْوَاءِ

Maana na chanzo

Kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na tabia mbaya na matendo mabaya, na matamanio mabaya"

Imepokelewa Imamu Tirmidhiy Daraja: Sahihi

Maelezo

Ilikuwa katika dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga" Yani: Ninaomba ulinzi na ukaribu "kwako" na si kwa asiyekuwa wewe, "kutokana tabia mbovu" alizozikataza Mwenyezi Mungu na Mtume wake, "katika tabia" kama chuki na husuda na kiburi, "na" mabaya "katika matendo" kama kutukana na kushutumu, "na" yote "matamanio", ambayo nafsi inayatamani hali yakuwa yanakwenda kinyume na sheria.

Faida

  • Ubora wa dua hii na kujibiwa kwake.
  • Muumini anapupia kuepuka tabia mbaya na matendo maovu, na anachukua tahadhari ya kufuata matamanio na kutumbukia katika matamanio.
  • Kugawanyika kwa tabia na matendo na matamanio katika maovu na mazuri.

Soma kwenye HadeethEnc.com

Maswali

Kuna nini kwenye ukurasa huu?

Dua za kujikinga: kila moja kwa Kiarabu, pamoja na maana yake, hadithi inakotoka, daraja yake na maelezo.

Tafsiri zinatoka wapi?

Kutoka HadeethEnc.com, Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa. Kila hadithi inaonyeshwa kama walivyoichapisha, pamoja na chanzo na daraja yake, na viungo vya asili.

Naweza kupata kikumbusho cha kila siku?

Ndiyo. Programu ya bure ya Qabas kwa Android inakukumbusha adhkar za asubuhi na jioni kila siku na ina kihesabu hicho hicho.