Dua ya kulala na adhkar za kabla ya kulala

Aliyokuwa akisema na kusoma Mtume ﷺ alipokwenda kitandani.

1 Mara moja

قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ ﴿١﴾ اللَّهُ الصَّمَدُ ﴿٢﴾ لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ ﴿٣﴾ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ ﴿٤﴾
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ ﴿١﴾ مِن شَرِّ مَا خَلَقَ ﴿٢﴾ وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ ﴿٣﴾ وَمِن شَرِّ النَّفَّاثَاتِ فِي الْعُقَدِ ﴿٤﴾ وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ ﴿٥﴾
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ﴿١﴾ مَلِكِ النَّاسِ ﴿٢﴾ إِلَهِ النَّاسِ ﴿٣﴾ مِن شَرِّ الْوَسْوَاسِ الْخَنَّاسِ ﴿٤﴾ الَّذِي يُوَسْوِسُ فِي صُدُورِ النَّاسِ ﴿٥﴾ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ ﴿٦﴾

Maana na chanzo

Imepokelewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa anapolala kitandani kwake wakati wa kila usiku alikuwa akikusanya viganja vyake, kisha akivipuliza na kuvisomea : {Qul-huwallahu Ahad}, na {Qul-A uudhu birabbil falaq} na (Qul-Auudhu birabbi naas } Kisha hujipaka kwa viganja hivyo sehemu awezayo katika mwili wake, anaanza kupaka kichwa chake na uso wake na sehemu ya mbele ya mwili wake, anafanya hivyo mara tatu.

Imepokelewa na Al-Bukhaariy Daraja: Sahihi

Maelezo

Ilikuwa katika miongozo yake Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- pindi anapopanda kitandani kwake kwa ajili ya kulala, ni kukusanya viganja vyake na kuviinua juu kama anavyofanya mwenye kuomba-na huvipuliza viganja hivyo kwa mdomo wake upulizaji wa taratibu pamoja na kutemea matemate kidogo na anasoma Sura tatu {Qul-huwallahu Ahadu} na {Qul-audhu birabbil falaq} na {Qul-auudhu birabbi naas} Kisha hupaka kwa kutumia viganja vyake sehemu anayoweza katika mwili wake; Kwa kuanzia kichwa chake na uso wake na sehemu ya mbele katika mwili wake, na hurudia kitendo hicho mara tatu.

Faida

  • Ni sunna kusoma suratul Ikhlaas na Muawidhataini (Sura mbili za kinga) kabla ya kulala na kupuliza kwa sura hizo, na kupakaa sehemu aiwezayo katika mwili wake.

Soma kwenye HadeethEnc.com

2 Mara moja

آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنْزِلَ إِلَيْهِ مِنْ رَبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ كُلٌّ آمَنَ بِاللَّهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِنْ رُسُلِهِ وَقَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ ﴿٢٨٥﴾ لَا يُكَلِّفُ اللَّهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِنْ نَسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِنَا رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا أَنْتَ مَوْلَانَا فَانْصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿٢٨٦﴾

Maana na chanzo

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayesoma aya mbili za mwisho wa suratul Baqara zitamtosheleza".

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Daraja: Sahihi

Maelezo

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayesoma aya mbili za mwisho katika suratul-Baqara usiku, basi Mwenyezi Mungu atamtosheleza na shari na kila lenye kuchukiza, na imesemwa: Zitamtosheleza na kisimamo cha usiku, na imesemwa: Zita

mtosha na nyiradi zote, na imesemwa kuwa: Ni kiwango kidogo kinachoweza kumtosheleza mtu na kusoma Qur'ani katika kisimamo cha usiku, na imesemwa kinyume na hivyo, na huenda yote yaliyotajwa yanakusanywa na tamko hilo.

Faida

  • Kumebainisha fadhila za mwisho wa suratul-Baqara, nazo ni kuanzia katika kauli yake Mtukufu: "Aamanarrasuulu..." mpaka mwisho wa sura.
  • Mwisho wa suratul-Baqara humzuilia mabaya msomaji wake na shari na Shetani atakaposoma katika usiku.
  • Usiku huanza kwa kuzama jua, na humalizika kwa kuchomoza Alfajiri.

Soma kwenye HadeethEnc.com

3 mara 3

اللَّهُمَّ قِنِي عَذَابَكَ يَوْمَ تَبْعَثُ عِبَادَكَ

Maana na chanzo

Kutoka kwa Hudheifa bin Yamaani -radhi za Allah ziwe juu yake-: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anapotaka kulala anaweka mkono wake chini ya kichwa chake, kisha anasema: "Ewe Mwenyezi Mungu nikinge na adhabu yako siku utakapowakusanya au kuwafufua waja wako".

Imepokelewa Imamu Tirmidhiy Daraja: Sahihi

Maelezo

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapochukua malazi yake kwa ajili ya kulala, anauchegemea mkono wake wa kulia na anauwekea shavu lake la kulia, akasema: "Ewe Mwenyezi Mungu" Mola wangu Mlezi "Nikinge" na unihifadhi kutokana na "adhabu yako" na mateso yako "siku utakapowakusanya au kuwafufua waja wako" katika siku ya hesabu, siku ya Kiyama.

Faida

  • Fadhila za dua hii yenye baraka, na sunna ya kudumu nayo kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  • Sunna ya kulalia upande wa kulia.
  • Amesema Assanadi: Kauli yake "Ewe Mwenyezi Mungu nikinge na adhabu yako" Inaonyesha kuwa inampasa mwenye akili aufanye usingizi kuwa nyenzo ya kukumbuka kifo na kufufuliwa kunakofuata baada yake.
  • Kinga dhidi ya adhabu ya Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama inakuwa kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake, kwa kumuwezesha mja kufanya matendo mema na msamaha wa Mwenyezi Mungu kwa madhambi yake.
  • Unyenyekevu wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Mola wake Mlezi na Mmiliki wake Mtukufu.
  • Kumethibitishwa kukusanywa na kurejea, na kwamba watu watarejea kwa Mola wao Mlezi ili awahesabu juu ya matendo yao, atakayekuta kheri basi na amshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu, na atakayekuta kinyume na hivyo basi asimlaumu yeyote isipokuwa nafsi yake, bali haya ni matendo ya waja anawakusanyia Mwenyezi Mungu kwao.
  • Pupa ya Maswahaba radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao katika kubainisha hali za Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kulala kwake.
  • Kauli yake: "Aliweka mkono wake wa kulia chini ya shavu lake" nayo ni katika kawaida yake rehema na amani ziwe juu yake kuanzia kulia katika kila kitu isipokuwa yale yaliyokuwa kinyume chake.
  • Kulalia upande wa kulia hurahisisha kuzinduka, kwa sababu moyo huwa hautulii katika hali hiyo, na huustarehesha moyo; kwa sababu huwa uko upande wa kushoto, endapo mja atalala kwa upande wa kushoto ataudhuru moyo kwa sababu ya viungo kuuelemea.

Soma kwenye HadeethEnc.com

4 Mara moja

سُبْحَانَ اللَّهِ (٣٣)، الْحَمْدُ لِلَّهِ (٣٣)، اللَّهُ أَكْبَرُ (٣٤)

Maana na chanzo

Imepokelewa kutoka kwa Ally -radhi za Allah ziwe juu yake-: ِAlikuja Fatma radhi za Allah ziwe juu yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akimlalamikia juu ya jiwe la kusagia lililokuwa likichubua mikono yake, na zilimfikia taarifa kuwa Mtume amejiwa na mjakazi, lakini alikuwa hajakutana naye, akalieleza hilo kwa Aisha, alipokuja Aisha akamwambia, anasema Fatma: Akaja kwetu hali yakuwa tumekwisha panda kitandani, basi tukaamka tukasimama, akasema: "Haina haja ya kusimama kaeni tu mahala penu" Akaja akakaa kati yangu na Fatma, mpaka nikahisi ubaridi wa miguu yake tumboni kwangu, Mtume akasema: «Je, nisikujulisheni kitu bora zaidi kuliko hicho mlichoomba? Mtakapokwenda kulala basi msabihini Mwenyezi Mungu; yaani (Sub-haanallaah) mara thelathini na tatu, na mhimidini (Al-hamdulillaah) mara thelathini na tatu, na mtukuzeni (Allahu Akbar) mara thelathini na nne, kufanya hivyo ni bora zaidi kwenu kuliko mfanyakazi.”

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Daraja: Sahihi

Maelezo

Fatima Mwenyezi Mungu amuwie radhi binti wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alilalamikia athari za mashine ya kusagia (Jiwe) aliyoipata mkononi mwake, hivyo alipokuja mtumwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuendea na kumuomba ampe mmoja kati ya watumwa hao, ili amsaidia kwa kazi za nyumbani, lakini hakumkuta Mtume nyumbani kwake, ila alimkuta Aisha Mwenyezi Mungu amuwie radhi, hivyo akamwambia kuhusu hilo, Alipofika rehema na amani ziwe juu yake Aisha akamueleza kuwa Fatma alikuja kwake kumuomba mfanyakazi. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaja kwa Fatma na Ally Mwenyezi Mungu awawie radhi, ndani ya nyumba yao wakiwa wamelala kitandani wakijiandaa kwa usingizi, akakaa katikati yao mpaka Ally radhi za Allah ziwe juu yake akahisi ubaridi wa miguu ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, juu ya tumbo lake, akasema: Hivi nisikufundisheni kilicho bora zaidi kuliko mlichoniomba, kuliko kukupeni mtumishi? Wakasema: Ndio, tufundishe, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Mtakapochukua nafasi zenu za kulala usiku, basi toeni takbira mara thelathini na nne, kwa kusema: Allahu Akbaru, Na toeni tasbihi mara thelathini na tatu, kwa kusema: Sub-haanallaah, Na himidini mara thelathini na tatu, kwa kusema: Al-hamdulillah; Dhikiri hii ni bora sana kwenu nyinyi kuliko kuwa na mtumishi.

Faida

  • Inapendeza kudumu na dhikiri hi iliyobarikiwa, kama ilivyoripotiwa kuwa Ally radhi za Allah ziwe juu yake hakuiacha amri hii ya Mtume iliyokusanya mambo mengi, mpaka katika usiku wa mapigano ya Swuffin.
  • Dhikiri hii haisemwi tu wakati wa kulala usiku, na maneno yake kwa mujibu wa Muslim yanatokana na riwaya ya Muadhi kutoka kwa Shu’ba: “Mkichukua vitanda vyenu wakati wa usiku.”
  • Muislamu akiisahau dhikri hii mwanzoni mwa usiku kisha akaikumbuka mwishoni mwa usiku, hakuna ubaya kuisema; Kwa sababu Ally Mwenyezi Mungu amuwie radhi, msimuliaji wa hadithi, anasema kwamba alisahau kuyasema katika usiku wa mapigano ya Swaffin mwanzoni mwa usiku, kisha akakumbuka na kuyasema kabla ya Alfajiri.
  • Amesema Al-Muhallab: Ndani ya Hadithi hii kunaonyesha kuwa mtu ailazimishe familia yake kufanya anayojilazimisha yeye, kama kutanguliza maisha ya Akhera kuliko Dunia hii ikiwa wana uwezo wa kufanya hivyo.
  • Amesema bin Hajar Al-Asqalani: Atakayedumu na dhikiri hii hatadhurika na wingi wa kazi, wala haitakuwa vigumu kwake hata akichoka.
  • Amesema Al-Aini: Suala la kuwa bora ni ima maana yake ni kuwa inahusiana na Akhera na mfanyakazi duniani, na Akhera ni bora zaidi na yenye kudumu, au ina maana kwamba kuhusiana na kile alichoomba atapata nguvu kwa sababu ya dhikiri hii ambayo itamuwezesha kufanya kazi zaidi kuliko uwezo wa mfanyakazi.

Soma kwenye HadeethEnc.com

Maswali

Kuna nini kwenye ukurasa huu?

Dua ya kulala: kila moja kwa Kiarabu, pamoja na maana yake, hadithi inakotoka, daraja yake na maelezo.

Tafsiri zinatoka wapi?

Kutoka HadeethEnc.com, Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa. Kila hadithi inaonyeshwa kama walivyoichapisha, pamoja na chanzo na daraja yake, na viungo vya asili.

Kihesabu kinafanyaje kazi?

Gusa kihesabu chini ya dhikri na kitahesabu kurudi nyuma hadi sifuri. Kipo kwenye ukurasa huu tu na hakuna kinachohifadhiwa.

Naweza kupata kikumbusho cha kila siku?

Ndiyo. Programu ya bure ya Qabas kwa Android inakukumbusha adhkar za asubuhi na jioni kila siku na ina kihesabu hicho hicho.