Adhkar za jioni (Adhkar al-masa) pamoja na maana

Adhkar zinazosomwa jioni, baada ya swala ya Alasiri hadi usiku, kama zilivyopokelewa katika hadithi sahihi.

1 mara 3

قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ ﴿١﴾ اللَّهُ الصَّمَدُ ﴿٢﴾ لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ ﴿٣﴾ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ ﴿٤﴾
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ ﴿١﴾ مِن شَرِّ مَا خَلَقَ ﴿٢﴾ وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ ﴿٣﴾ وَمِن شَرِّ النَّفَّاثَاتِ فِي الْعُقَدِ ﴿٤﴾ وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ ﴿٥﴾
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ﴿١﴾ مَلِكِ النَّاسِ ﴿٢﴾ إِلَهِ النَّاسِ ﴿٣﴾ مِن شَرِّ الْوَسْوَاسِ الْخَنَّاسِ ﴿٤﴾ الَّذِي يُوَسْوِسُ فِي صُدُورِ النَّاسِ ﴿٥﴾ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ ﴿٦﴾

Maana na chanzo

Kutoka kwa Abdillah Bin Khubaibi Radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa yeye amesema: Tulitoka katika usiku wa mvua kubwa na giza nene, tukimtafuta Mtume rehema na amani ziwe juu yake; ili atusalishe, anasema: Nikampata, akasema: "Sema" Nikawa sikusema kitu, kisha akasema: "Sema", Nikawa sikusema kitu, akasema: "Sema" Nikasema: Niseme nini? Akasema: "Sema Yeye ni Mwenyezi Mungu mmoja tu" na sura mbili za kinga unapofika nyakati za jioni na nyakati za asubuhi mara tatu, zitakutosheleza kila kitu".

Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na Nasaai Daraja: Sahihi

Maelezo

Anaeleza swahaba mtukufu Abdullah Bin Khubaib radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa wao walitoka katika usiku wenye mvua kubwa, na giza lilikuwa nene, kwa ajili ya kumtafuta Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake; ili awasalishe, wakamkuta, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: "Sema" Yaani: Soma, akawa hakusoma kitu, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akarejea kauli yake kwake, Abdullah akasema: Nisome nini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Soma suratul Ikhlaswi (Qul-huwallaahu ahadi), na sura mbili za kinga (Qul-Audhubirabbil-falaq), na (Qul-Audhubirabbin-naas), wakati wa jioni, na wakati wa asubuhi, mara tatu tatu, zitakuhifadhi na kila shari, na zitakukinga na kila baya.

Faida

  • Sunna ya kusoma Suratul Ikhlasi na sura mbili za kinga asubuhi na jioni, nakuwa sura hizo ni kinga dhidi ya kila shari.
  • Ubora wa kusoma suratul Ikhlasi na sura mbili za kinga.

Soma kwenye HadeethEnc.com

2 Mara moja

اللَّهُمَّ بِكَ أَمْسَيْنَا، وَبِكَ أَصْبَحْنَا، وَبِكَ نَحْيَا، وَبِكَ نَمُوتُ، وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ

Maana na chanzo

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: Yakwamba yeye alikuwa akisema anapoamka: "Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeamka, na kwako tunashinda, na kwako tunakuwa hai, na kwako tutakufa, na kwako tutafufuliwa" Na anaposhinda jioni anasema: "Kwako tumeshinda, na kwako tumeamka, na kwako tunakuwa hai, na kwako tunakufa, na kwako tutafufuliwa" Akasema: Na mara nyingine: "Na kwako ndio marejeo".

Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah Daraja: Ni nzuri (Hasan)

Maelezo

Alikuwa rehema na amani ziwe juu yake anapofikiwa na asubuhi nayo ni mwanzo wa mchana pamoja na kuchomoza Alfajiri anasema:

"Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeamka" tukiwa tumegubikwa na hifadhi yako na kufunikwa na neema zako, tukishughulika na kukutaja, tukitaka msaada kwa jina lako, tukienewa na taufiki yako, tukifanya harakati zenu kwa ujanja wako na nguvu zako, "na kwako tumeshinda, na kwako tunakuwa hai, na kwako tunakufa" yaani; hii ni kama lafudhi iliyotangulia isipokuwa hii imefanywa ya jioni, atasema: Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeshinda, na kwa jina lako Muhuishaji tunakuwa hai, na kwa jina lako Mfishaji tutakufa, "na kwako tutafufuliwa" na kufufuliwa baada ya kifo, na kusambaa baada ya kukusanywa, itaendelea hali yetu namna hii katika nyakati zote, na hali zingine zilizobakia, na wala sitoachana nayo wala sitoihama.

Na ikimfikia jioni baada ya Lasiri atasema: "Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeshinda, na kwako tumeamka, na kwako tunakuwa hai, na kwako tutafuka, na marejeo ni kwako" na marejeo katika dunia, na mafikio katika mwisho, wewe ndiye unayenihuisha na wewe ndiye unayenifisha.

Faida

  • Inapendeza kusoma dua hii asubuhi na jioni, kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  • Uhitaji wa mja kwa Mola wake Mlezi katika hali zake na nyakati zake zote.
  • Kilicho bora katika kusoma Adhkari, asubuhi ni kuanzia kuchomoza kwa Alfajiri mpaka kuchomoza Jua mwanzo wa mchana, na baada ya Laasiri mpaka kabla ya kuzama, ikiwa atazisoma baada ya hapo, yaani: Asubuhi akazisoma baada ya Jua kunyanyuka itafaa, na hata akizisoma baada ya Adhuhuri itafaa pia, na akizisoma baada ya Magharibi itafaa, huo ndio wakati wa kufanya Adhkari.
  • Mahusiano kati ya kauli yake "na kwako tutafufuliwa" na kusemwa asubuhi, kauli hii inamkumbusha kuhuishwa na kufufuliwa kukubwa pindi watapokufa watu na kufufuliwa siku ya Kiyama, huku ni kufufuliwa kupya, na siku mpya ambayo hurejeshwa roho ndani yake, na watu hutawanyika ndani yake, na wanapumua katika asubuhi hii mpya aliyoiumba Mwenyezi Mungu; ili iwe shahidi kwa mwanadam, na ili ziwe nyakati zake mida yake ni hazina ya matendo yetu.
  • Mahusiano kati ya kauli yake "Na kwako ndio mafikio" na kusemwa jioni, ni pale watakaporejea watu katika matendo yao na kutawanyika kwa kwenda katika masilahi yao na maisha yao, wanarejea katika nyumba zao, na wanadumishwa katika raha baada yakuwa wametawanyika, inamkumbusha kurejea kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka kwa hatima na marejeo na mafikio.

Soma kwenye HadeethEnc.com

3 Mara moja

اللَّهُمَّ أَنْتَ رَبِّي لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ خَلَقْتَنِي وَأَنَا عَبْدُكَ وَأَنَا عَلَى عَهْدِكَ وَوَعْدِكَ مَا اسْتَطَعْتُ أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا صَنَعْتُ أَبُوءُ لَكَ بِنِعْمَتِكَ عَلَيَّ وَأَبُوءُ لَكَ بِذَنْبِي فَاغْفِرْ لِي فَإِنَّهُ لَا يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا أَنْتَ

Maana na chanzo

Kutoka kwa Shadaad Bin Ausi Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na Amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Bwana wa Istighfari (Dua ya kuomba msamaha) Ni kusema: Allaahumma anta Rabbi Laa ilaaha illaa anta, khalaqtani wa anaa abduka wa ana a'laa a'hdika, wawa'dika mastatwa'tu, auudhubika min Sharri maa swana'tu, abuu ulaka bini'matika alaiyya, wa abuu ulaka bidhambi faghfirlii, fa innahuu laa yaghfirudh-dhunuuba illaa anta" Akasema: "Na atakayeisema dua hii mchana akiwa na yakini nayo, akafa katika mchana wake huo kabla hajafika jioni, basi atakuwa miongoni mwa watu wa peponi, na atakayeisema wakati wa usiku akiwa na yakini nayo, akafariki kabla hajafika asubuhi, basi huyo atakuwa miongoni mwa watu peponi".

Imepokelewa na Al-Bukhaariy Daraja: Sahihi

Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake anaeleza kuwa Istighfari (Kuomba msamaha) kuna matamshi mengi, nakuwa matamshi bora na makubwa zaidi ni mja kusema: "Ewe Mwenyezi Mungu wewe ndiye Mola Mlezi hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa wewe, umeniumba na mimi ni mja wako na mimi nipo juu ya ahadi yako na maonyo yako kwa kiasi niwezavyo, ninataka hifadhi kwako kutokana na shari niliyo ifanya, ninakiri kwa neema zako zilizo juu yangu, na ninakiri kwa madhambi yangu, basi nisamehe mimi, kwani hakuna afutae madhambi isipokuwa wewe. Hivyo basi mja anaanza kukiri upweke wa Mwenyezi Mungu, nakuwa Mwenyezi Mungu ndiye muumba wake na muabudiwa wake hana mshirika wake, na kuwa yeye yuko katika ahadi aliyomuahidi Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, miongoni mwa imani na utiifu kwake, kwa kadiri ya uwezo wake; kwa sababu mja kwa namna yoyote atakavyotekeleza ibada hawezi kutekeleza yote aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu, na wala hawezi kutimiza haki stahiki katika kushukuru neema, nakuwa yeye anajilinda kwa Mwenyezi Mungu, na anajikinga kwake, kwani yeye ndiye mwenye kutakwa ulinzi kutokana na shari zote alizozitengeneza mja, Nakuwa yeye anakiri na kukubali kwa hiari yake neema zake juu yake, na anairudia nafsi yake kwa kukiri na kukubali madhambi yake na maasi yake, Na baada ya kupitia kwa Mwenyezi Mungu, atamuomba Mola wake asitiri makosa yake na amkinge na dhambi zake kwa msamaha wake na fadhila zake na rehema zake, kwani hakuna awezaye kusamehe madhambi ila yeye Mtukufu. Kisha akaeleza rehema na amani ziwe juu yake kuwa dua hii ni katika dhikiri na dua za asubuhi na jioni, nakuwa atakayeisema kwa yakini na kwa kuhudhurisha moyo wake na kwa kuiamini, mwanzo wa siku yake, kwanzia kuchomoza kwa Jua mpaka kupinduka kwake, nao ni wakati wa mchana, akafa, ataingia peponi, Na atakayeisema usiku, nao ni kuanzia kuzama kwa jua mpaka kuchomoza kwa Alfajiri, akafariki kabla hajafika asubuhi, ataingia peponi.

Faida

  • Namna za kuomba msamaha zinatofautiana na baadhi yake ni bora kuliko zingine.
  • Nakuwa ni wajibu kwa mja apupie kumuomba Mwenyezi Mungu kwa dua hii; kwani ndio bwana wa dua zote za kuomba msamaha.

Soma kwenye HadeethEnc.com

4 mara 3

بِسْمِ اللَّهِ الَّذِي لَا يَضُرُّ مَعَ اسْمِهِ شَيْءٌ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ

Maana na chanzo

Kutoka kwa Abana bin Othman amesema: Nilimsikia Othman bin Affan radhi za Allah ziwe juu yake akisema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Yeyote atakayesema: Bismillaahi lladhi laa yadhurru ma'asmihi shai un fil Ardhwi walaa fis samaai, wahuwas samiiu'l 'aliim, (Kwa jina la Mwenyezi Mungu ambaye hakuna kinachoweza kudhuru pamoja na jina lake kitu chochote ardhini wala mbinguni, naye ni msikivu na mjuzi) mara tatu, basi halitomfika balaa la ghafla, mpaka atakapoamka, na atakayesema wakati wa asubuhi mara tatu, halitomfika balaa la ghafla mpaka atakapofika jioni" Akasema: Akapatwa na mtihani Abana bin Othman Al-Faaliji, basi yule bwana aliyesikia hadithi akawa anamtazama, akasema kumwambia: Vipi mbona unanitazama? Wallahi sijamsemea uongo Othman, wala Othman hajamsemea uongo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, lakini siku niliyofikwa na balaa, nilichukizwa na jambo fulani nikasahau kuisoma.

Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah na Ahmad Daraja: Sahihi

Maelezo

Ameainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema asubuhi ya kila siku baada ya kuchomoza Alfajiri, na jioni ya kila usiku kabla ya kuzama jua mara tatu: "Bismillaah" Ninataka msaada na ninajilinda dhidi ya kila chenye kuudhi "ambaye hakidhuru" kwa kulitaja "pamoja na jina lake" yaani "chochote" vyovyote vile kitakavyokuwa kikubwa "katika ardhi" na vinavyotoka ndani yake miongoni mwa mabalaa "wala mbinguni" na kinachoshuka kutoka humo miongoni mwa mabalaa "naye ni msikivu" wa kauli zetu "mjuzi" wa hali zetu.

Atakayesema wakati wa jioni halitomfika balaa la ghafla mpaka afike asubuhi, na atakayesema wakati wa asubuhi balaa halitomfika la ghafla mpaka afike jioni.

Akaipatia riwaya ya hadithi ya Abana bin Othman Al-Falij; Nayo ni kudhoofika kwa baadhi ya upande wa mwili, yule bwana aliyesikia kwake hadithi akamtazama Abana kwa kustaajabu?! Abana akasema kumwambia yule bwana: Mbona wanitazama?! Wallah sijamzulia uongo Othman, wala Othman hajamzulia uongo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, lakini leo yamenifika yale aliyoyakadiria Mwenyezi Mungu kwangu kuyasema, nimepatwa na hasira nikasahau kusema maneno haya yaliyotajwa.

Faida

  • Inapendeza kuleta dhikri hii asubuhi na jioni; ili mwanadam ahifadhike kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu lisimfike balaa ghafla au madhara ya msiba au mfano wa hayo.
  • Nguvu kubwa ya yakini kwa wema wa mwanzo kwa Mwenyezi Mungu na kuyasadikisha kwao yale aliyoyaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  • Miongoni mwa faida za kufanywa dhikri ziwe za asubuhi na ajioni ni kuondoa hali ya kughafilika kwa muislamu na kuvuta kwake picha endelevu kuwa yeye ni mja wa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Kwa kadiri inavyokuwa imani ya mtajaji Mwenyezi Mungu na unyenyekevu wake na kuhudhurisha kwake moyo, pamoja na kutakasa nia na yakini ndivyo itakavyozidi kupatikana athari ya dhikri.

Soma kwenye HadeethEnc.com

5 Mara moja

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْعَفْوَ وَالْعَافِيَةَ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ، اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْعَفْوَ وَالْعَافِيَةَ فِي دِينِي وَدُنْيَايَ وَأَهْلِي وَمَالِي، اللَّهُمَّ اسْتُرْ عَوْرَاتِي، وَآمِنْ رَوْعَاتِي، اللَّهُمَّ احْفَظْنِي مِنْ بَيْنِ يَدَيَّ، وَمِنْ خَلْفِي، وَعَنْ يَمِينِي، وَعَنْ شِمَالِي، وَمِنْ فَوْقِي، وَأَعُوذُ بِعَظَمَتِكَ أَنْ أُغْتَالَ مِنْ تَحْتِي

Maana na chanzo

Imepokelewa kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema: Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiacha dua hizi, kila anaposhinda jioni na kila anapoamka: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba unipe afya katika Dunia na Akhera, Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba msamaha na afya katika dini yangu na dunia yangu na familia yangu na mali yangu, ewe Mwenyezi Mungu sitiri uchi wangu -Au aibu zangu- na utie amani yote ninayoyahofia, ewe Mwenyezi Mungu nihifadhi toka mbele yangu, na nyuma yangu, na kuliani kwangu, na kushotoni kwangu, na juu yangu, na ninajilinda kwa utukufu wako nisijekuvamiwa tokea chini yangu".

Imepokelewa na Abu Daud, Nasai, Ibn Majah na Ahmad Daraja: Sahihi

Maelezo

Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiacha maombi haya pindi anaposhinda jioni na pindi anapoamka.

"Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba afya" na kusalimika na magonjwa na mabalaa na shida za dunia, na matamanio na fitina za kidunia "Katika dunia na Akhera" kwa au kwa baadae

"Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba msamaha" na kusalimika na aibu, "Katika dini yangu" kutokana na ushirikina na uzushi na maasi, "na dunia yangu" katika majanga na kero na shari, "na familia yangu" mke wangu na wanangu na ndugu zangu, "na mali yangu" na mali zangu na matendo yangu.

"Ewe Mwenyezi Mungu sitiri uchi wangu" Yaani: Na yale yaliyokwangu katika aibu na dosari na mapungufu na ufute dhambi zangu, "na utie amani hofu yangu" Mfadhaiko wangu na hofu yangu.

"Ewe Mwenyezi Mungu nihifadhi" Na uzuie kwangu balaa miongoni mwa yale yenye kuudhi na mabalaa, "mbele yangu na nyuma yangu, na kuliani kwangu, na kushotoni kwangu, na juu yangu" Kiasi kwamba aliomuomba Mwenyezi Mungu amuhifadhi kutoka pande zote; kwa sababu mabalaa na maafa humfika mtu na kumuelekea kutoka moja kati ya pande hizi.

"Na ninajilinda kwa utukufu wako nisijekuvamiwa" na nisichukuliwe hatua toka chini yangu ghafla, nikaangamia ghafla "kutoka chini yangu" nikaangamia kwa kudidimizwa.

Faida

  • Kudumu na maneno haya kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  • Mwanadam kama alivyo anaamrishwa kumuomba Mwenyezi Mungu afya katika dini, vile vile kaamrishwa kumuomba katika dunia.
  • Amesema Attwayibi: Imekusanya pande zote sita; kwa sababu maafa mengi hutokea katika pande hizo, na akatia mkazo katika upande wa chini kwa sababu maafa ya kutoka chini huwa mabaya zaidi.
  • Kilicho bora wakati wa kusoma Adhkari, wakati wa asubuhi: Ni kuanzia kuchomoza kwa Alfajiri mpaka kuchomoza Jua mwanzo wa mchana, na kuanzia baada ya Lasiri mpaka kabla ya Maghribi, ikiwa atasema baada ya wakati huo, yaani: Akazisoma asubuhi baada ya Jua kunyanyuka itafaa pia, na hata akisema baaada ya Adhudhuri itamfaa pia, na ikiwa atazazisema baada ya Maghrib itamtosheleza pia, huo ndio wakati wa kufanya dhikri.
  • Dalili ikionyesha kuwa dhikri inamuda maalum wakati wa usiku kama kusoma aya mbili za mwisho katika suratul baqara basi hii inakuwa ni baada ya kuzama kwa Jua.

Soma kwenye HadeethEnc.com

6 Mara moja

آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنْزِلَ إِلَيْهِ مِنْ رَبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ كُلٌّ آمَنَ بِاللَّهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِنْ رُسُلِهِ وَقَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ ﴿٢٨٥﴾ لَا يُكَلِّفُ اللَّهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِنْ نَسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِنَا رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا أَنْتَ مَوْلَانَا فَانْصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿٢٨٦﴾

Maana na chanzo

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayesoma aya mbili za mwisho wa suratul Baqara zitamtosheleza".

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Daraja: Sahihi

Maelezo

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayesoma aya mbili za mwisho katika suratul-Baqara usiku, basi Mwenyezi Mungu atamtosheleza na shari na kila lenye kuchukiza, na imesemwa: Zitamtosheleza na kisimamo cha usiku, na imesemwa: Zita

mtosha na nyiradi zote, na imesemwa kuwa: Ni kiwango kidogo kinachoweza kumtosheleza mtu na kusoma Qur'ani katika kisimamo cha usiku, na imesemwa kinyume na hivyo, na huenda yote yaliyotajwa yanakusanywa na tamko hilo.

Faida

  • Kumebainisha fadhila za mwisho wa suratul-Baqara, nazo ni kuanzia katika kauli yake Mtukufu: "Aamanarrasuulu..." mpaka mwisho wa sura.
  • Mwisho wa suratul-Baqara humzuilia mabaya msomaji wake na shari na Shetani atakaposoma katika usiku.
  • Usiku huanza kwa kuzama jua, na humalizika kwa kuchomoza Alfajiri.

Soma kwenye HadeethEnc.com

7 mara 10

لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

Maana na chanzo

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Ayub -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayesema: Laa ilaaha illa llaahu wahdahu Laa shariika lahu, Lahul-Mulku walahul hamdu Wahuwa a'laa kulli shai-in qadiir, mara kumi (10) atakuwa ni kama aliyewaacha huru watu wanne katika wana wa Ismail".

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Daraja: Sahihi

Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayesema: "Laa ilaaha illa llaahu wahdahu Laa shariika lahu, Lahul-Mulku walahul hamdu Wahuwa a'laa kulli shai-in qadiir", na maana yake nikuwa: Hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah peke yake asiye na mshirika, nakuwa Yeye Mtukufu amepwekeka kwa Ufalme uliotimia, na mwenye kustahiki kutajwa na sifa na mapenzi na kutukuzwa pasina mwingine asiyekuwa Yeye, nakuwa Yeye ni muweza hakuna chochote kinachomshinda. Atakayeirejea rejea dhikiri hii tukufu kwa siku mara kumi (10); Basi atakuwa kapata malipo mfano wa malipo ya atakayeondoa utumwa kwa watumwa wanne katika watoto wa Ismail bin Ibrahim -Amani iwe juu yao-, na ametaja kizazi cha Ismail -Amani iwe juu yake-; kwa sababu wao ndio watukufu zaidi kuliko wengine.

Faida

  • Ubora wa dhikiri hii iliyokusanya kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Uungu, na Ufalme, na sifa njema, na uwezo uliotimia.
  • Thawabu hizi anazipata atakayesema kwa mfululizo au tofauti tofauti.

Soma kwenye HadeethEnc.com

8 mara 100

سُبْحَانَ اللَّهِ وَبِحَمْدِهِ

Maana na chanzo

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayesema: Sub-haanallahi wabihamdihi, (Ametakasika Mwenyezi Mungu na sifa njema ni zake) kwa siku mara mia moja (100), yatafutwa madhambi yake hata kama yatakuwa na wingi mfano wa povu la Bahari".

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Daraja: Sahihi

Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa atakayesema kwa siku mara mia moja (100): "Sub-haanallaahi Wabihamdihi"; Yatafutwa makosa yake na yatasamehewa, hata kama yatakuwa mengi mfano wa taka nyeupe (povu) zinazoelea Baharini wakati mawimbi yanapotembea na yanapopiga.

Faida

  • Malipo haya anayapata atakayelisema neno hilo ndani ya siku nzima mfululizo au kwa nyakati tofauti tofauti.
  • Tasbihi: Ni kumtakasa Allah kutokana na mapungufu, na kumhimidi: Ni kumsifu kwa ukamilifu pamoja na kumpenda na kumtukuza.
  • Makusudio katika hadithi hii ni kufutwa madhambi madogo madogo, ama madhambi makubwa haya ni lazima yafanyiwe toba.

Soma kwenye HadeethEnc.com

Maswali

Kuna nini kwenye ukurasa huu?

Adhkar za jioni: kila moja kwa Kiarabu, pamoja na maana yake, hadithi inakotoka, daraja yake na maelezo.

Tafsiri zinatoka wapi?

Kutoka HadeethEnc.com, Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa. Kila hadithi inaonyeshwa kama walivyoichapisha, pamoja na chanzo na daraja yake, na viungo vya asili.

Kihesabu kinafanyaje kazi?

Gusa kihesabu chini ya dhikri na kitahesabu kurudi nyuma hadi sifuri. Kipo kwenye ukurasa huu tu na hakuna kinachohifadhiwa.

Naweza kupata kikumbusho cha kila siku?

Ndiyo. Programu ya bure ya Qabas kwa Android inakukumbusha adhkar za asubuhi na jioni kila siku na ina kihesabu hicho hicho.