Ufanye nini baada ya ndoto nzuri au mbaya

Unachofanya na kusema baada ya ndoto nzuri, na baada ya ndoto ya kutisha.

1 Mara moja

Maana na chanzo

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Katada -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Ndoto njema hutoka kwa Mwenyezi Mungu, na ndoto mbaya hutoka kwa Shetani, atakapoota mmoja wenu ndoto mbaya anayoiogopa basi na ateme kushotoni kwake, na aombe ulinzi kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari zake, kwani ndoto hiyo haitomdhuru".

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Daraja: Sahihi

Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ndoto nzuri yenye kufurahisha usingizini hutoka kwa Mwenyezi Mungu, na mtu kuota anayoyachukia na kumhuzunisha hutoka kwa Shetani.

Atakayeota yanayomchukiza basi ateme kushotoni kwake, na aombe kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake; kwani haitomdhuru, kiasi ambacho Mwenyezi Mungu amefanya hayo yaliyotajwa kuwa ni sababu ya kusalimika na hayo yenye kuchukiza yanayoambatana na ndoto.

Faida

  • Ndoto nzuri na mbaya ni yale mambo anayoyaona mtu aliyelala, lakini ndoto nzuri nyingi ni zile anazoota mtu katika mambo ya kheri au mambo mazuri, na ndoto nyingi mbaya huwa katika yale anayoyaona mtu katika mambo ya shari na mabaya, kila moja kati ya hayo hukaa mahala pa lingine.
  • Migawanyiko ya ndoto: 1- Ndoto njema, nayo ni ndoto ya kweli na ni bishara kutoka kwa Mwenyezi Mungu anayoiona au ikaonwa na mtu mwingine kwake, 2- Mazungumzo ya nafsi, nayo ni yale ambayo mtu huzungumza na nafsi yake akiwa macho (kisha yanajirudia akiwa usingizini), 3- Huzuni na hofu ya Shetani na vitisho vyake ili tu amhuzunishe mwanadamu.
  • Jambo la msingi katika mambo yaliyotajwa katika milango ya ndoto ni mambo matatu: Amshukuru Mwenyezi Mungu kwa ndoto hiyo, na ajipe bishara njema kwayo, na aihadithie lakini kwa yule anayempenda na si kwa anayemchukia.
  • Na la msingi katika yale yaliyotajwa katika adabu za ndoto mbaya ni mambo matano: Ajilinde kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake, na kutokana na shari ya Shetani, na ateme pale tu anashituka kutoka usingizini upande wa kushoto mara tatu, na kamwe asiisimulie kwa yeyote, na akitaka kurudi katika usingizi wake basi abadili ubavu aliokuwa awali; kwani ndoto hiyo haitomdhuru.

Soma kwenye HadeethEnc.com

2 Mara moja

Maana na chanzo

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa yeye alimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakapoota mmoja wenu ndoto anayoipenda basi ndoto hiyo inatoka kwa Mwenyezi Mungu, hivyo, amshukuru Mwenyezi Mungu kwa ndoto hiyo na aisimulie, na akiota ndoto kinyume na hiyo katika yale anayoyachukia, basi ndoto hiyo inatokana na Shetani, basi aombe kinga kutokana na shari yake, na wala asiisimulie kwa yeyote, kwani haitomdhuru".

Imepokelewa na Al-Bukhaariy Daraja: Sahihi

Maelezo

Ameeleza Mtume rehema amani ziwe juu yake kuwa ndoto njema yenye kufurahisha usingizini hutoka kwa Mwenyezi Mungu, na akaeleza amshukuru Mwenyezi Mungu kwa hilo, na akiota yanayomchukiza na kumhuzunisha basi hayo yanatokana na Shetani; aombe kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake, na wala asimsimulie yeyote; kwani ndoto hiyo haitomdhuru, kwani Mwenyezi Mungu ameyafanya hayo yaliyotajwa kuwa ni sababu ya kusalimika na kero zinazoambatana na ndoto.

Faida

  • Migawanyiko ya ndoto: 1- Ndoto njema, nayo ni ndoto ya kweli na ni habari njema kutoka kwa Mwenyezi Mungu anayoiona mtu au ikaonwa na mtu mwingine. 2- Mawazo: Nayo ni yale ambayo mtu huwaza mwenyewe akiwa macho. 3- Kutiwa huzuni na hofu na Shetani na vitisho kutoka kwake ili amuhuzunishe mwanadam.
  • Uhalisia wa haya yaliyotajwa katika mlango wa ndoto njema ni mambo matatu: Amshukuru Mwenyezi Mungu juu ya ndoto hiyo, na ajipe habari njema, na aihadithie, lakini asimueleze ila yule anayempenda nasi anayemchukia.
  • Na uhalisia wa hayo yaliyotajwa katika adabu za ndoto zenye kuchukiza ni mambo matano: Ajikinge kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake, na kutokana na shari ya Shetani, na ateme kushoto mara tatu pale anaposhituka kutoka usingizini mwake, na wala asiisimulie kamwe kwa yeyote, na anapotaka kurejea katika usingizi wake basi ageukie ubavu mwingine tofauti na ule aliokuwa mwanzo; kwani ndoto hiyo wala haitomdhuru.
  • Amesema bin Hajari: Hekima na lengo la kukatazwa kumsimulia asiyempenda nikuwa endapo atamsimulia huenda akamfasiria kwa mambo yenye kumchukiza, ima kwa sababu ya chuki au husuda, na huenda ikatokea kwa namna ile ile aliyomfasiria au akajiwahi mwenyewe kwa kuanza kuhuzunika na kukosa furaha, akaamrisha kuacha kumhadithia asiyempenda kwa sababu hiyo.
  • Kushukuru pale zinapotokea neema, na kujirudiarudia kwa mazuri, hilo ni sababu ya kuyadumisha mazuri hayo.

Soma kwenye HadeethEnc.com

Maswali

Kuna nini kwenye ukurasa huu?

Dua baada ya ndoto mbaya: kila moja kwa Kiarabu, pamoja na maana yake, hadithi inakotoka, daraja yake na maelezo.

Tafsiri zinatoka wapi?

Kutoka HadeethEnc.com, Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa. Kila hadithi inaonyeshwa kama walivyoichapisha, pamoja na chanzo na daraja yake, na viungo vya asili.

Naweza kupata kikumbusho cha kila siku?

Ndiyo. Programu ya bure ya Qabas kwa Android inakukumbusha adhkar za asubuhi na jioni kila siku na ina kihesabu hicho hicho.